Sitosahau siku tuliyotaka kufa kwa kicheko baada ya mwalimu kupiga chafya na kutokwa na puto kuubwa la kamasi lililokaribia kufunika uso.

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,684
Iilikuwa shule fulani huko maeneo ya kibaha kwenye miaka ya 2000s.

Tukiwa tumetulia ghafla kengele ya dharura ikagongwa na sote tukakimbilia parade kujua kunani. Kumbe ilikuwa kengele ya jambo jema; jamaa wa bank (ya posta kama sikosei) walifika kutoa zawadi kwa mwanafunzi fulani pale baada ya kushinda katika shindano la essay.......tsh 50,000/= akajinyakulia yule kijana wa Kilimanjaro. Kubwa hiyo kipindi kileee.

Wageni wakakaribishwa na kuongea, walipomaliza wakamkabidhi mwalimu kile kitita ili amkabidhi mwanafunzi husika.....hapo ndipo tatizo lisilotarajiwa lilipoanza. Kamwita mbele yule dogo, kafika kamshika mkono na kuunyanyua juu huku akitamka, ''........(jina la shule) oyeeeee!'' Nasi tukaitikia, ''oyeeee!". Mwalimu akapandisha mzuka, akatuamuru tuitikie kwa sauti zaidi. Akaanza tena, basi safari hii ile amemaliza tu kutaja jina la shule ikamjia chafya kubwa ya ghafla. Dah, mwalimu kuipiga ile chafya ebwana lilitoka puto moja kubwa la kamasi katika moja ya tundu la pua yake hata sijapata kuona.
Lile puto lilikaa kama sekunde mbili hz, mwalimu asijue la kufanya maana alikuwa amefadhaika na hakuwa na kitambaa (ilikuwa kipindi cha baridi na hakuwa anaumwa mafua hivyo kutembea na kitambaa haikuwa kipaumbele). Shukrani zimuendee yule madam aliyemuwahi na kufanya jambo. Sisi wengine kwakweli hakuha siku tulilazimika kucheka kama siku ile.......binafsi siyo mchekaji lakini siku ile nilishindwa kabisaa. Wanafunzi wote tuliishiwa nguvu kwa kicheko siku ile. Pekee walioweza kujizuia ni headboy, baadhi ya walimu na wageni wetu. Wanafunzi wengine walianguka kabisa kwa kicheko. Mwalimu alikuwa katika wakati mgumu sana siku ile.

Getman Mwandemele, mtaalamu wa namba kutoka Dar, utakuwa unakumbuka hili.
Hassan Haruna Nkya, mtaalamu wa Chemistry kutoka Klimanjaro, utakuwa utakumbuka hili.
Msika Aloyce, mtaalamu wa namba kutoka Mtwara, utakuwa unakumbuka hili.
Ramadhani Omari, mtaalamu wa Commerce kutoka Morogoro, utakuwa unakumbuka hili.

Muwe na w/end njema!!
 
Wakati tupo form 3, kuna siku aliingia mwalimu wa English class, Mr Chaponda huku amenyoa ndevu zote kitu ambacho sio kawaida yake watu wakabaki wanamshangaa kama dakika tatu, kuna mwenda wazimu mmoja akaropoka "bob chapii amekua kama anapuliza moto" watu walicheka mpaka English classes zikahairishwa kwa wiki nzima kusubiria ndevu za mwalimu ziote.
 
Kwakweli na me nimecheka hapa mpk watu wamenishangaa, esp hiyo ya Bob chapii kuwa km anapuliza moto

Askwambie mtu ukiwa na mazoea ya kuwa na ndevu af ukanyoa zote unakuwa km mdudu
 
Kwakweli na me nimecheka hapa mpk watu wamenishangaa, esp hiyo ya Bob chapii kuwa km anapuliza moto

Askwambie mtu ukiwa na mazoea ya kuwa na ndevu af ukanyoa zote unakuwa km mdudu
Mi nilinyoa nywele aisee.. nilitisha
 
kuna kipndi nko form two kuna teacher alikua anapita kila darasa anaanza kuwachana wanafunzi yaan ile bila aibu "nyinyi watoto mmeanza michezo ya kuto***na hujo mitaani tunapata taarifa zenu mmeota mav**i mnajifanya mnajua kila kitu acheni kuto***ana kapita kwenye madarasa ya form two yote nane nlicheka sana ile siku alikua anatukana hatari baadae wanafunzi wa madarasa yote tukawa tunahadisiana tu
 
Wakati tupo form 3, kuna siku aliingia mwalimu wa English class, Mr Chaponda huku amenyoa ndevu zote kitu ambacho sio kawaida yake watu wakabaki wanamshangaa kama dakika tatu, kuna mwenda wazimu mmoja akaropoka "bob chapii amekua kama anapuliza moto" watu walicheka mpaka English classes zikahairishwa kwa wiki nzima kusubiria ndevu za mwalimu ziote.
🤣🤣
 
Back
Top Bottom