SINGIDA: Dereva atiwa mbaroni kwa kuachia usukani na kuanza kucheza wimbo wa msanii Darasa

Aisee huyo dereva akatae hii video imeeditiwa

Hamna kesi hapooo

Mahakama zetu hazikubali ushaidi wa kielektroniki
 
KUNA SHIDA KUBWA KWENYE NCHII HII MIMI NILIDHANI NI GARI LAO BINAFSI KUMBE NI LA ABIRIA, NA KWANINI ABIRIA WAMESHINDWA HATA KUMPA MAKOFI MAWILI MATATU KUJUA ANACHOFANYA NI UPUUZI.

APEWE MIAKA MINGI NA VIBOKO VYA KUTOSHA ILI FUNDISHO KWA WENGINE
 
Mbona abiria wenyewe mizuka kibaoooo,wamchape vibao wamwache, ngoma yenyewe kali mno jamani unaweza hata kupitiliza safari.
 
Kuna mwalimu pia simu ya mwanafunzi iliita, badala ya kumkamata na kumuadhibu hyo mwanafunzi, mwalimu alianza kucheza na wanafunzi wakamuunga mkono.
 
Wacha mheshimiwa wetu kichwa chake kimuume tu,anakazi sana kuinyoosha nchi yetu .............Cpati picha ndo ingekuwa kwenye Bombadia zetu
bombardier wanaweza kuna auto pilot, pilot anaacha usukani anakuja wajulia hali abiria wake, lakini ni pake inapokuwa katika anga la kimataifa
 
bf2357032cf306a7479bf40ef5700d3b.jpg


Safi sana! Nadhani hao wamepotea njia kazi yao wanayopenda kufanya siyo hiyo ila ni nyingine. Inabidi waadhibiwe halaf wakimaliza adhabu wakatafute kazi inayowafaa. Mambo ya kijinga sana haya. Naona hapo makeke na kukatika viuno kote kumeisha wamekuwa wapole
 
Dereva huyo ambaye ameonekana kwenye video akiwa anaendesha gari aina ya Coaster ambayo inafanya safari zake Dodoma kwenda itigi akiwa anafanya kitendo cha hatari cha kuacha gari likiwa kwenye mwendo na kisha yeye kusimama na kuanza kucheza muziki huo akamatwa.

Kesho atapandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili yeye pamoja na wenzake ambao alikuwa nao kwenye Gari hilo.



Picha chini ni taarifa iliyotolewa na ROAD SAFETY AMBASSADORS(RSA)baada ya dereva huyo kukamatwa!
bf2357032cf306a7479bf40ef5700d3b.jpg


View attachment 443121
Hawa ndio wahusika walio kuwepo kwenye tukio hilo..

ila huu wimbo n kiboko
 
Sikubaliani na suala la kukamatwa hao mabwana.

1. Gari ilikua inatembea si zaidi ya speed ya 5kmph. Kwa kasi hii wala kusingekua na madhara yyte na alichokifanya dereve (angalia video uone speed ya gari)

2. Gari ilikua inatembea ktk barabara ya mtaani isiyokua na msongamano kabisa. Hivyo wala kusingekua na madhara yyte kwa tukio hilo.

3. Life is too short, we don't have to be serious all the time. Kuna wakati tunahitaji mdhaha na vicheko kwa kuzingatia usalama. Kipi ni hatari kati ya huyu jamaa anayefanya mbwembwe kwa speed ya 5kmph na yule anayesinzia 100kmph.
 
Back
Top Bottom