Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Singano tumesoma vizur kule kwa roma hongera. Kule kwa roma umemaliza vizur hongera ingawa kuna segment hazikuelezewa illishaje,mfano mpango lado ukawaje,na huku kusiwe na tusegment twing mwisho tukasahau mana hapa matukio meng,mara huyu kiajana ni kama supernatural jins unavyoelezea ila alizaliwa na mama chizi huko songwe,na anaonesha kashazunguka dunia nzima kwa sabab gani? Anyway sisi tunataka kuona kachkua mtoto regina ndio tunataka.connection iwepo mzee ajulikane,tayari wahuska wamekua wengi,usiache connection, tujue
Noted mkuu
 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.




.
.
.
.
.
.
.
.









.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.








🤣🤣🤣......






........














.......








..........


...........,










................


.
.
.
.
.
.m
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
..
..

.
..
.k.................




.
.
.




U
.
.
.
.
.
.
.
.m.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

..a.
.
.
.
.
.
.
.
.
.



.
.

.


.

.
.
.
.
.
.
..











































.
.
.
.
.


.
.................................,...








...m.

































.
.
.
.
.
.
.
.

.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR

SEHEMU YA 35.
Ndani ya ofisi hio alikuwepo Sebestiani Wambe, Willium Libeta ambao wote walikuwa ni wakurugenzi wasaidizi , kulikuwepo Shabani Chacha Mkuu wa idara ya fedha , Robinson Chenga wa idara ya Strategy, Nahida Mohamed mkuu wa idara ya Masoko na kuendelea.
Kilichomfanya Hamza kutabasamu ni mara baada ya kumuona mpenzi wake Eliza alievalia suti akiwa amekaa kwenye sofa pia .
Eliza hakutaka kabisa kuonyesha kufahamina na Hamza wakiwa kazini hivyo aliishia kutoa tabasamu tu.
“Huzijui sheria , huelewi kwamba ukiingia katika ofisi ya Afisa mtendaji mkuu wa kampuni unapaswa kugonga mlango?”Aliongea Mzee Sebastiani akionyesha hajafurahi.
Hamza alimpotezea na alitembea mpaka kwenye meza ya Regina na kisha aliweka yale matunda.
“Huyu ni msaidizi w angu , kama kuna wa kumkaripia basi ni kazi yangu hio”Aliongea Regina.
“Mkurugenzi hiki ni kikao cha siri kinachohusisha viongozi wa juu wa kampuni , msaidizi kama huyu anapaswa kuondoka”Aliongea Mzee Sebastiani.
“Hata mimi sitaki kushiriki pia , hivyo naondoka”Aliongea Hamza , hata hivyo hakutaka kujichosha kuhudhuria kikao ambacho hakikuwa kikimuhusu.
“Wewe Hamza kaa chini na usikilize kinachozungumziwa hapa kwa umakini”Aliongea Regina.
Kauli ile ilimshangaza Hamza na hivyo hivyo kwa wengine walionekana kushangaa pia , isitoshe sio jambo la kawaida, ilionyesha ni dhahiri Regina alikuwa akimwamini Hamza , maana hata msaidizi namba moja Linda hakuruhusiwa kuingia katika kikao hicho , sasa Hamza ambae ana siku chache ndani ya kampuni alikuwa akizingatiwa hivyo.
Upande wa Hamza hata hakufurahi kukaa na kusikiliza , angefurahi pengine kungekuwa na posho lakini hamna , aliona ni bora kwenda kuendelea kutafuta hela mtandaoni kutumia internet ya kampunni.
Lakini kwasababu bosi ndio alisema , hivyo aliona atii kauli yake na kusikiliza kinachozungumziwa.
“Mkurugenzi , una mpango wowote wa kudili na hii dharula ya kampuni ya Omega kupakuliwa na Zena?”Aliuliza Chenga mkuu wa idara ya mikakati na mbinu za ki uwekezaji kwa lugha ya kingereza.
“Omega has already officially signed a contract with the Zena Group today, this purchase is already comfirmed and irrevocable”Aliongea Regina akimaanisha kwamba Omega tayari rasmi imeweza kutia saini ya kimkataba na kampuni ya Zena na ununuzi huo hauwezi kubatilishwa.
Baada ya kauli hio Mzee Libeta na Willium walijikuta wakiangaliana huku wakitoa tabasamu la furaha la chini chini.
“Kama ni hivyo kwanini umeitisha kikao hiki leo hii?”Aliuliza Willium na Regina aliwaangalia hao wasaidizi wake kwa macho ya kichokozi kaba ya kujibu.
“Nimeitisha kikao hiki kuwatangazia kwamba kampuni yetu itakamilisha ununuzi wa kampuni nyingine haraka iwezekanavyo”
“Nini!?, Ununuzi mwingine , unazungumzia kampuni gani , sidhani ukiitoa Omega kuna kampuni nyingine inayojihusisha na uhandisi wa programu endeshi na akili bandia inayoweza kukidhi vigezo vyetu ndani ya Dar es salaam au Tanzania nzima”Aliongea Mzee Wambe.
“Makamu , unaweza kuwa sahihi , ndio maana nimefikia makubaliano ya kuinunua kampuni changa ya Moro technology na baada ya kikao cha wahisani pamoja na cha bodi ya wakurugenzi kumalizika ununuzi wetu utakuwa umekamilika”Aliuongea Regina.
Maneno hayo yalivyotamkwa , kila mmoja ndani ya ofisi ukiachana na Eliza walikuwa katika hali ya mshituko.
“Unamaanisha Moro Technology, hii kampuni ilioanzishwa na chuo cha sayansi Morogoro na kuingia katika orodha kumi ya kampuni changa ndani ya bara la Afrika?, nakumbuka chini ya idara yangu tulifuatilia na mmiliki mkubwa wa hisa ni raia wa Canada , Mkurugenzi ulianza mazungumzo ya ununuzi lini?”Aliuliza Chenga akiwa na mshangao.
“Wiki moja iliopita , kazi ya maongezi ya manunuzi ilisimamiwa na Eliza Mkuu wa idara ya mauzo na Moro walikubali kutuuzia hisa asilimia sabini hivyo tutachukua udhibiti na kuweka vipaumbele vyetu vya ki ufundi”
“Kumbe ndio maana Eliza alisafiri kikazi , kumbe ilikuwa ni swala hili , ndio maana hata idara yetu haina uelewa juu ya swala hili”Aliiogea.
Hata Nahida mkuu wa idara ya masoko alikuwa katika mshangao pia juu ya jambo hilo.
“Ili kuepusha makosa yasiotakiwa mimi na Eliza tuliamua kulifanya jambo hili siri mpaka hatua za mwisho”Aliongea Regina.
“Meneja Chenga naomba uniwie radhi juu ya hili , sikuwataarifu kwasababu ni maagizo kutoka kwa mkurugenzi”Aliongea Eliza.
“Hapana Eliza , huna haja ya kuomba msamaha , swala hili lina mchango mkubwa kwa kampuni , yaani bila ya kufanya makosa umeweza kukamilisha kazi kubwa hivi kwa kampuni , haha kama ilivyotarajiwa vijana mnaupiga mwingi kiasi cha kuwashinda wapinzani wenu”Aliongea Chenga akiwa na furaha.
“Nadhani kwasababu ni kampuni ambayo ilikuwa nje ya Dar ndio maana Mkurugenzi hakuiweka kama chaguo la kwanza , hivyo baada ya plan A kufeli akatumia plan B”
Mzee Sebastian na mzee Willium mara baada ya kusikia hivyo walijikuta paji za nyuso zao zikitoa jasho.
“Ukweli ni kwamba sikuwa na mpango wowote wa kuinunua Omega , Plan A niliokuwa nayo ni kuinunua Moro Technology”Aliongea Regina.
“Nini?”Kila mtu alishituka , Mzee Willum na Mzee Sebastiani walizidi kufubaa.
“Kama ni hivyo Mkurugenzi kwanini ulitupatia kazi
idara yetu kufanya mazungumzo na Omega?”Aliuliza Chenga.
“Kuna haja ya kuuliza kila kitu kipo wazi, Omega ilikuwa ni chambo kwa kampuni ya Zena ili kuinunua huku mpango mwingine ukipikwa?”Aliongea Hamza.
Mara baada ya kuongea hivyo kila mtu sasa ni kama alitoka usingizini , muonekano wao ulibadilika mara moja , wengine walikuwa wakishangaa wakati wengine walikuwa wakimwangalia Regina na hofu katika macho yao.
Hamza ambae alikuwa amesimama katika mlango aliinua macho yake na kumwangalia Regina na muonekano usioelezeka.
“Huyu mwanamke mbele yangu ni tofauti sana na
mwanamke wa jana aliekuwa akisindilia Doughnut”Aliwaza Hamza.
“Zena wameinunua kampiuni ya Omega kwa kiasi cha bilioni nne na sisi tumetumia milioni mia saba tu pekee kuinunua kampiuni ya Moro ili kutimiza malengo yetu , kingine msingi wa kampuni ya Moro ni mzuri sana kuliko wa Omega na ndani ya siku zijazo Moro itapiga hatua kubwa mno”
“Duuh , milioni mia saba tu , nadhani huu unuuzi una thamani kubwa ya muda kuliko wa Omega , vipi hakukuwa na mshindani?”
“Mshindani mkubwa wa kampiuni yetu ni Zena Group , sasa wamekamilisha malipo ya bilioni nne kuinunua Omega , unadhani wanaweza kuleta ushindani tena wa kujaribu kuinunua na Moro , isitoshe kwa taarifa nilizonazo wamefikia ukomo wa kuomba mkopo benki”Aliongea Regina.
“Mkurugenzi mbinu yako ilikuwa ni kuwasukumiza Zena kwenye kona kwa kuwaingiza kwenye mtego ili kujiondolea vikwazo vya kulenga shabaha bila tatizo”Aliongea Shabani kwa furaha kama zote.
Upande wa Wakurugenzi wasaidizi walikuwa wakitokwa na jasho sio kitoto , ilishakuwa wazi hawakuwa wakiisaidia Zena bali walikuwa wakiiharibu.
Ni sawa na kusema wameomba kisu kwa ajili ya kumuua Regina lakini wakati huo huo Regina akawatumia wao na kisu chao kuua mtu mwingine.
Regina mara baada ya kuona wazee hao walivyokuwa wakitokwa na jasho , tabasamu la kejeli lilimvaa , aliangalia muda kwenye saa ya ukutani na kisha alishika rimoti na kuwasha TV.
“Taarifa ya ununuzi kutoka Morogoro nadhani ishaanza , mnaweza kuangalia kila mtu”Mara baada ya kuongea hivyo kila mtu aliekuwepo hapo ndani aligeuka na kuangalia.
Ilikuwa ni kweli mkurugenzi wa kampuni ya Moro alikuwa akitaarifu waandishi wa habari juu ya maamuzi ya kampuni yao kuuza hisa asilimia sabini kwenda kwa mmiliki mwingine, huku habari ya kuaminika ni kwamba kampuni ya Dosam ndio imehusika na ununuzi wa hisa hizo.
“Haha CEO kazi nzuri , sisi wazee hakika umejua kutuweka gizani , huku ukitupiga chenga”Aliongea Mzee Chenga huku akiinua kidole gumba.
“Natamani kuona viongozi wa kampuni ya Zena watakavyojisikia baada ya kuona hii habari, nina uhakika Mzee Benjamini atatapika lita nne za damu haha..”Aliongea Nahida.
Mzee Willima na Sebastian waliona hali sio shwari , pumzi zao zilizidi kuwa nzito , walijua kabisa lawama zitaangushiwa kwao na kampuni ya Zena na moja kwa moja ingeonekana wao ndio wamecheza mchezo mchafu.
“Wewe mwanamke , tokea mwanzo ulikuwa ukitutumia kuvujisha taarifa makusudi kabisa kwenda Zena na kisha ukatugeuzia kibao”Aliongea Mzee Willium.
“Una moyo wa kishetani sana..”Aliongea Mzee Sebastian na wota kwa pamoja walisimama.
Wafanyakazi wengine wote walijikuta wakishangazwa na jambo hilo , ndio sasa wanaelewa kwanini walikuwa wakipingana na Regina kuinunua kampuni ya Omega katika kikao cha bodi ya wakurugenzi kumbe wao ndio walikuwa wasaliti.
Kwa kitendo cha kuwaingiza Zena Chaka sio rahisi kutoziepuka lawama na swala kama hilo haliwezi kupita kirahisi.
“Boss Wambe , Bosi Libeta, kwanini mfanye hivi , inamaana ndio nyie mliovujisha nyaraka za kampuni?”Aliongea Mzee Chenga.
“Nyamaza , unajua nini wewe , hii kampuni imeanzishwa na kizazi chetu cha watu wanaofanya kazi kwa bidii , taarifa kidogo tu inataka kumtoa jasho huyu msichana”Aliongea Mzee Willium.
Lakini Regina alikuwa kauzu na hakuwa na mabadiliko yoyote ya kimuonekano na aliishia kunyanyua bilauri ya maji na kunywa kidogo.
“Wakurugenzi wasaidizi , Mzee Sebastiani na Mzee Willium , nyie wote ni wazee katika hii kampiuni na niliwapa nafasi kutokana na vyeo vyenu mkagoma , nikawawekea mtego mkaingia wenyewe kwanini mnakasirika?”
“Unaongea ujinga ili hali unaujua ukweli , tokea ulivyochukua uongozi wa kampuni mpango wako ni kututoa sisi wazee na kuajiri vijana , huku ukiwa na uwezo wakufanya chochote utakavyo”
“Hii ni kampuni na sio sehemu ya kulelea wazee , kama huna uwezo wa kufanya kazi unaachia ngazi na kuwaachia nafasi wenye uwezo , acheni kuegamia katika vigezo vyenu ambavyo vimepitwa na wakati”
“Bullshit , wewe ni mwizi , usidhani hatujui unapanga pia kutupokonya hisa zetu , wewe ni mtoto wa mfanyakazi wa ndani tu uliezaliwa nje ya ndoa”Aliongea kwa hasira.
“ Unaruhusiwa kunifokea na kunitukana mimi mwenyewe ila sio mama yangu”Aliongea Regina.
“Sina haja ya kuendelea kubaki ndani ya hii kampuni hata hivyo , nani asiejua ukweli , mama yako ni kahaba tu aliekuja kujiuza kwa kujifanyisha mfanyakazi wa ndani , wengine wanaweza wasijue ila sisi tunaojua historia yako tunaujua ukweli”
Regina uvumilivu ulimshinda na palepale aliinua glasi ya maji kutaka kumwagia Mzee Willium lakini kaba ya kufanya hivyo mtu tayari ashajitokeza na kumpiga mzee Willium ngumi ya mdomo na kusababisha meno mawili kuchomoka.
“Hamza!!!?”
Wote walimaka, ilikuwa sahihi kwa mzee huyo kupokea kibano lakini tatizo pigo la Hamza lilikuwa la kuua mtu.
Mzee Willium alijikuta akitoa kilio, nusu ya uso wake wote ulivimba huku damu nyingi ikimtoka , alikuwa katika maumivu makali kiasi kwamba machozi yalikuwa yakimtoka. “Wewe.. unathubutu vipi kunipiga?”
“Mzee umeshindwa na msichana mdogo tofauti ya kukubali kushindwa unamtukannia mama yake , watu kama nyinyi kwanini nisiwashushie kipigo”Aliongea Hamza na alimsimamisha Mzee huyo na kisha alimlamba vibao viwili kulia na kushoto na akapoteza fahamu palepale na kisha alimgeukia Mzee Sebastiani.
Upande wa Mzee Sebastiani alikuwa akitetemeka kwa woga na aliishia kurudi nyuma kwa kujikokota.
“Usije kunisogelea , napiga simu polisi”Aliongea.
“Mkurugenzi muache apige simu polisi , kosa la kuvujisha nyaraka za kampuni, kuihujumu kampuni na kuiba hela , yote haya ni makosa ya jinai , tunaweza kuwaacha polisi wawakamate tu”Aliongea Hamza
Regina alijikuta akirudi katika hali ya kawaida baada ya mshituko usio na kifani , hakutegemea Hamza angechukua maamuzi ya namna hio.
“Kwanini umekuwa mkatili hivi , nimekuammbia mpige?”
“Si ndio maana umenibakisha hapa ili niwashughulikie , au unataka kusema umeniruhusu
kubaki hapa kusikiliza mnachozungumzia?”Aliuongea Hamza.
Regina alijikuta akinyamaza , ilikuwa ni kweli huo ndio mpango wake , alitegemea kabisa Mzee Willium na Mzee Sebastiani wakiujua ukweli lazima wapandwe na vichaa , hivyo alimfanya Hamza kubaki kuimarisha hali ya ki usalama, lakini tatizo Hamza amekuwa mkatili katika pigo lake mpaka kumng’oa mtu meno.
“Hii sio namna ya kitendo nilichotaka , ukimuumiza mtu hivi atakushitaki”
“Hehe,Mkurugenzi unachotakiwa kufanya ni kunitafutia Mwanasheria wa viwango vya juu , linaweza kuwa kosa ila mwanasheria anaweza kuligeuza na kuwa kitendo cha kishujaa cha kudumisha haki , au Self defence”Aliongea Hamza.
Regina asingeweza kumfanya chochote , lakini mara baada ya kuona namna ambavyo alimkingia kifua alijisikia vizuri.
“Haina haja ya kuita polisi”Aliongea na kisha alisogea hadi kwenye meza yake na kuongea na Linda kupitia simu.
“Linda waambie mapokezi wawaruhusu polisi kupandisha wawachukue wahalifu”Baada ya kuongea hivyo aligeuka.
“Nishakabidhi ushahidi , wanasheria wa kampuni na polisi watadili na hili”Aliongea Regina.
Kila mtu aliekuwa hapo ndani alishangaa kwa mara nyingine , kwahio Regina alikuwa amepanga kila kitu , yaani tokea mwanzo ilikuwa ni kama Mzee Willium na Sebastiani wanasomewa hukumu.
Hazikupita hada dakika nyingi polisi waliweza kufika na kumchukua Mzee Sebastiani na Mzee Willium na kuondoka nao , ilikuwa sasa ni wazi hawatoweza kurudi tena kama wakurugenzi ndani ya kampuni.
******
Muda huo huo katika eneo la Mbezi Beach , yalipo makao makuu ya kampuni ya Zena , ndani ya ofisi ya mwenyekiti , Mzee Benjamini alijihisi ni kama vile ukichaa umemvaa.
Alikuwa ameshikilia Golf club mkononi na kwa hasira alianza kuponda ponda vifaa vilivyokuwa vimewekwa ndani ya ofisi yake, ikiwemo tarakishi yenye thamni ya hela nyingi.
“Baba , kuna tukio kubwa limetokea”
Mlango wa kuingilia ofisini ulifunguliwa na alikuwa ni James aliekuwa akipiga kelele , ilionekana na yeye amekwisha kuziona habari za Dosam kuinunua Moro Technology corp, James mara baada ya kuangalia mazingira ya ofisi ya baba yake alisita kupiga hatua kuingia zaidi.
“Ushazipata habari tayari?”
“Yule mwanamke kahaba Regina .. alikuwa akijua kila kitu kuhusu sisi , Wambe na Libeta aliwapatia taarifa kuzileta kwetu ili tuingie mkenge kwa kuinunua Omega kwa pesa nyingi , ulikuwa ni mtego wake”Aliongea kwa hasira huku akilegeza tai.
“Baba kipi kifanyike sasa hivi , kwanini tusilifute dili letu na Omega”
“Unaoingea upuuzi gani , mkataba tushasaini unadhani ni rahisi kuufuta , , tutashitakiwa , tutalipa fidia ya kuvunja mkataba na juu zaidi taswira yetu
itaporomoka na kuzidi kumpa ushindi Regina”Aliongea kwa hasira.
“Basi tunaweza kuomba mkopo benki kwa namna yoyote ile na kisha tunainunua na hio Moro?”
“Wewe mjinga nini , unadhani watu watafufikiriaje tukinunua kampuni mbili zinazofanana , unadhani ni rahisi kupata mkopo benki”Aliongea huku akitamani kumpiga James , alijiuliza kwanini Regina ana akili nyingi kuliko mtoto wake ilihali wote wana umri mmoja.
“Kwa staili hii baba si tutashindwa kabisa kuipiku kampuni ya Dosam,Soko letu linazidi kuminywa na kampuni kubwa ndani ya Tanzania , muda si mrefu jina la kampuni yetu litapotea kabisa , hata kama niweze kumuoa Regina huko baadae kampuni yetu itamezwa”
“Unaongea ujinga gani , nani umuoe wewe mpuuzi?, mwanamke wa aina ya Regina ni kunguni , ni nyoka mwenye sumu kali , hawezi kuwa sehemu ya familia yetu kamwe, mtu ana uwezo wa kudanganya uongozi mzima wa kampuni
bila kujali hisia zao , na hajali kabisa , niseme tu alichoongea rafiki yangu Gabusha ni sahihi , kwenye maisha yangu sijawahi kutana na mwanamke wa aina hii”
“Sasa baba tutafanya nini , hatuwezi kurhusu kampuni ya Dosam kuendelea kuwa kubwa kama hivi , hisa zetu zinashuka thamani ni wazi kabisa kampuni yetu haina future”Aliongea James na palepale Mzee Benjamini alionekana kuwaza.
“Kwasababu huyu mwanamke ameshindikana kwa njia za kawaida , kilichobaki ni kumfanyia uharibifu”Aliongea na James aliishia kumeza mate na kutingisha kichwa kukubaliana na baba yake.
******
Upande mwingine masaa kadhaa nyuma Kanali Dastani alikuwa akihaha, kitu pekee ambacho kilimpa ahueni ni kwamba familia yake ilikuwa salama salimini.
Dakika chache mbele mara baada ya kuhakikisha usalama wa familia yake aliendesha gari kwa spidi kuelekea upande wa wa hospitali ya jeshi , kutoka alipokuwa akiishi na ilipo hospitali hio hapakuwa mbali hivyo ni dakika ishiririni tu zilimtosha.
Baada ya kufika hakutaka hata kuuliza tukio limetokeaje mpaka Amosi Jasusi mstaafu kutoweka , alienda moja kwa moja mpaka katika chumba cha mitambo ya kuongozea Kamera.
Na Luteni Usu , Afande Zakayo alimpa ushirikiano wa kutosha wa kuangalia Kamera hizo.
Sifa kubwa ya Kanali Dastani jeshini ni uwezo wake mkubwa wa akili , alikuwa akiaminiwa sana katika kazi za ki uchunguzi ambazo zilihitaji kutumia akili , udhaifu wake mkubwa ni kwamba hakuwa na uwezo mkubwa wa kimapambano , yaani alikuwa mwanajeshi wa kutumia bastora na bunduki pekee lakini ukimkuta hana siraha basi anakuwa kama Sele tu mnywa pombe , mateke yako matatu au matano tayari yupo chini anaugulia maumivu.
Hakujali kitambi chake kugusana na meza , alichotaka kuona katika tarakishi zilizokuwa mbele yake ni sura ya Amosi tu pamoja na watu waliohusika kumtoa Amosi hospitalini , alizidi kukodoa macho na hatimae alichotaka aliweza kukiona.
“Afande kuza hio picha ya mwanamke alievaa Hijab”Aliongea Kanali na Afande Zakayo alifanya kama alivyoambiwa, mwanamke ambae alikuwa akilengwa ndio alieonekana akiingia katika wodi aliolazwa Jasusi Amosi, lakini Kanali hakuweza kuitambua , kwani mwanamke yule alionekana kuwa Shombeshombe kama sio mwarabu.
“Zakayo unachoona hapa Amosi anaondoka kwa hiari yake au analazimishwa?”Aliongea Kanali , alikuwa ashaona kitu kilichomvutia macho lakini alitaka kuhakiki mawazo ya mwingine.
“Naona anaondoka kwa hiari yake mwenyewe”
“Angalia vizuri…”Aliongea lakini muda huo simu yake ilianza kuita na mara baada ya kuangalia jina linalopiga jasho la mikono lilianza kumvaa lakini hata hivyo alipokea.
“Jambo Afande”
“Dastani Rdui makao makuu haraka”Sauti ya kibabe iliongea kwenye simu.
“Lakini Afande..”
“Kama unafuatilia swala la Amosi achana nalo , Rudi kituoni nataka ripoti ya mauaji Zinga” Sauti iliongea mara ya pili na palepale simu ilikatwa.
Swali la kwanza lililomwingia akilini Kanali Dastani ni kujiuliza nini kinaendelea , inamaana makao makuu wanajua swala la kupotea kwa Amosi au kuna kitu asichokuwa akikifahamu.
“Afande hebu angalia Kamera za nje”Aliongea na Zakayo alienda moja wa moja mpaka kwenye picha zilizorekodiwa upande wa Kamera za nje , Amosi aliongeza umakini.
“Sh*t ni TISA hawa”Aliongea na palepale aliweza kuelewa nini kinaendelea ,Aling’;ata meno yake kwa hasira na kisha alitoka na kuondoka.
“Kwanini TISA wamekuja kumchukua Amosi , nini kinaendelea “Aliwaza Amosi huku wasiwasi ukiwa katika macho yake , kwa muda mrefu mpaka kitengo cha Tanzania intelligency Service Agency kuingilia jambo basi jua swala hilo limemfikia mheshimiwa Raisi moja kwa moja.
Ndani ya nusu saa tu Kanali alikuwa ashakaribia makao makuu ya jeshi kitengo cha MALIBU.
MALIBU na TISA ni vitengo viwili tofauti kabisa vyenye kubeba majukumu tofauti , hakukuwa na kirefu cha aina yoyote cha kitengo MALIBU bali ni jina la kiheshima kutoka kwa aliewahi kuwa Mkuu wa Majeshi Afande Athumani Abdalah Malibu.
Kama moja ya watu waliotoa pendekezo la jeshi kuunda kitengo kinachodili na nguvu zisizoonekana ndio maana jina lake la mwisho likachukuliwa na kufanywa ndio jina la kitengo hicho jeshini.
Miaka kadhaa nyuma katika historia ya moja ya nchi ya Afrika kuliibuka tukio la ajabu ambalo lilihusisha wanaume kupoteza viungo vyao vya uzazi, lilikuwa tukio la kushangaza na kugusa ambalo lilitikisa sana , jeshi la polisi kutoka nchi hio walijitahidi kuwinda muhusika wa tukio hilo lakini matukio ya namna hio yalizidi kupamba moto na wanaume walizidi kupoteza viungo vyao , mwisho wa siku jeshi la polisi walitoa ripoti tukio hilo halikuwa la kawaida na kulihusisha na nguvu za giza.
Baada ya tukio hilo miaka michache mbele likaibuka tukio lingine maarufu ambalo lilipatiwa jina la Popobawa ambalo lilianzia katika kisiwa cha Pemba na kusambaa mpaka jiji la Dar es salaam, tukio hilo na lenyewe lilikosa majibu na kuhusishwa na nguvu za giza.
Haikuwa tukio hilo tu , matukio mengi yaliweza kutokea ndani na nje ya Afrika ambayo yalihusishwa na nguvu za giza na kutokana na matatizo hayo serikali mbalimbali zilianzisha mpango wa kudhibiti hali kama hizo pale zinapotokea na hapo ndipo Afande Athumani Abdala Malibu alipopendekeza kuundwa kitengo cha kudili na nguvu ambazo sio za kawaida , ikiwemo uchawi na nguvu za giza na ndipo ilipozaliwa Malibu.
Mwanzoni Malibu haikuwa na nguvu sana lakini mara baada ya waanajeshi kupelekwa katika vyuo mbalimbali duniani ikiwemo China , Brazili na kwingineko hatimae kitengo cha MALIBU kikaanza kushamiri, lakini baadae sasa kitengo kilikosa kazi kwani matukio ya nguvu za giza yalikuwa machache hivyo kikapewa majukumu mengine ambayo ni kunasa mtu yoyote au kikundi chochote cha watu wanaotumia nguvu za ziada, kitengo hiki kilienda mbali mpaka kufatilia watumishi wa Mungu ambao nguvu zao zilikuwa sio za kawaida kabisa na kuanza kuwachunguza na pale inapobainika kuna ukakasi uchunguzi hufanyika mara moja.
Tukio la Zinga lilihusisha kukundi cha maninja kutoka kisiwa cha Samar , lakini ukweli ni kwamba ukisikia Samar utajua tu ni kisiwa lakini kuna kitu cha ziada kuhusu kundi hilo la maninja.
Inasemekana asilimia kubwa ya maninja wote waliopo chini ya Samar wanatokea katika mji unaoitwa Biringan.
Lakini ki uhaisia hakuna mji huo ndani ya Samar Ufilipino baki ni sehemu ambayo ipo katika hadithi tu , ni sawa na kusema Gamboshi sehemu ambayo ni ya kusemekana pekee au Antlatis.
Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama kweli maninja hao wanatokea Biringan lakini ni uhalisia kwamba Maninja kutoka Samar ambao waliingia Tanzania wanafahamika kama wawindaji(Bounty hunters) daraja B , uwezo wa hawa maninja sio wa kawaida, ki ufupi ni kwamba wana pua za mbwa , wanao uwezo wa kukuwinda kwa kuijua harufu yako tu jambo ambalo sio la kawaida kwa binadamu.
Sasa maninja kama wale wanakufa vifo vya ajabu namna ile ni dhahiri kwamba ni kesi ambayo inapaswa kuwa chini ya kitengo cha MALIBU.
Upande wa TISA ni kitengo cha usalama wa taifa ambacho kipo chini ya ofisi ya Raisi, kitengo hiki kinadili sana na ukusanyaji wa intellijensia ambazo zina ushahidi wa ki uhalisia.
Amosi alikuwa amepewa kazi na wabrazili kupitia Chriss na katika kazi hio anajikuta anaingia katika rada za watu kutoka kisiwa cha Binamu, lakini TISA wanakuja kumtoa Amosi kimyakimya hospitalini , ilimaanisha walitaka kumhoji au kuna kingine kinachoendelea.
Hayo ndio yaikuwa mawazo ya Kanali Dastani wakati akiwa katika gari akielekea makao makuu.
Zilimchukua dakika kadhaa tu kuingia makao makuu na alielekea moja kwa moja katika ofisi ya mkuu wa kitengo hicho , Brigedia Doswe, lakini kabla ya kuingia katika ofisi ya mkuu wake alipitia katika ofisi yake kwanza , alihitaji ripoti alioandaa kwa ajili ya kuitoa juu ya uchunguzi wa vifo vya maninja kutoka Samar.
Mara baada ya kupata ripoti yake moja kwa moja alielekea katika ofisi ya mkuu wake wa kazi kwa ajli ya kuripoti na mara baada ya kugonga mlango aliruhusiwa kuingia.
Bigedia Doswe alikuwa peke yake katika ofisi hio na kumfanya Kanali kuvuta pumzi , aliamini hali sio mbaya kama alivyodhania maana kama ingekuwa tofauti basi Kanali Msuya msaidizi wake asingekosekana ndani ya ofisi hio, baada ya kumsalimia, Afande Doswe alitoka katika meza yake na kwenda kuketi katika masofa.
“Dastani kabla ya kuzungumzia swala lililitokea leo , twende moja kwa moja kwenye ripoti, niambie umekwisha kumpata muhusika?”
“Afande japo hakuna ushahidi wa kutosha lakini nadhani mhusika tunae”Aliongea kanali na kumfanya Afande Doswe kumwangalia kwa macho yenye umakini na kanali alimpatia haraka mkuu wake karatasi kadhaa alizoshika mkononi.
Afande Doshwe alichukua karatasi zile na kuanza kuzisoma kwa umakini na macho yake yalichanua kidogo lakini hakuna mshangao katika sura yake.
“Huyu Hamza Mzee ndio muhusika, ukiachana na hii taarifa ya kuonekana katika gari ya Bosi wa Dosam je kuna kitu kingine kinachothibitisha hili?”Aliuliza.
“Hii ni Vidio iliopatikana juzi , anaeonekana katika vidio hio ni Hizza Joseph Mahimbo , nimefuatlia taarifa zake kupitia jeshi , amewahi kuwa mwanajeshi wa jeshi la Tanzania kabla ya kuachishwa kwa kosa la utomvu wa nidhamu , mwaka 1998 alihamia nchini Thailland , hakuna taarifa wakati alipokuwa Thailland alifanya nini ila mwaka huu amerudi nchini Tanzania , na kuna habari ambazo hazijathibitishwa katika kipindi chote alikuwa chini ya kundi la kininja la Black
Hawk .inaaminika ni moja ya wataalamu wakubwa wa matumizi ya mbinu ya kimapigano ya Vidole vya Tai na anafahamika kwa jina maarufu la Mzee wa Konki”Aliongea Dastani na kumfanya Afande Doswe kuvutiwa na taarifa hio na aliangalia Vidio hio kwa umakini mkubwa na sasa hali ya mshangao ilimvaa.
“Kama amefanikiwa kumdhibiti Yonesi basi sio wa kawaida , lakini swala la kudhibitiwa na huyu kijana…”Aliongea huku akionyesha mshangao.
“Nadhani sasa naelewa unachotaka kumaanisha Dastani , unaamini huyu Hamza ndio aliehusika na mauaji ya hawa wawindaji wa Samar?”
“Kwa maelezo ya bosi wa kampuni ya Dosam amekiri kutekwa na hii inadhihirisha watekaji walitumia gari yake kumpeleka mpaka kijiji cha wavuvi , anakiri pia Hamza ambae ni mpenzi wake ndio alimuokoa”
“Huyu Hamza mwenyewe anasemaje?”
“Amekiri kweli kumuokoa Regina , lakini anasema hakuhusika na mauaji na pili aliwapiga hawa maninja na baada ya hapo ndio akamuokoa mpenzi wake , tunaamini amehusika moja kwa moja na mauji yao lakini hakuna ushahidi, Hizi ni taarifa fupi zinazomuhusu Hamza Mzee”Aliongea na kisha alimkabidhi kishikwambi.
Afande Doswe alisoma kwa umakini na alionyesha ishara ya kukunja ndita kana kwamba hakuwa akiamini taarifa hio.
“Hii ripoti haina shida, uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa upo ,?” lakini kwanini adai uraia wake mara baada ya kuishi nje muda mrefu?, nadhani kuna taarifa ambayo haijaorodheshwa , hususani alipokuwa nje ya nchi alifanya nini kwa miaka kumi yote”
“Ndio Afande kwa tathimini ya tukio la Regina kutekwa inaonesha kabisa waliekuwa wakimlenga ni huyu Hamza , kama hisia zangu zitakuwa sahihi kuna kitu wanakitaka kutoka kwa Hamza na njia nyepesi ilikuwa ni kumtumia Regina kama Mateka”Aliongea na Afande Doswe alitingisha kichwa kukubaliana nae.
“Afande naomba unipe muda zaidi , nitafuatilia hili mpaka nilijue undani wake , nimejawa na shauku ya kutaka kumjua huyu Hamza ni nani”Aliongea Kanali Dastani.
“Haina haja ya kuendelea na hii kesi , kwa namna ilivyo haikidhi vigezo vya kuendelea kubakia chini
ya kitengo cha MALIBU hapa makao makuu ya jeshi”
“Afande lakini hawa Maninja sio wa kawaida, tuna kila sababu ya kutaka kujua wapo hapa Tanzania kwa ajili ya nini , watu kama hawa kufika Tanzania basi wanaemtafuta anaweza asiwe wa kawaida kama wao”.
“Wawe wakawaida wasiwe wa kawaida , uchunguzi uendelee ama usiendelee Dastani huwezi kuhusika na hii kesi itachukuliwa na watu wengine”
“Mheshimiwa unataka …”Kabla hata hajamaliza kuongea mlango wa mkuu wake ulifunguliwa na wanajeshi waliovalia Gwanda za kijeshi waliingia.
“Dastani mpaka sasa upo chini ya ulinzi kwa kosa la kusaliti jeshi na Jamhuri..”Aliongea Afande Doswe na palepale Kanali Dastani alijikuta akitokwa na macho huku akimwangalia mkuu wake kwa macho yasiokuwa ya kawaida.
“Afande sio kweli , naipenda nchi yangu , sijawahi kusaliti jeshi…”.
“Kama hujasaliti jeshi na Jamhuri itajulikana Dastani kwasasa utafuata utaratibu wa ki uchunguzi”Aliongea na palepale aliwapa ishara wale wanajeshi na kwa haraka sana Kanali Dastani alidhibitiwa na kutolewa.
Wakati mlango wa kuingia kwenye lift unafunguka ili Kanali Dastani kuingizwa lift hio ilionekana kuwa na mtu , Kanali mara baada ya kunyanyua macho yake alijikuta akipigwa na mshangao.
“Amosi!!!”
Alijikuta akimwemwesa midomo yake kwa mshangao, Amosi aliekuwa mbeleyake ni kama vile hakuwa ametoka hospitalini , alikuwa amevalia suti huku akipambwa na tabasamu.
Ndio alikuwa ni Amosi mwenyewe aliesalimika kuwawa kutoka katika mikono ya watu wa Binamu wakiongozwa na mwanamke Tresha Noah.
Amosi aliishia kumuonyeshea Kanali Dastani ishara ya bastora kwa vidole na kisha akatoka kwenye lift akiwa na tabasamu.
Kwa namna flani Kanali Dastani hisia zake zlimwambia Amosi alikuwa akihusika na kesi yake.
Amosi alienda moja kwa moja kuingia katika ofisi ya Afande Doswe na mara baada ya kuingia alipiga saluti ya kubana msuli na kisha alipewa ishara ya kukaa huku Afande Doswe akiwa na tabasamu.
“Amosi una muda mchache sana wa kututhibitishia kama Night Shadows wapo kweli au lah, kwanzia sasa ripoti ya misheni utaripoti kwangu moja kwa moja na sio kwa Kanali Dastani”
“Sawa Afande”
“Kabla ya hilo tunataka kujua kwanini kanisa la Wabrazili linafuatilia kesi ambayo ilifungwa zaidi ya miaka ishirini iliopita na kwanini Binamu wanazuia uchunguzi huu mpaka Kanali Dastani akakuuza , kwanzia sasa utaanza mahojiano yako na Kanali, Amosi tunataka kujua kila kitu ambacho Dastani anatuficha na muunganiko wake na Wiccan”
“Afande lakini vipi kuhusu agizo la mimi kuuwawa kutoka Binamu?”
“Hilo linashughulikiwa chini ya kitengo cha TISA , kwasasa tunahitaji akili yako kujikita kwenye
misheni yako, kingine jina lako halijabadilika , nadhani unaelewa nninachomaanisha?” “Ndio Afande”.
Dakika kadhaa mara baada ya Amosi kutoka katika makao makuu kwa siri sana aliweza kumpigia simu Chriss.
“Jasusi kwanini wiki nzima sikupati hewani?”Ndio swali la kwanza ambalo Amosi alisikia kutoka kwa Chriss , lakini ni kama alitegemea.
“Nitakuelezea baada ya kuonana ana kwa ana , tuonane saa mbili kamili usiku Las Vegas”Aliongea na mara baada ya kauli ile Amosi alikata simu na kisha alitoa tabasamu.









SEHEMU YA 37.
Wakati wa mchana wote taarifa ya Regina Afisa mtendaji mkuu kumpata msaliti wa kampuni zilisambaa kwa kila mmoja , lakini haikuwa hivyo tu pia kwa kitendo cha Regina kuwatumia wasaliti kuidanganya kampuni ya Zena ni moja ya habari hizo.
Kulikuwa hata na baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa wakitaka kuzijua habari hizo na kuzichapisha katika mitandao yao.
Wiki iliopita , wafanyakazi wengi walikuwa katika hali ya mawazo mara baada ya kampuni yao kushindwa kuipata Omega , lakini kumbe haikuwa mpango wa Regina kuipata Omega.
Regina alikuwa amedanganya kampuni nzima kwa kuwaaminisha kwamba alikuwa akitaka kuinunua Omega na kuikosa , hata kuigiza kabisa kuonekana kama vile alikuwa katika msongo wa mawazo.
Ijapokuwa wengi walimpongeza Regina kwa kumuua adui yake bila ya kumwaga damu lakini upande mwingine walimuona Regina kama mwanamke mkatili sana, haikuwa swala la kudanganya watu wa kampuni ya Zena tu lakini vievile amefannikiwa kuidanganya kampuni nzima kuamini alikuwa akitaka kuinunua Omega.
Baada ya kazi kama kawaida Hamza na Regina walishuka chini pamoja katika lift.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni walikuwa pia ndani ya lift hio na walimsalimia Regina kwa heshima , lakini kulikuwa na hali ya kumuogopa katika macho yao , kitu ambacho kilionekana wazi tofauti na mwanzo.
Tukio la siku hio licha ya kwamba lilikuwa na faida kwa kampuni , lakini lilifanya wafanyakazi kuzidi kumhofia.
Yaani ni kama mwanzoni walikuwa wakiamini Regina sio kama wanavyomfikiria , lakini mara baada ya tukio hilo waliamini Regina ni kama wanavyomfikiria.
Regina alikuwa akiiona hofu yao lakini aliishia kukaa kimya kama kawaida yae , hakujali watu walivyokuwa wakimfikiria.
Barabara kuelekea wanakoishi ilikuwa na msongamano sio wa kawaida hivyo gari ilikuwa ikisogea kidogo kidogo , Hamza hata yeye alionekana kuboreka kuendesha gari kwenye msongamano kama huo na aliishia kuangalia kioo cha nyuma kuona Regina anafanya nini.
Lakini Regina muda huo alikuwa akiangalia upande wa nje ya barabara huku akiwa na hali flani ya wasiwasi.
“Usiwe na mawazo hivyo , kwenye hii dunia usitegemee kupendwa na watu wote”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kushangaa.
“Nani ana mawazo , hebu endesha gari huko”
“Regina huoni tupo kwenye foleni , ila kwa tukio la leo kama ungekuwa mwigizaji ungekuwa maarufu
mno , wiki iliopita nilidhani ulikuwa katika mawazo kwa kuikosa Omega”
“Vipi … umekasirika kukuigizia?”
“Nikasirike , kwanini nikasirike?”Aliulia Hamza.
“Si ninekundanganya na wewe?”
“Kwannini swala hili linikasirishe , hili sio swala la kisheria kwamba lazima uniambie kila kitu , kucheza rafu sokoni ni swala la kawaida kwa wafanyabiashara, ijapokuwa watu wanaweza
kufikiria una roho ya kikatili , lakini yote umefanya kwa ajili ya kampuni , kama ningekuwa wewe pengine ningefanya hivyo hivyo, kama nilivyosema , huwezi kupendwa na watu wote kumbuka pia siku zote unapopata kitu jua unapoteza kitu”
“Na wewe unaamini hivyo?”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa.
“Ijapokuwa nimekudanganya mara kadhaa lakini hili namaanisha , ila siku nyingine Regina tukio kama hili likitokea ni kheri uniambie hata kwa siri sitowaambia watu, yaani nakuona una mawazo najaribu kukubembeleza kumbe napoteza nguvu zangu bure tu,itakuwa ni kujitia aibu tu”
“Sitaki unibembeleze , wewe ni nani kwangu mpaka unibembeleze , halafu kwanini nikuamini huwezi kutoa siri?”Aliongea Regina huku akikunja nne , lakini Hamza aliishia kucheka.
“Kwasababu mimi ni mpenzi wako , hivyo lazima unizingatie”
“Wewe sio mpenzi wangu , wewe ni mpenzi wangu wa maigizo tu , mpenzi wako ni huyo ulietoka nae out jana”Aliongea Regina kwa hasira.
“Kwahio vipi , nisipokuwa na mpenzi wewe utakubali kuwa mpenzi wangu , sidhani kama utakubali kutoka na mimi kimapenzi?”
“Nani kasema sitokubali”Aliongea lakini dakika hio hio alijua maneno yake hayakukaa sawa na kuulaumu mdomo wake kwa uropokaji , lakini jibu lile lilimshangaza Hamza.
“Regina kwahio unamaanisha unataka ku’date’ na mimi?”Aliuliza na kumfanya Regina kuona aibu kidogo.
“Kwannini unajiaminisha sana , ushawahi kuniuliza hilo swali?”
“Basi ngoja nikuulize sasa hivi , Regina je unataka tuwe wapenzi ki ukweli ukweli?”
“Mjinga wewe , Sitaki na sitotaka”Aliongea huku akimkodolea macho bila ya hisia.
Hamza alijikuta akikosa neno ,alijiambia ni kheri asingeuliza tu , maana jibu lilikuwa wazi.
“Hata mimi sitaki pia , kwanza nina mpenzi tayari na ni mpole na mchangafu kuliko wewe”Aliongea Hamza huku akionyesha furaha kabisa mara baada ya wazo la Eliza kumjia akilini .
Upande wa Regina ukauzu ulizidi kuonekana katika macho yake na aliishia kushika sketi yake kwa mikono yote miwili.
“Naona unamsifia sana huyo mpenzi wako , inaonyesha kabisa nimemzidi vitu vingi ndio maana unanilinganisha nae”
“Regina usiniambie unaona wivu , kwanini tokea jana nilipoanza kumzungumzia mpenzi wangu naona kuna kitu hakipo sawa kwako?”
“Nini, yaani mimi niwe na wivu na wewe , nimekuwa chizi , halafu ukiendelea kuongea ujinga wako sitokupa hata shilingi ya mshahara wako”
“Bosi usifanye hivyo , najua hunipendi lakini usinikate mshahara”Aliongea Hamza akijitetea.
Regina alikuwa na hasira sio ya kawaida kiasi kwamba kifua kilikuwa kikimpanda na kushuka , aliishia kuvuta mdomo na kisha akageuza kichwa chake na kuangalia nje.
Haikueleweka foleni ilisababishwa na nini , lakini muda ambao walifika nyumbani giza lishaingia tayari.
“Umeongea pumba zako kwenye gari mpaka umesababisha nimechelewa kufika nyumbani”Alilalamika Regina.
“Nunua gari lenye mabawa siku nyingine nitalipaisha , yaani unanilaumu kwa msongamano wa magari ambao sijausababisha”
“Ni makosa yako , ungetafuta njia nyingine, halafu usibishane bishane na mimi”
“Okey , samahani bosi kwa kukuchelewesha nyumbani na kukukwaza”Aliongea Hamza , hakuaka kuendelea kubishana na Regina juu ya swala hilo maana hata kosa lake hakuwa akilijua.
“Shangazi ni bora uwe unapika moja kwa moja na
kuendelea kula tu , usitusubiri ukiona tumechelewa”Aliongea Hamza.
“Nilijua mtachelewa sana , chakula cha kupasha sio kizuri ndio maana nachelewesha kupika , hii AC inapoozesha chakula kwa haraka, subirini kidogo nimalizie”Aliongea Shangazi huku akielekea jikoni.
Hamza hakutaka kusubiria chakula sebuleni na alienda jikoni pia .
“Shangazi unaonaje tukigawana upishi ili tumalize haraka, mimi nitatumia jiko la umeme”Aliongea Hamza na Regina aliekuwa amekaa kivivu sebuleni alishangaa baada ya kusikia kauli hio.
“Wewe unajua kupika?”
“Najua ndio , kwani kuna ugumu gani kupika?”
“Kwahio kumbe kila binadamu siku hizi ni mpishi?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kwa masikitiko.
“Ni hivyo tu sina mpango wa kuonyesha uwezo wangu leo hii , nina nyota tano za Michellin , likija swala la upishi”
“Michellin wanatoa nyota tatu tu za upishi , wewe hizo tano umezitolea wapi , unadhani wote sisi ni washamba?”Aliongea Regina akimkosoa.
“Natania tu , nilikuwa namaanisha ninao uwezo wa kuharakisha mapishi na yakawa ya kiwango”:Aliongea Hamza .
Shangazi alifurahi kuona amepata mtu wa kumsaidia hivyo alimwachia Hamza samaki aziunge.
Hamza mara baada ya kuanza kukatakata vitunguu na nyanya kwa spidi kali pamoja na mpangilio wake wa ki upishi jambo hilo lilimsahngaza Shangazi.
Ndani ya muda mfupi tu mboga saba zote zilikuwa zimeiva na kila kitu kilikuwa kipo kwenye meza.
Regina alijikuta akimeza mate kutokana na harufu nzuri ya chakula , mara baada ya kusogea mezani na kuangalia namna samaki alivyokatwa katwa katika vipande vya nyama , pamoja na namna ilivyopambwa na kachumbali kwa juu ilipendeza kwa macho.
“Regina , Hamza ni fundi mno kwenye upishi , mimi nashindwa kutumia jiko la umeme kukadiria moto lakini yeye ameweza na hakuna kilichoungua na chakula chake kinapendeza”Aliongea Shangazi kwa kusifia. “Shangazi chakuka kuonekana vizuri haimaanishi ni kitamu”Aliongea Regina na alichukua uma na kisha kuchukua kipande cha samaki na kupeleka mdomoni na kitendo cha kutafuta mara kadhaa muonekano wake ulibadilika mara moja.
“Haha ,, unaonaje , nishakuambia nina nyota tano”Aliongea Hamza kwa majisifu.
Regina aliishia kukosa neno la kuongea kwasababu radha ya hio samaki ilikuwa ni zaidi ya radha ambayo alikuwa akiipata kutoka kwenye chakula kinachopikwa na Shangazi.
Regina aliishia kujiambia kwanini huyu mwanaume kila kitu anajua , alijikuta akiishia kuchukia kwa kitendo cha Hamza kujua kila kitu.
“Regina kwa Hamza hapa nadhani sina wasiwasi hata nisipokuwepo baadae, hata kama usipojifunza kupika Hamza atakuwa yupo tayari kukusaidia”Aliongea Shangazi na mara baada ya kusikia kauli ile Regina alijikuta akiwa mwekundu.
“Shangazi kwanini unaongea hivyo”
“Nini , inamaana Regina hajui kupika , Shangazi huyu ukimuacha mwenyewe ataisha kula mayai ya kuchemsha au hotelini”
“Regina hata mayai ya kuchemsha hajui kabisa , anachojua ni kufanya biashara tu, nakumbuka alishawahi kuchemsha mayai mpaka maji yakakauka huku mayai yakipasuka na kubakia makasha tu”Aliongea shangazi na kuanza kucheka.
“Ili mradi hakuungua tu , inatosha”Aliongea Hamza.
“Nyamaza wewe , kwani kujua kupika ndio nini , nikiamua kujifunza nitaweza pia’”Aliongea Regina huku akiona aibu , ni kama anaona Hamza anamdharau kwa kutokujua kupika na kuonekana amekuzwa kimayai mayai.
“Regina usikasirike ni utani tu , hebu kaeni tule kwanza”Aliongea Shangazi lakini Regina alikuwa na hasira mno na kadri alivyokuwa akimwangalia Hamza ndio alivyokuwa akizidi kuchukia.
Muda huo huo simu ya Hamza iliita na alipangalia jina la mtu anaepiga ni Lau mfanyakazi wa Mgahawa wa Dina.
Hamza hakutaka Regina kusikia anachoongea hivyo alitoka nje na kupokea simu
“Lau vipi kuna tatizo?”
“Madam ameniambie nisikueleze , ila yupo kwenye matatizo makubwa”Aliongea Lau upande wapili akioyesha kuwa na wasiwasi.
 
Hello singanojr asante kwa mwendelezo wa story but naona unachanganya sana episode so kunakuwa na mkanganyiko, episode 35 umeirudia, then ikafuata 37......chini umeanza tena 37.....episode no. 36 iko wapi. Naomba link au untag sehemu ya 36 nianzie hapo, thanks!
 
Hello singanojr asante kwa mwendelezo wa story but naona unachanganya sana episode so kunakuwa na mkanganyiko, episode 35 umeirudia, then ikafuata 37......chini umeanza tena 37.....episode no. 36 imo wapi. Naomba link au untag sehemu ya 36 nianzie hapo, thanks!
Nimekosea kuname number tu ila mtiririko ni sahihi 36 ni 37
 
  • Thanks
Reactions: ram

Similar Discussions

Back
Top Bottom