Simba iliyoibiwa inatafuta mawakili wa kuwatetea Aveva!?

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,471
4,424
7778a553fed17e67089c9b9e3cba6b97.jpg
 
Ifike mahali tupunguze mihemko ya kishabiki na badala yake tujadili mambo kwa hoja za msingi.Utetezi ni haki ya kila mtuhumiwa awe mwenye hatia au kinyume chake.

Hawajatiwa hatiani bhana, sema wamefikishwa mahakamani.

Mahakama ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kuwatia hatiani au kuwaachia huru.
Umewahi kumuwekea wakili unayemtuhumu kukuibia? Common let's be logical. Kesi iliyoko mahakamani ni Aveva na Kaburu kuiibia Simba. Kwa mtazamo wangu, Simba walitakiwa waje juu dhidi ya wezi Hawa. Hii ni ajabu nyingine katika soka la TZ
 
Ni kama vile Tff wawatafute mawakili wakamtete malinzi
 
Sijapata kusikia wala kuona, mtu aliyeibiwa kuandaa mawakili wa kumtetea mwizi aliyekuibia....

Sijaelewa sababu za kuwakinga watu walioihujumu team,...

Au itakua mchongo wamehusika wengi?

Hii team inaonekana bila kaburu na Hanspope, hakuna mwenye akili angalau ya kuweza kuwaongoza hawa watu....

Klabu kwa sasa imeandaa jopo la mawakili litakalowatetea viongozi wetu na tunaamini Mahakama itatenda haki pande zote zinazohusika na shauri hilo. Tunawaomba

Watanzania, wapenzi na mashabiki wetu wawe watulivu wakisubiri taarifa rasmi ya kikao cha Kamati ya Utendaji,”imesema taarifa hiyo.

Baada ya kukosekana kwa Aveva na Kaburu, wanaobaki ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji tu, wa kuchaguliwa na kuteuliwa. Wajumbe wa kuchaguliwa ni Collins Frisch, Said Tuliy, Ally Suru, Iddi Kajuna na Jasmine Costa wakati wa kuteuliwa ni Zacharia Hans Poppe, Salim Abdallah ‘Try Again’, Mohammed Nassor, Kassim Dewji, Musley Ruweih.
Aveva na Makamu wake, Kaburu jana walipelekwa mahabusu hadi Julai 13, mwaka huu baada ya kunyimwa dhamana kufuatia kusomewa mashitaka matano Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.

Wawili hao walifikishwa mahakamani mapema asubuhi na kusomewa mashitaka hayo matano mchana, ambayo ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodai kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni Rais Aveva na Makamu wake, Kaburu kiasi cha dola za Kimarekani 300,000.

Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwenye benki ya CRDB tawi la Azikiwe mjini Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sharia, ambapo inadaiwa Rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.

Shitaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka kwenye benki ya Barclays tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu aliyemsadia Aveva kutakatisha fedha katika Barclays baada ya kughushi nyaraka.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali, Christopher Msigwa, washitakiwa hao walikana mashitaka yote na kupelekwa rumande hadi Julai 13, mwaka huu huku wakinyimwa dhamana.

Wawili hao walipandishwa kizimbani jana baada ya juzi kukamatwa na Maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi juu ya tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutokana na mchezaji Emmanuel Okwi.
Inadaiwa kuna ‘ufisadi’katika mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi kwenda klabu ya Esperance ya Tunisia dili ambalo liliripotiwa kugharimu dola za Kimarekani 300,000, zaidi ya Sh. Milioni 600 za Tanzania.

Lakini Aveva hakuwapo madarakani wakati Simba inamuuza Okwi mwaka 2013, bali Kaburu alikuwa Makamu wa Rais, chini ya Rais wa wakati huo, Alhaj Ismail Aden Rage.
Hata hivyo, Esperance ilichelewa kulipa fedha hizo na hadi Machi mwaka jana, wakati huo tayari Aveva ni Rais wa klabu na Kaburu ni Makamu wake, baada ya Rage kutogombea tena.

Okwi alinunuliwa na Etoile Januari mwaka 2013, miaka mitatu tu baada ya kujiunga na Simba mwaka 2010, lakini baada ya miezi mitatu akatofautiana na klabu ya Tunisia kufuatia na kufungua kesi FIFA akiomba aruhusiwe kucheza klabu nyingine kulinda kipaji chake wakati mgogoro wake na Etoile unaendelea.

Etoile ilisitisha huduma kwa Okwi, baada ya kukerwa na desturi ya mchezaji huyo kuchelewa kurejea kujiunga na timu kila alipokuwa anaporuhusiwa kwenda kujiunga na timu yake ya taifa Uganda.

Akasaini tena SC Villa katikati ya mwaka 2013 kabla ya Desemba mwaka huo, kuhamia Yanga SC- wakati wote huo kesi yake na Etoile ikiendelea FIFA na Simba walikuwa hawajalipwa fedha zao.
Simba nayo ilifungua kesi FIFA ikisistiza kulipwa fedha zake baada ya kumuuza mchezaji huyo Etoile Januari 2013.

Okwi na Simba wakaungana tena mwaka 2014 baada ya mchezaji huyo kutofautiana na Yanga pia, akidai ilishindwa kummalizia fedha zake za usajili, hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumruhusu kuondoka, naye akarejea Msimbazi.

Kabla haijapata fedha za kumuuza Okwi Etoile, Simba ikamuuza tena Okwi klabu ya Sonderjyske ya Denmark kwa dau la dola za Kimarekani 110,000 zaidi ya Sh. Milioni 230 za Tanzania.

Hata hivyo, Denmark nako aliposaini mkataba wa miaka mitano, aliondoka baada ya miaka miwili tu na kurejea SC Villa mapema mwaka huu, kabla ya juzi kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga tena na Simba kwa mara ya tatu...
 
Upuuzi! Yani Mimi nilieibiwa nitoe wakili kumtetea alieniibia...Hapo simba imebugi...simba ilitakiwa ikae kimya na asiwe upande wowote hadi hukumu itakapotoka ndo waseme kitu...ndo mana nasemaga hii nchi inawasomi wachache sana, hawazidi saba..."and this is the results "(by Magufuli)
 
Je kama aliyeibiwa ameridhika, au haamini kuwa ameibiwa?
 
Hata kama haamini kuibiwa kwake,alitakiwa akae kimya ili mahakama na pccb zifanye kazi yake coz huenda aliibiwa bila kujua
Huenda ni ishara ya ustaarabu uliotukuka. Kwenye nchi zilizoendelea, wakili ni haki ya kila mshtakiwa. Kwa hivyo hata ukishtakiwa kwa kosa kama la ugaidi nawe ukakosa wakili, Serikali hiyohiyo inayokushtaki ni lazima ikupatie wakili. Ndio maana hata magaidi walioshikiliwa Guantanamo walipatiwa mawakili na Serikali ya Marekani.
 
Unachanganya mada..ishu ya serikali na simba na US dhidi ya washtakiwa wake ni tofauti
 
Kwahiyo Tff nao watoe wakili wa kumtetea Malinzi?
 
Unachanganya mada..ishu ya serikali na simba na US dhidi ya washtakiwa wake ni tofauti
Hapana Mkuu, zinafanana! Hoja hapa ni kwa muathirika (Serikali ya Marekani/Simba) kuuhakikishia umma kwamba makosa ya mlalamikiwa (magaidi/Aveva, Kaburu) si ya kusingiziwa au ni kwa sababu ya udhaifu tu wa miundombinu ya utetezi; yamethibitika baada ya Walalamikiwa kupewa fursa zote za kujitetea.
 
Kwahiyo Tff nao watoe wakili wa kumtetea Malinzi?
Ndiyo, iwapo Malinzi hatakuwa na namna ya kupata wakili na ilivyokuwa Serikali bado haijawa na utaratibu wa kuwapatia raia wake huduma za wakili bila malipo kwa wasio na uwezo.
 
!
!
Katiba na miongozo mingine ya taasisi mbalimbali haswa binafsi, Zina kipengele cha kutoa msaada wa kisheria kwa mtumishi wake akiwa na madhila. Kuwapatia mawakili ni kutimiza hilo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom