Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi

Mag3,
Nafikiri unachanganya vitu sio kuwa upande mmoja ulishinda pale Znz 1991, Ad died a natural death. Ni kuwa sera za AD zilishindwa na hii ilikuwa wazi kwa kila mtu viwanda vilikufa, sera mbovu, uonevu, hakukuwa na uwazi na watu walikuwa hawana imani tena na AD. Nyerere alikuwepo na alilijua hilo sera zake run to the ground...vilevile ukumbuke wakati huo Berlin wall came down na wazi sera za kikomunisti zilifikia mwisho wake.

Ukweli ni kuwa hizi sera zilikuwa zinaonea watu, kama unakumbuka ule mpango wa kulazimisha vijiji bila kuwa na huduma muhimu, uonevu wa kimabavu, no democracy, no freedom of speech na maovu mengineo yalikithiri Tz. wengi wetu ilikuwa ni never ending nightmare ambayo mwisho wake ulikuwa wazi kuwa haukuwa mbali. Abraham Lincoln alisema 'You can fool some people some time BUT you can't fool all the people all the time'

Nawakilisha
 
Mimi tofauti na maoni ya wengi nakuwa na wasi wasi na msimamo wa wachangiaji wengi hapa. Inaonekana wazi kabisa kuwa si wote wamelisoma na kulielewa Azimio la Arusha na hivyo kutojua kwa nini swala lake linaanza kuibuka hivi sasa. Wanachojaribu ni kulitafsiri na kulihukumu kwa kuangalia wanachodhani yangestahili kuitwa mafanikio yake. Matokeo yake wanashindwa kuelewa malengo na sababu za kupitishwa kwa Azimio la Zanzibar na athari za kitendo hicho kwa Azimio la Arusha na mustakabali wa taifa kwa jumla. Nashauri watu watafute muda walisome kwanza kabla ya kuchangia ili wakwepe kukurupuka kama anavyokurupuka Mwinyi hivi sasa - ni ushauri tu.

Tuliokuwapo viwanja vya Mnazi Moja mwaka 1967 tuliziona sura nyingi zilizojaa matumaini na pia sura chache zilizofadhaika na kujaa woga. Tulijua vita vimetangazwa - vita iliyowaweka wananchi wenye moyo wa kujenga taifa lao upande moja na wenye meno ya kuila taifa upande wa pili. Ninachoweza kusema ni kuwa ilikuwa vita ngumu hasa kwa upande moja kwani pamoja na kuwa wengi, hawakuwa na nyenzo kama wenzao waliotumia nguvu ya pesa. Hivyo mwaka 1991 ushindi ulipatikana kwa upande moja huko Zanzibar na jemadari aliyeongoza hivyo vita ni Al Haj Ali Hasan Mwinyi. Leo hii anatokea na kudai hakushinda, sasa waliotangaza ushindi ni akina nani ?

- Mkuu una maana vita ilitayarishwa bila ya kuhakikisha kuwepo kwa nyezo za kuvifanikisha in advance au?

- Mimi ningeshauri kwamba wa-Tanzania tuachane na mambo ya kale tuanze kutafuta ya kutupeleka mbele maana hayo ya zamani simply yalishindwa na wote sisi wananchi na taifa zima ni wa kulaumiwa, sasa tutafakari na tutafute mbinu za kutupeleka mbele.

FMEs!
 
- Mkuu una maana vita ilitayarishwa bila ya kuhakikisha kuwepo kwa nyezo za kuvifanikisha in advance au?

- Mimi ningeshauri kwamba wa-Tanzania tuachane na mambo ya kale tuanze kutafuta ya kutupeleka mbele maana hayoya zamani simply yalishindwa na wote sisi wananchi na taifa zima ni wakulaumiwa, sasa tutafakari na tutafute mbinu za kutupeleka mbele.

FMEs!
Nakubaliana kabisa na wewe mkuu. Sasa hivi kuna vacuum ya vision yetu sisi kama Taifa. Hatuna Azimio la Arusha na hatuna ubepari. Tuna wizi wa mali ya umma.
 
My take

There is nothing wrong kumpenda na kumuheshimu Nyerere , bila matusi n.k

Tatizo ni pale tunapotaka kuamini it was the only solution ya kutatua matatizo yetu, tatizo na kutokubali kulikuwa na makosa na AD inataka kuwa dini na siyo reality, tatizo ni kutokuwa na watu shupavu wa kulisimamia kwa vitendo.,Kuhubiri na kushawishi watu, AD ni ushawishi zaidi,

Waberoya,

Ukisoma maelezo hayo juu, hasa yenye bold, naanza kuelewa kuwa unafahamu nini sisi wengine tunalilia. Ila kwa makusudi kabisa, unatafuta makosa ya AD na kuyatumia kuonyesha kuwa AD ni balaa ya Tanzania.

Hakuna anayesema THIS WAS ONLY. Narudia kusema, unafahamu nini sisi tunataka kusema ila unaPINDISHA kwa makusudi kabisa maelezo yetu ili tu kuonyesha kuwa tunafanya makosa makubwa kabisa.

Labda niandike kwa ufupi. Kuanzishwa kwa AD kulikuwa kumejaa makosa au nisema kulisaidia kwa wakati ule ila kabla JKN hajaondoka na hasa akifahamu kuwa tunaelekea kwenye vyama vingi (hili alisaidia lianzishwe Tanzania) kuna baadhi ya mambo ya AD alitakiwa kuyaingiza kwenye katiba ya nchi na yasiyofaa basi ayaaondolee mbali na yeye mwenyewe ALIUWE rasmi Azimio la Arusha. Nasema hivyo kwa sababu AD ilikuwa chini ya chama na nchi ilikuwa ni ya chama kimoja.

Wakaja wajanja wakanja wakaona hili ni tatizo kwao. Wakitumia njia mbalimbali na nina imani hata hao IMF na World Bank, wakaanza kulihujumu kidogokidogo kwa miaka mingi. Mwisho ikaoenekana kwa watu wengi (soma maelezo ya FMes hapo nyuma) kuwa AD inatajirisha watu wachache na kuwazuia wao. Ndipo wakamuweka sawa Mzee Mwinyi.
Mwinyi bila kufahamu/kwa kufahamu akauvaa mkenge na kwenda Zanzibar na kuliuwa kabisa AD.

Baada ya kuuwa AD rasmi, yale mabaya yote na mazuri ya AD yakawa yamekufa. Katika mazuri machache ya AD ilikuwa MIIKO YA VIONGOZI. AD ilikuwa na hili swala muhimu. Viongozi dunia nzima wana matatizo yaleyale ya kutaka kujitajirisha. Nchi za wenzetu huwa wanakwama kufanya hivyo kwa sababu ya miiko ya viongozi na kuwepo vyombo maalumu ambavyo vipo tayari kuwashughulikia mara wanapovunja hiyo miiko.

Kinachoendelea kwa sasa Tanzania ni vacuum ya MIIKO YA VIONGOZI. Kama Mwinyi angelivunja AD na kuichukua miiko ya viongozi na kuiingiza kwenye katiba ya Tanzania, naamini kuwa leo hii angelikuwa anaheshimika zaidi ya JKN. Baada ya miiko ya viongozi kuondolewa, leo hii viongozi wa Tanzania wanajifanyia chochote wanachokitaka bila ya kuogopa kuchukuliwa hatua yoyote.
Wizi wa EPA, Richmond, Deepgreen nk ni mifano michache ya viongozi kujisikia wako juu ya sheria. Kitendo cha waziri kwenda kuweka sahihi mikataba nje ya Tanzania na tena kwenye caffee inatia kinyaa.

Kikwete na ubovu wake, kama akirudisha miiko ya viongozi na kuweka chombo kinachojitegemea cha kulinda hiyo miiko, basi atakuwa ni shujaa wangu mkubwa. Ila hata miiko ikiwekwa na kuwepo chombo kama TAKURURU ambacho kinashughulikia vidagaa, basi ni kupoteza tu pesa.

Ndiyo maana wengine tunaamini kuwa kwa Tanzania inabidi aje kichaa ambaye risasi mbili tatu zitatembea kwa wale wote watakaokuwa wanataka kumpinga kwa vitendo. JKN hawakumpinga kwa maneno ila vitendo, wakammaliza na AD yake.
 
In few years, kutakuwa ni kuulizana "nani aliyesaini mkataba wa Jamhuri ya Muungano wa Afrika Mashariki".
 
Nimeuliza swali hilo hakuna aliyejibu , mtu aje na tangible proof kuwa jamani ehe! wakati wa AD mafaniko yalikuwa haya, na wakati wa Mwinyi tulidorora kiasi hiki!

AD was talks, na Mwinyi amejibu hizo talks na kusema hakuliua! we are living in the world of no talks! action ambazo zinaendana na hali halisi ya natural behaviour ya binadamu!

Ujamaa na kujitegemea (if it make sense) ili uwe effect basi lazima kiongozi awe dictator, kama Nyerere hakuwa na dictator basi maana yake alianzisha siasa ambayo asingeweza kuitekeleza bila kuwa dictator! which is again is another failure!

Somethings just happens, kutafutana uchawi wakati hatuwezi kupima mafanikio ya Azimio hili ni kudanganyana! Laws and order are far superior than AD au whatever!
Hali ya uchumi alipoingia Alhaj ilikuwa mbaya kweli, lakini unapotaka kufanya chochote kuna vitu vya msingi , na vingine ni vile vinavyo imarisha vitu vya msingi, na niliwahi kuongea na mtu moja ambaye ni swahiba/rafiki/ndugu wa alhaj ambaye ni mtu wa system mpaka leo, yeye alilalamika rukhsa ya mwinyi ambayo haikuwa na taratibu, yaani mambo yanajiendea holela holela.

Sasa nikirudi kwenye suala la uchumi wakati Alhaji anaingia ndio ulikuwa na mapungufu yake na hata mwalimu alisema yeye hakuwa malaika au hakukosea, sasa nini kilicho takiwa kufanywa na Alhaji, ni kujaribu kuondoa au kupunguza mapungu yalio tokea huko nyuma, nayo ni ya management za haya mashirika ambayo yalikula taji na mapungufu mengine. madhali yalionekana na mimi na wewe ni wazi na yeye na viongozi wake waliyaona. sasa ni ilitakiwa kifanyike, moja ilitakiwa kufanyika semina elekezi kwa viongozi wa hayo mashirika na makatibu wakuu na mawaziri kuwaelezea nini kinachotarajiwa toka kwao na faida ya kusimamia vizuri mashirika yalio chini ya wizara zao, kubadili mfumo wa uteuzi wa Bodi members, na kuachana na kuweka rafiki/shemeji nk wa kwenda kukuleta pororo.

Kupunguza mzigo wa kiuongozi kwa serikali/raisi angeongeza nguvu kwa bunge kuwa-grill viongozi wa haya mashirika kuhusu matokeo ya biashara zao, na pale walipo hiyaji kuuza iwe nyumba nk wange fanya tathimi ya njia bora ya kutekeleza hiyo sera. na kwa kuwa tulikuwa tunaelekea kwenye soko huria iwe soko la mitaji nk , basi wange ya tayarisha vizuri haya mashirika kufika huko na hata kutuwekea watanzania wote mazingira mazuri ya kununua hizo shares panapo majaliwa, iwe ni kiongozi au mtanzania wa kawaida.
lakini kilicho fanyika kipindi cha mzee ruksa ni mipango ya siku hadi siku, badala ya kuwa na mikakati ya muda mrefu.

Na kwa kuwa wewe naelewa unajua Management basi ni vizuri sisi sote tukajikita katika ile pyramid ya Management na aina ya mikakati ya kila moja.

Top Management 5 to 10 to 20 years
Middle management 1 year to 5 years
Operational level ni daily.

Lakini kilicho fanyika na Top management Yetu ( Baraza la Mawaziri ) ni kufanya Operational level decision, kwamba unauza shirika bila kujua baada ya hapo nini kitatokea, yaani hawakufanya Socio-economic impact assesment na ku-control hizo after effects za matokeo ya maamuzi yao, in short waliangalia maslahi binafsi zaidi kuliko ya nchi.

Hivyo ndio kosa la Mzee ruksa lilipo na litaendelea kutula mpaka atakapo tokea Dikteta moja akarekebisha hali.
 
Waberoya ndani ya Katiba yetu imetamkwa siasa ya nchi yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea ambao practical application yake ni kuchangiana harusi, misiba na kuomba omba wafadhili na wahisani. Aidha viongozi wakiiba tunawatetea wasinyongwe na wananchi na tunawalinda. Just look at our national character as a nation it evolves around kupenda vitu vya dezo na ujanja ujanja uliojikita kwenye ujinga.
 
Comp,
Azimio la Arusha Lilizinduliwa 1967 mpaka hapo inapodaiwa kuwa lilifutwa, ni hatua ipi ya kujitegemea liliwafikisha Watanzania, kati ya hizo ulizotaja?
Makoko wa Uk , kama upo kwa malikia basi utaona hoja za mwalimu zilivyo fanikiwa , mfano ukitaka kupeleka maji kwa watu na ukapunguza gharama si utawashauri wakae sehemu moja ili uweze kuwapatia hiyo bidhaa iwe shule hospitali, maduka, barabara nk na hapo ulipo utaona watu wana kaa kwenye estate, na kuwezesha kujenga miji kutokana na kuwepo kwa watu.

Enzi za UDA basi usafiri mpaka mid night kutegemeana na sehemu, na la asubuhi linaanza mapema. neighbour hood watch ndio sawa sawa na hizo nyumba kumi kumi na kutambuana nani anafanya nini, tatizo kikifanyika kwetu sisi waswahili, unalalamika fulani mnoko kweli.

Sera za Mwalimu ilikuwa ni kuwaondoa Wathungu na ....... ili maduka tushikilie thithi ngozi nyeusi bali ilikuwa ni gradual process ya sisi kujitambua kwamba tunaweza, tuimarishe elimu yetu hata ingefika wakati wa soko huria nk tungekuwa tunajua kutetea kilicho chetu, sio sasa hivi aliye kuibia akikuletea kapelo unamfrahia na kumuongezea nguvu akuibie zaidi.

Yaani Mwl alitekeleza sera za Idi Amini kwa kutumia technique.
 
Wamzz,
Kuna tatizo moja ambalo tunashindwa kulizingatia Azimio la Arusha ilikuwa ni Sera na Mawazo ya Mtu mmoja. Nae alitaka ahakikishe Linakubalika Hatakama alikubaliki, Linatekelezwa Hatakama Halitekelezeki. Mwl Aliamini na Ameondoka Duniani akiamini Hivyo kuwa Fikra zake ni sahihi siku zote hivyo hakuhitaji mchango/msaada wa Mawazo toka popote.

Wakati tunagutishwa "Zidumu Fikra sahihi za Mwenyekiti", Washauri wake wanadai kuwa "Mzee Haambiliki".Sidhani sera inayokwenda mrama isipokubali ushauri na kufanyiwa marekebisho ingeweza kufika au kumfikisha yeyote alipokusudia.
Nyerere alielewa alipokosea na hata alipotoka alisema Yeye hakuwa malaika, tatizo ni pale tunapoacha vitu vya msingi, nalo ni la kujithamini kama tunaweza. Nakumbuka Alipokuwa PM sokoinne kuna mambo aliyo fanya chini ya uongozi wa Mwl ilikupunguza adha kwa watu Mfano kuanzishwa kwa Dala Dala, hata kipindi cha Salim Ahmed Salim kuna vitu alifanya na Mwalimu alikubali.
 
Mag3 kumbe ulikuwepo Mnazi Mmoja 1967, basi labda tulipigana vikumbo au tukionana tunaweza kukumbukana sura zetu.

Nilikuwapo ndugu yangu, ni siku ambayo ni vigumu kuisahau kama ulikuwapo lakini rahisi kuikebehi kama ulikuwa hujazaliwa. Hamasa, mwamko na mtumaini ya Watanzania na hasa vijana wakati huo yaliweza kuutikisa ulimwengu. Nakumbuka heshima aliyopewa Mtanzania nje ya mipaka yetu kwa aliyebahatika kusafiri wakati huo, ni kubwa. Hofu ilitanda si kwa majirani tu bali hata kwa mashirika ya kitaifa - kote walijiuliza itakuwaje hii kitu ikifaulu. Hapana, hali hii isiruhusiwe katu na vibaraka wakapatikana humu humu nchini na wakatumiwa ipasavyo kuihujumu.

Kama kuna watu wananipa kichefu chefu, ni huyu Mwinyi. Angekuwa mtu makini siku alipoombwa kugombea Uraisi angeweza kabisa akasema, thanks but no thanks, hivi viatu siviwezi - siwezi kuvuka huu mto kwani sijui kuogelea. Lakini Mwinyi being what he is, akatumbukia majini akiikokota nchi ya heshima - matokeo yake sasa tunayaona na kuyashuhudia. Okay, kabla yake tuliitwa masikini, sawa tulikubali na kukataa kuburuzwa, naam si masikini jeuri ? Na sasa tuko wapi ? Wezi wa kutupwa na tunamwibia nani ? Sisi, watoto wetu na wajukuu zetu. Mwinyi akae kimya, period.
 
Waberoya,

Ukisoma maelezo hayo juu, hasa yenye bold, naanza kuelewa kuwa unafahamu nini sisi wengine tunalilia. Ila kwa makusudi kabisa, unatafuta makosa ya AD na kuyatumia kuonyesha kuwa AD ni balaa ya Tanzania.

Hakuna anayesema THIS WAS ONLY. Narudia kusema, unafahamu nini sisi tunataka kusema ila unaPINDISHA kwa makusudi kabisa maelezo yetu ili tu kuonyesha kuwa tunafanya makosa makubwa kabisa.

Labda niandike kwa ufupi. Kuanzishwa kwa AD kulikuwa kumejaa makosa au nisema kulisaidia kwa wakati ule ila kabla JKN hajaondoka na hasa akifahamu kuwa tunaelekea kwenye vyama vingi (hili alisaidia lianzishwe Tanzania) kuna baadhi ya mambo ya AD alitakiwa kuyaingiza kwenye katiba ya nchi na yasiyofaa basi ayaaondolee mbali na yeye mwenyewe ALIUWE rasmi Azimio la Arusha. Nasema hivyo kwa sababu AD ilikuwa chini ya chama na nchi ilikuwa ni ya chama kimoja.

Wakaja wajanja wakanja wakaona hili ni tatizo kwao. Wakitumia njia mbalimbali na nina imani hata hao IMF na World Bank, wakaanza kulihujumu kidogokidogo kwa miaka mingi. Mwisho ikaoenekana kwa watu wengi (soma maelezo ya FMes hapo nyuma) kuwa AD inatajirisha watu wachache na kuwazuia wao. Ndipo wakamuweka sawa Mzee Mwinyi.
Mwinyi bila kufahamu/kwa kufahamu akauvaa mkenge na kwenda Zanzibar na kuliuwa kabisa AD.

Baada ya kuuwa AD rasmi, yale mabaya yote na mazuri ya AD yakawa yamekufa. Katika mazuri machache ya AD ilikuwa MIIKO YA VIONGOZI. AD ilikuwa na hili swala muhimu. Viongozi dunia nzima wana matatizo yaleyale ya kutaka kujitajirisha. Nchi za wenzetu huwa wanakwama kufanya hivyo kwa sababu ya miiko ya viongozi na kuwepo vyombo maalumu ambavyo vipo tayari kuwashughulikia mara wanapovunja hiyo miiko.

Kinachoendelea kwa sasa Tanzania ni vacuum ya MIIKO YA VIONGOZI. Kama Mwinyi angelivunja AD na kuichukua miiko ya viongozi na kuiingiza kwenye katiba ya Tanzania, naamini kuwa leo hii angelikuwa anaheshimika zaidi ya JKN. Baada ya miiko ya viongozi kuondolewa, leo hii viongozi wa Tanzania wanajifanyia chochote wanachokitaka bila ya kuogopa kuchukuliwa hatua yoyote.
Wizi wa EPA, Richmond, Deepgreen nk ni mifano michache ya viongozi kujisikia wako juu ya sheria. Kitendo cha waziri kwenda kuweka sahihi mikataba nje ya Tanzania na tena kwenye caffee inatia kinyaa.

Kikwete na ubovu wake, kama akirudisha miiko ya viongozi na kuweka chombo kinachojitegemea cha kulinda hiyo miiko, basi atakuwa ni shujaa wangu mkubwa. Ila hata miiko ikiwekwa na kuwepo chombo kama TAKURURU ambacho kinashughulikia vidagaa, basi ni kupoteza tu pesa.

Ndiyo maana wengine tunaamini kuwa kwa Tanzania inabidi aje kichaa ambaye risasi mbili tatu zitatembea kwa wale wote watakaokuwa wanataka kumpinga kwa vitendo. JKN hawakumpinga kwa maneno ila vitendo, wakammaliza na AD yake.

Kaka sikonge umeeleza vizuri na umeeleza tatizo letu na udhaifu wetu, hujaeleza kamwe ni kwa vipi azimio la arusha lilikataza viongozi kuiba na leo kwa sababu halipo viongozi waibe tu! haujaeleza nguvu ya AD kisheria zaidi ya kuwa ni imani tu! kama Mwinyi alidanganywa na nani? waliomdanganya mwinyi si watanzania? kwa nini hawakulitaka?

AD ka maelezo yako ni kma vile kiti tofauti, special, kiko external ya mwili wa mwnadamu kama speed governor au Helmet kuwa ukivaa tu kama wewe mwizi unaacha, kama wewe mvivu unaacha, it is like a charm!

Mramba na Yona wameenda mahakamani kwa sababu gani ya AD? na je kutokufungwa kwao ni kwa sababu hatuna azimio? ebu tukae chini tu-evaluate tabia zetu , kuanzia ngazi za familia mpaka taifa, tuone matendo yetu yamejaa umimi au uzalendo??, yanajali sisi wenyewe au yanaangalia na wengine. Forget about leaders angalia middle class wanayoishi Tanzania!

Siamini kabisa miiko ya uongozi inapatikana kwenye AD, sijui ma-mesenja na ma-secretary na wanaoficha chenji na kuforge risiti wana miiko gani? wale wale wahandisi, wahandishi , wafanyakazi wa Tanesco, pilisi, manesi, madaktari n.k wanaokula rushwa na kurubuniwa azimio lao liwapi??
 
Nilikuwapo ndugu yangu, ni siku ambayo ni vigumu kuisahau kama ulikuwapo lakini rahisi kuikebehi kama ulikuwa hujazaliwa. Hamasa, mwamko na mtumaini ya Watanzania na hasa vijana wakati huo yaliweza kuutikisa ulimwengu. Nakumbuka heshima aliyopewa Mtanzania nje ya mipaka yetu kwa aliyebahatika kusafiri wakati huo, ni kubwa. Hofu ilitanda si kwa majirani tu bali hata kwa mashirika ya kitaifa - kote walijiuliza itakuwaje hii kitu ikifaulu. Hapana, hali hii isiruhusiwe katu na vibaraka wakapatikana humu humu nchini na wakatumiwa ipasavyo kuihujumu.

Kama kuna watu wananipa kichefu chefu, ni huyu Mwinyi. Angekuwa mtu makini siku alipoombwa kugombea Uraisi angeweza kabisa akasema, thanks but no thanks, hivi viatu siviwezi - siwezi kuvuka huu mto kwani sijui kuogelea. Lakini Mwinyi being what he is, akatumbukia majini akiikokota nchi ya heshima - matokeo yake sasa tunayaona na kuyashuhudia. Okay, kabla yake tuliitwa masikini, sawa tulikubali na kukataa kuburuzwa, naam si masikini jeuri ? Na sasa tuko wapi ? Wezi wa kutupwa na tunamwibia nani ? Sisi, watoto wetu na wajukuu zetu. Mwinyi akae kimya, period.

Mzee Mag3, naomba unisaidie hasa sisi tulikokuwa hatupo kipindi hicho; maswali yangu siyaamini sana

1. Mlikuwa wavivu na hamkujua kufanya kazi mpaka mlipoambiwa muache uvivu ndiyo mfanye kazi?

2. AD lilikuwa na nguvu gani kisheria?

3. Je ipi bora kuweka systems zitakazowafanya watu wafanye kazi, au kuongea kuwa watu wafanye kazi?

4. Je ukiwa kaka kijana wa wakati huo na umeona hali ya sasa unasemaje? je watu hawajitegemei siku hizi kwa sababu hawana azimio?

5. Unaweza kurodhoseha mafanikio ya Nyerere mpaka Mwinyi anachukua nchi? na unaweza kusupport kuwa hili tatizo ambalo halikuwepo kipindi cha Nyerere na hili limetokea baada ya Mwinyi?

6. Azimio la Arusha lilikuwa ni siasa ya mlioamua wote au Nyerere tu na wengine 'mkasema zidumu fikra' zako? na kama ni moto uliokuwa kwa wote iweje Azimio lilikufa suddenly baada JKN kutoka madarakani? je si alama ya kuwa halikupokelewa na wengi? ni kama mtu anahubiri kanisani watu waache dhambi na akitoka hapo ni jukumu la kila mmoja kuamini au kukataa!

Mzee Mag3, kinachoendela hapa si kuwa watu hawajasoma azimio la arusha, wala kumtetea mwinyi, Ni kweli hakuna kingozi aliyeweza kuvaa viatu vya Nyerere, lakini kwa mantiki ipi?

1. Kupiga kura ya ndiyo na hapana?
2. Kusema zidumu fikra zako?
3. Kuwa non approachable?
4. Kutokuwa na demokrasia
5. Kupinga watu fulani wanaoleta mawazo ya maendeleo, typical example akiwa Mtei?

Au unasema kuvaa viatu vya Nyerere kama

1. Kupenda watu
2. Kupenda taifa lake
3. Kujitoa?

Yupi ambaye unafikiri angeweza kuvivaa viatu vya mwalimu?

Mimi naona sio kutokuvaa au kuvaa naona results ya mfumo wa kijamaa ambayo haukufanya watu wawe free kuwaza, kusema , kukosoa n.k ni athari mpaka leo hii

Ninaposema hayo msikosee na kusema namdharau MWALIMU hapana-he is a person who inspired me to think like him! but I amnnot to forcing people to agree with me! ni katika uwazi huu tutajua alikosea wapi na sisi tufanye nini!

Mag3 leo unaishi, unafanya kazi na watoto wako wanafanya kazi. ulishawahi kutangaza azimio la nyumbani kuwa kila mtu sasa afanye kazi??

AD was meant for UNITY, kuamsha ARI, kuleta UMOJA, kufanya mapinduzi ya KUJITEGEMEA kama taifa; lakini

1. Haukuwa msahafu!
2. Ilikuwa ni Imani ambayo mtu ana hiyari kupokea au kukataa!
3. Haikuwa system itakayomlazimisha kila mtu kuifuata!

Ili binadamu wanyoke na ku-obey Na wote kuwekana sawa lazima

1. weka/fuata katiba
2. weka/fuata sheria
3. weka system zitakazowalazimisha watu wazifuate !

Failure ya leo siyo kwa sababu ya AD, ni matatizo yetu makubwa sana; nimesema kama leo hii wakatokea watu na kusema AD is the only way, then inabidi tuwe na azimio lingine kabla ya Arusha! AZIMIO LA WATU BADILIKA NA KUFUATA SHERIA NA KATIBA

sijasema content za AZIMIO na hasa ujamaa wenyewe, uliotudumaza mpake leo hii!

Kaja Mkapa, Kaja Kikwete, matatizo mnataka mumtupie Mwinyi, then kuna wengine watamtupia Nyerere!

Lowassa, RA, Karamagi,Chenge, Balali, ... wote hawa wanasubiri azimio litangazwe ndio tuwapeleke jela!

Au mimi niliyezaliwa baada ya azimio nikiingia serikalini niibe, mkinikamata nijitetee kuwa Azimio halipo, it is not documented anywere that I should not steal!

wakubwa mtusaidie otherwise maswali haya hayakwepeki hata siku moja!

Yaani kwa watanzania ili viongozi wao waache wizi tangaza azimio la arusha au kigoma! au wapeleke Ngurdoto kwenye semina ya uongozi!!

We have problems, tatizo si kuwa au kutokuwa na azimio la arusha, tusipopata kiini cha tatizo letu then tutablame kila mtu dunia hii, we are living today, JKN alishapita na mchango wake tumeuona tunampa marks were he did right na mkasi where he didi wrong, si alikuwa binadamu?

Tusichanganye imani/beliefs na mambo ya kitaifa!

By the way, waafrika wote na matatizo yao walikuwa hawana maazimio!
 
Waberoya ndani ya Katiba yetu imetamkwa siasa ya nchi yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea ambao practical application yake ni kuchangiana harusi, misiba na kuomba omba wafadhili na wahisani. Aidha viongozi wakiiba tunawatetea wasinyongwe na wananchi na tunawalinda. Just look at our national character as a nation it evolves around kupenda vitu vya dezo na ujanja ujanja uliojikita kwenye ujinga.
Haya maneno nimeyakubali kamili kamili mkuu. Hakuna nchi isiyo na dira. Sisi lazima tukubali kuwa tunaenda enda tu kwa ujanja ujanja tena kwa hasara yetu wenyewe maana sijui ipi ni siasa tunayoifuata.
 
Waberoya ndani ya Katiba yetu imetamkwa siasa ya nchi yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea ambao practical application yake ni kuchangiana harusi, misiba na kuomba omba wafadhili na wahisani. Aidha viongozi wakiiba tunawatetea wasinyongwe na wananchi na tunawalinda. Just look at our national character as a nation it evolves around kupenda vitu vya dezo na ujanja ujanja uliojikita kwenye ujinga.

Tukijitazama kwenye kioo, tukaangalia majirani zetu, tukiangalia makazini, mashuleni , na maofisini, unaona kabisa tunajaribu kukimbia matatizo yetu.

watu wanafanya harusi za milioni 50, the very same people ukiangalia vijiji wanavyotoka , jamii za huko hawana madawti achilia mbali uwezo wa shule, kenya wao walishajifunza kutoa michango ya elimu!

Kuna wakati tunajisahau sana

Mabadiliko yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja! tukiulizana humu na style zetu za maisha kama zinaendana na hali ya kitanzania na ndugu maskini na wahitaji kibao utaona kabisa tuna kufuru!
 
- Mwalimu alituletea Mwinyi, Mwalimu alituletea Mkapa wote tumeona kazi zao, tumekwama sasa tutafute njia a kujinasua tulipokwama, badala ya kulaumiana yaliyopita yamepita, kwenye hizi chaguzi Mwalimu alikosea hawa hawakuwa na sifa hata moja ya urais, tukubali na tusonge mbele! Hatujakwama kwa sababu ya Azimio, hapana ni kwa sababu ya uongozi mbovu toka tupate uhuru miaka 47 yote imekwua ya bure! Sio kosa la Mwinyi wala la Mwalimu ni wananchi wote na hili taifa kwa ujumla.

Respect.

FMEs!
 
Waberora,

Azimio la Arusha liliweka miiko. Ila kwa vipi lilikataza kuiba, hicho kitu hakipo duniani.

Hata leo Tanzania ukiuwa unaweza kunyongwa kikatiba, ila hiyo sheria haizuii watu kuuwa. Sasa unaponiuliza hilo, sijui uma maana gani. Isije kuwa yale ya kuuliza pua iko wapi wakati mdomo unauona.

Sasa hivi hiyo miiko tu haipo. Sasa hata Yona na Mramba kuwashitaki na kushinda ili jamaa waende jela hicho kitu hakipo. Walau zamani mtu anaweza kushtakiwa na akafungwa au kufukuzwa kazi. Lowassa pamoja na kuvunja miiko, bado WALIMUOMBA aangalie kipi cha maana akifanye. Yes, aangalie na si ashtakiwe na kufukuzwa kazi na mwisho kufungwa. Hii ndiyo hali mbaya ya vacuum iliyotokea baada ya kuvunjwa kwa AD.

Kukaa chini na kuangalia tabia zenu hilo ni kupoteza muda. tabia zetu pote duniani ziko sawa kabisa. Ila wenzetu wanafuatilia sana sheria. Kama JKN angelifahamu hili na kujenga kitu kama FBI, CIA na Sherrif/POLISI basi ninaimani leo hii watu kama Rostam Azzi, Lowassa na akina Mramba wangelikuwa wafanyakazi bora wa Tanzania huku wakiiletea Tanzania faida kubwa. Siwezi kushangaa kuwa hawa watu walikuwa na moyo sana ila wakakatizwa tamaa na wale wengine wa zamani. Kama Kikwete aliona wanavyoiba wengine, leo hii kawa juu unafikiri yeye ataacha? Ila kama kuna chombo chochote kinafanya ULINZI na USALAMA wa rasilimali zetu unafikiri ataiba?

Haijalishi AD au katiba au chochote kile wewe utakaa na kusema tukifanye. Tanzania inabidi tuwe na chombo cha kuwalinda viongozi. Wabunge tumeshaona haliwezekani. Kama tukiwa na FBI yetu na hawa jamaa hawafanyi mchezo (kumfunga paka kengele) basi mchezo utakuwa umeisha. Miiko iwepo na chombo maalumu kisimamie. Huu ndiyo mzizi wa fitina.

Kama kuna kiongozi hafai, basi sidhani kama atakwenda juu. Leo hii tunasikia Mrema wa TANROAD kaajiliwa kwa mlango wa nyuma. Boss mpya wa NHC kaajiriwa kwa mlango wa nyuma. Pesa kibao zimetumia kumchagua CEO na watu wanakuja kuajiri kivyao na hakuna kitu kinatokea kwa hawa Mawaziri. Sasa unategemea huyu boss wa NHC atakuwa kweli makini? Kwanza ataambiwa achote pesa aipe CCM na hatapinga kwani wamemuajiri kwa kutumia penseli. Wanamtisha kuwa ukileta ya kuleta, form one utafutwa.
 
Mzee Mag3, naomba unisaidie hasa sisi tulikokuwa hatupo kipindi hicho; maswali yangu siyaamini sana.............

Mkuu Waberoya, I wish I had the time lakini hata hivyo nitatafuta muda nitoe majibu kwa kiasi ninachoweza. Bahati mbaya najaribu kufanya shughuli nyingi kwa wakati moja ingawa napitia humu kila nikipata muda mfupi.

Hata hivyo kabla sijaanza naomba tuelewane kitu kimoja. Kwanza, pamoja na kuwa kijana wakati huo, sikuwahi kujiunga na TANU hata siku moja wala sikuwahi kukipigia kura TANU (au CCM) hata siku moja. Sababu kubwa ni kuwa toka nikiwa shuleni sikuamini katika demokrasia ya chama kimoja na hata shuleni nilishiriki sana katika mijadalo kama ilivyoitwa "debate" wakati huo. Pili, sikuwahi kufanya kazi serikalini kama civil servant, kwani toka nimalize shule nilifanya kazi nje ya nchi kwenye makampuni mbalimbali - kazi nilizozitafuta mwenyewe.

Lakini pamoja na yote niliheshimu msimamo ulioonyeshwa na uongozi wa wakati huo. Nchi iliheshimika kwa kuwa na vision ya kitaifa na kuwa na kiongozi aliyekuwa tayari kuitetea kwa nguvu za hoja. Nilichoweza kugundua mapema kabisa ni kuwa ingawa wananchi wa kawaida wengi walimpa support, wako ambao mchana walihubiri maji lakini usiku walikunywa mvinyo. Mkuu Waberoya, nikipata nafasi tena nitapitia hoja zako moja baada ya nyingine kama ulivyozitoa ila tu naomba uelewe ni katika misingi niliyoyaelezea hapo juu.
 
Waberora,

Azimio la Arusha liliweka miiko. Ila kwa vipi lilikataza kuiba, hicho kitu hakipo duniani.

Hata leo Tanzania ukiuwa unaweza kunyongwa kikatiba, ila hiyo sheria haizuii watu kuuwa. Sasa unaponiuliza hilo, sijui uma maana gani. Isije kuwa yale ya kuuliza pua iko wapi wakati mdomo unauona.

Sasa hivi hiyo miiko tu haipo. Sasa hata Yona na Mramba kuwashitaki na kushinda ili jamaa waende jela hicho kitu hakipo. Walau zamani mtu anaweza kushtakiwa na akafungwa au kufukuzwa kazi. Lowassa pamoja na kuvunja miiko, bado WALIMUOMBA aangalie kipi cha maana akifanye. Yes, aangalie na si ashtakiwe na kufukuzwa kazi na mwisho kufungwa. Hii ndiyo hali mbaya ya vacuum iliyotokea baada ya kuvunjwa kwa AD.

Kukaa chini na kuangalia tabia zenu hilo ni kupoteza muda. tabia zetu pote duniani ziko sawa kabisa. Ila wenzetu wanafuatilia sana sheria. Kama JKN angelifahamu hili na kujenga kitu kama FBI, CIA na Sherrif/POLISI basi ninaimani leo hii watu kama Rostam Azzi, Lowassa na akina Mramba wangelikuwa wafanyakazi bora wa Tanzania huku wakiiletea Tanzania faida kubwa. Siwezi kushangaa kuwa hawa watu walikuwa na moyo sana ila wakakatizwa tamaa na wale wengine wa zamani. Kama Kikwete aliona wanavyoiba wengine, leo hii kawa juu unafikiri yeye ataacha? Ila kuna chombo chochote kinafanya ULINZI na USALAMA wa rasilimali zetu?

Haijalishi AD au katiba au chochote kile wewe utakaa na kusema tukifanye. Tanzania inabidi tuwe na chombo cha kuwalinda viongozi. Wabunge tumeshaona haliwezekani. Kama tukiwa na FBI yetu na hawa jamaa hawafanyi mchezo (kumfunga paka kengele) basi mchezo utakuwa umeisha. Miiko iwepo na chombo maalumu kisimamie. Huu ndiyo mzizi wa fitina.

Kama kuna kiongozi hafai, basi sidhani kama atakwenda juu. Leo hii tunasikia Mrema wa TANROAD kaajiliwa kwa mlango wa nyuma. Boss mpya wa NHC kaajiriwa kwa mlango wa nyuma. Pesa kibao zimetumia kumchagua CEO na watu wanakuja kuajiri kivyao na hakuna kitu kinatokea kwa hawa Mawaziri. Sasa unategemea huyu boss wa NHC atakuwa kweli makini? Kwanza ataambiwa achote pesa aipe CCM na hatapinga kwani wamemuajiri kwa kutumia penseli. Wanamtisha kuwa ukileta ya kuleta, form one utafutwa.

Sk mkuu,
Miiko ipi hiyo mnayoizungumzia??? Wakati Sheria na Hukumu zipo toka Enzi za Torati: USIUE USIIBE USIZINI USIMTAMANI MKE WA JIRANI YAKO nk. Na Hukumu ya Mwizi na Akatwe mkono na Mzinzi apigwe Mawe Mwuwaji Auwawe nk, pamoja na kuzilainisha pia zimetushinda kuzifuata.

Sasa tunasingizia miiko miiko miiko miiko, miiko gani zaidi ya hiyo; Mkapa kaiba, Lowasa kaiba, Chenge, Mramba na wote wanaojulikana na ushahidi upo sasa Azimio la Arusha lingesaidiaje? linahitajika la nini? Kwa kesi kama hizi wakati Sheria zipo Jeshi la polisi lipo Ofisi/Idara ya Mwendesha Mashtaka ipo sasa habari za FBI nk zajia nini?
 
Makoko,
Nadhani Sikonge anazungumzia miiko ya uongozi. Hata Marekani wanayo miiko hiyo licha ya kwamba wanazingatia sana utawala wa kisheria. Akina Mkapa na Lowassa waliweza kuiba kwa sababu walijua hakuna atakayewatia hatiani baada ya Azimio la Zanzibar kushika hatamu. That is a big difference to me.
 
Back
Top Bottom