Sikutegemea kama mdogo wangu Nape naye angelimia meno, wengi mjiandae

Magufuli ni upepo tu hana alilolifanyia nchi hii zaidi ya kujineemesha yeye na kundi lake ujenzi hana mfano mzuri hadi leo amekataa kutoa ripoti ya CAG maana ujenzi kulikuwa na madudu na hadi amewanyima fedha mwaka huu za kufanyia kazi Magufuli ni mfano mbovu kuwahi kutokea Tanzania vigezo vyote vya kimaendeleo kiuchumi kisera,kisheria na kijamii ni zero kama yule laiyemweka mkoa wa Dar es salaam
 
"Matendo bila dira Ni kupitisha muda tu Na dira bila matendo ndoto za mchana; Lakini dira pamoja Na matendo vinaweza kubadili Ulimwengu". Alipata kusema Mandela.Ukiwa unajua unakoelekea Na dira Ni nzuri hakuna kutazama nyuma.Hakuna kurudi nyuma wala kukubali kugeuka jiwe.Kristu aliwahi kubainisha nadharia hiyo kupitia kwa Mwinjili LUKA; 9:62. Kwamba yoyote aliyekwisha kutia mkono kulima kwa Plau kisha akatazama nyuma hafai katika Ufalme wa Mungu.Na Mtakatifu Augustino alisema:" Mashariki ikikuita usitazame Magharibi".

Kwa kipindi cha miaka 30 nchi yetu ilikosa dira na matendo.Kuna wakati tulijikuta tuko Na dira tu Lakini hakukuwa Na hatua zozote kuelekea tulikokuwa tunakuona.Kuna wakati tulikuwa tunatembea kuelekea kusikojulikana.Hakuna wakati wowote tulitumia dira na matendo pamoja.

Safari ya Wana-israel iliacha Watu kadhaa njiani wamekufa kwa sababu walitaka short cut.Walitaka Mungu afanye kadri ya hisia Na matakwa yao. Ni wale waliovumilia ndio waliofika nchi ya ahadi.

Wale ambao hawakuelewa kuwa furaha ya kukombolewa ingekuja baada ya magumu njiani hawakufika kabisa Kanaani.Ulimwengu ulipatikana toka kwanza katika ukiwa.Uumbaji ulifanyika kwa sababu kulikuwa Hakuna chochote.Kulikiwepo udhaifu (nothingness).

Wana-israel walipopata Faraja kutoka ushaifu(magumu/mateso). Yesu Kritu akaleta ukombozi baadaye Lakini mwanzo wake ukiwa kuzaliwa katika Kinyesi cha Ng'ombe.Mitume wa Yesu wakachukuliwa Wadhaifu(wavuvi, mafisadi/watoza ushuru). Zaidi ya yote ukombozi ukapatikana kwenye mti wa Msalaba.Kifo cha aibu.Yote haya yatoshe kutufundisha watanzania.Hakuna Neema yoyote itamwagika bila kupitia magumu.

Raisi Magufuli asonge mbele.Kama nyuma (sasa) Ni Giza Basi mbele Ni kweupe.Kama Sasa Ni njaa muda ujao Ni shibe.Asitazame nyuma kama kufanya hivyo Ni kuambulia makelele ya Watu wasio Na maono.Asitazame nyuma kama kufanya hivyo Ni kuona " machozi na maiti" tu za mafisadi waliokuwa wananeemeka Na jasho la Wengi.Musa akusitasita wala kupepesa macho kwenye kuipiga bahari ili iwafunike Farao Na wanamtandao wake.

Kuna Watu Wengi sana walipoteza muda Na mali zao juu ya Taifa hili.Mwalimu Nyerere akapoteza ajira hadi akawa analala kwenye kijumba kisicho Na heshima kule Butiama Hata baada ya kutumikia nchi kwa miaka zaidi ya 20.

Kuumia mkono kwa Nape Sio warranty ya kuwa Na sauti ya mwisho juu ya Taifa hili. Sio warranty ya kukosa unyenyekevu Na utii.Kristu mwana wa Mungu Na Mungu alitii hadi SAA ya Mauti yake.Basi karibuni tulimie meno kwani ndio njia ya kufikia mafanikio Na maendeleo ya Taifa letu.
 
Kwahiyo una mnanga nape huku ukiwa umejificha nyuma ya keyboard !!!!
Pamoja na mapungufu ya Nape ila katika suala la vita dhidi ya madawa ya kulevya na uvamizi wa clouds alikuwa sahihi zaidi kama kiongozi ukilinganisha na makonda au sizonje.
Siku likikukuta utalimia makalio afadhali nape kalimia meno na Bado kaonekana shujaa na jamii.

Mwafaa!!!!

Jojipoji koromije
 
Una kila dalili kuwa humjui vizuri
Marehemu Kanali Moses Nnauye na mchango wake uliotukuka ktk Directorate of mass mobilization ndani ya TANU na baadaye CCM , nashauri anzisha thread ya swali upewe msaada.
 
Mimi Nape aliniacha hoi pale aliposema eti ameipigania CCM tangu Baba yake na kuitoa shimoni, hapo ndipo nilipochoka, kama Nape anasema hivyo Watoto wa Sokoine waseme nini ambao Baba yao alikufa akiwa kazini kuipigania CCM? Huyu Nape amepotea sana na ameniboa sana!
Uelewa wake mdogo sana, Je Kinana atasemaje? yy alikuwa mwajiliwa wa CCM na alipaswa kufanya kazi kwa budii.
 
Nape anavuna alichopanda wala hatuna sababu ya kumhurumia, anatafunwa na uovu aliofanya huko nyuma na bado utamtafuna hadi kaburini. Kumbekeni pia mbali na uhuni, ushenzi.udhulumati na wizi ktk uchaguzi wa 2015 NI NAPE ALIPIGANA SANA KUHAKIKISHA UHURU WA HABARI UNAMINYWA, DEMOKRASIA INAKANDAMIZWA! Nilitamani yule jamaa aliyetoa silaha angempiga japo kidole cha mguu ibaki kumbukumbu kichwani kwake
 
Ipo siku tutashangaa kusikia na wewe unalimia meno.
Hakuna aliye salama, Nape na wewe unadhani ni nani aliyemsifia?
 
Nape ilikuwa lazima alipe gharama ya yale matusi aliyokuwa anatukana bila "kidhibiti mwendo". Naamini sasa anajua kuwa yapo maisha baada ya uchaguzi. God must be fair
 
Mimi Nape aliniacha hoi pale aliposema eti ameipigania CCM tangu Baba yake na kuitoa shimoni, hapo ndipo nilipochoka, kama Nape anasema hivyo Watoto wa Sokoine waseme nini ambao Baba yao alikufa akiwa kazini kuipigania CCM? Huyu Nape amepotea sana na ameniboa sana!
yaani kwako mfia chama mpaka awe amekufa? una akili ndogo kweli wew umeona sokoine tu je baada ya sokoine hawapo wengine? hujui hata umeongea nini mimi sio ccm ila nape na kinana mchango wao kwa ccm hakuna asiujua hata kuna usemi wake wa goli la mkono wew acha tu ili tu ccm irud madarakani
 
ndugu mleta mada! ni vizuri kuweka akiba ya maneno! napelembe ni kada wa ccm kindakindaki kuliko wewe! bado yupo moyoni mwa rais magu!

siku akilamba shavu lingine utatamani uyameze maneno yako!
 
Nape naye angekuwa ni miongoni mwa walimia meno kwa jinsi alivyojidai eti yeye ni Kada kindakindaki.

Sasa wanaLumumba wanakulana nyama!!! Kama mwalimu alivyosema " ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha" We are spectators!!
 
Back
Top Bottom