Siku ya 5 hakuna Maji Dar, Serikali kimya...

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
nashangaa watanzania tulivyowapole. ni siku ya tano jiji la dar halina maji, na wananchi wake kimya. ukipita muhimbili harufu inayosikika ni mbaya sana. sijui ni lini magonjwa ya mlipuko yataanza. hivi wananchi wenzangu ni wajinga zaidi ya serikali au serikali ndio wajinga zaidi ya wananchi. siendi kazini leo siku mbili sijaoga...nawasilisha
 
Muulize huyu....Dar haina maji yeye yuko Iringa kwenye shareha za siku ya amaji duniani

8E9U6566.JPG
 
Tarifa za hivi punde ni kwamba matengenezo yatakamilika kesho.

Hivyo msitarajie maji kabla ya jumamosi.

Mnashauriwa kuchimba vyoo vya shimo kukabiliana na hali hii
 
"Tuendeleeni kuvumilia, hiki ni kisiwa cha amani, tunajivunia", should I say that? Hapana wa-tz tuamke, tujifunike shuka kabla hakujakucha.
 
nashangaa watanzania tulivyowapole. ni siku ya tano jiji la dar halina maji, na wananchi wake kimya. ukipita muhimbili harufu inayosikika ni mbaya sana. sijui ni lini magonjwa ya mlipuko yataanza. hivi wananchi wenzangu ni wajinga zaidi ya serikali au serikali ndio wajinga zaidi ya wananchi. siendi kazini leo siku mbili sijaoga...nawasilisha

Kwani chi hii kuna serikali? Kuna genge la mafisadi wanaojiita serikali.
 
Bomba kubwa la kussuply maji toka Ruvu limepasuka maeneo ya Kerege. Bomba hili hili lilipasuka mwaka jana sehemu hiyohiyo na kusababisha usumbufu huu huu.
Swali la kujiuliza ni Je, hili bomba lilitengezwaje? Tutegemee kuwa na hali hii hii mwakani?
 
sijui lini wananchi watajua haki zao,maji hakuna na watu wamekaa tuu,tatizo viongozi wetu wala hawajui kama maji hayapo coz wao nyumba zao lazima ziwe na maji..Maji ni kitu cha muhimu sana!!
 
watanzania tunatakiwa tuache kukubali excuse za kipuuzi kila kukicha, mara cjui bomba limepasuka, mara matengenezo yatakamilika lini cjui, tunatakiwa tudai maji tu huo upuuzi mwingine hautuhusu, kitaalamu walitakiwa wawe na alternative route, pili walitakiwa wawe na reservoir somewhere ambayo itakua ikitumika kipindi cha emergency tu inamaana siku bomba lote likitakiwa kufanyiwa major overhaul hatutapata maji mwezi mzima au zaidi mpaka zoezi hilo likamilike! tena mtu anaweza akazungumza kitu kwa confidence kubwa kabisa eti bomba limepasuka ndo tunarepai na akaona hakuna tatizo katika alichokizungumza!
 
Yaani mimi nawashangaa sana mnaolalamika kuhusu Dar kukosa maji. Labda mimi ni punguwani....Hivi mbona mimi sioni maji Dar. Kila kukicha mimi nanunua maji kutoka kwa wale wauzao maji kwa magari. Bajeti yangu ya maji kwa mwezi nadhani ni kama Laki moja. Huku ninapokaa kuna ule mradi wanaosema ni wawachina. Mabomba yanaota kutu tu. Hamna lolote. Hem naomba muache kudiscuss hii mada ya eti Dar yakosa maji. Yakosa? Give me a break. Na mnisamehe kama nitawakwaza.
 
Bado mambo hayajawa magumu.Yakichachamaa kila mtu ataandamana mwenyewe.Maandamano ya kimapinduzi hayahitaji JF,TWITTER wala Facebook...
 
Sasa serikali ndiyo mabomba?

Radhia Sweety wakati mwingine huwa unanishangaza sana katika kutetea kwako serikali. Kwa hiyo unataka tuyalalamikie mabomba na siyo serikali? Yaani serikali inasherekea wiki ya maji duniani ili hali watu hawapati maji tena ni Dar ambapo kuna makao makuu ya wizara inayohusika na maji!

Ila kuna jambo la kushangaza, nakumbuka hata mwaka jana wakati wa sherehe za wiki ya maji Dar haikuwa na maji wiki nzima! Sijui maana yake nini.
 
Sasa serikali ndiyo mabomba?

ndiyo yale yale maswali ya sasa mimi ni mvua ninyeshe nijaze mabwawa?
Sasa serikali si mabomba, raisi sio mvua ya nini iwepo serikali na viongozi wanao tumia kodi yetu kulipwa mishahara.
Kwakuwa hawawezi solve matatizo kwakuwa wao si mabomba, wao si mvua, wao si umeme na wao si pesa acha tuwe hatuna serikali matatizo yataji solve yenyewe.
Umenishangaza sana kwa mawazo yako yani ngoja nisiendelee maana bado najiuliza your level of reasoning mpaka sasa
 
Msamehe bure Radhia Sweety nadhani alisoma darasa moja na Faiza Fox. Utetezi wao kwa serikali huja kwa nguvu zote bila kupima hoja husika.
 
watanzania tunatakiwa tuache kukubali excuse za kipuuzi kila kukicha, mara cjui bomba limepasuka, mara matengenezo yatakamilika lini cjui, tunatakiwa tudai maji tu huo upuuzi mwingine hautuhusu, kitaalamu walitakiwa wawe na alternative route, pili walitakiwa wawe na reservoir somewhere ambayo itakua ikitumika kipindi cha emergency tu inamaana siku bomba lote likitakiwa kufanyiwa major overhaul hatutapata maji mwezi mzima au zaidi mpaka zoezi hilo likamilike! tena mtu anaweza akazungumza kitu kwa confidence kubwa kabisa eti bomba limepasuka ndo tunarepai na akaona hakuna tatizo katika alichokizungumza!

Umenena Bona haya si matusi tukisema tunaongozwa na bunch of fools and ******,kila siku tunatoa visingizio visivyo na kichwa hata mkia.
 
Back
Top Bottom