Siri za utajiri ambazo hamna mtu anayeweza kukwambia

Huu ujumbe ni special kwa ndugu Deborah9007 , maana nilikuwa kwenye mfungo, na Mungu akaniambia niongee na wana JamiiForums juu ya jambo hili.

Ili uwe tajiri na udumu katika utajiri wako, eidha wa nuruni au wa gizani ni lazima uwe na vitu viwili vikubwa.

1. MADHABAHU
2. AGANO.

Madhabahu ni sehemu ambayo unakutana na nguvu yako ya utajiri. Kama niguvu yako ni uchawi, basi hapa huwa ndipo unapatenga kwa ajili ya mambo yako, ila sisi ambao utajiri wetu umetoka kwa Mungu, MADHABAHU ni sehemu ambayo huwa nakutana na Mungu wangu, na huwa ninamtengea muda maalum. Muda huo na simu nazima kabisa, najikabidhi kikamilifu.

Namwita Mungu wangu, na huwa muda wetu wa kukutana madhabahuni ni saa tisa usiku hadi kumi na moja na nusu alfajiri kila siku.

Ninampa Mungu hesababu zangu za mapato na matumizi. Vitabu vyangu vya hesabu vinalala madhabahuni.

Namkabidhi Mungu mipango na ratiba zangu za asubuhi na siku nzima inayofuata.

MADHABAHU peke yake ndio inayoweza kukushindia vita zako zote. Kila vita yako ikabidhi madhabahu nayo vita itaisha.

2. AGANO
AGANO ni patano ambalo limebeba ahadi na sheria. Hamna tajiri ambaye hana AGANO. AGANO linakupa standing orders, do's and dont's. Ufanye nini na usifanye nini.

Kwenye agano hapa ndio kwenye masharti ya utajiri. Wengine wana majeraha yasiyopona. Hilo jeraha ndilo agano lenyewe, kwamba jeraha likipona tu utajiri umekwisha, hivyo ili uendelee kuwa tajiri ni lazima uhakikishe kidonda hakiponi.

Wengine wanaambiwa wasile vyakula fulani fulani, wengine wanaambiwa wasilale vitandani, walale kwenye sakafu mbichi iliyolowa maji.

Sisi wa nuruni pia tuna maagano yetu na aliyetutajirisha. Binafsi agano langu linatoka kitabu cha Yakobo 1:27 na Ufunuo wa Yohana 22:2.

Utajiri ni siri, siwezi kumwaga hapakila kitu kwani kwenye agano langu sitakiwi kuropoka hadi nipate ruhusa.
NB:-

CHAKULA CHA MADHABAHU NI SADAKA AMBAYO INAPATIKANA KWENYE AGANO.

KWENYE AGANO KAMA MLIKUBALIANA KILA IJUMAA YA MWANZO WA MWEZI UTATOA SADAKA YA NG'OMBE MZIMA, BASI USITOE MBUZI AU KUKU, KWANI UTAJIRI WAKO UTAPUKUTIKA.

SADAKA INA NGUVU SANA
Deborah9007 naamini kuna kitu umenasa.
Kheri wamtegemeao Bwana
 
Sawa mkuu inaonekana unafahamu mengi, hatakama kutakuwa hakuna ukweli kwenye ulicho kiandika.

Ila mimi nina swali moja tu, lakini unipe jibu lisilo na kona kona.

Mungu uliye ingia naye agano(pact), unamfahamu kwa jina lipi?
Hahaha
 
Unakuta kamtu kana hela nyingi kila siku saa tatu kanaenda ku deposit ila afya imekongorokaaa kumbe kanalazwa sakafuni mbavu zimesha ota sugu kiuno hakinasi vyema suriali
au daily kanakula ugali dagaa, yaani kanakula vyakula vya mifugo
 
Back
Top Bottom