Siloam church

Hata Mimi sielewi kuhusu hili dhehebu mwenye taarifa atujuze

Hilo ni moja ya cults zilizopo duniani.
Mafundisho yao yanakinzana na mafundisho ya biblia.
Waumini wake wanalishwa mafundisho ya uongo kama biblia inavyosema" Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa".
Jamani someni maandiko acheni uvivu wa kujisomea biblia ndo maana watu wanapelekwa na kufuata kama bendera.
Mara mnaombewa kwa pesa biblia inawaagiza hao wachungaji kuwa wamepewa bure watoe bure.
 
Kama wahudumu hupagawa wakiombea mtu hawa ni Vodoo. Imaniya huko Haiti. hivi the pool of Siloam na Nabii Elia Original uhusiano ni upi? nijuavyo Siloam iko katika agano jipya lile birika yule mlemavu alikuw anashindwa kuingia kuoga ili apone hadi Yesu alipomponya. Jina Yesu kwa Siloam ni kifo na laana.Wao humtaja Kristo ambaye ni Elia AD2 miaka 2000.Kuliko nijiunge SILOAM bora niwe Banian. Wabaguzi na wana Roho zza Kuzimu. Imani gani hata ndugu na wazazi unawatenga eti wana laana!
 
Mnaumana wenyewe mnanifurahisha.Ila mwisho wa siku najifunza kuwa haya makanisa mengi ya 'kiroho' ni chenga na chanzo cha magonjwa ya akili na mfadhaiko wa nafsi
 
tuko huru na dhambi,Yesu katuweka huru,dhambi haipo maana yesu amelipa garama zake.

Damu ya yesu imetutakasa kabisa na kutuweka huru,Yesu katupa uhuru wa kufanya chochote.

Ukisema kuna dhambi uniambie Yesu alikuja kufanya nini?

Naupenda ukristo kwa sababu moja tu nayo ni kwamba zambi zangu zote zilishabebwa na Mtu mmoja anaitwa Yesu hivyo niko huru.
Yesu kweli alishazilipia ata kabla hatujazitenda kwa kuwa yeye ni Mungu na alishaona, sasa wewe ukitenda unakuwa umefanya remix na unamtesa upya.
 
Hata mimi siwaelewi,wana watu wanajiita sijui kuhani miaka 1000,kuhani amani na upendo,watakatifu,na majina ya ajabu ajabu.juzi waliniletea gazeti lao ndani kuna kalenda ina majina ya miezi yasiyoeleweka.

Anyway ukristo una mambo mengi,hivyo kutoa fursa vikundi vingi vya kidini kuanzishwa wakiwa na tafsiri yao wakiwemo masalia,babu wa loliondo,davidians etc.

Nachoupendea ukristo ni jambo moja tu,unafundisha kwamba Yesu alifuta dhambi zote kwa hiyo hakuna dhambi duniani. Tuko huru kufanya chochote maana hakuna dhambi,Yesu alilipa garama ya tukifanyacho. Thank you Jesus.

naona ukristo wa digital huu wa kwamba Yesu alifuta dhambi zote
 
Huyu bwana ameelewa hayo maswali? mbona hajajibu kabisa au hana majibu katika maswali yaliyoulizwa? Mzito Kabwela jibu hayo utueleweshe hiyo imani. Usikimbie maswali hayo mafundisho yako utayatoa tukipata majibu ya hayo maswali!!
 
Huu sio mtazamo wangu ndiyo mafundisho yanavyotaka, l

Ni mafundisho yanavyotaka kwa tafsiri yako unayoelewa wewe. Kwa tafsiri ya wengine wanavyoelewa si hivyo ndio maana kuna madhehebu tofauti yanayotafsiri mafundisho yale yale mistari ile ile tofauti.

Kwa mfano wewe unaweza niona mimi nimepotoka lakini na mimi nakuona na wewe umepotoka vile vile.Na tukiachwa tuendelee kubishana ngumi zitawaka sababu kila mmoja ana tafsiri yake ya nani muislamu zaidi kuliko mwingine na nani anayejua mafundisho kuliko mwingine.

Ndio maana nikasema tukubaliane kutokubaliana.
 
Yesu alishalipa garama za wakifanyacho na kufuta tuhuma juu yao.

Mkuu BT in kwa wale waaminio na kumfuata
Sio eti ndo tuendelee kutenda dhambi kisa zilishalipiwa gharama bila toba no...lazima utubu na umpokee kuwa Bwana na mwokozi wako hapo ss unakuwa umelipiwa
 
asante kwa ufafanuzi mzuri...nimejifunza pana watu wanabisha tu bila kujua...
kama dhambi hakuna...kitabu cha ufunuo ni cha kazi gani?!!
pana mtu mmoka alikuwa anasema chochote unachambiwa na mchungaji au mtume nk ni lazima umuulize maswali kama kwa nini+kivipi nk na kukaa tu kama mfu.

kuna haja ya #unknown aje na andiko kitakalo justify hayo madai yake. kwamba hakuna dhambi duniani.

Yesu amekuja kutoa second chance (nafasi ya upendeleo) ili watu tutubu.

Hahaaa
Huyo anaitwa pastor maboya ni noma.
Lazima uhoji unachoambiwa na mtumishi sio kupelekeshwa
 
Ni mafundisho yanavyotaka kwa tafsiri yako unayoelewa wewe. Kwa tafsiri ya wengine wanavyoelewa si hivyo ndio maana kuna madhehebu tofauti yanayotafsiri mafundisho yale yale mistari ile ile tofauti.

Kwa mfano wewe unaweza niona mimi nimepotoka lakini na mimi nakuona na wewe umepotoka vile vile.Na tukiachwa tuendelee kubishana ngumi zitawaka sababu kila mmoja ana tafsiri yake ya nani muislamu zaidi kuliko mwingine na nani anayejua mafundisho kuliko mwingine.

Ndio maana nikasema tukubaliane kutokubaliana.

Kumbuka kwamba mimi sikulazimishi uamini kile ninachokiamini mimi isipokuwa najaribu kukuelewesha uelewe hili jambo kwa mujibu wa uislam, nimekutolea mifano mingi lakini naona bado hunielewi, labda nikwambie tu kwenye mafundisho ya uislam hakuna mkanganyiko kila kitu kiko clear, hakuna aya zinazokinzana, wala hakuna hadith na sunnah za mtume (s.a.w) zinazokinzana na Qur-an, mbali na hilo, wanazuoni wote wa kiislam toka enzi hizo hadi sasa hakuna mwanazuoni aliyetafsiri au kutoa mafundisho yanayokinzana na Qur-an, Hadith na Sunnah za Mtume (S.A.W), hivyo wewe ukileta jambo jipya kwenye uislam lazima watu watakushangaa na wewe mwenyewe utakuwa umepingana na mafundisho ya dini na kwa maana hiyo utakuwa umejitoa kwenye uislam kwasababu utakuwa umeanzisha mafundisho yako mwenyewe. Mf. uislam unasema Mtume Muhammad (S.A.W) ndio mtume wa mwisho na hatakuja mtume mwingine hadi kiama kinasimama, (mwisho wa maisha ya dunia), lakini sasa kuna hao wewe unaowaita kuwa ni madhebu ya kiislam akina ''Shia'' wao wanapinga qur-an na kusema mitume inaendelea sasa hao ni waislam? mi nataka uilewe hivi kwanza, sio suala la kukulazimisha au kupigana ngumi au kukubaliana kutokubaliana, kwanini tusikubaliane wakati mambo yako wazi.
 
Hahaaa
Huyo anaitwa pastor maboya ni noma.
Lazima uhoji unachoambiwa na mtumishi sio kupelekeshwa

yeah niliona clip yake kwa watsapp jina likawa limenitola thanks.

yeah lazima uhoji maana hata Bwana Yesu alipokuwa akifundisha enzi zile wanafunzi na watu waliomsikiliza walikuwa na maswali.

why not you kutomhoji huyo mwalimu wako leo hii.?!
 
Back
Top Bottom