Sisi ni Washenzi, Hukumu ya Kifo Bado ni Stahiki Kwetu!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Miaka michache tu iliyopita mie nilikua ni miongoni mwa watu tuliokuwa tunapinga kwa nguvu zote hukumu ya kifo! Siku moja, nikiwa katika pita pita yangu nikasikia taarifa za mwanaume libaba jitu zima limembaka mtoto wa miaka mitatu hadi mtoto yule akafariki!

Bado nina kumbukumbu za namna gani nilighadhibika siku ile kiasi cha kutamani kumtafuta huyo mshenzi na kummininia risasi kadhaa za miguu hadi avunjike avunjike kabisa! Haikunichukua muda kugundua kwamba nilichokuwa nakifikiria kisingewezekana lakini chuki zangu hazikupungua na bado hazijapungua hata punje!

It's like sikuwahi kufuatilia matukio ya namna hiyo hapo kabla kwani haikunichukua muda kubaini kujirudia rudia kwa matukio hayo ya kishenzi! Taratibu nikaanza kujiona nilivyo mnafiki ninapotaka eti adhabu ya kifo iendelewe... nilijiona mnafiki baada ya kujiridhisha bila shaka kwamba endapo namkutia/namfumania mtu mshenzi anayefikia kubaka katoto ka miaka mitatu, walahi ningemtwanga risasi hapo hapo hata kama huyo mtoto hanihusu! Huyu ni mshenzi asiyestahili japo dakika moja duniani.

Ghafla, zikaibuka tabia zingine za kishenzi kama hizo za kubaka watoto hadi wanakufa... watu wakaanza kuua Albino kwa sababu za kishenzi kabisa! Chuki yangu dhidi ya wauaji ikaongezeka na taratibu nikajikuta naanza kuwachukia hata wale ambao tulifanana kimtazamo hapo awali... wale wanaotaka adhabu ya kifo iondelewe!

Juzi juzi tu hapa nikasikia habari nyingine ya kishenzi zaidi ambayo ilipekelea mtoto wa miaka 7 kufa! Katika tukio husika, vijana ambao bado sijafahamu idadi yao walimwingilia mtoto huyo wa kiume hadi umauti ukamkuta. Tukio kwa mara kwanza liliripotiwa na Gea Habibu wa Clouds. Kwa mujibu wa mashuhuda, walimkuta mtoto akiwa amechafuka vibaya sana huku tundu la haja kubwa likiwa wazi... kwa maana kwamba mtu akingeweza kuingiza kitu kupitia tundu hilo bila kuguza kuta za tundu la haja kubwa! Ikasemekana kwamba, kuna uwezekano mkubwa walimwingilia wakati mtoto huyo akiwa ameshakufa na ndio maana njia ya haja kubwa haikurudi katika hali yake ya kawaida!

Napenda kuwauliza wale maswahiba na maswahibu wangu wa zamani tuliokuwa tunapinga adhabu ya kifo. Hivi kweli washenzi kama hawa wanahitaji kuwapo duniani? HIvi washenzi wanaofikia kubaka mtoto kwa zamu hadi njia ya haja kubwa inabaki ipo wazi ni watu wanaohitaji kuwa na watetezi kweli hawa? Nafahamu wazi kwamba wengi wenu mnaopinga adhabu ya kifo hiyo ni moja ya kazi zenu zinazowapa mkate wenu wa kila siku, lakini amini amini nawaambia, ujira mwingine ni ujira tunaopaswa kuungalia mara mbili mbili.

Hoja kwamba adhabu ya kifo hampi mtu fundisho, hoja ambayo hata mimi nilikuwa naiunga mkono nimefikia kubaini ni hoja ya kijinga isiyo na maana wala mantiki! Haina mantiki kwavile wakati tunadai adhabu ya kifo haimpi muhusika nafasi ya kujutia kosa lake bado tunaunga mkono kifungo cha maisha kwa washenzi kama hao. Sasa ikiwa mnaunga kifungo cha maisha kwa wauaji, hata akijutia atatumia wapi matunda ya majuto yake wakati anabaki behind the bar maisha yake yote? Mtu akijutia ushenzi wake basi tunapaswa kumuona akiwa mtu mwema mbele ya jamii... sasa kuna maana gani kwa mtu kujutia wakati hana nafasi ya kuionesha jamii kwamba amejutia ushenzi aliofanya? Kama mnataka, semeni adhabu ya kifo iondolewe na kifungo cha maisha kiondolewe vile vile ili hata wale washenzi wauaji wakifanya ushenzi wao baadae warudi mtaani na kuchanganyika jamii huku waki-prove kwamba wao ni watu wema sasa vinginevyo hii hoja ya kwamba wanakosa nafasi ya kujutia ni hoja isiyo na maana yoyote wala mashiko!

Kwa sasa naweza kuunga mkono wanaotaka wigo wa adhabu ya kifo upanuliwe kwavile tunakuwa washenzi zaidi kila uchao kuliko kutaka adhabu hiyo iondolewe! Kwanini kodi tunazokatwa ziendelee kuhudumia washenzi wasio na haya wakati tunafahamu kwamba hawana tena nafasi ya kuja kuhudumia jamii? Badala ya kutaka adhabu iondolewe ni heri tu-include mafisadi wakubwa wa nchi hii kwenye adhabu ya kifo kwavile hawa nao ni washenzi wasiohitaji huruma wala utetezi... haiwezekani hospitali hazina dawa halafu anatokea mshenzi mmoja anafanya mambo yanayosababisha hospitali zisiwe na dawa halafu tukamuona huyu nae ni mwenzetu!!

Hebu niwaulize wale wanaotaka adhabu ya kifo iondolewe! Assume umeagana na mtoto wako wa miaka 5 asubuhi wakati unaenda kazini na yeye anaenda shuleni! Saa chache baadae unapigiwa simu kwamba mtoto wako uliyemwacha mzima wa afya asubuhi, amekutwa kichakani amekufa baada ya kuingiliwa kinyume na maumbile hadi njia ya haja kubwa imebaki kama shimo! Je, hivi kweli mtaendelea kupiga adhabu ya kifo au ni kwavile bado hayajawakuta and you don't care yanayowakuta wengine? be honest on this.

Nichukue nafasi hii kumataka radhi Rais Ally Hassan Mwinyi ambae zamani nilimuona ni muuaji na muovu mkubwa baada ya kuripotiwa kwamba katika utawala wake ali-approve hukumu nyingi za mauaji! You did the right thing old man... tuwaache hawa akina JK wanaoota tuzo ya utawala bora na haki za binadamu huku nikiamini kama kweli kuna mungu na siku ya mwisho, basi viongozi hawa wafahamu kwamba kuna watoto wadogo wanaingiliwa hadi kufa na hawa ndio watakuwa mashahidi mbele ya kiti cha haki!
 
Mkuu NasDaz Umeeleweka..Naunga mkono hoja ..
 
Last edited by a moderator:
Nasdaz unachosema kina ukweli,lakini hata hiyo adhabu ya kifundo cha maisha ni nadra watu wa iana hii kupata.Hata ile ya miaka thelathini kwa kubaka pia imechakachuliwa utakuta baba mzima amebaka mtoto wa miaka 14 utaambiwa binti alitaka mwenyewe na baba huyu sana ataishia kifungo cha miaka mitatu au faini ya vijisenti tu.

Na hata pengine asipate adhabu yoyote kwani kwa sasa HAKI ya mtu ni pesa aliyonayo.Akishahonga hawa mahakimu wakuteuliwa na Rais basi kesi itaenda enda mwisho wa siku utasikia hakuna kesi.

Ndiyo maisha ya dunia yetu ya sasa,cha msingi kama jamii tunatakiwa kuwa waangalifu na kuona mtoto wa mwenzako ni mtoto wako,umlinde na kumpa haki zake za msingi mmojawapo uhuru wa kuishi.

Hawa wanaharakati wanaosema kila mtu anahaki ya kuishi hivi huyu muuaji hakuwa anajua mtoto aliyeua ana haki ya kuishi.Huwa siwaelewi wanaharakati kabisa,linapokuja mtoto amekufa sababu ya kulawitiwa au kubakwa hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kujionesha kwenye vyombo vya habari lakini linapokuja mtuhumiwa wa mauaji ya makusudi tunaambiwa eti ana haki ya kuishi,huwa hainiingii kwenye akili yangu hata kidogo.
 
Hivi sasa ndipo nimeanza kujiuliza endapo nimetumia lugha mzuri manake nimeamka na hasira sana dhidi ya hawa watu!

Mkuu kweli umeamka na lugha kali kasi, lakini inaeleweka. Kumbuka tu Japan na Marekani zinasheria ya adhabu ya kifo. Ni Ulaya tu, na katika sehemu bili tatu ambako hakuna adhabu kama hii.
 
Mimi nasema adhabu ya kifo ni muhimu iwepo, ili hao wanaoua wenzao wajue kabisa kwamba watakapothibitika kuwa wameua tena kwa mambo ya kishenzi kama hayo adhabu yao iwe kifo.
 
Ungebadilisha kwanza heading ikasomeka hivi "Mimi ( NasDaz )ni mshenzi na adhabu ya kifo nastahili" ndio nitakuja kutoa comment zangu.
 
Ungebadilisha kwanza heading ikasomeka hivi "Mimi ( NasDaz )ni mshenzi na adhabu ya kifo nastahili" ndio nitakuja kutoa comment zangu.

Lol, hapa inabidi utuweke wazi mkuu tumjue huyu jamaa, asije akawa kwenye kundi la watu wanafiki
 
NasDaz tena mtu kama huyo anawekewa wakili na anamtetea mwisho wa siku akishinda kesi ....anamlipa japo anajua ukweli na wakili anaambiwa ukweli.
lkn wakili anapindisha coz yupo kwenye biashara
 
Last edited by a moderator:
lkn NasDaz tukirud nyuma hupaswi kuhukumu kwa kuwa anayehukumu ni m1 tu
 
Last edited by a moderator:
Mwenye uwezo wa kumuhukumu mtu KIFO ni MUNGU pekee yake .kwani hata hawa mahakimu watahukumiwa na MUNGU siku ya mwisho
 
Back
Top Bottom