Siri ya mapenzi ni nini?

The Listener

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
993
213
Mi ni mtu mzima kwa sasa na nimeishi na mke wangu yapata miaka 12 ya ndoa sasa. Ninampenda sana na ninaishi naye vyema pamoja na wanetu wawili; wa kike na wa kiume. Nimekuwa nikisikia matatizo mengi tu ya kimahusiano na wakati mwingine nimekuwa mshiriki kusuluhisha mahusiano ya baadhi ya rafiki zangu. Mara nyingi huwa natumia uzoefu wa namna ninavyoishi na mama watoto wangu.

Kufuatia suala la mahusiano kuwa na complications nyingi toka pande zote za me na ke kuna siku nikawaza (baada ya kuongea na rafiki yangu ambaye alimpenda sana girl friend wake ingawa yeye alikuwa akimsumbua kwa kutoka na jamaa mwingine) ni nini hasa kiko 'nyuma ya pazia' juu ya haya mapenzi.

Kwa mwenye kujua hasa historia ya suala hili la mahusiano (mahusiano ya kimapenzi kati ya me na ke) iwe ni kihistoria, kiimani au toka angle yoyote ile na atujuze kwa faida ama ya kudumisha ndoa zinazoenenda vyema, kurekebisha ndoa au mahusiano yanayoyumba kwa sababu mbalimbali au kutoa somo kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wanao au wana mipango ya kuwa na wenza
 
Kwani wewe ni nani alikufundisha mapenzi mpaka ukaweza kuishi na huyo mke wako kwa miaka uliyoweza kuishi naye ? Au ni nani aliyekwambia umpende yeye na usimpende mwingine ?

Kama jibu ni hakuna utagundua kwamba hili jambo ni natural wala halina formula, hence halina historia, chanzo wala muanzilishi.

Ila kama swali ni siri ya kudumu katika mahusiano (which is not necessarily the same na mapenzi) ni UVUMILIVU na UPENDO
 
Kusikilizana - namaanisha msikilize wife nayeye akusikilize pia maana wengine hawapendi kusikiliza wake zao, kujali familia-hapa naongelea kufaham familia yako inahitaji nini wamekula nini na wameshindaje? Amani - namaanisha kuondoa hofu za kijingajinga wife akitoka kidogo mara umemtafuta simu ikiingia mara umekagua, Uaminifu-hakuna kubwa na zito kama hili kuacha kabisa MICHEPUKO, zawadi ndogo ndogo umerudi home una parcel ata ya apples au chocolate sometime piza au kuku wa merry brown (mie penda this kuku jamani watamuje) yaani hapo amani itakuwepo kabisa, na upate muda wa kuwa nao sio kurudi home saa 5 usiku kutoka saa 11 alfajiri haifai, usisahau kusaidiana kazi ndogo ndogo yaani wife anapika basi wewe unasimamia homework ya watoto sio mpaka wife amalize kupika ndio aje kusimamia homework jamani inachosha, ukiyafanya hayo ndoa yako itakuwa mpya kila siku
 
Inatokea kwa kila mtu mkuu isipokuwa kwa wale naweza sema wenye matatizo hasa ya kisaikolojia. Ukiniuliza nilianzaje mkuu ni kwamba it happens nilipoanza kuwa matured kuwa na feelings ambazo zilifikia wakati fulani kuumia nilipopishana na nilompenda. Bado sielewi hasa what real happens behind love. But nashukuru kwa jibu
 
Unajua mwanzo katika makuzi yangu nilijua mapenzi is all about sex, but ulikuja muda nikawa napata hiyo sex tena bila kikomo nikawa bado sifurahii nahisi kuna kitu nakosa na nahitaji kukipata, nikagundua there is something precious in love which is happy, kumbe ukiwa na furaha katika mapenzi unaweza kufurahia kila kitu ikiwemo sex, na asikuambie mtu ukipata unaempenda lazima utafurahia kila kitu
 
una akili mnoooooooo safiiiiiiiiiiiiii
Kwani wewe ni nani alikufundisha mapenzi mpaka ukaweza kuishi na huyo mke wako kwa miaka uliyoweza kuishi naye ? Au ni nani aliyekwambia umpende yeye na usimpende mwingine ?

Kama jibu ni hakuna utagundua kwamba hili jambo ni natural wala halina formula, hence halina historia, chanzo wala muanzilishi.

Ila kama swali ni siri ya kudumu katika mahusiano (which is not necessarily the same na mapenzi) ni UVUMILIVU na UPENDO
 
Inatokea kwa kila mtu mkuu isipokuwa kwa wale naweza sema wenye matatizo hasa ya kisaikolojia. Ukiniuliza nilianzaje mkuu ni kwamba it happens nilipoanza kuwa matured kuwa na feelings ambazo zilifikia wakati fulani kuumia nilipopishana na nilompenda. Bado sielewi hasa what real happens behind love. But nashukuru kwa jibu

Okay Love / Upendo, Mapenzi (na sio mahusiano) ni Chemistry.., yaani chemical reaction inayotokea kwenye Ubongo. Mara nyingi inaanza kwa Lust (kutamani) Attraction (Kuvutiwa) na mwisho Attachment ingawa sio lazima upite kwenye stages hizo zote, na sababu ni Chemistry na si jambo la kuamua tu kwamba nianze au niache utaona kwamba sio jambo la kufundishwa wala kulazimishwa it just happens. Labda kwenye kudumisha ndoa / mahusiano ni mtu tu kujua jinsi ya kuishi na huyo mwenza wake (kuna watu wengi wanapendana sana ila hawawezi kuishi pamoja kutokana na tofauti au kukosa uvumilivu)
 
they say real love has roots..

fuatilia waliopendana toka utotoni, mapenzi yao huwa si ya kusumbuana sumbuana!

wanaokutania ukubwani, kwa vile hawakuwa na muda wa kufahamiana vizuri kwa muda mrefu,

utakuta mahusiano yao yanadoda sana...
 
love is a myth..mi siamini ,naona it's full of deceit,games,ujanja mwingi,km sikuhzi mhhh,me mguu ndan nje...smtym u may stay together js out of comfort bt hakuna penzi...anyway
 
Okay Love / Upendo, Mapenzi (na sio mahusiano) ni Chemistry.., yaani chemical reaction inayotokea kwenye Ubongo. Mara nyingi inaanza kwa Lust (kutamani) Attraction (Kuvutiwa) na mwisho Attachment ingawa sio lazima upite kwenye stages hizo zote, na sababu ni Chemistry na si jambo la kuamua tu kwamba nianze au niache utaona kwamba sio jambo la kufundishwa wala kulazimishwa it just happens. Labda kwenye kudumisha ndoa / mahusiano ni mtu tu kujua jinsi ya kuishi na huyo mwenza wake (kuna watu wengi wanapendana sana ila hawawezi kuishi pamoja kutokana na tofauti au kukosa uvumilivu)
chemistry ndo hyo ht 6 months nyingi inafifia,u need more than that
 
Kusikilizana - namaanisha msikilize wife nayeye akusikilize pia maana wengine hawapendi kusikiliza wake zao, kujali familia-hapa naongelea kufaham familia yako inahitaji nini wamekula nini na wameshindaje? Amani - namaanisha kuondoa hofu za kijingajinga wife akitoka kidogo mara umemtafuta simu ikiingia mara umekagua, Uaminifu-hakuna kubwa na zito kama hili kuacha kabisa MICHEPUKO, zawadi ndogo ndogo umerudi home una parcel ata ya apples au chocolate sometime piza au kuku wa merry brown (mie penda this kuku jamani watamuje) yaani hapo amani itakuwepo kabisa, na upate muda wa kuwa nao sio kurudi home saa 5 usiku kutoka saa 11 alfajiri haifai, usisahau kusaidiana kazi ndogo ndogo yaani wife anapika basi wewe unasimamia homework ya watoto sio mpaka wife amalize kupika ndio aje kusimamia homework jamani inachosha, ukiyafanya hayo ndoa yako itakuwa mpya kila siku

Kwa mujibu wa maelezo yako, ni wazi unamanisha wanaume ndio tatizo ktk ndoa!!!
Kwa mantiki hiyo unakesi ya kujibu, na kwa kutaka kusuluhisha kesi yako, JILETE MWENYEWE PIEMO tuyamalize kimya kimya!
Na welewako usije!
 
chemistry ndo hyo ht 6 months nyingi inafifia,u need more than that
Hivi kama nilikupenda mwaka jana siwezi nikakuchukia leo ?, au mapenzi hayakui au kufa ?, au nikikuchukia leo siwezi nikakupenda kesho ? Point yangu ni kwamba kufifia kwa mapenzi haimaanishi kwamba mwanzo sikukupenda. Ndio maana nikasema kwenye swali la mdau mapenzi na mahusiano are not necessarily the same. Kama swali anauliza jinsi ya kudumisha mapenzi yasiishe na kuendelea kukua that is another Topic entirely na hapo ndio mtu unaweza kumshauri. Ila kupenda its just chemistry which happens within ones brain.
 
Sasa mkuu miaka yote 12 hamna ulichojifunza..?
Me nilitegemea japo una wazo flani..!
napata mashaka na great thnkr huyu!
 
Kwa mujibu wa maelezo yako, ni wazi unamanisha wanaume ndio tatizo ktk ndoa!!!
Kwa mantiki hiyo unakesi ya kujibu, na kwa kutaka kusuluhisha kesi yako, JILETE MWENYEWE PIEMO tuyamalize kimya kimya!
Na welewako usije!

Hahahaha lol PM katika mada hii au kuna mapya huko? ya hapa yanaishia hapahapa
 
Okay Love / Upendo, Mapenzi (na sio mahusiano) ni Chemistry.., yaani chemical reaction inayotokea kwenye Ubongo. Mara nyingi inaanza kwa Lust (kutamani) Attraction (Kuvutiwa) na mwisho Attachment ingawa sio lazima upite kwenye stages hizo zote, na sababu ni Chemistry na si jambo la kuamua tu kwamba nianze au niache utaona kwamba sio jambo la kufundishwa wala kulazimishwa it just happens. Labda kwenye kudumisha ndoa / mahusiano ni mtu tu kujua jinsi ya kuishi na huyo mwenza wake (kuna watu wengi wanapendana sana ila hawawezi kuishi pamoja kutokana na tofauti au kukosa uvumilivu)

asante
 
Back
Top Bottom