Sitta afichua bajeti Wizara ya Afya kugomewa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

JUMANNE, JUNI 19, 2012 06:31 NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA



MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Magreth Sitta, amesema kamati yake iligoma kupitisha bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hadi Serikali itoe majibu ya msingi yaliyofikiwa kati yake na mgogoro wa madaktari.
Alisema mbali na hatua hiyo, Kamati hiyo imeitaka Serikali kuangalia namna ya ulipaji wa deni linalodaiwa na Idara ya Bohari ya Madawa (MSD), linalofikia Sh bilioni 41.

Alisema deni hilo, limesababisha MSD, ishindwe kutoa huduma zake na sasa inaanza kusuasua, jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa vijijini.

Sitta, alitoa kauli hiyo jana mjini hapa, alipokuwa anazindua Mtandao wa Wadau wa Kuboresha Manunuzi ya Dawa nchini.

“Kamati yangu iligoma kupitisha bajeti ya wizara hii muhimu hadi pale itakapopata taarifa ya mgogoro baina yake na madaktari na tuliitaka waje mbele ya kamati waeleze hatua zote muhimu zilizofikiwa katika kumaliza jambo hili.

“Licha ya kuitaka Serikali kutatua mgogoro huo, pia tumeitaka kulipa deni la MSD Sh 41 bilioni, kwani deni hilo ni kubwa linachangia idara hii kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi… MSD ipo kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano wa Abuja, ambapo kila nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Serikali za Afrika, zinatakiwa kutenga asilimia 15 ya bajeti kwa ajili ya afya kila mwaka.

“Tulikataa bajeti, ilikuwa ndogo sana, kiasi cha Sh bilioni 61 kilichotengwa kwa manunuzi ya madawa ni kidogo sana, kati ya Sh 198 ambazo ziliombwa na wizara hiyo,” alisema Sitta.

“Baada ya kuikataa bajeti hiyo, Serikali imeongeza kiasi cha Sh bilioni 5 katika wizara hiyo, kiasi ambacho bado ni kidogo… wastani Wizara ya Afya, bajeti ya mwaka huu ni asilimia 9 ya bajeti, tofauti na miaka iliyopita ambayo ilikuwa ni asilimia kati ya 12 na 13 ya bajeti,” alisema Sitta.

Naye Mwenyekiti wa mtandao huo, Dk. Joseph Mhando, alisema kuboresha manunuzi ya dawa (MSG Pharm), ni umoja wa wadau wa sekta ya madawa wanaoguswa na hali isiyoridhisha ya upatikanaji wa madawa nchini.

Alisema hadi sasa, asasi 13 zimejiunga na mtandao huo, ambapo hadi sasa umekuwa na wadau wengine, taasisi 60 na katika mkutano huo pia, kutakuwa na mafunzo ya ufuatiliaji wa mikataba ya ununuzi wa madawa kwa wajumbe wa asasi za kiraia zilizo katika mtandao huo, mafunzo ambayo yatatolewa na Wataalam wa Mamlaka ya Manunuzi (PPRA) na wataalam kutoka vyuo vikuu.

Mtandao huo, unafadhiliwa na Benki ya Dunia na sasa unaratibiwa na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Dodoma.

 
Magamba wanaiharibu nchi,harafu wanaishia kufuza makanda ndani ya mjengo,hawa jamaa mavi kabisa.
 
Bajeti Mwaka huu ni kazi haswa, hapo ndipo itapima Mawaziri sasa itakuwa Vigumu kuchukuwa Uwaziri kiurafiki sababu

Sio barabara ya mteremko tena kama huko zamani ilikuwa ni shukrani na upendeleo; Sasa hivi ni kazi haswa inabidi

Usilale utetee utumbo ulionao Wizarani la sivyo Bajeti haipiti na kama haipiti hapo mengi yanaweza kutokea...

Sasa naona Marafiki wengi wa Marais wataomba kuwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Mabalozi na Wapambe kuliko Uwaziri

Vizuri Upinzani... Mnawatendea Mazuri Wananchi na Taifa kwa Ujumla
 
Nae afukuzwe bungeni kwa kuisema serikali ya ccm, Hawa Magamba ni dhaifu bado wanatumia mamlaka kuzima juhudi za wapenda maendeleo ili 2 waendelee kutawala hata kama hawana uwezo wa kuongoza, Hii ni Aibu kwa ccm na Aibu Kwa serikali ya CCm. Hamuwezi kuzuia Nguvu ya UMMA
 
hana lolote naye huyu..anasema hivyo ikifika wakati wa kusema ndio anapaza sauti ndiyoooooooo..atoke zake hapa
 
arudishe kwanza alivyoiba wizara ya elimu ndo ntakuwa na imani naye,vile vyuo vya ualimu alivyojenga na kutovipa majina ya kutambulika ni mali azofisadi uma.
 
Back
Top Bottom