Siri ya Kikwete TRA yaanikwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
RAIS wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, ndiye chanzo cha mwendelezo wa ufisadi wa kutisha katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Raia Mwema likidokezwa kwamba, mafaili ya siri za uvundo wa ufisadi yaliwasilishwa ofisini kwake bila kuchukuliwa hatua madhubuti.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya gazeti hili, Kikwete alipelekewa taarifa kamili za uchunguzi wenye vielelezo vya wazi vikitaja wahusika kwa majina, uliofanywa na vyombo vya dola.

Hatua hiyo ya Rais Kikwete kutofanyia kazi kwa umakini taarifa hizo inatajwa kuwahi kuvunja moyo maofisa waadilifu wa juu wa vyombo vya dola, ambao, iliwabidi wasubiri ujio wa Rais mpya, wa Awamu ya Tano, ili aweze kufanya kazi iliyofumbiwa macho na Kikwete, kwa sababu zinazodaiwa kujulikana na Kikwete mwenyewe.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, hatua pekee iliyokuwa ikichukuliwa na Kikwete ni kufanya mabadiliko ya hapa na pale ya bodi za taasisi husika, hatua ambayo inafananishwa na ‘mzaha' kwa kulinganisha mzizi wa ufisadi kwenye taasisi husika.
Inaelezwa kwamba taarifa za ufisadi zilianza kukusanywa miaka zaidi ya mitano nyuma na hata gazeti hili la Raia Mwema, katika toleo lake la Juni 9, mwaka 2010, lilichapisha ripoti maalumu kuhusu ufisadi ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, na kama kawaida, yote hayo yalifumbuliwa macho hadi wakati huu wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli.

"Tatizo kubwa lilikuwa ni Rais Kikwete, mafaili ya ufisadi TRA na Bandari yalifikishwa Ikulu, alikabidhiwa Rais, lakini alikaa kimya na kuendelea na shughuli nyingine. Kwa kweli alikatisha tamaa wakuu wengi waadilifu wa vyombo vya dola ambao hawakuwa na la kufanya kwa sababu yeye ndiye Rais na Amiri Jeshi Mkuu, ilibidi wavumilie kuona kama Rais ajaye ataweza kutafuna mfupa wa ufisadi na kwa kweli kuna dalili nzuri," kilieleza chanzo chetu cha habari kutoka miongoni mwa maofisa waandamizi katika masuala ya upelelezi.

"…kuna ushahidi mkubwa sana wa kufanikisha kufunga watu jela na hata kuwafilisi. Subiri kazi ndio imeanza na itafanikiwa tu. Nchi lazima irudi kwenye misingi ile ile aliyoijenga Mwalimu Julius Nyerere pamoja na waadilifu wenzake. Tunataka kurejesha heshima ya mamlaka ya Rais, asiwe mtu wa kuyumbishwa na magenge, kwa mfano ya wafanyabiashara wakwepa kodi," alieleza mtoa habari wetu huyo kwa masharti ya kutotajwa gazetini jina lake.

Katika taarifa hizo za ‘uzembe' wa Kikwete katika kukabili mafisadi na ufisadi, Raia Mwema limeelezwa kwamba Tanzania, baada ya miaka kati ya mitano hadi saba, inaweza kujitegemea kwa bajeti bila msaada wa wahisani kama ukusanyaji na wigo wa kodi utaimarishwa, na uhuni wa kukwepa kodi kwa kushirikisha viongozi waandamizi utadhibitiwa.
Raia Mwema miaka 5 iliyopita

Gazeti hili, miaka mitano iliyopita, Juni 9, 2010 katika toleo lake namba 137, lilichapisha ripoti maalumu iliyopewa kichwa cha habari "Ufisadi ushuru wa forodha siri nzito"; wahusika watajwa; waporomosha maghorofa Kariakoo; washirikiana na vigogo, maofisa wa TRA.
Habari hiyo ilikuwa ni mwendelezo wa ile ya awali, iliyohusu ufisadi huo huo hapo bandarini.

Habari hiyo ilisomeka: "TAARIFA zimekuwa zikimiminika chumba cha habari cha Raia Mwema kuelezea zaidi mtandao wa wizi wa mapato yatokanayo na ushuru katika Bandari ya Dar es Salaam ya kuwa ni mpana zaidi na unawahusisha wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa vigogo.

Taarifa hizo ni za maelezo ya ziada juu ya habari kuu ya gazeti hili ya wiki iliyopita iliyoandikwa chini ya kichwa: Ripoti Maalumu; Ufisadi wa kutisha Ushuru wa Forodha.

Familia ya wafanyabiashara vijana wenye asili ya Kiarabu, imeelezwa kujilimbikizia mali kwa ufisadi huo katika ukwepaji kodi na sasa wamekuwa wakijenga majumba makubwa katika maeneo ya Kariakoo na pembezoni mwa Dar es Salaam.
Wakiongozwa na kaka yao, vijana hao wa Kiarabu wapatao watatu kwa sasa wanaelezwa kuingiza faida ya zaidi ya Shilingi bilioni tatu kwa wiki.

Katika baadhi ya taarifa hizo, Raia Mwema limetajiwa wafanyabiashara na wanasiasa wakubwa, wa zamani na wa sasa, ambao ni washiriki katika mtandao huo lakini kwa sababu za wazi, na hasa kwa kuwa hawakuweza kupatikana, majina yao hayatatajwa kwa sasa.

"Tunasubiri kuona kama mtaandika tena. Msije nanyi mkapewa (Sh.) milioni 50 au 100 mkaacha. Wizi huu una mtandao mpana na unahusisha wafanyabiashara wakubwa na vigogo. Mnaweza nanyi mkapewa fedha mkanyamaza, au wakakunyamazisheni kwa mbinu nyingine, " alisema msomaji mmoja katika ujumbe wake kwa Raia Mwema wiki iliyopita akijitaja kuwa ni mfanyabiashara wa Dar es Salaam aliyekerwa na kuathiriwa na mtandao huo.

Alisema mwingine: "Kama ni kuchangia Chama Cha Mapinduzi (CCM) sisi tumekuwa tukichanga hata katika wakati ambao hawa (anataja jina la kampuni) hawakuwapo na chama hakikuwa na wachangiaji wengi.

"Nakuambieni mlichoandika ni jambo linalofahamika wazi pale TRA (Mamlaka ya Mapato). Ni kilio cha wateja na wafanyabiashara wote wanaohusika na uingizaji na utoaji mizigo bandarini. Hata huyo Kamishina Kitilya (Harry Kitilya, Kamishina Mkuu wa TRA) anajua kinachoendelea, katika majibu kwenu amejibaraguza tu.

"Nina ndugu yangu amekuwa akisumbuliwa kwa miezi sasa ili kutoa mizigo yake, mara barua, mara bima, mara sijui nukta gani kwenye barua, basi ili mradi asumbuke mpaka apitie kampuni yao."

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, baadhi ya wafanyabiashara waliokwisha kukerwa na usumbufu huo bandarini Dar es Salaam na katika ofisi za TRA na Tiscan, wamekuwa wakipitisha mizigo yao katika bandari za Beira, Msumbiji na Mombasa, Kenya.
"Sasa tazama, Serikali kila mara inalia kwamba mapato hayatoshi, lakini hayatoshi vipi wakati inaruhusu wizi katika moja ya vyanzo vikubwa na muhimu vya mapato?

Fikiria hawa wanaokwenda kupitisha mizigo Beira na Mombasa ni Watanzania, tena wengi wao wakazi wa Dar es Salaam. Wanakubali kuingia shida ya kwenda mbali lakini wafanye kazi nzuri ambayo sasa inaingiza mapato Kenya na Msumbiji," anasema mfanyabishara huyo kwa masharti kwamba jina lake lisitajwe.

"Kwenu waandishi wa Raia Mwema, kwanza sina budi kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya kwa kutupatia habari za uhakika na bila kuonea mtu. Leo (wiki iliyopita) najitokeza kuliunga mkono gazeti lenu katika jitihada za kufichua ufisadi ambao kila kukicha Serikali imekuwa inaupigia kelele," ndivyo alivyoanza msomaji mwingine ambaye kwa sababu za wazi naye hatutamtaja jina.

Aliongeza: "Habari yenu ya ukurasa wa mbele toleo namba 136 ni ya kweli. Vijana hawa wako watatu (anataja majina) wana asili ya Saudia japo ni Watanzania.

"Ni kweli walianzia uwakala Tanga na Holili. Walihama baada ya ofisa mmoja wa forodha, namkumbuka kwa jina la Banny, aliyehamishiwa huko, kuwabana sana.

"Wanashirikiana na viongozi wa juu wa TRA na wamejenga mtandao kuanzia bandarini, na ICD zote. Wanafanya wanavyotaka saa yoyote na wakati wowote kama vile hakuna Serikali. Ofisa yeyote atakayebisha kufanya wanavyotaka huhamishwa kituo mara moja.
"Wamesababisha maofisa kadhaa kufukuzwa kazi. Nawakumbuka baadhi ya maofisa waliofukuzwa kazi pale Longroom; DICD na Container Terminal na wengine wamehamishwa vituo.

"Kwa kawaida kampuni zote hufuata taratibu za kiforodha lakini kampuni zao hupita njia za mkato kwa kuandika barua ya kuomba provisional clearance na nyingi za barua hizo zinalenga kukwepa kodi.

"Hizo barua za provisional clearance mara nyingi huandikwa Longroom kwa maelekezo ya vigogo wa TRA na zinakuwa zinaruhusiwa kutoa mizigo bila ukomo wa idadi na muda kwa bidhaa ambazo hazina sifa za kupewa provision.

"Bidhaa zenye sifa ni kama malighafi za viwandani,vyakula na bidhaa za Serikali na za balozi. Si nguo, vitenge, kanga, saruji na nondo kama inavyofanywa sasa. Tafadhali pokeeni nakala za baadhi ya barua za aina hii za karibuni zaidi kwa uthibitisho wa mambo yanavyofanywa na wakubwa TRA kwa kushirikiana na mtandao huu."

Taarifa zilizotufikia wakati tukienda mitamboni jana Jumanne, zilisema kwamba ukaguzi mkali wa ndani umekuwa ukifanyika TRA kutaka kubaini nini ambacho kimekuwa kikendelea kuhusiana na ukwepaji ushuru.

Wiki iliyopita (ya Juni, 2010), gazeti hili likikariri malalamiko miongoni mwa wafanyabiashara na wateja wapitishao mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam lileleza ya kuwa wakati Bajeti ya Serikali inasuasua kutokana na uhaba wa fedha za ndani, familia moja ya Dar es Salaam inayomiliki kampuni inayojihusisha na bishara ya bidhaa za nyumbani imejiingiza katika uwakala wa forodha kwa staili ya aina yake ikiwa ni pamoja na kujikita katika kuwasaidia wengine kukwepa kodi katika mtandao unaohusisha wanasiasa.

Biashara hiyo ya aina yake ya uwakala wa ukwepaji kodi, imedaiwa imekuwa inaipotezea Serikali mabilioni ya shilingi ambazo zilistahili kukusanywa kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wanaoingiza bidhaa mbalimbali kutoka China na Dubai.

"Sasa ni vigumu sana, na kwa kweli hakuna wakala mwigine anayethubutu kutoa bandarini bidhaa za nguo kwa kuwa nyaraka za kampuni nyingine zifikapo Tiscan au Longroom huwekewa bei za juu ambazo hazilipiki ili kuwakatisha tamaa waagizaji ambao kwa sasa wamechoshwa na huduma za vijana hawa zilizojaa kiburi na dharau.

"Hali hiyo imewafanya waagizaji kukosa pa kwenda bali kwa vijana hao na wakabaki wakisikitika jinsi vyombo vya dola vinavyowekwa mfukoni kwa hasara ya jumla ya Taifa. Waagizaji wanalalamika kwamba hawana tena uhuru kwa kuwa wanalazimika kutumia kampuni moja tu ambayo bei zake hazina majadiliano. Ukienda kubembeleza unaambiwa katafute wakala mwingine ambaye hata hivyo huwezi kumpata kwa kuwa hawa wamehodhi kila kitu," alieeleza mtoa habari Raia Mwema aliyeko ndani ya sekta ya kodi.

Mfanyabiashara mwingine alisema kwa hali halisi iliyopo kwenye mfumo wa ukusanyaji kodi, ni vugumu kukwepa ushuru kwa kudanganya kiasi (idadi) cha mali kilichomo kwenye kontena (false declaration) au kuweka bei ndogo au ya chini ya ile bei halisi (under invoicing), lakini kwa kampuni hii hilo linawezekana kwa kuwa mfumo mzima tangu serikalini, Tiscan na TRA umekuwa nyuma yao kutokana na nguvu kubwa ya kifedha waliyonayo.
Imeelezwa kwmaba kwenye kampeni za mwaka 2005 kampuni hiyo ilichangia chama tawala Sh. Milioni 200 na kwamba katika mwaka huu wameahidi kuchangia milioni 500.

Ili kufahamu kiasi cha mapato ya Serikali yanayopotea angalia hesabu hizi (kwa wakati huo-mwaka 2010): Kontena la nguo za kawaida lenye urefu wa futi 20 laweza kuwa na thamani ya Dola za Marekani 60,000.00 hadi Dola za Marekani 80,000.00 kutegemeana na aina, ubora na idadi ya nguo zenyewe. Ushuru wa jumla ni 48% ya thamani halisi (cif value). Kwa hiyo kama thamani ni Dola za Marekani 60,000.00 x 48% = Dola za Marekani 28,000. Kwa thamani ya Dola 1 ya Marekani = Sh.1400, ushuru kwa kontena hili katika shilingi ni 40,320,000.

Kama kontena ni la thamani ya Dola za Marekani 80,000, ushuru ni 80,000.00 x 48% ambazo ni sawa na Dola za Marekani 38,000.00 na kwa Sh ni 53,760,000.

Kwa mujibu wa habari za ndani ya TRA, kampuni hii hukadiria gharama zote kwa meta za ujazo kutoka China hadi Dar es Salaam, na hivyo kontena la futi 20 ambalo lina meta za ujazo 36, ina maana gharama zote zitakuwa ni Dola za Marekani 450 x 36 = Dola za Marekani 16,200 ambazo ni sawa na Sh. milioni 22.68.

Ikiwa utaondoa gharama halisi za kusafirisha kontena hadi Dar es Salaam ambazo ni Dola za Marekani 2,500, basi kinachobaki ni Dola za Marekani 16,200 – 2500 = Dola za Marekani 13,700.00 au Sh. 19,180,000.

Uchunguzi wa Raia Mwema (kwa wakati huo 2010) ulionyesha kwamba sehemu kubwa ya fedha hutumika katika kulipia ushuru kidogo, rushwa kwa maofisa sehemu mbalimbali husika, gharama za bandari na usafiri wa bandarini kwenda kwenye maghala yao.
"Kwa uzoefu wangu kampuni hii kwa kontena la nguo la futi 20 hawalipi zaidi ya Sh. milioni 10. Hii ina maana ya kuwa badala ya kulipia gharama halisi ya zaidi ya Sh. milioni 40 wao wanalipa milioni 10 tu. Kwa hiyo, kwa mfano mmoja tu, Serikali hupoteza Sh. milioni 30 kwa kila kontena la nguo la futi 20 linalotoka bandarini. Ikiwa makontena 100 yanaweza kutoka bandarini kwa wiki moja, ina maana Serikali hupoteza milioni 30 x 100 = bilioni 3 kwa wiki. Kwa mwaka mmoja hii ni sawa na shilingi bilioni 156," alieleza mtaalamu wa kodi ambaye kwa sasa ni mstaafu.
Waziri Mkuu Majaliwa

Wakati taarifa za Kikwete kukalia ripoti ya ufisadi wa Bandari, TRA na taasisi nyingine za umma, mara baada ya kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dk. John Magufuli, Novemba 27, mwaka huu, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa aliwasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu wa TRA kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
Majaliwa alitoa uamuzi huo katika mazungumzo yake na viongozi wa Bandari pamoja na TRA katika ziara ya kushtukiza aliyoifanya Ijumaa, Novemba 27, 2015.

Waliosimamishwa na Majaliwa ni aliyekuwa Kamishna wa Forodha, Tiagi Masamaki; Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya; Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Haruni Mpande na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Eliachi Mrema. Miongoni mwao tayari wamekwishafikishwa mahakamani.

Hata hivyo, mbali na hao, Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade na mapema wiki hii,
Rais Magufuli alivunja Bodi ya TPA na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Profesa Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadhi Massawe.

Vile vile Rais alitengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjaka, ambaye ilielezwa kwamba atapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa maelezo yaliyoambatana na taarifa hiyo, Rais amevunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa viongozi hao kutokana na utendaji mbovu wa muda mrefu wa Mamlaka ya Bandari na kwa kitendo cha viongozi hao kutochukua hatua kwenye vyanzo.

Naye Katibu Mkuu huyo alisimamishwa kazi kwa sababu ya kutosimamia kwa makini mashirika mawili ya Bandari na Reli ambayo yako chini ya wizara yake ambako Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa alizuru Shirika la Reli (TRL) Desemba 3, 2015 na kukuta ubadhirifu wa shilingi bilioni 16.5.

Chanzo: Raiamwema
 
Lambalamba walikuwa wakiambiwa humu kuwa JK ni msanii wanatoka mapovu!
 
Muda wa kusoma ripoti angeupata wapi, mbona mnamuonea bure.

hicho kiti cha enzi alikikalia saa ngapi maana siku zote alikuwa wima, akikaa yuko safarini.
 
yaaaani...ila huwezi jua....labda kuna kitu tusichokijua...
natumaini jk aliwaacha hawa vigogo ili wachunguzwe vizuri ili badae washughulikiwe....ka mnakumbuka kauli ya IGP Mwema kuwa mafisadi tukiwafuata hovyo wangeweza kupindua nchi.
Tusimlaumu JK ili halihuko kulikuwa na watumishi tena wenye mishahara minono...
Naona ni kama kumshika mkeo anakusaliti afu wamlaumu JK ili hali anajua miiko ya ndoa
 
Na baada ya kuumbuka badala afiche upumbavu wake bado anakuja na vijembe eti, msinilaumu mimi, Mgufuli ndio kawashinda, mnajisumbua mie sigombei tena, sijui mwanaume wa aina gani huyu, maswala ya msingi yana ongelewa yeye analeta siasa. Aliharibu kwa kuwa alijua hagombei tena, lakini rizione ana gombea kule kwao ambako wanachgua tu mradi ccm. Anyamaze asimtie doa magufuli amuache afanye yale aliyoshindwa.
 
yaaaani...ila huwezi jua....labda kuna kitu tusichokijua...
natumaini jk aliwaacha hawa vigogo ili wachunguzwe vizuri ili badae washughulikiwe....ka mnakumbuka kauli ya IGP Mwema kuwa mafisadi tukiwafuata hovyo wangeweza kupindua nchi.
Tusimlaumu JK ili halihuko kulikuwa na watumishi tena wenye mishahara minono...
Naona ni kama kumshika mkeo anakusaliti afu wamlaumu JK ili hali anajua miiko ya ndoa
Hivi unajua JK alikuwa ni Rais wa nchi hii!!! Kama hakujua jua hakujua kazi yake. Tuache kutetea masula haya au hili unaliona ni tamko sahihi kama si kujidhalilisha tu endelea.....Kikwete: Sihusiki na ukwepaji kodi - Kitaifa | Mwananchi
 
He's such a disgrace. Mzaha Mzaha tu.

Hata mm ananiboa kwa mizaha huyu jamaa. Mfano jana alipokuwa akiongea baada ya usafi akasema "kuna waandishi wanasema hapa JK hachomoi....kwani nimechomeka mini??"
Mambo ya kiswahili kwenye issue serious. Waandishi walitaka kujua kama amewahi kutoa makontena pale bandarini kwa vimemo ama kumdaidia mfanyabiashara yeyote kukwepa kodi akaanza kuchekacheka na kufanya mizaha kama hiyo.
Nchi yetu hakika ilikuwa kwenye likizo ya kiuongozi.
 
He's such a disgrace. Mzaha Mzaha tu.

Hata mm ananiboa kwa mizaha huyu jamaa. Mfano jana alipokuwa akiongea baada ya usafi akasema "kuna waandishi wanasema hapa JK hachomoi....kwani nimechomeka mini??"
Mambo ya kiswahili kwenye issue serious. Waandishi walitaka kujua kama amewahi kutoa makontena pale bandarini kwa vimemo ama kumsaidia mfanyabiashara yeyote kukwepa kodi akaanza kuchekacheka na kufanya mizaha kama hiyo.
Nchi yetu hakika ilikuwa kwenye likizo ya kiuongozi.
 
Bado kodi ya mapato kwa makampuni makubwa (Corporate tax) pamoja na misamaha yake (Exemptions). Maana kuna wawekezaji wamekuwa wakibadilisha majina tu ili waendelee kusamehewa kodi wakati nchi haipati manufaa husika kama vile ongezeko la ajira na uchumi kukua.
 
Hata mm ananiboa kwa mizaha huyu jamaa. Mfano jana alipokuwa akiongea baada ya usafi akasema "kuna waandishi wanasema hapa JK hachomoi....kwani nimechomeka mini??"
Mambo ya kiswahili kwenye issue serious. Waandishi walitaka kujua kama amewahi kutoa makontena pale bandarini kwa vimemo ama kumdaidia mfanyabiashara yeyote kukwepa kodi akaanza kuchekacheka na kufanya mizaha kama hiyo.
Nchi yetu hakika ilikuwa kwenye likizo ya kiuongozi.


Uyu jamaa ni hopeless kabisa mtu mzima anaongea maneno machafu usitegemee itatoka busara kinywani mwake
 
Hivi unajua JK alikuwa ni Rais wa nchi hii!!! Kama hakujua jua hakujua kazi yake. Tuache kutetea masula haya au hili unaliona ni tamko sahihi kama si kujidhalilisha tu endelea.....Kikwete: Sihusiki na ukwepaji kodi - Kitaifa | Mwananchi

sio kutetea mkuu...kama nilivyosema sie kuna mengi tusiyoyajua....kuna watu walikuwa na dhamana hiyo.
ila kumbuka kuwa yule jamaa aliingia kwa kagoda...kwahyo ilimpasa kuondoa u boyz 2men kumpata magufuli....hawawez kumchafua maguful kwa maana kaingia kwa kura za watz ka utakumbuka mafisadi walienda muunga mwenzao na kuangukia pua
 
Back
Top Bottom