Badala ya kujivua gamba kumbe mwenyekiti alikuwa anaandaa mbinu ya kutafuta mrithi wake ambaye anatakuwa wa type yake.
Pamoja na kubadili safu ya uongozi mjini Dodoma, CCM pia ilitangaza kwamba wanachama wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe la sivyo wataondolewa kwa nguvu. Wanachama hao wanatajwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, na wabunge wawili, Andrew Chenge na Rostam Aziz. Ni kweli matajiri hawa hawapendwi na Watanzania wengi isipokuwa wa majimboni mwao tu.
Lakini pia watu hawa watatu wana sifa nyingine: kwamba ndio tishio pekee na la kweli dhidi ya mpango wa Kikwete wa kusaka Mwislamu wa kumrithi. Watu hawa nia yao kubwa si udini; bali ni ulaji. Wanataka kumweka Lowasa kwenye urais mwaka 2015, mtu ambaye pengine hatalazimika kumheshimu Kikwete na kumlinda. Lakini tatizo kwa Kikwete ni kwamba Lowassa si Mwislamu.
Kundi hili lina urafiki wa karibu na Makamba ambaye inadaiwa kuwa ndoto yake kubwa haikuwa udini kwa mwaka 2015, licha ya kuwa naye amesikika mara nyingi akijiingiza kwenye siasa za udini; bali anaota mwanae aje kuachiwa urais mwaka 2025 na kundi hili. Makamba hutamba kwamba mwanae anafaa kuwa kiongozi na hakuna ubishi kwamba alihakikisha mwanae anapata ubunge, uenyekiti wa kamati ya Bunge, na kisha kuingia kwenye Sekretarieti ya CCM.
Aidha, mtoto wa Makamba pia anaelezwa kuwemo kwenye kundi linalowaunga mkono watuhumiwa hawa wa ufisadi ambalo lina idadi kubwa ya wabunge na viongozi wa CCM wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Hii ndiyo sababu tangu CCM ilipoanza kushambulia mafisadi hadharani, yeye amepotea jukwaani!
Kimsingi kuna kutofautiana kati ya Makamba na Kikwete kuhusiana na nani awe rais mwaka 2015 na hawa watuhumiwa wa ufisadi wafanyejwe. Hivyo, tangazo la kujivua gamba pamoja na kutajwa kwa watuhumiwa hao ambao Kikwete mwenyewe aliwapigia kampeni mwaka jana kwenye uchaguzi wa wabunge, ni geresha tu. Kikwete alikuwa anaunda timu itakayomrithi mwaka 2015.

Kimsingi, hadi sasa Kikwete ameshawaacha wabaya wake wote nje ya Kamati Kuu ambao dhambi yao kuu ni kuutaka urais wa mwaka 2015. Watu hawa ni Membe, na hili kundi la mafisadi pamoja na Prof. Mark Mwandosya ambaye licha ya kushindwa mwaka 2005 na umri kumtupa mkono, inadaiwa bado anataka kujaribu tena 2015.
Njama hizi za Mwenyekiti Kikwete ambazo zinaelezwa kwamba ni zoezi la CCM kujisafisha, ingawa upo ukweli pia kutokana na kuigopa CHADEMA, ndizo chanzo na mwisho wa zoezi la kujivua gamba. Hakuna cha zaidi.

Hivyo basi, hakuna ushujaa wala maamuzi magumu yaliyofanyika Dodoma. Ulikuwa ni usanii tu, na ndiyo sababu hakuna kiongozi wa CCM anayepigia kelele mafisadi zaidi ya kijana Nnauye ambaye anaganga njaa na kulipa fadhila za kupewa ukuu wa wilaya na cheo kwenye chama. Hata Chiligati aliyejitokeza mwanzoni sasa ameingia mitini.
Makamba mdogo naye amekaa mbali; kwani mafisadi hao ndiyo wafadhili wake wakuu kisiasa na maswahiba wa baba yake. Hofu yake ni kwamba, akiwachafua leo na wao watamwacha huko mbeleni au watamngoa kwenye siasa.

Malalamiko ya Joseph Butiku hivi juzi kwamba viongozi wa CCM wamemwachia Mwenyekiti mzigo wa kupambana na mafisadi, yamekuja bila kujua ukweli wa mambo. CCM haiko kwenye mapambano na mafisadi; bali Mwenyekiti ndiye anapambana na maadui zake ila tu amepata bahati kwamba watu hao hao ndio wanaolalamikiwa kwa ufisadi. Ni bahati tu ya mtende iliyotoa nafasi ya fitna hii kuchezwa!
Source (Raiamwema, 25-31, Mei 2011)
Source (Raiamwema, 25-31, Mei 2011)