Siri 17 ambazo hutakiwi kusema ili kulinda uhusiano wako

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Kama upo kwenye mahusiano ya mapenzi yawe mapya au ndio yako ya kwanza chunga sana mdomo wako usiseme mambo haya kwa mpenzi wako

1. Hofu kuhusu uhusiano wako
Katika kila uhusiano, uwe wa karibu au wa mbali, kuna mambo unayoyashuku, hisia zisizokufurahisha na maswali mengi.

Ni vyema kutosema na mpenzi wako kuhusu maswala hayo ikiwa sio za maana sana kwa kuwa zinaumiza mioyo na kusambaratisha uaminifu wengi.

Mambo hayo huenda yakapotea tu baada ya muda.

2. Jinsi unavyotumia pesa zako
Pesa husababisha ndoa nyingi kuvunjika. Ni vyema kumfungulia mpenzio akaunti yake ya benki na kutafuta pesa zako.

Ni vyema kujivinjari, mradi tu pesa unazotumia zisihitilafiane na pesa za matumizi nyumbani.

3. Siri za ndani za kifamilia
Haina maana kumwambia mpenzi wako kuhusu babako anafanya dhuluma nyingi nyumbani au mamako asiyejukumika ipasavyo.

Ukimwambia mpenzi wako mambo ya ndani kihistoria ya familia yako, utakuwa unampa silaha dhidi yako na usishtuke siku moja ukiambiwa “Babako alimdanganya mamako pia na mpenzi mwingine”.

4. Kutoa mimba
Hakuna mwanamume anayetaka kumuoa msichana aliyetoa mimba mara kadhaa.

Wakiamua kuyapuuza, wanakuwa wepesi wa kulaumu wakichelewa kupata mtoto.

5. Marafiki waliokuzingua
Kumfanya mpenzi wako ajue marafiki waliokuzingua kunamfanya mpenzi wako kutokuamini.

Wanaume sawia na wanawake hawapendi kujua kuwa rafiki anaenziwa na mpenzi wake wa maisha.

Wakati mwingi, wao huwafukuza marafiki wa wapenzi wao kwa kukosa uaminifu.

6. Kuwaarifu mashemeji mambo ya uhusiano wenu

Kueneza habari zenu nje, hasa kwa jamaa na mashemeji huharibu mambo. Hali hiyo inaweza kusambaratisha uhusiano wenu ikiwa mume wako anamwamini na anamuenzi jamaa husika katika familia yenu.

7. Kitu ambacho hupendi kumhusu mpenzio
Hakuna aliye mkamilifu. Ikiwa hulipendi pua lake, nywele, … chochote kile, usimwambie. Angalia uzuri wake na kumsifia kwa hayo

8. Maoni mabaya
Usimwambie hisia mbaya kumhusu kutoka kwa marafiki na jamaa. Mambo hayo yatamuumiza anaweza kuyatumia kudai jamaa wa familia yako hawakumpenda.

Dunia ina mambo mabaya, mkinge mpenzio kwa mapenzi tele

9. Kuchunguza anaowasiliana nao
Wanawake wengi hupenda kujua mpenzi wao anawasiliana na akina nani kwa simu, hali inayowafanya kuvizia simu zao.

Utaonekana mtu asiyemwamini. Akiacha simu yake nyumbani, kuwa mwaminifu na usipekue

10. Jumbe za mpenzi wa zamani
Ikiwa unazungumza na mpenzi wako wa zamani, usimuonyeshe au kumwacha aone jumbe hizo. Acha jumbe hizo ziwe zako pekee.

Sio wanaume wengie wanaoweza kuishi wakijua jambo hilo linafanyika.

11. Ikiwa umewahi kudanganya
Kila mtu ameteleza kwa wakati mmoja, lakini kuwa makini na maneno unayomwambia mpenzi wako kwa kuwa huenda yakapanda mbegu akilini mwao na kuwageuza kuwa watu tofauti kabisa.

12. Mahaba ya zamani
Usilizungumzie hili. Usiulize wala kulizungumzia, labda tu likichipuka kwenye mazungumzo.

Wataalamu wanasema kuwa kuzungumzia mahaba ya zamani na mpenzi wako wa sasa hakutakusaidia.

13. Mahusiano ya pembeni kazini
Ikiwa ulikubali mahaba na mtu ofisini, usilizungumzie na mpenzi wako.
Ukifanya hivyo, utavunja uaminifu kwa mpenzi wako kwa kuwa sio rahisi kusahau jambo kama hilo.

14. Mtu anayekuzingua
Sio lazima mpenzi wako ajue hisia zako kwa mtu fulani. Ikiwa itakuwa una hisia kwa ndugu yake au marafiki zake na umwambie, hali itakuwa mbaya

15. Kumlinganisha na mpenzi wako wa zamani

Wazo la kumlinganisha mpenzi wako na yule wa zamani sio la busara. Hata ikiwa una hasira, usifanye hivyo.

16. Uroda hauna raha tena
Ikiwa mahaba yenu kitandani yamepungua asali, ni jukumu lenu wawili kuyaimarisha. Myazungumze hasa mbinu mpya kuimarisha mapenzi yenu.

Hakuna anayetaka kusikia “Sidhani nina hamu yako tena”.

17. Ngono nzuri zaidi
Ikiwa uroda uliokuzingua sana haukuwa kutoka kwa mpenzi wako wa sasa, usilizungumzie, au sivyo utajitia matatani.

Mpenzio anataka kujua yeye ndiye gwiji kitandani. Mfanye ajue hiyo au sivyo, utahangaika kwa taabu za kujitakia.
 
Mapenzi hayana formula kwamba ukipatia calculation utapata the correct answers, hapo hakuna iyoo.

Unaweza fanya hili, ukaharibu lile, ama ukaharibu iki na kupatia lile, ama uharibu kabisa.

Unaeza kuwa na hela, yaan unamuonga mpnz wako kila kitu lkn akaja chepuka na shambaboy hapo home, na unaeza kuwa masikini ukamjali sana mpnz wako lkn akakusaliti kwa kuchepuka na masikini mwenzako, yaani yule jamaa wa masix prts, na unaweza iga kuweka hayo masix parts jusui pack, na bado ukaachwa vile vile

Chamsingi ni kukomaaa tu na maisha yako
 
Unaweza usimwambie yote hayo na mengine zaidi ila ukapigwa KIBUTI asubuhi tu na mapema..

Pia unaweza weka wazi yote hayo kwa huyo mpenzi wako na bado mahusiano yakadumu kabisa...

Mapenzi hayanaga formula, inategemeana na jua limechomozea angle ipi au limezamia angle ipi...

Mwisho, ishi kwa kumuomba MUNGU sana akupe mtu aliekua sahihi, hata kama ana mapungufu kiasi yanayorekebishika usimwache. Nusu + Nusu = Kitu kimoja perfect.
 
Sijafanya yote uliyosema lakini Penzi halijamaliza hata Miezi nimeachwa hata Uroda sijapata dadek
Utakuwa huna hela mkuu. Ukiona mwanamke wa Tz kakuacha ujue hela huna. Kama hela ipo ataanzia wapi kukuacha?

"Tafuta pesa usiachweachwe na wanawake mkuu"
 
Siku hizi mademu kama hupigi picha kali utaachwa tu na mihela yako..nilichogundua we ishi maisha ya kufake utawala wengi sana
 
Kama upo kwenye mahusiano ya mapenzi yawe mapya au ndio yako ya kwanza chunga sana mdomo wako usiseme mambo haya kwa mpenzi wako

1. Hofu kuhusu uhusiano wako
Katika kila uhusiano, uwe wa karibu au wa mbali, kuna mambo unayoyashuku, hisia zisizokufurahisha na maswali mengi.

Ni vyema kutosema na mpenzi wako kuhusu maswala hayo ikiwa sio za maana sana kwa kuwa zinaumiza mioyo na kusambaratisha uaminifu wengi.

Mambo hayo huenda yakapotea tu baada ya muda.

2. Jinsi unavyotumia pesa zako
Pesa husababisha ndoa nyingi kuvunjika. Ni vyema kumfungulia mpenzio akaunti yake ya benki na kutafuta pesa zako.

Ni vyema kujivinjari, mradi tu pesa unazotumia zisihitilafiane na pesa za matumizi nyumbani.

3. Siri za ndani za kifamilia
Haina maana kumwambia mpenzi wako kuhusu babako anafanya dhuluma nyingi nyumbani au mamako asiyejukumika ipasavyo.

Ukimwambia mpenzi wako mambo ya ndani kihistoria ya familia yako, utakuwa unampa silaha dhidi yako na usishtuke siku moja ukiambiwa “Babako alimdanganya mamako pia na mpenzi mwingine”.

4. Kutoa mimba
Hakuna mwanamume anayetaka kumuoa msichana aliyetoa mimba mara kadhaa.

Wakiamua kuyapuuza, wanakuwa wepesi wa kulaumu wakichelewa kupata mtoto.

5. Marafiki waliokuzingua
Kumfanya mpenzi wako ajue marafiki waliokuzingua kunamfanya mpenzi wako kutokuamini.

Wanaume sawia na wanawake hawapendi kujua kuwa rafiki anaenziwa na mpenzi wake wa maisha.

Wakati mwingi, wao huwafukuza marafiki wa wapenzi wao kwa kukosa uaminifu.

6. Kuwaarifu mashemeji mambo ya uhusiano wenu

Kueneza habari zenu nje, hasa kwa jamaa na mashemeji huharibu mambo. Hali hiyo inaweza kusambaratisha uhusiano wenu ikiwa mume wako anamwamini na anamuenzi jamaa husika katika familia yenu.

7. Kitu ambacho hupendi kumhusu mpenzio
Hakuna aliye mkamilifu. Ikiwa hulipendi pua lake, nywele, … chochote kile, usimwambie. Angalia uzuri wake na kumsifia kwa hayo

8. Maoni mabaya
Usimwambie hisia mbaya kumhusu kutoka kwa marafiki na jamaa. Mambo hayo yatamuumiza anaweza kuyatumia kudai jamaa wa familia yako hawakumpenda.

Dunia ina mambo mabaya, mkinge mpenzio kwa mapenzi tele

9. Kuchunguza anaowasiliana nao
Wanawake wengi hupenda kujua mpenzi wao anawasiliana na akina nani kwa simu, hali inayowafanya kuvizia simu zao.

Utaonekana mtu asiyemwamini. Akiacha simu yake nyumbani, kuwa mwaminifu na usipekue

10. Jumbe za mpenzi wa zamani
Ikiwa unazungumza na mpenzi wako wa zamani, usimuonyeshe au kumwacha aone jumbe hizo. Acha jumbe hizo ziwe zako pekee.

Sio wanaume wengie wanaoweza kuishi wakijua jambo hilo linafanyika.

11. Ikiwa umewahi kudanganya
Kila mtu ameteleza kwa wakati mmoja, lakini kuwa makini na maneno unayomwambia mpenzi wako kwa kuwa huenda yakapanda mbegu akilini mwao na kuwageuza kuwa watu tofauti kabisa.

12. Mahaba ya zamani
Usilizungumzie hili. Usiulize wala kulizungumzia, labda tu likichipuka kwenye mazungumzo.

Wataalamu wanasema kuwa kuzungumzia mahaba ya zamani na mpenzi wako wa sasa hakutakusaidia.

13. Mahusiano ya pembeni kazini
Ikiwa ulikubali mahaba na mtu ofisini, usilizungumzie na mpenzi wako.
Ukifanya hivyo, utavunja uaminifu kwa mpenzi wako kwa kuwa sio rahisi kusahau jambo kama hilo.

14. Mtu anayekuzingua
Sio lazima mpenzi wako ajue hisia zako kwa mtu fulani. Ikiwa itakuwa una hisia kwa ndugu yake au marafiki zake na umwambie, hali itakuwa mbaya

15. Kumlinganisha na mpenzi wako wa zamani

Wazo la kumlinganisha mpenzi wako na yule wa zamani sio la busara. Hata ikiwa una hasira, usifanye hivyo.

16. Uroda hauna raha tena
Ikiwa mahaba yenu kitandani yamepungua asali, ni jukumu lenu wawili kuyaimarisha. Myazungumze hasa mbinu mpya kuimarisha mapenzi yenu.

Hakuna anayetaka kusikia “Sidhani nina hamu yako tena”.

17. Ngono nzuri zaidi
Ikiwa uroda uliokuzingua sana haukuwa kutoka kwa mpenzi wako wa sasa, usilizungumzie, au sivyo utajitia matatani.

Mpenzio anataka kujua yeye ndiye gwiji kitandani. Mfanye ajue hiyo au sivyo, utahangaika kwa taabu za kujitakia.
Mkuu hii ni hekima kubwa sana ya mahusiano...Ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom