Sitta avunja kanuni kumhujumu Warioba. TBC wahusishwa, UKAWA waja juu

Mkakati wa ccm na mwenyekiti wa bunge hadi sasa ni kuhakiki tbc inakata matangazo wakati wa uwasilishaji wa hotuba ya warioba mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, watanzania wasipate ukweli juu ya mambo waliyopendekeza katika tume ya mabadiliko ya katiba.

Kazi kwelikweli, umeona bunge sasa kilichotoke na TBC wakakata faster... asante startv.
 
Katika hali isiyotarajiwa na wengi Wabunge wa Bunge maalum la katiba wamezomea jioni yaleo na kusababisha bunge maalumu la katiba kuhairishwa pale aliyekuwa Mwenyekiti wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi jaji Warioba kufika jioni ya leo nakutaka kuwasilisha rasimu ya katiba;iliyopelekea mwenyekiti wa bunge hilo Mh Sita kuhairisha bunge hilo baada ya yeye kushindwa kutumia njia ya kumfanya jaji Warioba kuendelea kuwasilisha rasimu hiyo. MUNGU SAIDIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUPATE KATIBA MPYA
 
Watu wengi walimsifia sana mh. Sitta alipochaguliwa kuliongoza bunge hili, huku wakisahau ya kuwa huyhuyu ndiye aliyekwamisha hatma ya RICHMOND kipindi kile akiwa Spika katika bunge la tisa. Mh. Sitta lazima atatekeleza matakwa ya CCM ili aje apendekezwe kugombea urais na chama chake, hivyo wananchi tutegemee KATIBA ya CCM na wala siyo ya TAIFA. Inasikitisha sana kuona CCM yenye wana chama wasiozidi milioni tano, inakandamiza matakwa ya watu milioni 45. CCM inafikiria hii nchi ni ya wana CCM pekeyao.
Mwalimu Nyerere alisema 'ukila nyama ya utaendelea tu huachi', ndio mazowea ya kwenye uchaguzi haya.
 
Nilisema mapema kuwa sita ni mnafiki hapa jamvini mkampigia debe bila kujua ccm walimnyima uspika leo iweje wampendekeze na hilohilo jitu linataka urais mwakani litafanya liwezalo kujipendekeza mi nalichukia naomba liumwe ghafla likafie bondeni kama wengine lisicheze na katiba ya tanzania
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!

Natania tu wakuu!!!!!!!!? Kuna watu walikuwa wanamzomea warioba wanadai eti anawasilisha hoja yake kinyume na kanuni.
 
Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!
Wewe nae tumia akili hapo Kalenga inaingiaje??Hujasikia Sita amevunja kanuni!!Punguzeni ushabiki wa ajabu!!
 
Sababu ni kwamba kanuni inamtaka Rais wa JMT kuzindua bunge ndipo M/kiti wa tume aje kuwasilisha rasimu ya katiba katika BMK. Kinyume na matarajio ya kanuni ambazo wao wenyewe wajumbe wa bunge hilo walizipitisha wiki iliyopita, Mh. SS kama M/kiti wa bunge hilo analazimisha kutengua kanuni ili Warioba awasilishe rasimu hiyo na ndipo Rais aje azindue bunge hilo. Kwa mujibu ya wabunge waliokuwa wanapiga kelele wanaotaka kanuni zifuatwe na siyo ivujwe kama Mh. SS anavyotaka.
 
Sababu ni kwamba rais JK alitakiwa azindue bunge kwanza na baadaye ndio Warioba awasilishe rasimu. Ndivyo ilivyokuwa iwe ila huo utaratibu ulitenguliwa na kuwa Warioba ndiye aanze na baadaye rais JK afuate. Kuna wajumbe hawakuafiki huo utenguzi na ndio hao walioamua kuzomea.
lakini kwa kawaida si kila uamuzi unaokubalika kwa wote.Mara nyingi uamuzi unaokubaliwa na wengi ndio hutekelezwa.Utaratibu wa kuvuta muda tu mimi sikubaliani nao.Haiwezekani kama kuna dharura na rais hayupo kwa sasa halafu warioba kashafika, basi wabunge wakae tu eti wanasubiria hadi rais atakapokuja.Hii haiko sawa ndio maana mimi naweza simply kusema tu kwamba "Jaji warioba afanyiwa njama; Hasira za kalenga zamshukia ndani ya Bunge,.Busara zake binafsi pamoja na busara za mwenyekiti sita zamuokoa. Bonge laahirishwa mpaka hapo itakavyotangwazwa tena.Hili bunge lina watu wenye akili za ajabu sana!" tehe! kichwa cha gazeti la kesho.
 
Katika hali isiyotarajiwa na wengi Wabunge wa Bunge maalum la katiba wamezomea jioni yaleo na kusababisha bunge maalumu la katiba kuhairishwa pale aliyekuwa Mwenyekiti wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi jaji Warioba kufika jioni ya leo nakutaka kuwasilisha rasimu ya katiba;iliyopelekea mwenyekiti wa bunge hilo Mh Sita kuhairisha bunge hilo baada ya yeye kushindwa kutumia njia ya kumfanya jaji Warioba kuendelea kuwasilisha rasimu hiyo. MUNGU SAIDIA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUPATE KATIBA MPYA

Mkuu, jitahidi/jizoeze kutumia vituo kwenye uandishi wako ili unachokiandika kisomeke kwa urahisi.

Ni ushauri tu!
 
Back
Top Bottom