voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Mtu yule huenda kama angepata watu wa kumsikiliza kabla na au baada ya kupelekwa gerezani.
Yawezekana alikuwa na ushuhuda mkubwa sana juu ya alichokuwa ameoteshwa kuhusu madhara ya lile Genge la wanamtandao lililokuwa nyuma ya Kampeni za Kikwete kwa wakati huo.
Ilikuwa ni katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza. Kwenye kampeni za aliekuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM 2005,Ndugu Kikwete.
Ni tukio ambalo lilistusha na kushangaza wengi,kwa jinsi lilivyotokea baada ya mtu yule kuweza kujipenyeza hadi kufanikiwa kumfikia Kikwete pale jukwaa kuu.
Baadae alimng'ang'ania mguu akijaribu kumshusha jukwaani mgombea aliekuwa akiendelea na hotuba yake ya kampeni. Kabla ya kudhibitiwa na wanausalama na hatimae kukamatwa.
Mtu yule baadae alihukumiwa kwenda jela. Na baadae alimaliza adhabu yake na hatimae akarudi uraiani. Ingawa haikuchukuwa muda mrefu baadae iliripotiwa kwamba alifariki Dunia.
Binafsi ninashangazwa na habari hizo zote kutopatikana katika mitandao yote ya kijamii kwa sasa. Na hii inadhihirisha genge lile lilivyokuwa limejipanga.
Lakini kwa wale tulio na kumbukumbu za mambo ya siasa za nchi hii. Bado tukio lile tunalikumbuka vizuri sana.
Nimetafakari juu ya Ujio wa Kikwete na wanamtandao wake na jinsi nchi hii ilivyo na inavyoelekea.
Ndio nikamkumbuka huyo mwamba.
Samahani kama nitawakwaza baadhi yenu kwa kumbukumbu hii ya kitambo kidogo.