Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye, amevitaka vyombo vya Habari nchini kutoa nafasi sawa kwa wanasiasa wote bila ya ubaguzi.
“Vyombo vyote vya habari wapeni uwanja sawa wanasiasa watimize majukumu yao. Mtu akisemwa, wa upande wa pili apewe nafasi ya kujieleza. Ndio namna ambavyo tutaendesha siasa za nchi yetu. Rais Samia kupitia 4R zake ameelekeza, tuvumiliane, tufanye maridhiano, na haya ndiyo mambo ya kufanya, na Rais ameonesha kwa mfano.” – Nape Nnauye
Kwa upande mwengine Waziri nape amesema,
“Nitoe wito kwa wanahabari, timizeni wajibu wenu kwa kufuata sheria, Serikali haina mpango wa kuingilia uhuru wa wanahabari kutimiza majukumu yao. Kama kuna mahali watu wanaamua kutumia content [maudhui] yoyote wafanye kwa kufuata sheria, lakini hakuna kiongozi yeyote wa serikali ambaye ana mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vyetu vya habari kutimiza majukumu yao.”–Nape Nnauye
Nini maoni yako?
Written by Mjanja M1 ✍️