Sitajiuzulu kwa sababu ya Mgawo wa Umeme - Ngeleja

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
WAZIRI wa Nishati na Madini, Willium Ngeleja amesema ni ngumu kujiuzulu kwa kuwa tatizo la umeme si la wizara yake pekee na kuwafumba midomo wale wanaotaka ajiuzulu licha ya Bajeti yake kukataliwa Bungeni
Aliyasema hayo Mjini Dodoma wakati wabunge wengi wakitaka ajiuzulu mara tu bajeti yake ilipokataliwa bungeni kwa kuonekana hotuba hiyo haionyeshi tatizo la umeme Tanzania litaisha lini

Hivyo Ngeleja alisema hawezi kujiuzulu kutokana na matakwa ya watu na kujitetea kuwa tatizo hilo si lake peke yake bali ni tatizo la serikali nzima

Wabunge wanamtaka ajiuzulu ili kuwapisha watu wengine wanaoweza kukabiliana na wizara hiyo ili kuweza kuondoa tatizo la giza linaloendelea nchini ambao umeme linaonekana ni janga la kitaifa kwa kuwa watanzania hawana uhakika wa umeme

“Bajeti si ya wizara pekee, na mimi si ndiye niliyetenga kiasi cha fedha kinacholeta utata, muhimu tukae chini kwa muda tuliopewa kutafakari tufanye nini ili kuweza kulinusuru Taifa kuondokana na janga la umeme nchini, kuliko kunitaka kuachia ngazi” alisema Ngeleja

Wizara jhiyo imepewa muda wa wiki tatu kuja kutoa bajeti hiyo upya na kufafanua ni jinsi gani wamejipanga kukabiliana na tatizo la umeme linaloendelea nchini kote

Tatizo la umeme ni janga sugu linaloendelea nchini Tanzania ambapo wajasiriamali wengi kuonekana kufunga ofisi zao kutokana na kukosekana kwa umeme kwa muda mwingi wakiwemo Saloon, Stationary, migahawa ya vinjwaji baridi, wanaotumia mashine mbalimbali ikiwemo na mashine za kusaga nafaka na hali hiyo kupelekea kuondoa ajira za watu waliokuwa wakiendesha ofisi hizo


Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Anayosema ni kweli kabisa. Tatizo halikuanzia kwake, hivyo kuna wengi wa kuwajibika. Katika wengi hao, Ngeleja ni mmoja wao!
 
Anayosema ni kweli kabisa. Tatizo halikuanzia kwake, hivyo kuna wengi wa kuwajibika. Katika wengi hao, Ngeleja ni mmoja wao!
La mgao wa umeme kuwa historia? Lilianzia kwa nani? Atajiuzulu kama mgao hautakuwa history of course!!!
 
  • Thanks
Reactions: HT
Kweli atakufa njaa .RA nguvu yake ndo hivyo tena hana ujanja tena huyo Njegele ahhh Ngereja
 
Ajiuzulu, anatuletea zengwe tu, watu hatufanyi kazi kwa ujinga wa wizara for several years hii wizara imejaa utumbo na upupu mtupu.

Either the govt is not serious with the welbeing of its people or there might be a good number of 'bird brain' people who don't have uchungu at all bcoz wao wana majenereta ambayo sie wananchi kodi zetu ndiyo wananunulia mafuta.

Let's try waishi kwa mshahara walipie mafuta for running their generators am pretty sure watabadilika fikra but nani wa kumfunga paka kengele.

At one time we were told by some people tukawaona wajinga example aliyekuwa katibu mkuu b4 Mhando, tulikuwa na muda wa kujiandaa 4 all these but tuliuchezea lets swallow the pills and we stop lamenting.
 
Hapa cha msingi ni wabunge kuikataa tena bajeti yake bungeni.

Sidhani kama watakuja na jipya tena zaidi ya nadharia na porojo tu na kuweka vitu ambavyo deep down in their hearts wanajua havitekelezeki, lengo ikiwa ni kupitisha bajeti mwaka huu tu na kusuburi mengineyo mwakani tena
 
Anayosema ni kweli kabisa. Tatizo halikuanzia kwake, hivyo kuna wengi wa kuwajibika. Katika wengi hao, Ngeleja ni mmoja wao!
Ni kweli hata kama tatizo halikuanzia kwako that does not mean you cannot be held accountable.

He is a part of the problem, anaombwa kujiuzulu kwa sababu ya yeye kukosa solution ya matatizo ya umeme nchini hata dokta ugonjwa unamposhinda ujitoa na kumuachia mwingine na linigine linalopigilia msumari wa mwisho ni swala la Jairo.

Kwa hiyo huyu hivi sasa is dead man walking kwani you have to be out of your mind not know what is going on in your own house.

Ngeleja was supposed to be fired long time it is beyond me why he is still there!
 
La mgao wa umeme kuwa historia? Lilianzia kwa nani? Atajiuzulu kama mgao hautakuwa history of course!!!
Hapo ktk red unakumbuka "maisha bora kwa kila mtanzania?"
 
Sisi hatujataka wewe ujiuzulu kwa ajiri ya mgao sie tunataka ujiuzulu kwa uwajibikaji wako mbovu wakuto jali maslahi ya nchi hii.

Huwezi ukawa madarakani kwa kipindi chote hicho kwenye wizara nyeti Nchi hii ukawa unatupa ahadi kila siku lukuki na sababu ngini za ongezeko za miradi isiyokuwa na utekelezaji na hakuna majibu au suruhisho la umeme limetendeka.

Still unasema hujiuzulu huoni hata haya mbele ya watanzania?
 
akikutana na nguvu ya uuma atakubali... even mubarakalisema hivi lakini sasa hivi anagoma goma kula
 
Akitaka kupata heshima ajiuzulu. Kosa ndiyo siyo lake lakini kisiasa anawajibika.

Yeye kama Ngeleja amefanya nini kurekibisha hayo makosa ukizingayia kuwa amekuwepo kwenye hii wizara kwa muda tangu akiwa naibu waziri.

Anataka kutuambia kuwa bado anataka kuendelea kubaki hapo. Kama akibaki atafanya nini kipya.

My take hata asipojiuzulu atarudi kuwa back bencher muda siyo mrefu.
 
Uliona wapi, tangu lini mawaziri wa CCM kukubali kosa? Wamelelewa hivyo na Chama chao hatushangai bwana
 
Ngeleja hawezi kujiuzuru. Hatuna utaratibu huo. Boss wake kimsingi keshasema tatizo la umeme si kosa la Ngeleja - ni kosa la Mungu kutunyima mvua
 
Ni kweli tatizo la umeme ni story ndefu. Lakini mheshimiwa hii kashfa ya mlungula unaionaje? Kusimamishwa kwa katibu wako ni dhahiri wizara yako ni usanii mtupu. Jairo hakufikia uamuzi ule peke yake. Wewe na Malima achieni ngazi kama EL na Msabaha. Msingoje rais awang'oe, jiheshimuni tafadhali.
 
Back
Top Bottom