Simba inazidiwa na Yanga kwa propaganda

Hizo takwimu ni Yanga kaxitoa? Mbona Hao hao walipotoa kuhusu Simba ulikuwa unapita road na kidedea?
Sasa ndugu bila kujali nani katoa Takwimu ,hivi inakuingia akilini au hata moyoni tu,kuwa Yañga ni Bora kuliko Mamellod! Inashika no 3 ! Hebu tusimkufuru Mungu Kwa kutumia vizuri uuambaji,ikiwemo kufikiri Kwa viungo husika!
 
Sasa ndugu bila kujali nani katoa Takwimu ,hivi inakuingia akilini au hata moyoni tu,kuwa Yañga ni Bora kuliko Mamellod! Inashika no 3 ! Hebu tusimkufuru Mungu Kwa kutumia vizuri uuambaji,ikiwemo kufikiri Kwa viungo husika!
Sasa inakuwaje uje hapa uilaumu Yanga? Mtu yeyote anayefanya research anajua mwenyewe kwa vigezo vyake alivyoweka kupata conclusion hiyo,so mnapopayuka payuka as if hizo takwimu kaleta Ali Kamwe ni zaidi ya umbumbumbu, then pambaneni na timu yenu Ahmed jana alikuwa analia lia huko Tunduma
 
SIKUTAZAMA moja kwa moja mechi ya Tanga ya fainali ya Ngao ya Jamii, mechi ya Simba na Yanga. Nilichoamini tangu siku hiyo kilikuwa tofauti mno na nilichokiona nilipoyatazama marudio ya maonesho ya mechi hiyo. Awali niliaminishwa kuwa Yanga walicheza peke yao! Simba hawakucheza kabisa. Kwa nini nisiamini hivyo wakati kila mtu aliandika hivyo?

Kilichonishangaza, nilichokiona kilikuwa tofauti kabisa kwani Simba walishambulia na Yanga walishambulia. Nilimuona Baleke akipiga chenga wachezaji kibao wa Yanga na kuachia kiki iliyopaa. Angefanya hivyo Musonda au Mzize, ningelifahamu hilo kwani lingepambwa sana.

Niliona Onana akikabiliana na kipa Diarra aliyefanya ujasiri mkubwa kuokoa hatari hiyo nje ya 18. Yanga walipiga pasi zilizofika na Simba walipiga pasi zilizofika. Matokeo ya suluhu yalikuwa ya haki kwa jinsi mpira ulivyochezwa lakini tulichoshawishiwa kuamini ni kwamba Simba walizidiwa sana. Haikuwa kweli.

Yanga ni wazuri mno kwa propaganda wakitumia mashabiki wao wa kila sehemu. Wengi wanaaminishwa Yanga ina timu nzuri ikiwa na wachezaji mahiri tupu kila idara na kocha bora sana huku Simba ikichorwa kuwa ni timu mbovu, kocha m-bovu na ina wachezaji wa uwezo wa chini lakini ukifikiri ubora wa Kapombe, Inonga, Che Malone, Zimbwe, Miquissone, Ngoma, Mzamiru, Onana, Chama, Kramo, Kanuti, Phiri, Kibu nk hawana ubora kweli?

Mimi naona kote Yanga na Simba kuna wachezaji bora sana lakini propaganda ya Yanga inawainua wa Yanga na kuwaweka chini wa Simba.

Hebu tafakari sauti kubwa mno baada ya Yanga kuzifunga ASAS 5-1, KMC 5-0 na JKT Tanzania 5-0. Halafu tafakari ilivyoonekana si jambo kubwa Simba ilipozishinda Singida United 8-0, Coastal Union 8-0, Coastal Union 7-0, Prisons 7-2, Horoya 7-0, Polisi Tz 6-1, Mtibwa Sugar 5-0 nk.

Kama zile penalti tatu alizookoa Ally Salim Tanga zingeokolewa na Diarra, muziki wake wa misifa usingechuja mapema! Lakini Ally Salim alitafutiwa kitu cha kumfanya apunguziwe sifa kwamba alitoka mstarini. Huwezi kuokoa penalti bila kutoka mstarini. Hutakiwi kutoka KABLA mpigaji hajaugusa mpira. Akiugusa tu, unatoka.
Propaganda ilienezwa sana kuwa Simba imekuwa ikinyanyaswa na Yanga kwa miaka hii na watu waliamini hivyo.

Sijui kwa nini sare zao nyingi zilichukuliwa kwamba Yanga alikuwa mwamba wa Simba. Kwenye ligi kuu, Simba walishinda kwa goli la kichwa la Kagere. Ukaja ushindi wa Yanga free kick ya Morrison kisha deflection ya Zawadi Mauya. Wamemaliza na 2-0 za Inonga na Kibu. Zilizobaki ni sare. Ushindi mbili kwa mbili. Lakini ilienezwa sana Yanga walikuwa wababe wa Simba. Kivipi? Ngao mbili walibeba Yanga.

Sasa Simba wana moja. Azam Shirikisho, Simba alimshinda Yanga 4-1 nusu fainali kisha kubeba kombe fainali. Wakabeba tena Simba kwa Yanga 1-0 Kigoma. Yanga wakawapiga Simba nusu fainali Mwanza 1-0. Simba wamewapiga Yanga mara mbili na Yanga mara moja. Ukitathmini yote hayo, hakuna mbabe wala mnyonge kati yao lakini propaganda ilitengenezwa kuwa Yanga ni mbabe wa Simba licha ya sare zao nyingi.

Ukweli Yanga ni wajuzi sana wa propaganda, hata kelele za Robertinho hafai, aondoke na kwamba hata Krismasi hafiki nyingi zinaanzishwa na mashabiki wa Yanga lakini kuna watu wa Simba wanaingia kichwa kichwa kumshambulia kocha wao mjuzi sana. Ni mashabiki wa Yanga ndiyo wasiofurahi Robertinho kuendelea kuwepo Simba.

Watu wa Yanga wamefikia kumtengeneza shabiki wa Yanga aitwaye Meja akitambulishwa kila siku kuwa shabiki wa Simba akitumika na East Africa TV kuipondaponda Simba siku zote na kuipamba sana Yanga.

Kwa bahati mbaya yeye ni mjinga kama wanaomtumia kuivuruga Simba walivyo wajinga. Kumtambulisha kila siku kuwa yeye shabiki wa Simba kisha kuisema vibaya Simba na kuieleza vizuri Yanga ni ujinga wa kwanza. Kumtambulisha kila siku kuwa shabiki wa Simba kama hilo ni jina lake kunaleta mashaka. Kwa nini lazima ushabiki wake utajwe?

Ujinga wao wa pili ni kutomshauri siku chache chache aongee mazuri ya Simba kuhadaa watu kuhusu usimba wake. Afanye usanii tu wa hivyo ili akiponda atetewe kuwa huongea kwa haki kwani huisemea mazuri timu yake wakati fulani. Walivyo wajinga hilo halimo vichwani mwao.

Tatu, wangekuwa wanamshauri avae jezi ya Simba hapo studio kama mashabiki wengine wa timu hizo wafanyavyo waendapo kuhojiwa. Huyu hawezi kuvaa hivyo kwani yeye ni Yanga na jezi za Simba ni najisi kwake. Pia naamini anaogopa Yanga wenzake watamchukuliaje. Angevaa tu ili atimize kiuhakika mkakati wao.

Kwa ujumla Yanga wako vizuri mno kwa propaganda inayopotosha mengi.
Naunga mkono hoja. Idara ya propaganda ya Yanga iko vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom