Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread

kipofu baada miaka 3 kaona mwezi shida!!!

The true Champs have returned. Mwaka huu tunachukua kombe la CAF na mwakani tunachukua CAF champions League. Itabidi CAF wafanye marekebisho tuweze kutetea pia ubingwa wetu wa kombe la CAF ambalo kanda mbili mtashiri lakini kama kama kawaida yenu mtaishia raundi ya kwanza.
 
M-mbabe tunashukuru sana... bila kauli kama hizi ubingwa hauwi mtamu!!

SIMBA BINGWA, KAMA HUTAKI BASI!!!
atleast huku tushachukua ,sasa bado epl au sio? mwaka huu unaweza kuwa mzuri kwangu kama wiki ijayo utafanya kweli ha ha ha.


simbaa oyeeeeeee.
 
hivi itakua vipi tukiwapanga simba kids hiyo mechi na kandambili??
E bwana hili ni wazo hasa kama mechi hii itapigwa kabla ya mpambano wetu na Lengthern yeboyebo wanaweza kutuumizia wachezaji ilikutuharibia tutoke kama walivyong'olewa wao.
 
maeneo niliopo ushindi hata haunogi,manake washabiki wengi wa yanga wamejificha baada kujua kwamba ukiwa mshabiki wa Yanga unaoneka mshamba mshamba.
 
pooopo po eeeh kidedea popooo po popo

simba simba
simba simba
eeee kidedea popooo popo
 
The true Champs have returned. Mwaka huu tunachukua kombe la CAF na mwakani tunachukua CAF champions League. Itabidi CAF wafanye marekebisho tuweze kutetea pia ubingwa wetu wa kombe la CAF ambalo kanda mbili mtashiri lakini kama kama kawaida yenu mtaishia raundi ya kwanza.

return of the titans!!!
 
Week end hii taamu jamani.. Nadhani na golden boot (Mgossi) tutapata pia ..
 
Ubingwa raha jamani.............ila vijana wanastahili jamani!!!
Hongera wachezaji
Hongera Kocha
Hongera viongozi
Hongera wanachama & mashabiki wa Simba!
Kweli umoja ni nguvu.
Hongera SIMBA- MABINGWA 2009/2010
 
wawooooooooo!!! Eeeeh Kidedea!! Kandambili tumemubwaga, eeeeh kidedeaaa!!!!
Ah leo ngoja nikaburudike kwa ushindi huu wa aina yake. Sidhani kama yupo wa kuvunja record yetu ya kutangaza ubingwa bila kufungwa.
 
mie naona mechi ya Yanga ndio tutumie kukabiziwa kombe rasmi au watatufanyia fujo? ha ha haha

Mkuu wanaweza wakaliiba Kombe lenyewe na hata kutuumizia Wachezaji wetu, sasa sidhani kama Viongozi wanaweza ku afford hilo ukizingatia Majukumu Mazito ya Kimataifa ambayo Simba amekabidhiwa. Mkuu Zingatia Macho na Matumaini ya Watanazania Zaidi ya Millioni 37 yako Kwa SIMBA
 
Sishangai nikisikia simba inastaili kopokwa point 5 na sababu zkatolewa, kwa ufuatiliaji wangu, Mika miwili iliyopita yumekoswa ubingwa kwa kupokwa point. MAFUBA YA MANJI OFCOURSE
 
Sishangai nikisikia simba inastaili kopokwa point 5 na sababu zkatolewa, kwa ufuatiliaji wangu, Mika miwili iliyopita yumekoswa ubingwa kwa kupokwa point. MAFUBA YA MANJI OFCOURSE
Manji keshawachoka yanga... so dont worry
 
wawooooooooo!!! Eeeeh Kidedea!! Kandambili tumemubwaga, eeeeh kidedeaaa!!!!
Ah leo ngoja nikaburudike kwa ushindi huu wa aina yake. Sidhani kama yupo wa kuvunja record yetu ya kutangaza ubingwa bila kufungwa.


"Simba imetwaa ubingwa kwa kushinda mechi 18 na kutoka sare mechi mbili.


Hii ni mara ya kwanza nchini Tanzania, kwa timu kuchukua ubingwa bila kufungwa hata mechi moja"....... Source: BBC SWAHILI
 
SIMBA BINGWA LIGI KUU YA VODA TANZANIA BARA !!!!!

* Ni baada ya kuilamba Azam 2-0
SIMBA Bingwa 2009-2010, hivyo ndivyo ilivyo baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Azam FC katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mike Barasa ndiye aliyeipatia Simba ubingwa baada ya kuifungia timu hiyo mabao yote mawili, na kuamsha shamrashamra na nderemo kwa mamia ya mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Kutokana na matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote hata kama itafungwa michezo yake miwili iliyobaki dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar. Ushindi huo umeipatia tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, mwakani.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, timu zote zilianza mchezo kwa kasi huku Simba ikisaka ushindi wa mapema.
Ndivyo ilivyokuwa, kwani dakika ya nane tu, Mike Barasa aliwanyanyua vitini mamia ya mashabiki wa Simba baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza, akiunganisha pasi iliyopigwa na Hilary Echeza.
Baada ya bao hilo, Simba ilizidisha mashambulizi na kutawala sehemu kubwa ya mchezo, huku wachezaji wa Azam wakionekana kupoteana na kuwaachia wachezaji wa Simba kutamba kwa kupeana pasi fupi fupi.
Azam nao walijaribu kutafuta mpira na kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni kwa wapinzani wao, lakini umaliziaji mbovu uliifanya timu hiyo kuambulia patupu.
Simba iliendelea kufanya mashambulizi makali langoni kwa wapinzani wao na dakika ya 32 nusura Barasa aipatie timu yake bao lingine, lakini shuti kali alilopiga lilipaa juu ya goli na kutoka nje.
Dakika tano baadae, Azam ilijibu shambulizi hilo baada ya mabeki wa Simba kufanya makosa na kumpa nafasi, lakini John Boco alishindwa kumalizia mpira huo na uliotoka nje.
Kipindi cha pili kilipoanza, timu zote zilifanya mabadiliko. Simba iliwatoa Ramdhani Chombo, Ulimboka Mwakingwe na Mike Barasa, nafasi zao waliingia Uhuru Selemani, Mohamed Kijuso na Jerry Santo.
Azam iliwatoa Malika Ndeule, Danny Wagaluka na Said Sued na kuwaingiza Mau Bafio, Ally Manzi na Suleyman Kassim.
Baada ya mabadiliko hayo timu zote ziliendelea kucheza kwa kasi huku zikishambuliana kwa zamu na dakika ya 57 nusura Simba ipate bao la tatu, kupitia kwa Echeza aliyepiga mpira wa faulo uliogonga mwamba na kurudi uwanjani.
Laiti kama Boco na Shaaban Kisiga wangetumia vyema nafasi walizopata, wangeweza kuifungia timu yao mabao, lakini walishindwa kutumia nafasi hizo na kuwaacha wapinzani wao kuondosha hatari zote.
Baada ya mchezo kumalizika, wachezaji wa Simba walimbeba juu kocha wao huku wakimpongeza, hali iliyoamsha shangwe uwanjani hapo.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba. Patrick Phiri, alisema amefurahi kuona timu yake ikipata ubingwa ambao alikuwa akiuota.
Phiri alisema ligi hiyo ilikuwa ngumu, lakini kwa uwezo wa Mungu ameweza kufanikiwa kushinda na kusema ushirikiano ndani ya timu yake ndio uliofanikisha kutwaa ubingwa huo huku ikiwa ina mechi mbili mkononi.
Simba iliwachezesha Juma Kaseja, Haruna Shamte, Juma Jabu, Juma Nyoso, Kevin Yondan, Mohamed Banka, Hilary Echesa, Ramadhan Chombo/Jerry Santo, Mussa Hassan 'Mgosi', Mike Barasa/Mohamed Kijuso na Ulimboka Mwakingwe/Uhuru Seleman.
Azam: Vladmir Niyonkuru, Ibrahim Shikanda, Malika Ndeule/Mau Bofu, Tumba Swed, Salum Sued, Himid Mao, Danny Wagaluka/Ally Manzi, Salum Aboubakar, John Boco, Shaban Kisiga na Said Sued/Suleyman Kassim.
 
Back
Top Bottom