Simba yangu kinachoniuma tunautaka utamu halafu tunautafuta kulee?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,129
7,898
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeipigania sana Simba huku mitandaoni ila ikafika wakati nikaamua kupumzika maana kuna mambo yanakatisha tamaa sana ndani ya Simba yangu.

Simba ina wachezaji bora sana shida ni jinsi wanavyotumika. Kuna mentality inabidi ibadilishwe pale kuanzia kwa viongozi fulani, hadi baadhi ya wachezaji. Inaonyesha hakuna spirit ya teamwork pale Simba, kila mtu anajiangalia yeye kama yeye kwanza. Kukaa benchi au kuanzia nje, kuna wachezaji wanaona kama watadharaulika. Kuna approach ambayo Yanga wameichukua inawasaidia sana. Kwa mfano upande wa mabeki, wamewachukua wachezaji wanaopendana sana na wengine wanaotoka sehemu moja. Hii inawafanya hali yote ya husda, au kuharibiana kwa njia za ajabu ajabu isiwepo. Na inachowasaidia zaidi, kila mtu anapewa fursa ya kucheza.

Mimi nikimuangalia Chilunda najiuliza huyu anakosa hata mechi moja ya ushindani na kupewa dakika 15, kweli? Hivi Phiri amekuwa mchezaji wa kuingia dakika za nyongeza, kweli? Kuna wakati kisingizio kilikuwa bado hajapona, sasa hivi kisingizio ni nini? Achana na rekodi za zamani alipoingia Simba akawa anaibeba Simba katika mabega yake hadi kuingia makundi, angalia aliporudi baada ya majeraha, hata alipokuwa anapewa vidakika vichache, kuna mechi muhimu sana kwa mfululizo yeye ndiyo alikuwa anatoa assist za magoli muhimu. Angalia sasa, mechi ngapi muhimu ambazo anaingizwa vidakika vya mwisho na bado yeye anakuwa mwokozi wa timu lakini hayo yote hayawashtua hao wanaopanga timu? Nitaingia katika maombi maalumu Phiri aende Yanga na siku tukikutana nao watuchakaze vibaya sana.

Hivi kweli wenye mamlaka ya hii timu wanaitakia mema hii timu? Simba imekuwa na baadhi ya wachezaji walevi, wahuni, wakorofi na walikuwa hawasugui benchi. Hakuna anayeamini Phiri ana sifa zozote mbaya kustahili kusugua benchi. Alishaprove uwezo wake na wote tunaujua. Sasa unamuacha anasugua benchi kwa sababu zisizoeeleweka, eti visingizio kuwa hakabi, eti siyo mrefu, hao wanaopangwa badala yake wanajigonga gonga tu uwanjani, mechi inaanza hadi anatolewa hajapiga pasi hata moja, hayawin hata mpira mmoja wa juu au wa 50/50. Ninavyoamini mimi, kama mechi inahitaji kuongeza mchezaji mkabaji, viungo ndiyo wachezaji sahihi wa kujaza siyo striker tena ambaye siku zake zimeisha kitambo. Mchezaji anapangwa ili tu aotee kagoli kamoja wapate nafasi ya kutunanga tunaokosoa maamuzi yao.

Na nyie mnaotetea ujinga unaoendelea tunajua mnalinda maslahi yenu yanayotokana na ukaribu mlionao na timu na viongozi ila ukweli wote tunauona. Kuna msemo wa kilatini unaosema "Vox populi, vox Dei", yaani "sauti ya watu ni sauti ya Mungu". Wengi tunayasema haya na tunayasema kwa kuwa ndiyo ukweli wa nafsi zetu, nyie mnaongea ukweli wa matumbo yenu. Haya mambo ya kuishia njiani kila msimu ni matokeo ya kujitakia tu. Wiki hii nimeshuhudia wanasimba wengi wanaangalia mechi zake kwa unyonge sana maana wanajua uwezo wa timu na wanaona kabisa inakwama wapi. Wengi wanasononeka na kulalamika kwa sauti ya chini ili wasionekane wanaleta chokochoko au hawataki kuwapa mtaji upande wa pili. Wengine tulishayaona haya yanakuja ndiyo maana tulishaanza kukaa pembeni ili mioyo yetu isiumie. Na tusipojirekebisha na kuacha mapuuza haya group stage safari hii hatuvuki, hatutakuwa tena mwakarobo tutakuwa mwakakundi hadi tutakapojielewa.

Hii naweza kulinganisha na suala la utamu, yaani unataka utamu wa asali, halafu unaenda kuutafuta kwa kitu kichungu. Unataka utamu halafu unaenda kuutafuta kwenye sehemu isiyo safi. Kuna uzi nilileta mwanzoni mwa msimu nikisema Yanga watakuwa na mafanikio bora msimu huu kimataifa kuliko Simba na hizi ndiyo sababu zilizopelekea kusema hayo.

Tukisema haya wanasema tuna chuki binafsi, je hao wanaosugua benchi wakati uwezo wao tunaujua tusemeje?
 
NILIWAAMBIA MAPEMA KUWA MJIAMDAE KISAIKOLOJIA.

MICHEZO MINNE YA KIMATAIFA USHINDI 0
CAFCL 2 ushindi 0
AFL. 2 ushindi 0

KWENYE NBC PLEMIER LEAGUE PAPATU PAPATU NA AKINA TATU WANATUOKOA.

VIONGOZI WENU ni wabishi sana kupokea ushauri.

Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeipigania sana Simba huku mitandaoni ila ikafika wakati nikaamua kupumzika maana kuna mambo yanakatisha tamaa sana ndani ya Simba yangu.

Tukisema haya wanasema tuna chuki binafsi, je hao wanaosugua benchi wakati uwezo wao tunaujua tusemeje?
Pole mtani
 
Ukweli Simba Kuna ujinga, tuna wachezaji wazuri lakini kocha anaacha kuwatumia. Kuna wachezaji Kila mechi wanapangwa hata walijaribu mechi ijayo wanaanza. Wachezaji wengi hawajitumi na sababu wameshajua namba zile Zina watu. Usajili huwa ni bahati nasibu lakini kwa Simba ni uzembe, Kramo kasajiliwa bila kupimwa afya, kipa wa Brazil.

Kabla ya kusajili kipa toka nje wengi tulipinga lakini viongozi walijiona wajuaji kumbe wanakula ten percent za usajili. Simba isiyo na pesa ilisajili kwa kuangalia nahitaji ya timu Ila hii inayojifanya Ina pesa usajili ni ovyo kabisa.

Hivi Ally Salim ndio kipa wa kudaka Simba mechi kubwa, hivi tumeshindwa kutafuta wabadala wa mabeki was pembeni. Hivi Boko na Saidoo kwa umri wao wanaweza kutupa ubingwa was Afrika?
 
Umeandika Vizuri sana

Lakini Moses phiri ni No 10

Tangu Enzi za Zolan Mark
Hata Robertinho Hawa ni Professionala Coach wote wanamuweka Benchi.

Phiri ni Mshambuliaji WA pili
(Second straiker)
Au force No 9
Uwe na mshambuliaji kamili kama Baleke ALAFU uende na Phiri HAIWEZEKANI.

UDHAIFU WAKE.
1. Anapoteza sana Mipira.
2. Hawezi ku Link up team kutoka chini.
3. Hawezi kuwa Target man.
4. Anakuwa Off position ya No 10.
5.Mfupi WA kimo nk.
6.Anaanguka anguka sana.
7. Huwa anapoteana kwenye michezo mikubwa eg wakati WA Mgunda alicheza na Yanga
1-1 Azizi ki na Okrah. Hakuonekana hata dk 1

8. Majeraha ya mara kwa mara.

NB.
NILIWAAMBIA mchezaji mzuri Huwa HAUMII (si injury prone otherwise Afanyiwe Upasuaji unaomuweka Nje muda mrefu?)
Phiri anasinhizia majeraha

UIMARA.
1.Analijua sana Goli
2. Kasi.
3. Uwezo WA kutumia Miguu yote.

Phiri si MCHEZAJI MZURI.
Kama Ningekuwa kamati ya UFUNDI ama usajili Moja ya Wachezaji wa Kupunguzwa ni Moses phili.

NIKIONA mtu anamtetea Phili najua huyo mtu hajuhi Mpira.
Wajuzi wa mpira wa bongo utawajua tu.
Force no 9 ndiyo False Number 9 ?
 
Wajuzi wa mpira wa bongo utawajua tu.
Force no 9 ndiyo False Number 9 ?

ANDIKO Bora limetukuka kiufundi
Ukaona spelling ndio sehemu pekee ukosoe.

Hoji mambo ya maana ya kiufundi, na si Typing Error.

WENZIO wanafaidi na kuiba KUONDOKA na haya MAARIFA yanayotolewa na Mimi nakuwafowardia wachambuzi wenu, wewe umekomaa na spellings

FICHA UPUMBAVU WAKO NA UFIKICHE AKILI

Pathetic shame
 
Mkuu naomba kuuliza utamtambuaje false #9 kimajukumu yake uwanjani?
Kazi yake nini?
Namtofautishaje na natural #9?
Second striker, #10 na false #9 ni kitu au mtu mmoja kimajukumu?

Note: Sijui soccer na sijacheza popote hata kiwango cha ligi daraja la chini kabisa.
 
Umeandika Vizuri sana

BINAFSI MIJITU INAYONIBOA ZAIDI NI WATETEZI WA MOSES PHIRI

Tangu Enzi za Zolan Mark
Hata Robertinho.
Hawa ni Professional Coaches wote wanamuweka Benchi.

(Jiulize kwanini MAKOCHA wote wawili wakuweke Benchi).

Phiri ni Mshambuliaji WA pili
(Second straiker)
Au false No 9
Uwe na mshambuliaji kamili kama Baleke HALAFU uende na Phiri hili halikubaliki na HAIWEZEKANI.

UDHAIFU WAKE.
1. Anapoteza sana Mipira.
2. Hawezi ku Link up team kutoka chini.
3. Hafai kuwa hata Target man.
4. Anakuwa Off position ya No 10.
5.Mfupi WA kimo na Hana low center of gravity Compare to Saido, KIBU Miquissone na mzamiru.

6.Anaanguka kupita kiasi na ni mwepesi.

7. Huwa anapoteana kwenye michezo mikubwa eg wakati WA Mgunda alicheza Simba na Yanga Ya 1-1 wafungaji Azizi ki na Okrah. Hakuonekana hata kwa Dakika 1

8. Majeraha ya mara kwa mara.

NB.
NILIWAAMBIA mchezaji mzuri Huwa HAUMII (si injury prone otherwise Afanyiwe Upasuaji utakao muweka Nje kwa muda mrefu?)
Phiri anasingizia majeraha tu

UIMARA.
1.Analijua sana Goli
2. Kasi.
3. Uwezo WA kutumia Miguu yote.

JUZI kaingia Dk 89
Anapata kigugumizi na Kutaka kuichomesha Simba mbele ya Alahly.

Phiri si MCHEZAJI MZURI.
Kama Ningukuwa kwenye kamati ya UFUNDI ama usajili, Moja ya Wachezaji wa Kupunguzwa ni Moses phiri.

NIKIONA mtu anamtetea Phiri
najua huyo mtu hamna kitu na hajuhi Mpira.

Pathetic
 
Mkuu naomba kuuliza utamtambuaje false #9 kimajukumu yake uwanjani?
Kazi yake nini?
Namtofautishaje na natural #9?
Second striker, #10 na false #9 ni kitu au mtu mmoja kimajukumu?

Note: Sijui soccer na sijacheza popote hata kiwango cha ligi daraja la chini kabisa.

USIJALI

False #9, au "striker wa uwongo," ni nafasi ya mchezaji wa soka ambaye anacheza kama mshambuliaji wa kawaida, lakini anaweza kuwa na majukumu tofauti na mshambuliaji wa kawaida (#9 asilia).

Mchezaji alicheza kama false #9 mara nyingi ana jukumu la kuvuta walinzi wa upande wa kushambulia kutoka eneo lao la kawaida, ( Anawavuta Mabeki Hadi kati kati na kuacha gape kwa chini, au kuwapeleka Mabeki WA kati pembeni pembeni hivyo kutoa nafasi kwa wenzake kushambulia.

Wanaweza kushuka nyuma na kushiriki katika kujenga mchezo wa timu(build up), na wakati mwingine hufanya kazi kama kiungo wa ziada. Wana jukumu la kutengeneza nafasi na kutoa pasi muhimu.

MUGALU aliweza kucheza Katika nafasi hizi zote.
Sema Alikuwa akipigwa misumali mikali sana na watesi wake na kumfanya kukosa KOSA MAGOLi Kila mala.
(Kagere Boko na yanga)
Alikuwa anawapa nafasi akina Chama MIQUISSONE kufunga,

Pia Boko na Kagere walikuwa wanafunga.
MUGALU Alikuwa Top top straiker
I

Tofauti kati ya false #9 na mshambuliaji wa kawaida (#9) ni kwamba mshambuliaji wa kawaida huwa na jukumu kuu la kufunga mabao, wakati false #9 anaweza kutoa mchango wa kufunga lakini pia kujenga nafasi na kuwa mchezaji wa timu.

Kuhusu tofauti kati ya false #9, second striker (#10), na kiungo wa kati, wanaweza kuwa na majukumu tofauti kwenye uwanja. Second striker (#10) mara nyingi anacheza kama mchezaji wa kiungo wa kati lakini pia ana majukumu ya kushambulia. Kiungo wa kati ana majukumu ya kusambaza pasi, kudhibiti mpira, na kushiriki katika kujenga mchezo.
Eg Chama ,pakome ,saido au KDB.

Majukumu na jukumu la mchezaji linaweza kutofautiana kulingana na mkakati wa timu na mfumo wa mchezo, lakini kwa ujumla, false #9, second striker (#10), na kiungo wa kati wanaweza kuwa na majukumu tofauti na kuchangia tofauti kwenye mchezo.

Nadhani nimekujibu kwa kiasi chake.
Karibu kwa swali lingine
 
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeipigania sana Simba huku mitandaoni ila ikafika wakati nikaamua kupumzika maana kuna mambo yanakatisha tamaa sana ndani ya Simba yangu.

Simba ina wachezaji bora sana shida ni jinsi wanavyotumika. Kuna mentality inabidi ibadilishwe pale kuanzia kwa viongozi fulani, hadi baadhi ya wachezaji. Inaonyesha hakuna spirit ya teamwork pale Simba, kila mtu anajiangalia yeye kama yeye kwanza. Kukaa benchi au kuanzia nje, kuna wachezaji wanaona kama watadharaulika. Kuna approach ambayo Yanga wameichukua inawasaidia sana. Kwa mfano upande wa mabeki, wamewachukua wachezaji wanaopendana sana na wengine wanaotoka sehemu moja. Hii inawafanya hali yote ya husda, au kuharibiana kwa njia za ajabu ajabu isiwepo. Na inachowasaidia zaidi, kila mtu anapewa fursa ya kucheza.

Mimi nikimuangalia Chilunda najiuliza huyu anakosa hata mechi moja ya ushindani na kupewa dakika 15, kweli? Hivi Phiri amekuwa mchezaji wa kuingia dakika za nyongeza, kweli? Kuna wakati kisingizio kilikuwa bado hajapona, sasa hivi kisingizio ni nini? Achana na rekodi za zamani alipoingia Simba akawa anaibeba Simba katika mabega yake hadi kuingia makundi, angalia aliporudi baada ya majeraha, hata alipokuwa anapewa vidakika vichache, kuna mechi muhimu sana kwa mfululizo yeye ndiyo alikuwa anatoa assist za magoli muhimu. Angalia sasa, mechi ngapi muhimu ambazo anaingizwa vidakika vya mwisho na bado yeye anakuwa mwokozi wa timu lakini hayo yote hayawashtua hao wanaopanga timu? Nitaingia katika maombi maalumu Phiri aende Yanga na siku tukikutana nao watuchakaze vibaya sana.

Hivi kweli wenye mamlaka ya hii timu wanaitakia mema hii timu? Simba imekuwa na baadhi ya wachezaji walevi, wahuni, wakorofi na walikuwa hawasugui benchi. Hakuna anayeamini Phiri ana sifa zozote mbaya kustahili kusugua benchi. Alishaprove uwezo wake na wote tunaujua. Sasa unamuacha anasugua benchi kwa sababu zisizoeeleweka, eti visingizio kuwa hakabi, eti siyo mrefu, hao wanaopangwa badala yake wanajigonga gonga tu uwanjani, mechi inaanza hadi anatolewa hajapiga pasi hata moja, hayawin hata mpira mmoja wa juu au wa 50/50. Ninavyoamini mimi, kama mechi inahitaji kuongeza mchezaji mkabaji, viungo ndiyo wachezaji sahihi wa kujaza siyo striker tena ambaye siku zake zimeisha kitambo. Mchezaji anapangwa ili tu aotee kagoli kamoja wapate nafasi ya kutunanga tunaokosoa maamuzi yao.

Na nyie mnaotetea ujinga unaoendelea tunajua mnalinda maslahi yenu yanayotokana na ukaribu mlionao na timu na viongozi ila ukweli wote tunauona. Kuna msemo wa kilatini unaosema "Vox populi, vox Dei", yaani "sauti ya watu ni sauti ya Mungu". Wengi tunayasema haya na tunayasema kwa kuwa ndiyo ukweli wa nafsi zetu, nyie mnaongea ukweli wa matumbo yenu. Haya mambo ya kuishia njiani kila msimu ni matokeo ya kujitakia tu. Wiki hii nimeshuhudia wanasimba wengi wanaangalia mechi zake kwa unyonge sana maana wanajua uwezo wa timu na wanaona kabisa inakwama wapi. Wengi wanasononeka na kulalamika kwa sauti ya chini ili wasionekane wanaleta chokochoko au hawataki kuwapa mtaji upande wa pili. Wengine tulishayaona haya yanakuja ndiyo maana tulishaanza kukaa pembeni ili mioyo yetu isiumie. Na tusipojirekebisha na kuacha mapuuza haya group stage safari hii hatuvuki, hatutakuwa tena mwakarobo tutakuwa mwakakundi hadi tutakapojielewa.

Hii naweza kulinganisha na suala la utamu, yaani unataka utamu wa asali, halafu unaenda kuutafuta kwa kitu kichungu. Unataka utamu halafu unaenda kuutafuta kwenye sehemu isiyo safi. Kuna uzi nilileta mwanzoni mwa msimu nikisema Yanga watakuwa na mafanikio bora msimu huu kimataifa kuliko Simba na hizi ndiyo sababu zilizopelekea kusema hayo.

Tukisema haya wanasema tuna chuki binafsi, je hao wanaosugua benchi wakati uwezo wao tunaujua tusemeje?

Kuna ujinga pale Simba mpaka unajiuliza shida ni Nini? Ngoja Yanga aingie robo na Simba itolewe makundi tuone hai Viongozi watafanya Nini kuanzia Mo mpaka Try again Wanajiangalia wao sio Simba.
 
Ukweli Simba Kuna ujinga, tuna wachezaji wazuri lakini kocha anaacha kuwatumia. Kuna wachezaji Kila mechi wanapangwa hata walijaribu mechi ijayo wanaanza. Wachezaji wengi hawajitumi na sababu wameshajua namba zile Zina watu. Usajili huwa ni bahati nasibu lakini kwa Simba ni uzembe, Kramo kasajiliwa bila kupimwa afya, kipa wa Brazil.

Kabla ya kusajili kipa toka nje wengi tulipinga lakini viongozi walijiona wajuaji kumbe wanakula ten percent za usajili. Simba isiyo na pesa ilisajili kwa kuangalia nahitaji ya timu Ila hii inayojifanya Ina pesa usajili ni ovyo kabisa.

Hivi Ally Salim ndio kipa wa kudaka Simba mechi kubwa, hivi tumeshindwa kutafuta wabadala wa mabeki was pembeni. Hivi Boko na Saidoo kwa umri wao wanaweza kutupa ubingwa was Afrika?

Inasikitisha Sana. Nadhani Viongozi walisharidhika hapa tulipofika. Simba kuanzia Viongozi na wachezaji kila mtu anaenda kivyake.
 
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeipigania sana Simba huku mitandaoni ila ikafika wakati nikaamua kupumzika maana kuna mambo yanakatisha tamaa sana ndani ya Simba yangu.

Simba ina wachezaji bora sana shida ni jinsi wanavyotumika. Kuna mentality inabidi ibadilishwe pale kuanzia kwa viongozi fulani, hadi baadhi ya wachezaji. Inaonyesha hakuna spirit ya teamwork pale Simba, kila mtu anajiangalia yeye kama yeye kwanza. Kukaa benchi au kuanzia nje, kuna wachezaji wanaona kama watadharaulika. Kuna approach ambayo Yanga wameichukua inawasaidia sana. Kwa mfano upande wa mabeki, wamewachukua wachezaji wanaopendana sana na wengine wanaotoka sehemu moja. Hii inawafanya hali yote ya husda, au kuharibiana kwa njia za ajabu ajabu isiwepo. Na inachowasaidia zaidi, kila mtu anapewa fursa ya kucheza.

Mimi nikimuangalia Chilunda najiuliza huyu anakosa hata mechi moja ya ushindani na kupewa dakika 15, kweli? Hivi Phiri amekuwa mchezaji wa kuingia dakika za nyongeza, kweli? Kuna wakati kisingizio kilikuwa bado hajapona, sasa hivi kisingizio ni nini? Achana na rekodi za zamani alipoingia Simba akawa anaibeba Simba katika mabega yake hadi kuingia makundi, angalia aliporudi baada ya majeraha, hata alipokuwa anapewa vidakika vichache, kuna mechi muhimu sana kwa mfululizo yeye ndiyo alikuwa anatoa assist za magoli muhimu. Angalia sasa, mechi ngapi muhimu ambazo anaingizwa vidakika vya mwisho na bado yeye anakuwa mwokozi wa timu lakini hayo yote hayawashtua hao wanaopanga timu? Nitaingia katika maombi maalumu Phiri aende Yanga na siku tukikutana nao watuchakaze vibaya sana.

Hivi kweli wenye mamlaka ya hii timu wanaitakia mema hii timu? Simba imekuwa na baadhi ya wachezaji walevi, wahuni, wakorofi na walikuwa hawasugui benchi. Hakuna anayeamini Phiri ana sifa zozote mbaya kustahili kusugua benchi. Alishaprove uwezo wake na wote tunaujua. Sasa unamuacha anasugua benchi kwa sababu zisizoeeleweka, eti visingizio kuwa hakabi, eti siyo mrefu, hao wanaopangwa badala yake wanajigonga gonga tu uwanjani, mechi inaanza hadi anatolewa hajapiga pasi hata moja, hayawin hata mpira mmoja wa juu au wa 50/50. Ninavyoamini mimi, kama mechi inahitaji kuongeza mchezaji mkabaji, viungo ndiyo wachezaji sahihi wa kujaza siyo striker tena ambaye siku zake zimeisha kitambo. Mchezaji anapangwa ili tu aotee kagoli kamoja wapate nafasi ya kutunanga tunaokosoa maamuzi yao.

Na nyie mnaotetea ujinga unaoendelea tunajua mnalinda maslahi yenu yanayotokana na ukaribu mlionao na timu na viongozi ila ukweli wote tunauona. Kuna msemo wa kilatini unaosema "Vox populi, vox Dei", yaani "sauti ya watu ni sauti ya Mungu". Wengi tunayasema haya na tunayasema kwa kuwa ndiyo ukweli wa nafsi zetu, nyie mnaongea ukweli wa matumbo yenu. Haya mambo ya kuishia njiani kila msimu ni matokeo ya kujitakia tu. Wiki hii nimeshuhudia wanasimba wengi wanaangalia mechi zake kwa unyonge sana maana wanajua uwezo wa timu na wanaona kabisa inakwama wapi. Wengi wanasononeka na kulalamika kwa sauti ya chini ili wasionekane wanaleta chokochoko au hawataki kuwapa mtaji upande wa pili. Wengine tulishayaona haya yanakuja ndiyo maana tulishaanza kukaa pembeni ili mioyo yetu isiumie. Na tusipojirekebisha na kuacha mapuuza haya group stage safari hii hatuvuki, hatutakuwa tena mwakarobo tutakuwa mwakakundi hadi tutakapojielewa.

Hii naweza kulinganisha na suala la utamu, yaani unataka utamu wa asali, halafu unaenda kuutafuta kwa kitu kichungu. Unataka utamu halafu unaenda kuutafuta kwenye sehemu isiyo safi. Kuna uzi nilileta mwanzoni mwa msimu nikisema Yanga watakuwa na mafanikio bora msimu huu kimataifa kuliko Simba na hizi ndiyo sababu zilizopelekea kusema hayo.

Tukisema haya wanasema tuna chuki binafsi, je hao wanaosugua benchi wakati uwezo wao tunaujua tusemeje?
Kumbe muda mwingine akili mnazo lakini mnajitoaga tu ufahamu kuogopa kuonekana amuitakii mema timu yenu, lakini mkumbuke ni Bora KUNYWA dawa chungu ili upone maradhi yako, na Simba wataangushwa na propaganda uchwara za viongozi wao wakati uhalisia ni zero bin sifuri, yanga anawaacha mdogo mdogo maana keshatoka uko anafanya vitu vinavyoonekana na sio kufurahisha genge mkija kushtuka mtakuwa hoi bin taaban!
 
Kuna ujinga pale Simba mpaka unajiuliza shida ni Nini? Ngoja Yanga aingie robo na Simba itolewe makundi tuone hai Viongozi watafanya Nini kuanzia Mo mpaka Try again Wanajiangalia wao sio Simba.

UNAMUACHA Golikipa wa maana kama John Noble unaaza kuhangaika na Ayoub MDAKA panzi.

Ally SALUM NDIO KIPA WA KUDAKA mbele ya Alhly kweli !!!!???

MBELE YA RAIS WA FIFA????

Inakatisha tamaa sana.

Pathetic
 
Back
Top Bottom