Xav Emmanuel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 214
- 315
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (01)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
----------------------------------------------------- - -
SEHEMU YA KWANZA
Kelele za hapa na pale ziliendelea kusikika katika kila kona ya baa, hakukuwa na usikilizano kati ya sauti za binadamu na sauti za vifaa vya umeme vilivyoendelea kuburudisha mule ndani. Mwenye sauti nyembamba alisikika, nene ilisikika itaachaje sauti ya kukoroma sasa!. Hakukuwa na kiongozi yeyote mwenye kukeleekwa na kelele hizo, na hakuna aliyethubutu kuchukulia hatua suala hilo, kila mtu alikuwa huru na mambo yake.
Mimi nilikaa karibu na mlango wa kuingia na kutoka nje ili iwe rahisi kutoka pindi nimalizapo kinywaji changu.
Sikuwa mlevi wa kupindukia kuogopa kuchafua sare za kazi yangu. Nilipenda sana kazi yangu, kwani inahitaji mtu wa heshima, mtu ambaye hana chembe ya skendo.
Nilikuwa maridadi kuangaza kila kona ya upande kuona kama kuna tukio nzito naweza kulipata ili kesho liangukie katika vichwa vya habari vya magazeti. Niliambulia tu kuona watu wakiingia na kutoka wengine wakishikana mashati na kuachana, wengine wakikumbatiana na kuachana, wengine walitokomea nisikokujua. Kweli baa ni baani...
Zilinichukua takribani dakika saba kusikia vishindo vya wababe wakiingia ndani ya baa hiyo, niliwapokea na kuwasindikiza kwa macho hadi walipokaa. Hakuna alieagiza kitu chochote kile kati yao, zaidi walikuwa wakilaumiana sana, huku mmoja aliyejaa misuli iliyoshiba akikunja sura na kurusha mikono huku na kule kama mtu aliyechoshwa na tabia mbaya za wenzake.
Wanasema “kiburi ni mwanzo wa kifo” hivyo nikaona vyema kuondoka sehemu ile kabla mambo hayajawa mambo: niliogopa kwa ujio wao. Taratibu nikachukua kinywaji changu na kukimiminia mdomoni, nilivyoshusha tayari kilikuwa kimeisha, nikaangaza kopo kwa sekunde kama mbili hivi kwa kukagua kama kweli nilikuwa nimemaliza. Macho yangu yalithibitisha mwisho wa kimiminika kile, mara baada ya kukutana na maandishi tu ya lebo ya kinywaji kile “Fanta”. Nikasoma na kuliacha kopo ilo taratibu na kutoka ndani ya baa ile.
Nikatoka nje na kuangaza kila kona ya baa hiyo. Mikono ilikuwa kiunoni na mdomo ukiwa unaendelea kufuta tamu ya mwisho ya soda niliyotoka kuburudika nayo. Macho yangu yakapambana na bango kubwa la baa hiyo lililopo mbele kabisa jirani na mlango wa kutokea; “La Charz Bar” nilijisomea kimoyomoyo huku nikiangaza kuitafuta njia ya kwenda nyumbani. Nilikuwa sina mwendo wa haraka sababu ya kuwa bado ilikuwa ni mapema.
“Saa mbili kasoro! Aagh! Bado ni mapema mno. Daladala zipo chungu nzima”. Basi niliendelea na mwendo wangu wa maringo kama kinyonga katika mti aupendae.
Kichochoro nilichokuwa napita kilikuwa kimya kiasi na kupisha sauti za pikipiki na magari zikirindima mita chache katika eneo la barabara kuu. Nilisikia tu mihemo ya matairi ya magari hayo katika ngoma za masikio angali bado nipo vichochoroni kuitafuta njia kuu.
Kagiza ambako kanaanza kushonana tayari kalianza kuonesha udhaifu wa mji huu wa Songea, watu wanalala mapema sana. Nikazipiga hatua za haraka haraka kuhofu ukimya wa mtaa huo.
Toka nilipo na baa ilipo, ni umbali mchache sana kutoka eneo kuu la barabara. Nilikua napenda sana kuhudhuria baa hiyo kwani ni moja ya baa kubwa Songea Mjini, hakuna aina ya watu wanaokosekana sehemu hiyo. Kwa kazi yangu ya Mwanahabari ni pahali panapofaa kuchukua matukio ya siku, kwa maana ‘penye miti mingi hapakosi wajenzi’.
Wakati nafanya jitihada za kuchepukia katika barabara kuu, nilipokea onyo la mtetemeko wa kitu kama ndoo hivi likianguka!, “Alaah!!” nikagutuka mwenyewe na kusimama wima. Mlio niliousikia ni ule wa ndoo la takataka ambalo limeanguka. Woga wa mapema ukanikamata.
“Nani kaangusha?!!.., panya, paka..... anha panya.... No!!, mlio ni mkubwa, Mbwa!, Yes! Mbwa” nilianza kuhisi kwa kutaja kitu ambacho kinaweza kuwa na nguvu za kuangusha ndoo hilo lenye uchafu. Hayo yote yaliendelea kuongelewa moyoni.
Nikatoa hatua moja kuelekea mbele lakini nilisikia tena vishindo. Kwa sasa vilikuwa ni vishondo vya binadamu ambao walikuwa kasi kupita maelezo. Na walikuwa nyuma yangu kutokea upande ambao ipo baa niliotoka. Nikahofu kukumbana na vibaka muda ule takatifu, nikasogea pembeni kupata sehemu ya kujibanza. Nikajificha kuwaruhusu kwanza wao wapite.
“Deo! Umeona unavyozungua mwanangu?, Unazingua wewe, unazingua. Mi nakuambia ukweli. Wapi sasa?, wapi unadhani tunampata?” mmoja ya vijana wanne aliongea kwa uchungu kuwageukia wenzake.
Walipofika eneo ambalo nipo karibu nimejificha walisimama kwa mda kupisha malalamiko yachukue nafasi. Nilizikumbuka sura zile vizuri kwani ndizo nilizokutana nazo kule baa. Nikaendelea kujibanza sehemu wasije niunganisha bure katika harakati zao. Jambo jema kulikuwa na mwanga usiolidhisha eneo hilo. Ulikuwa unawaka kwa hafifu sana.
“Sikia mzee!, hana pa kwenda, Yule chapu tu yani paap!. Yule!, Yule haoni! Sema kuna sehemu kajificha tu. Hapa hatuna namna tuvamie kila kona bosi hawezi elewa mzee!.” Mwingine ambaye alikuwa hana mwili wa kutisha aliongea. Ilionekana wanamtafuta mtu ambaye kwa makosa yao amewatoroka. Walipewa kazi ya kumshikilia.
“Daaah! tumefanya kosa sana kutokuwa karibu nae, kwa sasa akiingia mikoni mwangu mimi, hakuna cha bosi, namaliza mchezo, kwa bosi napeleka macho tu kama ushaidi, yaani... alaaaah. Shit!” mwingine ambaye yeye alionekana kupagawa kabisa aliongea.
Huyu wa mwisho alikua na umbo la miraba minne ambalo alitosha kabisa kuingia katika masumbwi na kupigana kwa niaba ya taifa. Umbo lake ni kama huyu baunsa wa rahisi mmoja hivi nchi jirani hapa!.
Nani huyu! Aagh! Ni maharufu sana yani sema basi tu jina lake limenitoka. Jamaa huyo ulikuwa na ghadhabu zilizomfanya kuvua hadi shati na kuegeza begani. Niliendelea kushudia malumbano yao huku wakijongea taratibu sehemu niliyojificha. Wakasimama tena.
“Tusitembee kizembe sasa, tuwe tunaangalie hata huku ukutani, kwa jinsi nilivyo na hasira mwanangu.... Me ntaekutana nae tu mda hu, naosha dadeki!.” Kauli, kauli mzee, chunga kauli yako. Kijana wa kwanza Aliongea kauli mbavu ambayo ilinigusa hasa.
Kwani mimi ni mmoja kati watu ambao nipo maeneo hayo. Kwa vipi wangeniona?. Lakini nashukuru walipita salama. Walikagua eneo lililofuata baada ya nilipojificha mimi Walipita na kuenda zao nikawa nahakikisha tu kwa macho kama wamesongea mbali nami niokoze karoho kangu kepesi kuelekea makwangu..
Nikaanza kujikwamua toka pale nilipo huku mkono wangu ukiambaa kati ya moja ya mfuko wangu wa nyuma kuangalia kifaa chochote ninacho weza tumia kufutia jasho na kamasi. Pumzi ndefu ikafuata kukaribisha kuanza tena hatua mpya.
Nikajipanga kupiga hatua lakini wanasema ‘safari ya kifo haikosi maangaiko’. Pale pale nilipo zilisika pumzi za mtu mwingine, zilikuwa ndefu kipita za kwangu, kama ulishawai angalia kionjo chochote yeyote kile cha mchekeshaji maarufu wa kipindi hicho aitwae “Charles Champline” nadhani unajua kwa jinsi alivyo mwepesi wa mwili; usiombe atimue mbio, aisee mtapotezana.
Nilijisikia mtu ambaye napaswa kutoa kila aina ya haja sio ndogo tu, hadi kubwa. Nikahisi siku hiyo imekuwa mbaya kwangu. Mikosi imeniandama. Wepesi wa mwili wangu haukuwa tatizo kunifanya niweze kutimua mbio mahali pale, nilijikuta ganzi imenishika ghafla na mwili kusisimka. Nikaganda kusubiri hukumu na kuacha moyo uendelee tu kudunduliza mapigo ya mwisho mwisho.
ITENDELEA...
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (02)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: Xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
Social Net: @star_xav

Nikajipanga kupiga hatua lakini wanasema ‘safari ya kifo haikosi maangaiko’. Pale pale nilipo zilisika pumzi za mtu mwingine, zilikuwa ndefu kipita za kwangu, kama ulishawai angalia kionjo chochote yeyote kile cha mchekeshaji maarufu wa kipindi hicho aitwae “Charles Champline” nadhani unajua kwa jinsi alivyo mwepesi wa mwili; usiombe atimue mbio, aisee mtapotezana. Nilijisikia mtu ambaye napaswa kutoa kila aina ya haja sio ndogo tu, hadi kubwa. Nikahisi siku hiyo imekuwa mbaya kwangu. Mikosi imeniandama. Wepesi wa mwili wangu haukuwa tatizo kunifanya niweze kutimua mbio mahali pale, nilijikuta ganzi imenishika ghafla na mwili kusisimka. Nikaganda kusubiri hukumu na kuacha moyo uendelee tu kudunduliza mapigo ya mwisho mwisho.
ENDELEA SEHEMU YA PILI
“Kaka... Dada,... ewe mtu uliopo mbele yangu, tafadhali!!!. Tafadhali naomba msaada wako. Mimi mtu mwema tu. Wananitafuta!!, ndugu yangu naomba nitazame mara kwa mara kabla hujaniacha mwenyewe maeneo haya. Sijui hata nilipo ndugu. Nakuomba”. Maneno mageni ya mtu nisiye mfahamu yakagonga kwenye ngoma za masikio yangu. Nikawa tayari kama askari kanzu lindoni. Hofu ya kutambua nani anaongea na mimi ilinijia.
“Inamaana bado hajanijua e!” nilijisemea kwa moyo baada ya kusikia kwa masikio yangu mawili kuwa alikua anabashiri nani yupo karibu yake, maana alianza na dada akamaliza na kaka.
Likaja wazo lingine na kuongeza kwenye mawazo yangu mengine ya mwanzo, wazo hilo jipya ndiyo lilinikumbusha kuwa kweli kuna mtu anatafutwa. Tena anatafutwa haswa!, nimsaidie?, hmmm wakijua?. Nimwache! Afu nikimwacha hii dhambi itakuwa ya nani? Bila shaka ni yangu. Naogopa dhambi kuliko lawama. Nikaamua liwalo na liwe nikageuka.
“Ndugu yangu nipo hapa, nakuomba tafadhali, nakuomba wema wako wa leo tu unanisubiri mimi ili nisipotee. Nakuomba tafadhali....” sauti ya sasa ilikuwa ni ya machozi ambayo inakalibiana na kwikwi ili vitoke kwa pamoja, sikuthubutu kwenda mbele, nikageuka nyuma na kuangaza mtu huyo ambaye ni adimu kwa macho ya watu wanne waliotangulia wakimtafuta.
“We.. we ni nani?” nikahofu kwa kuuliza. Lakini mtu yule hakujubu zaidi ya kupapasa tu ukuta na kujitokeza kando ya giza alipojificha. Mtaa huo ulikuwa na taa chache sana kutokana na nyumba nyingi kutowasha au kutoweka taa kabisa za nje, kwani ukiweka usiku taa basi asubuhi huikuti. Imekwenda na maji.
“Ni mimi kaka!, mi..mi... nakuomba nisaidie nitoke hapa, nitakueleza zaidi huko mbele, nakuomba kaka angu. Usiniuze tena nakuomba?”. Aliongea kwa msisitizo. Inaonekana tulijificha sehemu moja lakini sikumuona. Nikabaki natafakari tu neno lake la usiniuze tena. Ina maana aliuzwa?. Maswali kedekede yakaandama kichwa changu.
“Kukuuza tena?” Nilihoji.
“Ah nisaidie kaka, watanikuta hapa” aliongea tena kwa hisia. Nikaamua kuchukua uamuzi wa kutoa msaada kwake, kwani hata katika sekta niliyopo niliona ni bora kutoa msaada na nisingeweza katu kumwacha mtu huyo akiangaika na kutokomezwa pasipo julikana.
“Aya njoo sogea!” nilitoa amri kuonesha ukali ili kama ulikuwa ni mpango wa kuniangamiza mimi basi apatwe na woga.
Kijana huyo alijitokeza kwa kupapasa tena ukuta kisha kusogea hatua chache na kusimama, aliinua mikono yake kama anamtafuta mtu hivi, dalili zote za kuonesha kwamba ni kipofu zikaonekana. Roho ya huruma ikanivaa na kunishinikiza kudondosha chozi. Lakini nilikomaa.
“Oh pole.. Kwa hapa, ah. Taratibu e!” nikamshika na kumsaidia kutoka pale. Roho iliniuma sana kuona mtu mwenye tatizo kama lile na bado anaangaika. Alikuwa kipofu mtu yule.
Wazo la mwanzo la kupanda daladala likayeyuka. kwani tungeweza kuonwa kwa haraka zaidi na wanao mtafuta. Tukajongea kwa haraka huku hisia na macho yangu zote zikiwa wazi kusikiliza nini kitatokea nikiwa bado barabarani. Uzuri hatukuwa katika sehemu ambayo inatisha sana, kwani kuchepuka tu tukakutana na dereva pikipiki akisubili pesa yake ya kukeshea kilabuni.
“Elfuu na mia tano, tupo wawili, Msamala”. Niliongea vile kwa kutotaka kupoteza muda, kwani nauli ni elfu moja kwa mtu mmoja kwa umbali niliotaja. Pesa niliyotaja haikuwa na mjadala kwa watu wawili kwenye chombo kimoja.
-----------
Nilifika nyumbani na kupokelewa na mke wangu ambaye toka naingia alikuwa ananiangalia tu kama mtu mwenye hasira. Hakujali sana uwepo wa mgeni niliye mbeba siku hiyo. Baada ya kumweka mgeni wangu kwenye kochi, mke wangu alipatwa na hekima ya kunivutia kando kunihoji.
“Mume wangu!, We si hata mwezi tu haujaisha toka tumalize kesi ya kupigana?!, Umepigana tena?”. Aliuliza mke wangu bila kusubiri hata dakika ipite.
“Hhahahahahahahaha..” baaada ya kujibu swali la huzuni kutoka kwa mke wangu nikajikuta nacheka kupita kipimo hadi nikajistukia na kuziba mdomo. Sikutegemea kabisa maneno kama yale. Huzuni yangu ikakimbia mbali na kuruhusu furaha kutoka kwa mke wangu.
“Ebu mwandalie chakula mgeni na maji ya kuoga. Tutaongea!!”, niliagiza huku nikitoa mkono wangu mdomoni baada ya kumaliza kucheka.
Mke wangu alijua nimefanya vurugu mara baada ya kuona shati langu jeupe limetapakaa tandu za buibui na uchafu kila pande. Na huo ulikuwa sio mwonekano wangu wa kila siku, hivyo akapata hofu na kutumia hekima ya kunitoa chemba kumaliza shauku yake. Nikapotezea swali lake na kuelekea nilikomwacha mgeni wangu. Alibaki kunishangaa tu kwa kutikisa kichwa huku mikono yake akishikilia kiuno.
“Pole sana!, unajisikiaje?” nilimuuliza mgeni yule huku nikimtazama kwa makini.
“Ndugu yangu najiskia tu ni katika dunia salama kabisa. Hisia zangu zinaniongoza kukuongezea thawabu zangu zote kwako. Sitaki kufa mimi, sitaki kufa kabisa, sitaki kufa nakuambia! hadi nilichonacho kifike sehemu husika. Baada ya kufika basi nitakufa lakini dunia lazima ijifunze..”. aliongea bila kupepesa maneno hadi nilianza kupagawa kwa kuzitazama hisia za mgeni wangu. Nikataka kujua kila kitu kilichomsibu. Kwa maneno yake hayo machache yalinijulisha kuwa anamengi ya kuhadithia dunia. Nikabaki kuduwaa.
“Kuwa huru! Upo sehemu salama. Kuna tatizo gani kwani? Wanakudai?”. Nilijikakamua kuhoji nipate mkanda kamili.
“Nani!!?, Nani anidai.. Mimi?!, na wananidai nini?, eeh! ndio labla! Labda kweli wananidai!. Nakuomba nisaidie haraka nitue huu mzigo nilionao. Unaniumiza. Unanitesa. Wananidai uhai. Uhai ni wangu lakini wananidai. Wanataka waniue!!” safari hii mgeni wangu alianza kulia kwa nguvu hadi mke wangu aliyekuwa mbali mda wote akitushangaa akasogea.
“Kwani kuna nini baba?” mke wangu akanigeukia na kunitwanga swali lingine ambalo nalo lilipita hewani kama lile la mwanzo bila kujibiwa. Ningejibu nini wakati hata mimi sifahamu chochote?.
“Loh! Pole sana. Tutaelekea polisi kesho kutoa taarifa kwa usalama zaidi!” nilimpa pole mgeni wangu kwa shida iliyompata. Sikuwa na habari na mke wangu, wala kuangaika kujibu swali lake.
“Polisi?, Ndugu yangu umesema Polisi e? Loh! Polisi!, polisi!, polisi!!... Hapana walewale tu. Nimeenda zaidi ya neno nimeenda. Lakini napelekwa kubaya kulekule nilikotoka. Wametapakaa kila sehemu wabaya wangu, hadi kwa viongozi wa dini” mgeni huyo bado aliendelea kunichanganya kwa vitu mbalimbali alivyokuwa anagusia.......
ITAENDELEA..
Sent using Jamii Forums mobile app