vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,361
- 2,499
Leo mtoto mpendwa wa TFF alikuwa anacheza kiporo chake alichosogezewa mara kwa mara na baba yao mlezi TFF, Simba walikuwa na mazingira mazuri zaidi ya kushinda kuliko Azam. Na sababu kuu ya Simba kushinda ni kwasababu wana match fitness.
Kikosi cha Simba ndio timu pekee ambayo wamepata nafasi ya kucheza mechi mara kwa mara kuliko timu zote Tanzania. Wamecheza mechi zote za kombe la Mapinduzi, kisha hao hao wakacheza mechi ya federation cup na kisha wakacheza michezo miwili ya ligi kuu kabla ya kukutana na Azam.
Wakati huo Azam wachezaji wao waliishia kwenye hatua ya pili ya kombe la Mapinduzi na wakati huo hawakutumia wachezaji wao wote kwenye hayo mashindano. Baada ya Mapinduzi hawakucheza mchezo wowote hadi leo walipokutana na Simba.
Azam waliokuwa fit zile counter hawakuachi kizembe, na spidi yao isingekuwa balaa kwa viungo na mabeki wa Simba wanaokatika katika. Mmeshindwa kuifunga Azam hii basi hakuna mechi nyingine mtakayoshinda dhidi yao labda TFF wawatengenezee mazingira kama haya