inasikitisha sana"Makamanda nimetoka gereza la Keko jana Alhamisi Desemba 15, 2011 kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini bond ya shilingi milioni 5 na mdhamini mmoja kuweka rehani hati ya nyumba yake yenye thamani ya shilingi 42 milioni. Kwa sasa naomba tu niseme: "Wameniweka kizuini kwa zaidi ya wiki moja lakini mawazo yangu hawakuyazuia hata kwa dakika moja, wamenilaza kwenye mazingira magumu ya mateso lakini ubongo wangu hawakuugusa, wamedhoofisha mwili wangu kwa kiasi fulani lakini roho yangu ya ujasiri imeimarika maradufu" Samson Mwigamba, Desemba 16, 2011."
" Keko nilipokelewa kishujaa sana. Bahati nzuri niliingia na kombat kama ya kamanda wa anga. JIna langu kule lilikuwa "mwanaharakati". Nilipewa heshima kubwa na naweza kuwahakikishia kwamba nilikula ugali wa magereza siku mbili kwa maana ya siku ya Jumatano nikiwa rumande ya kituo kikuu cha polisi Dar na Alhamisi nilipoingia kwa mara ya kwanza gereza la Keko. Na siku hiyo ndo nililala 'mchongoma'. Kuanzia kesho yake Ijumaa ndo makamanda wengi zaidi wakagundua kwamba niko mle. KLewanza ambaye sitamsahau ni rafiki yake Nanyaro ambaye walifanya na Nanyaro kazi pale Leopard tours anaitwa Wilson William ambaye amekaa ndani ya gereza hilo akiwa mahabusu tangu mwaka 2008 hadi leo na nimemwacha na kesi haijaanza kusikilizwa. Yeye ndiye alinifanyia mpango kwa kijana ambaye ni kiongozi wa cell moja na ambaye alikuwa akigombea udiwani huko Ukonga wenzake wa CCM walipoona atashinda wakampa kesi ya wizi wa kutumia silaha. Yuko humo tokea Julai mwaka jana na kesi haijaanza kusikilizwa. Huyo kijana akanipangia mahali pa kulala kwa unafuu kidogo ambapo alinipa kigodoro changu peke yangu cha kama futi mbili hivi. Kuanzia hiyo Ijumaa nilikuwa nikiitwa na makundi mbalimbali kula kwao tokea chai hadi lunch ambapo tulikuwa tunakula wali wanaoletewa na ndugu zao. Ingawa gerezani ratiba ni kula mara moja kwa siku kwenye saa 9 mchana na uchi kiduchu asubuhi saa moja, lakini mimi nilikuwa nakula milo mitatu. Maana walikuwa wakitunza chakula na usiku tukiwa ndani ya cell wananiita nakula nao. Mengi zaidi nitayasimulia kupitia makala zangu. Msikose."
tukumbushane kidogo. Huyu mwigamba ni nani tena?
hivi ban maximam siku ngapi mods,maana nilifikiri kumpa jibu huyu jamaa,anatuzuga tumkumbushe wakati jana alipishana naye mlangoni akitokea master bedroom!!!!
mwigamba ni nani, sio wote tunamjua.
"Makamanda nimetoka gereza la Keko jana Alhamisi Desemba 15, 2011 kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini bond ya shilingi milioni 5 na mdhamini mmoja kuweka rehani hati ya nyumba yake yenye thamani ya shilingi 42 milioni. Kwa sasa naomba tu niseme: "Wameniweka kizuini kwa zaidi ya wiki moja lakini mawazo yangu hawakuyazuia hata kwa dakika moja, wamenilaza kwenye mazingira magumu ya mateso lakini ubongo wangu hawakuugusa, wamedhoofisha mwili wangu kwa kiasi fulani lakini roho yangu ya ujasiri imeimarika maradufu" Samson Mwigamba, Desemba 16, 2011."
" Keko nilipokelewa kishujaa sana. Bahati nzuri niliingia na kombat kama ya kamanda wa anga. JIna langu kule lilikuwa "mwanaharakati". Nilipewa heshima kubwa na naweza kuwahakikishia kwamba nilikula ugali wa magereza siku mbili kwa maana ya siku ya Jumatano nikiwa rumande ya kituo kikuu cha polisi Dar na Alhamisi nilipoingia kwa mara ya kwanza gereza la Keko. Na siku hiyo ndo nililala 'mchongoma'. Kuanzia kesho yake Ijumaa ndo makamanda wengi zaidi wakagundua kwamba niko mle. KLewanza ambaye sitamsahau ni rafiki yake Nanyaro ambaye walifanya na Nanyaro kazi pale Leopard tours anaitwa Wilson William ambaye amekaa ndani ya gereza hilo akiwa mahabusu tangu mwaka 2008 hadi leo na nimemwacha na kesi haijaanza kusikilizwa. Yeye ndiye alinifanyia mpango kwa kijana ambaye ni kiongozi wa cell moja na ambaye alikuwa akigombea udiwani huko Ukonga wenzake wa CCM walipoona atashinda wakampa kesi ya wizi wa kutumia silaha. Yuko humo tokea Julai mwaka jana na kesi haijaanza kusikilizwa. Huyo kijana akanipangia mahali pa kulala kwa unafuu kidogo ambapo alinipa kigodoro changu peke yangu cha kama futi mbili hivi. Kuanzia hiyo Ijumaa nilikuwa nikiitwa na makundi mbalimbali kula kwao tokea chai hadi lunch ambapo tulikuwa tunakula wali wanaoletewa na ndugu zao. Ingawa gerezani ratiba ni kula mara moja kwa siku kwenye saa 9 mchana na uchi kiduchu asubuhi saa moja, lakini mimi nilikuwa nakula milo mitatu. Maana walikuwa wakitunza chakula na usiku tukiwa ndani ya cell wananiita nakula nao. Mengi zaidi nitayasimulia kupitia makala zangu. Msikose."
Vipi hawajakufanyia ule mchezo wao!..
acha hasira mkuu utapasuka. Sijakuuliza wewe unaanza kuropoka.
Yaani ulichokiona uko ni huo mlo wa kutwa mara 3?