Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Mzee uko Deep! Deep, kuchimba taarifa man, na kufukua vilivyofukiwa,

Jamaa mpaka kaogopa kaomba mods wamfutie thread yake....kasahau hata thread ikifutwa but kama kuna mtu alishai-quote, unakuwa hujafanya chochote!👇👇👇..

Ukiwa muongo, uwe na👇 kumbukumbu!👇....

Naona hii ndio njia Yako ya kujiajiri kupitia ICT uliyoamua kuitumia.....

Perfect kabisa....... but imetiwa doa! KWA kuwa ni fiction story mzee....

Anyway tuburudike tu......
 

Attachments

  • Screenshot_20230524-190513.png
    Screenshot_20230524-190513.png
    33.2 KB · Views: 26
  • Screenshot_20230524-190638.png
    Screenshot_20230524-190638.png
    35.4 KB · Views: 23
  • Screenshot_20230524-190705.png
    Screenshot_20230524-190705.png
    28.9 KB · Views: 23
Mzee uko Deep! Deep, kuchimba taarifa man, na kufukua vilivyofukiwa,

Jamaa mpaka kaogopa kaomba mods wamfutie thread yake....kasahau hata thread ikifutwa but kama kuna mtu alishai-quote, unakuwa hujafanya chochote!
 
Nikisoma hivi hlf Mimi mwaka wa nne huu natafuta mchawi wa kunilogea watu sipati, nabakia kusema hiiiiiiiii
Halafu nahitimisha kuwa uchawi haupo.
Usiongee sana nenda kwamsisi halafu tangaza kwa sauti kubwa NATAKA KULOGWA MWENYE HUO UBAVU AJITOKEZE


fasta sana wanakuwahisha

Utatumika kama demo ya kutestia teknik mpya za ndumba
 
SEHEMU YA 7

Niliporudi kutoka kwenye kuupumzisha mwili sikumkuta Sitti pale alipokuwa amekaa. Nilijaribu kumuulizia ila kila niliyemuuliza alisema hajawahi kuona mtu kama huyo, kwani niliwalezea kwa jinsi alivyokuwa amevaa na kwa jinsi alivyokuwa akionekana, walibaki kunishangaa tu niliogopa kurudi nyumbani bila yeye nilikaa pale msibani mpaka watu wote wakamalizika kuondoka. Nami nikakata shauri la kuondoka eneo lile la tukio nilipokuwa nikiondoka nilisikia sauti ya mtu akiniita kwa jina langu ilikuwa ni sauti ya wana Kingalu. "Mwanangu Soka!" niligeuka nikamfuata.

Nilimtazama mwanamama huyu aliyekuwa amesha zeeka haswa ngozi yake iliyokunjamana na sura yake kukosa nuru. "Bila shaka unamtafuta rafiki yako Sitti?" aliniuliza. "Umejuaje mama, ni kweli namtafuta kwa maana ninajua asingeweza kuondoka bila ya kuniaga." "Unaikumbuka hii?" ananionyesha khanga aliyokuwa amejitanda. "Imeokotwa huko mtoni walipokwenda kuteka maji." (ni kawaida kwa wanawake kushiriki kazi kwenye eneo la msiba), "Kuna watu wameiokota," kisha alinikabidhi niliichukua ile khanga kuna fundo lilifungwa nikalifungua nikakutana na kikaratasi chakavu kimeandikwa.

"Kwako Mwalimu Soka, ukipokea barua hii utambue kuwa rafiki yako Sitti yupo kwenye mikono salama, lakini uhai wake uko mikononi mwako, endapo tu utatuletea ile hirizi ya Simba, tuna kupa sikumbili za kusubiri, ukishindwa kufanya hivyo uhai wa huyu binti utakuwa mashakani, ni mimi Mbwana." ilimaliza sehemu ya barua hiyo.

Yule kijana alikuwa na dawa ya kupumbaza wasichana awatakao, dawa huitwa ndele. Humsogelea msichana akiwa amepaka mafuta yake ya mvuto usoni, humpiga na kifimbo chake kidogo utosini na yule msichana humfuata mwenyewe popote aendapo, nahisi alitumia mbinu hii kumuiba Sitti.

"Hirizi ya Simba?!" nilishtuka nikaingiza mkono mfukoni kujipapasa na kuitoa kile kitu nilichokitoa kwenye mwili wa marehemu wakati wa kumuosha na kisha nikakitazama kwa sekunde kadhaa, bado kilikuwa kina pumua. "Bila shaka hii ndio yenyewe na kwanini hasa wanaitaka?" Nilikuja kugundua kwamba hirizi ya Simba ni moja kati ya mazindiko makubwa sana ya wachawi pia hutumika na viongozi wakubwa wa serikalini ili kuwafanya waogopwe na kila mtu, pia ukiwa nayo hii ni kinga dhidi ya wachawi.

Kumbe ndio maana mzee Kingalu alikuwa akiogopwa na kuheshimiwa na kila mtu na ndio maana kwenye msiba wake ilipigwa ngoma, sikila mtu akifa hupigwa ngoma ni kwa watu wachache wenye hadhi fulani na heshima fulani mbele ya jamii. Kwahiyo Mzee Kingalu alikuwa na kauli ya mwisho juu ya maamuzi yoyote pale Kijijini, labda hii ilitokana na kumiliki hirizi hii ya simba. Niliondoka kuelekea nyumbani kwangu huku macho yakiwa yanatazama chini niliichukua ile khanga ya Sitti nikaizungusha shingoni, ile barua niliifunga palepale ilipokuwa.

Nilifika nyumbani saa moja kasorobo hivi usiku niliwakuta walimu wenzangu wakinisubiri kwa hofu, nilivyo waona wamekaa pale nje kibarazani nilikaza mwendo kuwawahi kwani niliona kama nachelewa kuwafikia, nilifika nikaanza kulia niliwaeleza yote yaliyotokea na jinsi Sitti alivyopotea kimiujiza tulijadiliana kila mtu alitoa wazo lake, wapo waliosema kwamba tupige simu wilayani ili watume polisi kuja kuwakamata wahusika wote lakini wazo hili lilipingwa vikali na mwalimu mkuu.

Inaonekana kama aliogopa kibarua chake kuota nyasi ama labda aliwaogopa wazee wa Kwamsisi, kufanya jambo lolote bila kuwahusisha wao ni kujihatarishia maisha yako nilimwachia mwalimu mkuu ile khanga yenye ile barua mimi nikaingia ndani ili kujipumzisha kwakuwa nilikuwa nimechoka sana sikutaka hata kula kwani hamu ya kula sikuwa nayo kwa usiku ule, pia mchana nilikula msibani. Nilisali kabla ya kulala na kumuombea Sitti awe mzima huko aliko.

Nilipitiwa na usingizi nikiwa bado nimepiga magoti pale kitandani, nilishtuliwa na sauti ya mtu aliyekuwa akigonga mlango wangu, baadaye akahamia dirishani dirisha lilikuwa na wavu na pazia tu. "Soka Soka..!" sauti ya mtetemo ilisikika nilifungua pazia kutazama nje mbalamwezi ilikuwa ikiangaza kila upande sauti ilisikika tena, "Soka Soka, kwanini mliuzika mwili wangu mapema?" Nilifikicha macho kutazama mzimu wa Mzee Kingalu ulikuwa ukinitazama kutoka dirishani sura ni yakwake lakini macho yalikuwa yaking'aa sana kama yale ya paka.

"Kwani we' walikupeleka wapi?" nilimhoji. "Walinipeleka nyumbani kwa mzee Samasimba wanataka kunifanya msukule." ulijibu ule mzimu wa Mzee Kingalu. "Umewezaje kufika hapa?" "Nimetoroka." niliogopa nikawa nikitetemeka mwili mzima jasho likiwa linanitoka nikashtuka usingizini na kutazama pazia lilikuwa limefunguliwa na wala sikuona kitu chochote pale dirishani inamaana nilikuwa naota? Niliamka pale nilipokuwa nimepiga magoti nikalala vizuri na kujinyoosha kitandani.

ITAENDELEA...
Akiendelea mnishtue
 
Sasa kama mwandishi hawe muongo au mkweli tatizo liko wapi? Mbona movies tuna angalia na ni fiction hatu lalamiki kikubwa story ina eleweka burudani basi una soma una pita hivi .watu mna chukulia seriouse sana kila jambo
Watu humu wa ajabu sana...kwani ni mahakama hii au nyumba ya ibada? Mara wahoji bangili,mara ualimu kasoma lini mara chumvi imezidi sijui.. hizo zote ni dalili za mastress na madepression...kama story iwe ya fiction au real hayo hayatuhusu ni juu yake msimuliaji...sisi hapa ni burudani tu!
Hebu tujifunze kumind business zetu sio kuingilia sana mambo ya watu... Ingekuwa ni somo linapotoshwa ingekuwa sawa ila sio simulizi ya mtu.
 
SEHEMU YA 8

Niliamka asubuhi kisha nikachukua mfuko wa nailoni nikaizungusha ile hirizi na kuchimba pale chumbani kwangu na kuifukia. Sakafu ya nyumba yangu ilikuwa ni ya udongo na hivyo ilikuwa rahisi kuchimba kule ndani. Nikakumbuka kwamba nilipewa masaa 48 na hapo tayari nilisha tumia masaa 12 ili niikabidhi ile hirizi kwenye himaya ya Mzee Samasimba kupitia kwa kijana wake Mbwana aliyemteka Sitti kichawi. Siku hii ya jumamosi ilikuwa siku ya tofauti kidogo kwani ilianza na kawingu kamvua za rasharasha na na baadaye jua likawaka, ni siku moja tangu tumzike Mzee Kingalu.

Niliingia bafuni kuoga, nilipotoka hata kabla ya kuingia chumbani nilikutana uso kwa uso na Mganga mkuu. "Kijana jiandae tuondoke!" Nilimtazama usoni hakuwa na maneno mengi na mimi sikuwaza sana niliingia ndani na kuvaa kisha nikatoka nje nilichukua baiskeli yangu kwani naye alikuwa na yakwake. Tukatoka kwenda mpaka Mkata mjini kununua vingira (vifaa vya kiganga) kwa ajili ya shughuli kubwa kwa siku hiyo. Kumrudisha mtu aliyepotea na kumrudisha mtu aliyechukuliwa Msukule.

Tulifika Mkata majira ya saa 6 mchana tukanunua vifaa vinavyo hitajika akiwemo mbuzi dume (beberu), kuku jike mwekundu (koo) pamoja na dawa nyingine za asili hatukutaka kupoteza muda, tulirudi na moja kwa moja tukaingia kilingeni. Tiba ya kwanza ilikuwa ni ya kunitengenneza mimi kimwili, mganga alinifanyia dawa za kunifanya nisionekane katika ulimwengu wa roho yaani nisiweze kabisa kuingia kwenye rada za wachawi wowote wale. "Mwanangu umeshaingia vitani huna budi kujivika mavazi ya chuma," alisema yule Mganga.

Alinichanja chale kwenye viwiko vya mikono, kifuani na miguuni kisha kunipaka dawa iliyokuwa kwenye ile tunguli yake ni dawa iliyotokana na mchanganyiko wa miti zaidi ya saba na viambatanishi vingine vilivyochomwa kwa pamoja na kunuiziwa kisha kuchanganywa na mafuta ya mnyonyo na asali na kuwekwa kwenye tunguli hiyo. Baada ya kazi hiyo aliniambia imebaki kazi moja nayo ni tambiko litakalo fanyika huko porini kwenye mti mkubwa sana nikamuitikia kwani kwa wakati huo tulikuwa na kazi kubwa sana ya kuwaokoa ndugu zetu hao kwahiyo zoezi hili la kunitengeneza tukalisitisha kwa muda.

Tukaingia kwenye kazi rasmi ya kumtafuta mtu aliyepotea/ aliyeibwa kichawi. Utambue kuwa mtu aliyepotea ki mazingira ni tofauti kabisa na mtu aliyechukuliwa msukule hivyo namna ya dawa zake pia huwa ni tofauti. Mganga aliweka maji kwenye chungu na kuyanuizia kisha kuchanganya na dawa kadhaa ikiwemo mzizi wa kata njia, makombe ya hirizi pamoja na mavumba mengine akafunika kwa kutumia kinu. Baada ya muda alipofunua niliweza kuiona sura ya Sitti kwenye kile chungu cha maji, alionekana mwenye huzuni nyingi na kukata tamaa. "Huyu atakuwa amefungiwa huko kwenye eneo la mbali wamemtelekeza kwenye kisima kirefu cha zamani kwahiyo inapaswa kuokolewa," alisema yule mganga baada ya kuangalia kwenye ramli yake.

Nilimueleza Mganga kuhusu kile kitu nilichokipata kutoka kwenye mwili wa marehemu naye akaniambia kwa sasa nikihifadhi kwanza kama nilivyo fanya baadaye kitakuwa na kazi kubwa. "Umefanya jambo jema mwanangu hawa watu haitakiwi uwakubalie kwa kila kitu watakacho kuambia ni lazima ujue namna ya kupambana nao bila hivyo watakuburuza. Baada ya kugundua kwamba Sitti hakufichwa mbali na eneo la kijiji, ilibidi ifanyike dawa maalum ya kuwafunga wasimpeleke mbali zaidi tulikwenda kwenye njia panda usiku wa saa 2 hivi.

Ilikuwa ni jambo gumu kwangu mimi kama mwalimu na heshima zangu kuonekana nikifanya mambo ya kishirikina hadharani, ingawa hakuna aliye nishangaa kwani wanakijiji wa Kwamsisi uchawi kwao ni kama mila, na tiba za asilia hufanywa hadharani bila kificho chochote kwa hiyo ndani ya muda mfupi niliokuwa pale niliweza kuzoea mazingira na maisha ya pale na hivyo kuto kuogopa kufanya shughuli za kiganga hadharani.

Hivyo tukapasua nazi kumi na mbili kwa ajili ya kuvunja mipango yao kisha yule kuku alimchinja na kumuachia achague njia tunayoweza kuifuata. Baada ya yule kuku kuchinjwa alirukaruka na kuangukia kwenye njia ya upande wa mashariki, mganga akiwa ameshikilia vifaa vyake ikiwemo tunguli mbili moja ameivaa shingoni na nyingine ameishikilia mkononi pamoja na mwengo na pembe ndogo alisimama kwenye ile njia kwa dakika kadhaa huku akinuizia maneno akapiga ukelele wa hali ya juu sana na kuita "Sitii njoo, njoo!" kisha akapuliza ile tunguli yake. Kumbe tulifanya makosa kwani kwa kufanya hivyo tungewaamsha wachawi wakajua kumbe tunawafuatilia, walijiandaa vyema kutukabili ila tuliwazidi ujanja.

"Enyi Subiani, enyi Makata, enyi Maimuna njooni sasa mnisaidie kumtafuta kilembwe changu!" Nawaita muje sasa hivi mganga aliwaamrisha majini yake yamuingie basi baada ya muda akapandisha mashetani yake maramoja akaondoka huku akiwa anakimbia nilimfuata nyuma huku nimebeba ule mkoba wenye zana za kazi tulitembea mpaka mashambani, tukaingia kwenye msitu mnene kidogo ndipo tukaisikia sauti ya vilio na maombolezo tulikaa kutazama Sitti alikuwa amewekwa kwenye kisima kirefu jambo la ajabu hawakumuwekea ulinzi wowote, labda walijua kwamba itakuwa ngumu kwa sisi kufika huko.

Nilimulika na tochi kutazama kisimani, kilikuwa kirefu sana na hatukuwa na ngazi yoyote ilibidi nimtupie kamba tuliyokwenda nayo na bila kutarajia Sitti aliweza kuipanda ile kamba na tukaweza kumtoa alilia na kunikumbatia kwa furaha. Mganga alituamuru kuondoka eneo hilo kwani wale wachawi lazima wataanza kutufuatilia kuna taarifa ambayo wamesha ipata. Tulitoka tukapita njia ya tofauti. Tulivyokuwa njiani tukawaona wanakuja kwa kasi huku wakiwa na mienge mikononi mwao tulijificha pembeni ya mbuyu wakapita kuelekea eneo walikokuwa wamemficha Sitti baadaye tukatoka tukikimbia kuelekea nyumbani kwa Mganga.

ITAENDELEA

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-9
 
Usiporejea ntakukutukana kila siku! Mimi nlienda kumzoa mume wangu huko kwa msisi eneo linaitwa BICHWA NG'OMBE alikaa miezi miwili hajarejea alifuata mbao.

Nikamkuta anaishi na kibibi kuliko mama yake. Ishukuriwe damu ya YESU.
Hahaaaahaaa hiyo kali
 
Back
Top Bottom