Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 618
- 1,570
Hii klabu kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa bingwa wa kuua vipaji vya wachezaji vijana pindi inapowasajili, imekuwa na tamaa ya kuwasajili lakini wamekuwa wazito kuwatumia wachezaji husika!
Angalia David kameta(duchu) kabla hajaenda Simba alikiwasha sana wakamsajili akasugua benchi mpaka akatolewa kwa mkopo kwenda biashara kisha Geita na Mtibwa wakaona anakiwasha wakamrudisha ameishia kupiga picha za uzinduzi wa jezi kwa sasa!
Nenda kwa dogo Mohamed mussa kutoka Zanzibar walisajili kwa mbwembwe nyingi lakini sikumbuki amecheza mechi ngapi mpaka Sasa tokea asajiliwe na nasikia wanataka kumtoa Tena kwa mkopo dirisha dogo!
Nenda kwa wakina jimysoni mwanuke walikotoka walikuwa wanakiwasha wameenda Simba mda mwingine ata kukaa benchi tu hawakai!
Kuna orodha ndefu ya wachezaji vijana ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu sana waliposajiliwa pale Simba. Nafikiri kuna tatizo kubwa kwenye scouting yao aidha hawamshirikishi Kocha husika ama wanasajili kisiasa tu wakisikia gazeti limeandika Yanga inamtaka fulani wao wanakurupuka kwenda kumalizana na mchezaji aliyetajwa matokeo yake anakuwa haendani na mfumo wa kocha anaishia kusugua benchi!
Sasa wamemgeukia LADACK CHASAMBI dogo wa Mtibwa, nasikia wamemalizana nae, swali ni je, watamtumia?
Kijana bado ni mdogo sana kiumri na wakienda kumpiga benchi ndio inakuwa wanaua kiwango chake bado anahitajika kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kulinda kiwango chake!
Nafikiri na wasimamizi wa Hawa wachezaji awako makini ata kidogo wanachoangalia ni mpunga tu wakishapewa awaangalii kesho yake itakuwaje kwa kipaji cha mchezaji, Simba kwa sasa sio sehemu sahihi ya kumpeleka mchezaji kijana ni Bora wangemtafutia timu nyingine ya level za mtibwa ili kijana aendelee kupata nafasi ya kucheza tofauti na Simba ambayo inahitaji wachezaji waliokwisha komaa ndio wanaowaamini watawavusha!
Pamoja na fedha wanazovuna wasimamizi wa hawa wachezaji inatakiwa pia waangalie wanavyolinda vipaji vya wachezaji husika!