Sitaki unisalimie...

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,499
14,360
Wana MMU... Habari za week end?
Naleta kwenu hii thread ili tumsaidie rafiki yangu, kuna mshikaji wangu wa karibu sana ana mahusiano mabaya sana na Baba yake mzazi, kwa muda wa miezi nane sasa baba yake hataki salamu ya mwanae, kisa kilianza kipindi ambacho jamaa alikua anasoma Ruaha University College alikua anafunga nywele yaani (Afro), aliporudi likizo kwao Dar akaambiwa akate nywele yeye akawa hataki, Baba yake akamwambia kama hutaki kuanzia leo USINISALIMIE'' si unajifanya Bob Marley? Jamaa akadhani utani mpaka leo mzee amegoma kuitikia salamu ya Mwanae, na aliambiwa fanya kila kitu Kula, lala lakini Usinisalimie wewe Baba yako ni Bob Marley sio mimi, sio siri jamaa hii ishu inamtesa sana Kisaikolojia na ameshaomba msamaha lakini Dingi kamwekea ngumu, story nyingine kama kawaida wanaongea lakini Salamu tu Mzee wake hataki, na jamaa ameniambia ukweli hili jambo linamuumiza sana moyo wake.
Naomba mawazo yenu tumsaidie Kijana mwenzangu!
 
Awatafute wazee wenye busara hapo mtaani kwao ili wakamuombee msamaha kwa huyo mshua wake.
 
Ndio shida za kula kulala hizi...ila angenyoa hilo Afro kisha amfuate mzee wake privately ampigie magoti!
 
Anyoe tu,...
ni ulimbukeni kwanza kusuka mwanaume.
Labda kama kaingia kwenye ulimwengu wa kupunguza idadi ya wanaume.

Nampongeza sana baba yake.Honestly.
 
Madingi wengine noma sana! Atakuamulia kila kitu mpaka mke atakuchagulia! Kila mtu anatakiwa awe na uhuru wake bana, especially toto kubwa kama hilo ambalo liko chuo!
 
Madingi wengine noma sana! Atakuamulia kila kitu mpaka mke atakuchagulia! Kila mtu anatakiwa awe na uhuru wake bana, especially toto kubwa kama hilo ambalo liko chuo!

Hili sio kwamba ana mwamulia.
Ana msaidia kutoka kwenye ujinga,...utasukaje mwanaume?we shoga?
 
Mwambie anyoe nywele,then aone km haitikia salam!!!
Anashindwa kutofautisha thaman ya nywele na ya baba yake mzazi?!!!
Sidhan km elimu yake inamsaidia!!
 
Hivi nywele zina nini kwa mwanaume angekuwa mwanamke sawa lakini mwanaume? Mwambie aache upumbavu kukosana na mzazi wake eti kisa nywele kwani hizo nywele zinampa nini
 
Hivi nywele zina nini kwa mwanaume angekuwa mwanamke sawa lakini mwanaume? Mwambie aache upumbavu kukosana na mzazi wake eti kisa nywele kwani hizo nywele zinampa nini

utadhani mtoto wa primary vile kumbe yuko chuo sijui kamaliza.
Kweli kusoma sio kuelimika.
 
wakuu nywele alishanyoa na jamaa anafanya kazi yake, na sio kwamba haongei na mshua wake wanapiga story fresh lakini Dingi ndio hataki salamu
 
wakuu nywele alishanyoa na jamaa anafanya kazi yake, na sio kwamba haongei na mshua wake wanapiga story fresh lakini Dingi ndio hataki salamu

Mmmh,hiyo sasa kesi nyingine.
Labda ndo culture yao,ukisha kuwa mkubwa usinipe "shikamoo"
 
Mmmh,hiyo sasa kesi nyingine.
Labda ndo culture yao,ukisha kuwa mkubwa usinipe "shikamoo"

hahaaa yaani hata mimi huyu mzee simuelewi, na sio kwamba hana furaha na kijana wake yaani wanaongea vizuri, lakini ikija kwenye salamu mzee anamwambia sitaki SALAMU yako, sio siri jamaa anateseka kisaikolojia
 
Huyo mdingi basi naye anazeeka vibaya au isije ikawa mtoto kipindi kile ana nywele anajihisisha na mambo ya kutoa tigo sasa kanyoa nywele lakini katabia bado kapo
 
hahaaa yaani hata mimi huyu mzee simuelewi, na sio kwamba hana furaha na kijana wake yaani wanaongea vizuri, lakini ikija kwenye salamu mzee anamwambia sitaki SALAMU yako, sio siri jamaa anateseka kisaikolojia
Huyo mdingi ana matatizo yake,au kuna jambo jamaa hajakuweka wazi,
Haiwezekana km nywele keshanyoa na mdingi wanaongea vizuri isipokuwa salam tu!!!
Kamuulize vizuri inawezekana kuna kitu alishamjibu kuhusiana na kutoitikia salamu yake na jamaa alishasahau maana mambo ya ujana nayo ni utata mtupu!!!
 
Aah mi nadhani tatizo sio nywele tena ila labda kijana alionesha utovu wa nidhamu pale the way alivyomjibu mzee wake kuwa hataki kunyoa nywele ukizingatia bado yupo kwny himaya ya baba yake. Ila kama jamaa anafanya kazi, yupo kwa baba mpk leo anafanya nn? Kama unataka kukaa kwa baba yako basi fuata masharti, kama hutaki masharti HAMA UKAPANGE ufuge mpaka afro za sehemu flani flani.
 
Awatafute wazee wa nini mkuu uamuzi anao yeye akate hizo nywele aone kama baba atakataa kuitikia salamu yake vitu vingine ukiwa chini ya milki ya wazazi inabina ukubaliane na masharti yote pindi atakapo toka apo na kwenda kuanzisha serikali yake sasa ni uamuzi wake afuge ata afro la kwenye vuz.i hakuna wa kumuuliza
Awatafute wazee wenye busara hapo mtaani kwao ili wakamuombee msamaha kwa huyo mshua wake.
 
Kwanza salamu kitu gani. Kusalimiana kila mara ni dalili za ujinga na umasikini. Kusalimiana si maana yake kujuliana hali? Sa kama wanakutana na kula stories na kufurahi hapa na pale kuna zaidi ya hilo? Acheni mambo ya kiswahili ya kupotezeana time kwa masalamu marefu yasokuwa na tija.
 
Mwambie anyoe haraka sana na amfate babake akiwa sehemu ametulia amuombe msamaha na asirudie tena.
 
Back
Top Bottom