Simu za Google Pixel zina shida gani?

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,485
3,134
Wadau wiki mbili zilizopita, dada mmoja, simu ya google pixel 4 ilizima ghafla, akaipeleka aliponunua China plaza.

Walipompeleka kwa fundi, fundi akamwambia anazo zingine 2 nazo zimezima ghafla, wanajaribu kupasha motherboard kwa masaa 24 labda zitawaka.

Juzi rafiki yangu, google pixel 7, haina hata miezi 5 tangu anunue 700,000/ Kariakoo, imezima ghafla, leo amepeleka aliponunua, eti motherboard imekufa, kulikuwa na ambayo imekufa kioo, kwa hiyo wamebadilisha motherboard ndo imewaka hizi simu zina shida gani wataalam!.
 
Shida sio simu tatizo ni TBS, Tanzania sasa hivi ni dampo la vifaa vya electronics fake na vyakula visivyo ba ubora.
Na mbaya zaidi zaidi ya 99% ya watanzania hatuna ujuzi na mambo ya electronics ndio kabisa.

Nchi ya hovyo sana hii,hamna control kabisa-wafanyabishara wanafanya wanacho taka ili mradi wanapata faida.
 
Mkuu umeenda kabisa kununua simu china plaza bila kuwa na idea au pakoje? Pale bila kubonyezwa unapigwa nje nje hizi simu.

Ni sawa na Makumbusho tu pale huwa napaona hivo. Umenikumbusha mdogo wangu alivopigwa Makumbusho, kipindi hiyo J7 ndio zimeingia, kaja nduki na box lake jipyaa, kuchaji imechaji fresh tu kuiwasha aisee simu inachemka kama inapikwa.
 
Na pixel 3a hapa toka July 2021 ipo poa tu nilinunua huko huko kariakoo kipind hazijazagaa

Hii miaka miwili iliyopita viduka uchwara vya simu vimekua ving sana hapa mjin nakushauri ukitaka simu jichanhe ununue mpya...

Simu used zilikua reliable before 2022
 
Wadau wiki mbili zilizopita,dada mmoja, simu ya google pixel 4 ilizima ghafla, akaipeleka aliponunua china plaza.

Walipo mpeleka kwa fundi, fundi akamwambia anazo zingine 2 nazo zimezima ghafla, wanajaribu kupasha motherboard kwa masaa 24 labda zitawaka...
Natumia Pixel tangu 2021 mpaka sasa 2024 haujawahi kuzima wala motherboard kufanya nini umewahi kuingia kwenye maji mara 3 haujafa chochote ishanyeshewa na mvua na haujawahi kuchemka battery unakaa na chaji vizuri tu, shida ya Pixel ni moja tu ukipiga picha ukazoom to 100% inakua na ukungu ukungu kitu ambacho sikupendi Ila vingine vyote IPO sawa
 
Wadau wiki mbili zilizopita,dada mmoja, simu ya google pixel 4 ilizima ghafla, akaipeleka aliponunua china plaza.

Walipo mpeleka kwa fundi, fundi akamwambia anazo zingine 2 nazo zimezima ghafla, wanajaribu kupasha motherboard kwa masaa 24 labda zitawaka...

Hao walionunua hizo simu sio kwamba walinunua zile "used from Dubai"?
 
Back
Top Bottom