Sitta avunja kanuni kumhujumu Warioba. TBC wahusishwa, UKAWA waja juu

Rais hawezi kuhutubia Bunge kabla ya Bunge kuwa na Ajenda Mezani na Ajenda ndio itayowasilishwa na Warioba. Sasa badala ya kukosoa akina Lissu walioandaa kanuni ki Layman mnalaumu alierekebisha kosa hilo la kisheria.
Ina maana mpaka leo wewe na kikwete hamjui agenda ya bunge hili maalumu?Ufunguzi wa jambo lolote anazindua mgeni rasmi kisha watoa mada wanaendelea
 
Mkuu, jitahidi/jizoeze kutumia vituo kwenye uandishi wako ili unachokiandika kisomeke kwa urahisi.

Ni ushauri tu!
Mimi namuomba Mungu tuendelee kwa style hii tu,naamini ipo siku wale wote mnaojifanya hamelewi leo mtaelewa tu.

Kwanini Kanuni itenguliwe?na imetenguluwa lini? Ia
Pili walisema Raisi ndiye atakae zindua Bunge iweje leo wabadili.

Siri nayoiona hapa ni Rais amejipanga ili apangue hoja za Warioba na kuweka misimamo ya CCM.
Naunga mkono ahutubie bunge na kulufungua halafu Warioba awakilishe maoni ya wananchi yajadiliwe,hatukuwatuma kujadili hotuba ya Kikwete.

Haya mambo yana mwisho ndugu.
 
bethlehem hebu tambua sheria ziliwekwa ili zifuatwe km alikua aanze mzee wa kaya km sheri au utaratibu ulivyosema swala la dharura wajumbe wangejuzwa tu hizo ni rafu tulizokwisha zoea na unaingiza jambo la kalenga kwenye jambo muhimu linaloongelea mstakabali wa taifa cyo poah pengine hata kalenga rafu ilichezwa
 
Sababu ni kwamba kanuni inamtaka Rais wa JMT kuzindua bunge ndipo M/kiti wa tume aje kuwasilisha rasimu ya katiba katika BMK. Kinyume na matarajio ya kanuni ambazo wao wenyewe wajumbe wa bunge hilo walizipitisha wiki iliyopita, Mh. SS kama M/kiti wa bunge hilo analazimisha kutengua kanuni ili Warioba awasilishe rasimu hiyo na ndipo Rais aje azindue bunge hilo. Kwa mujibu ya wabunge waliokuwa wanapiga kelele wanaotaka kanuni zifuatwe na siyo ivujwe kama Mh. SS anavyotaka.
Naona sita ameanza na mguu mbaya!!mgema akisifiwa sana tembo ulitia maji,toka amechaguliwa amekuwa akitoa kauli kama vile yeye ni zaidi ya kanuni!!,sijui ni kwanini walipoteza muda wa kuziandaa na kuzijadili kama mwenyekiti anaweza kuamua nje ya kanuni,kisa eti busara ya mwenyekiti.
Ameshindwa kutambua kuwa bado ana maadui wengi hasa wa mapambano ya urais wanataka avuruge ili wapete,yeye kwa kulewa sifa wanamchomekea mambo ya ajabu naye anaropoka,namsubiri kwenye kura ya wazi au ya siri.
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!

Natania tu wakuu!!!!!!!!? Kuna watu walikuwa wanamzomea warioba wanadai eti anawasilisha hoja yake kinyume na kanuni.

Makuuu weee, mayala mkubwa kalenga imeingiaje???? manina nn weeewe
 
Huyu bwana hafai. Huwa anasema nchi ina wenyewe. Ameshafanya ziara za mipakani east africa. Yeye huwa ni kutisha tu watumishi. Hafai hata kidogo
 
Zingine hofu tu bila kuwa na sababu za msingi mzee wa viwango ni mtu wa kuzingatia sheria na kanuni tatizo lenu bavicha mnataka kufanya mambo kwa nguvu kama mko kwenye mikutano ya siasa mambo hayaendi hivyo jamani.

mkuu hivi ukikaa kimya si utakuwa unaficha u.ji.nga wako.
 
Majibu y Sitta asubuhi na kutengua kanuni itakuwa fundisho kwenye maamuzi ya wanakubali waseme ndiooooooooooooooo na wana sema Siooooooooooooooo waseme sioooooooooooooo! Waliosema ndio wameshinda. Sitta alifikiri ni lile bunge lake la kipindi kile viwango na kasi anavyovutaa Sitta vitamshinda kama alifikiri kuwa akili alizokuwa akitumia kipidi kile cha bunge la Muungano ndio kipindi hichi..................asipokwenda na wakati atakuwa miongoni mwa maspika dhaifu
 
Sababu ni kwamba kanuni inamtaka Rais wa JMT kuzindua bunge ndipo M/kiti wa tume aje kuwasilisha rasimu ya katiba katika BMK. Kinyume na matarajio ya kanuni ambazo wao wenyewe wajumbe wa bunge hilo walizipitisha wiki iliyopita, Mh. SS kama M/kiti wa bunge hilo analazimisha kutengua kanuni ili Warioba awasilishe rasimu hiyo na ndipo Rais aje azindue bunge hilo. Kwa mujibu ya wabunge waliokuwa wanapiga kelele wanaotaka kanuni zifuatwe na siyo ivujwe kama Mh. SS anavyotaka.

Hakuna kanuni inamyomtaka raisi afungue bunge Raisi hana nafasi yoyote kwenye hili bunge he is just ceremonial
 
Afadhali azomewe mzimu wa Nyerere unamuandama, msaliti mkubwa huyo!
 
warioba charii

Tuangalie mazingira, wakati Warioba alikupokuwa anazomewa wabunge walikuwa wanatamka nini, pia tuangalie matendo yao hili kujua walikuwa wanamaanisha nini?. Je ni kweli kanuni huwa haitenguliwi? Je Warioba hakufuata ratiba iliyokwisha kupangwa ambapo Mh. Rais labda alichelewa au kuhairisha kufika kama ratiba inavyoonyesha?

Kwa hali hii ya bunge hili linalowakilisha wananchi kama ndio liko na sura hii, napata shaka kuwa maendeleo kwa nchi hii hayatakuja kwa mapema.

Sijui kama ni kweli wabunge wachache watapinga na kuzomea mawazo ya wananchi walio wengi?
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!

Natania tu wakuu!!!!!!!!? Kuna watu walikuwa wanamzomea warioba wanadai eti anawasilisha hoja yake kinyume na kanuni.

Ni kweli kuwa alikuwa anawasilisha rasimu kinyume na kanuni walizojiwekea wenyewe. Kwa mujibu wa kanuni Rais anapaswa kufungua bunge kwanza ndipo Warioba awasilishe rasimu ya pili ya Katiba. Kwa kuwa Mwenyekiti ambaye alishiriki pia katika kutunga kanuni hizo alitumia busara yake kuvunja kanuni basi wale wanaopenda kutii walichokuwa wamekubaliana katika kanuni walisimamia kanuni. Katika hili Mwenyekiti wa Bunge la katiba Mh. Sita anapaswa kulaumiwa kwa kutokutii kanuni walizojiwekea wao wenyewe na kujaribu kupindua pindua mambo. Hilo halikubaliki tena.
 
naziheshimu sana kauli za dr slaa alishawai kusema sitta ni mnafiki mkubwa nchi hii.
 
Natania mkuu, ishu ni kwamba kuna watu walikuwa wanamzomea Warioba ili ashindwa kuwasilisha hoja yake kwa hoja kwamba kanuni zilitaka Rais azindue bunge kwanza ndio Warioba awasilishe lakini kanuni zikatenguliwa ili warioba awasilishe kwanza.kwa hiyo wale ambao hawakuridhishwa na utenguzi wa kanuni; bila shaka ndio waliokuwa wanazomea.Hata hivyo utaratibu wa utenguaji wa kanuni ni wa kawaida ndio maana nimewashangaa waliokuwa wanazomea na nikaamua kuleta utani tu maana......!

Tushawahi kuwa na bunge la katiba before?
Mambo yakusema kuvunja kanuni ni jambo la kawaida kwenye mabunge mengine hyo sio hoja mkuu,hili ndiyo bunge letu la kwanza tena maalumu na sio kama mabunge mengine ya JMT,tusipopigania kutunza na kulinda kanuni zetu bs mwenyekitu atatuburuza vibaya sana.

Rais anajua kuwa anahitajika dodoma kuzindua bunge maalumu la katiba kisha mzee wetu awasilishe rasimu ya katiba na kanunu zinasema hivyo,pamoja na kumpa mwenyekiti wa bunge maalumu mamlaka makubwa ila hakupaswa kuendeshwa na utashi wake wa kisiasa.

Wajua kwa nini watendaji wengi wa serikali hawatii sheria za nchi? Mpk wengine kule tanga wanatia sign bila kumshirikisha hata wakili na mkurugenzi wa jiji kama sheria inavyomtaka? Tujitahidi kuheshimu kanuni then sheria za nchi
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!

Natania tu wakuu!!!!!!!!? Kuna watu walikuwa wanamzomea warioba wanadai eti anawasilisha hoja yake kinyume na kanuni.

Nimetambua uji-nga wako leo
 
YANGU MACHO(nitawachafulia luga waache kuelewana wenyewe kwa wenyewe)
YAMETIMIA YA KAKOBE
 
Nilisema hapa, Sita (na Mwakyembe) ni wanafiki sana walituharibia movie yetu ya Richmond, baba Ridhwani alikuwa ang'oke!
Sasa hivi ni kama punda tu anawatumikia mabwana zake wenye chama
 
Back
Top Bottom