Siri za ndani...

hehehe upo swity?
Noana huyo dada wa intrn ofc kwenu baada ya dada mwingine kwenda kumpelekea mmewe ikawaje ulimwambiaje? Duh nae alienda kutest zali hahahaha


nipo swity wangu......nlickilizia malumbano kwa mbali, mdada mwenye mume alikuja kunimba radhi kwa knisema vibaya, kamejirekebisha cku hizi, hata mkikaa mnaongea vitu vinavyoeleweka.....
 
nipo swity wangu......nlickilizia malumbano kwa mbali, mdada mwenye mume alikuja kunimba radhi kwa knisema vibaya, kamejirekebisha cku hizi, hata mkikaa mnaongea vitu vinavyoeleweka.....

hehehe kalikuwa mapepe si mwanzo wa ndoa kwa hiyo kalikuwa kanajiona uspoon kuongelea maswala hayo au kuna watu hawajaolewa hapo ndo maana kalikuwa kanajitapa.
 
Kwa uzoefu wangu, was maika kadhaa sasa kwa kweli sijawahi kuona wala kusikia mwanaume akisimulia wanaume wenzake kuhusu jinsi mke wake anavyomfurahisha au anavyomkera. Mara nyingi labda wanaweza kuzungumza mambo hayo wakati akiwa na girlfriend lakini akishaoa habari hizo hufutika kabisa. Hata kama atabanwa mahali anaweza kusema tu kwa utani na kwa ujumla bila kwenda kwenye details. At lease ndo uzoefu wangu kwa watu ambao nimekutana nao.

I think tabia hii iko sana kwa wanawake zaidi. Hata katika ugomvi nyumbani nimeona ni rahisi sana mwanamke kumsimulia shost wake au dada yake kukusu tatizo lake la nyumbani na mumewe ili apate ushauri kuliko mwanaume kusimulia ugomvi wake wa nyumbani na mewe kwa wanaume wenzake. Hizi ni tofauti za kiuumbaji tu na hazina tiba, that's how women are and that's how men are. Wanawake wengi hawawezi kuwa na mioyo migumu ya kuweza kudeal na matatizo yao bila ya kumshirikisha mtu wakati wanaume wengi wanaona kuwa kila kitu ni lazima akisolve yeye mwenyewe, labda mpaka pale kinapokuwa kikubwa mno na akakubali kwamba sasa nahitaji mawazo. But either way kama nilivyosema inaoneakana hizi ni tofauti za kiuumbaji kwa hiyo hata watu wapige kelele vipi kuhusu wanawake tabia hizi ni ngumu kutoweka. This is for all women all over the world.
 
hehehe kalikuwa mapepe si mwanzo wa ndoa kwa hiyo kalikuwa kanajiona uspoon kuongelea maswala hayo au kuna watu hawajaolewa hapo ndo maana kalikuwa kanajitapa.


ma single ni intern wenzake, halafu ni viwango vya juu, alivyoona yaliyotokea akajua mr ndio basi tena maana alichukua kitu kiwango sana.
 
Kwenye mijadala ya wanaume mara nyingi ni kinywaji tu! Jana ilikuwa hivi na vile, nilitoka baa hii nikahamia baa ile. Hata kama aliondoka na Baa maid hataki washikaji zake wamuone wa chini... alichukua baa maid??

Hata kama demu matawi ya juu, kama kamjaribu kashindwa, utasikia ... aaa yule kicheche. Lakini akipata kimyaaa. Washikaji wengi hata kama anakula ukimuuliza vipi yule demu ataruka mita mia!

Wale wanaopenda kujipakazia .... mara nyingi huwa ni waongo.... utasikia tu wakijisifu yule nilishakula. Huwezi sikia details zaidi ya hapo. Tena ukisikia mwanaume mzima anajisifia eti kala, ujue hapo ni 70% uongo!

Wanawake wengi huingia hadi kwenye graphical details.
 
...Wengi wetu tu wepesi kusimulia hadharani kama si kwa mashostito basi hata humo saluni au maofisini tunasimulia mambo yetu ya chumbani au waume wetu. Utasikia ah shost mie wangu mlevi sana bwana hadi anakera akirudi ye ni kukoroma tu hata hakumbuki ka kalala na mwanamke, au mh nimechoka leo, maana shughuli niliyopewa na shemeji yenu hata si ndogo!n.k...

...Hebu fikiria mara mbili, unawasimulia udhaifu wa mume wako, mara: “Mimi mume wangu akiona paja tu basi, ‘wazaramu’ wanampanda, bila kumpa ‘staftahi’ hapo ujue ‘network’ hazitosoma.” Kesho, shoga yako akikuta bar atamkaribisha shemejiye na kumfunulia paja hiyo ni kumdatisha, si umeshamuambia kuwa ‘wazimu’ wake upo kwenye mapaja?

Habari hii imenifanya nijiulize kama wanaume nao huwa wanazo tabia kama hizi, hivi huwa wanatusema kwa marafiki zao? Au wao mazungumzo yao ni tofauti?
Bila ya shaka kuwa mwanamke ndiye mtu wa karibu sana kwa mume wake, mwanamke huyu, anakuwa ndiye mwanamke aliyefanikiwa katika uhusiano wake wa mapenzi na mume wake...

Hivyo basi, suala la kuhifadhi siri ni jambo zito kwa mtu na ni amana aliyoichukua. Sisi ambao tuna imani na dini zetu tunafundishwa kuwa ...ikiwa mtu atazungumza na mtu mwengine kisha wakaachana basi huwa ni amana (yaani mazungumzo yale waliyozungumza huwa ni amana kwa kila mmoja) Haifai kwenda kuyasimulia mbele bila idhini ya yule uliye zungumza naye kwanza.

Tunafahamishwa kuwa:
“Hakika katika watu wabaya wenye shari siku ya Qiyaamah ni mtu aliyefanya tendo la ndoa na mke wake kisha mume au mke akatoa siri ile ya mume wake au ya mke wake”

Jambo la kuhifadhi siri ni la wajibu kwa mume na mke na ni jambo lililokuwa muhimu sana katika jamii na ndilo linalohifadhi amani na maadili mema katika jamii husika. Kwa hakika kutoa siri za mwanamme ndani ya nyumba yake au mwanamke, matengamano ya mume kwa mkewe, watoto wake, na kila alichokuwa nacho katika mali yake na mengineyo itakuwa ni fedheha kwa watu wengi. Uislamu umemuusia Muislamu kumsitiri na kumfichia siri nduguye Muislamu, na ya kuwa, Muislamu atakayemsitiri nduguye Muislamu basi Mwenyezi Mungu Atamsitiri yeye siku ya Qiyaamah.

Pamoja na kuwa kuhifadhi siri kwa ujumla ni jambo muhimu sana na ni wajibu, hata hivyo kuhifadhi siri ya unyumba baina ya mume na mke ni jambo la wajibu zaidi na ni jambo tukufu ambalo halifai kutolewa kwa hali yoyote ile. Ama wajinga wa zama zetu leo hii hawapendezwi na maneno isipokuwa ni maneno haya na yote hayo yanatokana na ukosefu mkubwa walionao wa imani na udhaifu wao.


Mtume (Saw) ametahadharisha hali hii ya kutoa siri ya jimai (tendo la ndoa) kwa watu, aliposema,

“Huenda mtu akasema anachomfanyia mke wake, na huenda hilo likafanywa na mwanamke pia (watu wakanyamaza baada ya maneno hayo) mwanamke akauliza, ee, kweli kabisa na wengi hufanya hivyo katika wanawake na wanaume, Mtume (Saw) akasema, ‘Basi msifanye hivyo, mfano wa jambo hilo ni kama Shaytwaan aliyekutana na Shaytwaan mwenzake wa kike na akawa anamuingilia hapo njiani na watu wakiwa wanamwangalia”

Kwa hakika huu ni mfano mbaya sana wa kufananishwa na shetani. Hivyo hili ni onyo kali kwa wenye tabia hiyo waiache ili wasiwekwe katika daraja ya chini Siku ya Kiyama wala wasifanane na mashetani.

Jamii zinavunjika kwa tabia hii ambayo imezagaa katika vigaro na mabaraza yetu kwa kuzungumzia mas-ala nyeti na ya ndani kama haya.
 
majuzi tulikuwa kwenye kikao cha usuluhishi wa ndoa tuliyoisimamia, mwanaume amemwambia hawara mambo yote kuhusu mke wake na akamuomba amzalie mtoto wa akiba, wana mtoto 1 wa mwaka sasa mwanaume anataka wa nje tofauti na mkewe, mimba ya hawara ikaharibika ndipo hapo mambo yakachuja mpaka nyumbani, hawara kuanza kumcal mke na kumtuc mchawi ndo kamsababishia mimba yake imetoka na hivi na vle, mume kuja kuhojiwa na mke akakubali ni kweli amecheza rafu mgogoro ukawa mgogoro mpaka tukaitwa tusuluhishe...waume zetu jamani tabia kaam hizi sio nzuri kabisa....

..... Huu ndio niliokuwa nautafuta so kumbe ni kweli kuwa sometimes baadhi ya waume husimulia mambo ya wake zao nje!!.
 
Kuna ka dada bwana kazini ka geni kameingia mtu mmoja akaingia akapata....kutoka kasema jamani....huyu mtoto ni balaa anafanya utafikiri kesho haipo...

Kosa kubwa sana kuwaambia fisi wengine namna hiyo sasa jamaa wakati anasema alifirini kapata bahati kumbe sasa ndio fungulia uwanja watu wakaanza kuacha mishahara hapo kumpa...kila ane enda anapata dozi kali....kamewapanga sasa wamefika watano hakuna anaye taka kuacha....imebidi wakubaliane kwa wiki wawili wawili bila dada kujua..kwa shughuli wanayo pata...ila watoto wambamba jamani ni balaa....mikunjo yote pindo zote wamo......

Red1: huyo mbaba akasimulia kwa kuwa ni mapoozeo au alipania kuoa?
Red2: Duh kimbembe yaani anatoa dozi kama za hospital?
Blue: Ina maana sie matipwa hatukunjiki? Tutake radhi tafadhali.
 
huu.. Na mara nyingi sana wanawake huwa wanapenda sana haya mambo. Na mara nyingi ukiona mwanamke kaweka siri kuwa Mumewe yuko vipi ujue kuwa kweli anampenda kwa dhati na hataki Mwanamke mwingine ajue vile yu mtamu.

Nilishawahi kupata story Moja kuwa kulikuwa na Jamaa mmoja alikuwa na Jogoo mkubwa sana. Sasa hiyo alitoa mmoja kati ya mwanawake aliyewahi kuwa naye yule jamaa. Baada ya kutoa hiyo siri eti wale wa mama katika ile kambi wakawa wanataka kujaribu mbona mamoja alilazwa Hospitali Hoi...

Hii ni ile kutoa siri za ndani,
Siri ya ndani iwe kama vile mtu anamungamia Mungu wake...

Duh kwa hiyo ni wazi kuwa kusimulia kunavuta wengine wajaribu duh hii ni fundisho tosha
 
kusimulia kuna hatari zake. Maana anayesimuliwa na yeye atataka akajaribu aone je ni kweli?
 
Back
Top Bottom