Siri ya Vyura wa Kihansi kutunzwa Marekani

Siyo kirahisi hiiivyo kama unavyosema. Kwanza wale walitoka porini moja kwa moja kwa hivyo mazingira yake halisi (kama vile mahitaji ya chakula na kadhalika) yalikuwa hayaeleweki vizuri na ilibidi wataalamu watumie muda na fedha nyingi kufanya studies tafauti mpaka kupata uelewa wa ecological requirements zao. Kwa hivyo siyo kitu cha kusema tu unawaondoa hapa na kuwaweka pale na mambo yatakuwa sawa.

Pili Wildlife Conservation Society ya USA imetumia fedha nyingi hapo awali katika kufanya hizo studies, pamoja na kupeleka wataalamu Marekani ili kwenda kujifunza mambo mbali mbali kuhusu uhifadhi wa vyura hawa.

Unadhani serikali ya Tz ingeweza kuwapa wataalamu wetu mapesa hayo kwa ajili ya kufanya utafiti wa chura? Hata hizo captive breeding facilities zilizojengwa UDSM na Kihansi ni fedha za World Bank.
Umeelezea vizuri lakini sidhani kama kwa Tanzania nzima ambako ndio Asili ya hao viumbe ikosekane kabisa mahali pa kuwahamishia na kufanyia project zao za kitafiti mpaka wakaone USA ndio mahali sahihi
Hivi ni lini mzungu akawa na mapenzi na Afrika? Mzungu hakuna kitu atafanya bila maslahi.. Ameona kwenye vyura kuna maslahi ndio maana akaamua kuwekeza kwao na si kwamba anatupenda sana
 
Of course yeye akifanya utafiti credit inakwenda kwake moja kwa moja na anaongeza ujuzi na maarifa yeye.

Hakuna mapenzi kutoka kwa mzungu lakini sisi ndiyo hatujipendi kwani kama nchi hatuwekezi kwenye utafiti wa kina ambao ndiyo unaleta maendeleo katika kila nyanja.

Nakuhakikishia kwamba laiti wangehamishwa kienyeji tu basi saa hizi tungekuwa tunasema RIP Kihansi Spray Toad.
 
Back
Top Bottom