Singida Big Stars tunatengeneza timu ya vijana (U20), njoo ufanye majaribio

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Watu wa Soka,

Leo nimeleta habari njema kwa vijana wenye vipaji.

Singida Big Stars tumeanza kutengeneza timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20. Kama una vigezo njoo utuoneshe uwezo wako au mlete kijana wako, tukiridhika na kiwango tunasajili.

Majaribio yatafanyika Jumamosi 30/07/2022 hadi tarehe 06/08/2022 kuanzia saa 2 hadi 5 asubuhi katika uwanja wa Bombadia uliopo Halmashauri ya Manispaa - Singida.

Majaribio yatahamia wilayani Iramba katika uwanja wa CCM Kiomboi tarehe 08/08/2022 kuanzia saa 2 hadi 5 asubuhi.

Katika kipindi hiki cha majaribio, timu haitahusika na gharama za chakula na malazi. Kila anayekuja kwa majaribio atalazimika kujigharamia hadi pale atakapobahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa.

Kila la kheri!
 
Je hamtakuwa na majaribio kwa vijana wa U23, nina mdogo wangu mashine ya kazi, mwanzo alikuwa future stars, then akapata Azam ya wadogo lakini ikatokea kutokuelewana vyema, ikabidi arudi shule. Kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza masomo
 
Hapana mdau, kwa sasa ni U20 Trial pekee. Kama tutakuwa na ratiba nyingine tutatoa taarifa mapema. Mwambie asiache kufanya mazoezi na kuwa tayari muda wote.
 
nje ya mada nilikuwa napenda uniwekee list ya wachezaji wa SINGIDA BIG STAR watakaokuwa ligi kuu nikiwa kama supporter wenu kuanzia mwanzo wa ligi hadi mwisho wa ligi.
 
Singida unnited nn kimeua Kwanza mnk naona ilikufa kifo vibaya Sana timu sinazoanzishwa wanna siasa akiwa ktk pick ya uongozi akisha poteza hyo nafsi aliyepo timu nayo inapotea mfano gwambina fc mm Niko singdia hap hap mjin kifo Cha singida United nilikiona hata inamungo kifo chake chaja
 
mchukuwe u20 kweli sio vijeba kama wale jamaa wa mbeya kwanza 🤣 🤣 🤣
Mimi natamani aje hapa atueleze vigezo watakavyotumia kupata wachezaji halisi wa U - 20!

Maana kwenye mashindano ya U 20 yaliyopita hivi karibuni, timu nyingi zimechezesha wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 20!
Na madhara ya kufanganya umri ni makubwa sana kwenye maendeleo ya soka nchini.

Naongea hivi nikiwa kama bosi mstaafu wa timu fulani hivi ya vijana huko Iringa. Ilifikia wakati unaangalia mchezaji mwenye umbo dogo, au yule aliyechelewa kuota ndevu! Anashushwa umri kutoka miaka 24, 25, au 26! Mpaka miaka 18! Na usipofanya hivo, basi ujiandae kuwa kibonde wa mashindano.
 
Je hamtakuwa na majaribio kwa vijana wa U23, nina mdogo wangu mashine ya kazi, mwanzo alikuwa future stars, then akapata Azam ya wadogo lakini ikatokea kutokuelewana vyema, ikabidi arudi shule. Kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza masomo
Sikuhizi hakuna U23
 
Mimi natamani aje hapa atueleze vigezo watakavyotumia kupata wachezaji halisi wa U - 20!

Maana kwenye mashindano ya U 20 yaliyopita hivi karibuni, timu nyingi zimechezesha wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 20!
Na madhara ya kufanganya umri ni makubwa sana kwenye maendeleo ya soka nchini.

Naongea hivi nikiwa kama bosi mstaafu wa timu fulani hivi ya vijana huko Iringa. Ilifikia wakati unaangalia mchezaji mwenye umbo dogo, au yule aliyechelewa kuota ndevu! Anashushwa umri kutoka miaka 24, 25, au 26! Mpaka miaka 18! Na usipofanya hivo, basi ujiandae kuwa kibonde wa mashindano.
Bora wee umeonga ukweli mtupu. Tunadanganyana sana tuu mashindano wachezaji vijeba alafu tunakaa kabisa na kusema ni u20. Sie hatupo serious ndio maana tunaishia kuruhusu foreign players 12.

We dnt wana pay the price that success demands. Hawa wenyewe wanajibaraguza tuu hapa ila i doubt kama watapata wachezaji u20.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom