Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Mbona kimnya

DAUDI 1 leta uamuzi wa Julie....duh! patamu hapo.

Jamani mbona nasubiria kwa hamu,

Yuko wapi Daudi 1 jamani

Jaman daudi mbona unatufanyia hivyo ,


Mnamuonea bure Daudi, hili sio kosa lake, ni kosa la akina Shigongo kwa kuchelewa kutoa sehemu inayofuatia ya hadithi hii, na bila akina Shigongo kuitoa hakuna namna ya kuicopy na kuipaste hapa.

Unaweza kuifuatilia moja kwa moja hapa......NI SHIIDA!-22 - Global Publishers..wataiupload tu, vumilieni.
 
ILIPOISHIA
...Likishaondoka zake tu nitakwambia Bitu wangu wala usiwe na shaka!"
"Haya bebi wangu, nakupenda! Wewe ndo kila kitu moyoni mwangu.."
SEREBUKA NAYO SASA...


Baba Juliana aliisoma meseji ile aliyoituma Bitungu kwa hasira kali. Akaizima kabisa simu ile na kuiweka pembeni kisha akainamisha kichwa chake chini na kujikaza kiume. Moyoni alikosa raha, hakuwa na amani tena.

"Hivi mama Juliana wa kunifanyia hivi? Kitu gani ambacho simridhishi mwanamke huyu?"
Alijiongelea na kujijibu mwenyewe. Aliamua kutoka nje ya ofisi lengo likiwa kwenda kupata hewa zaidi. Kile kiyoyozi kilichokuwa kimefungwa ofisini kwake alikiona hakitoi hewa yoyote.
***
Siku nzima mama Juliana alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kila muda alikuwa akimuita Juliana bila kumwambia chochote. Wakiwa wametulia jikoni mara simu ya Juliana ikaita.
"Haloo!"

"Mama yako yupo wapi?"
"Niko naye hapa!"
"Nipe niongee naye."
Bado hasira za maneno kutoka kwa Bitungu aliyokuwa ametumiana naye kwa njia ya meseji hazikuwa zimemuisha.

"Mama! Simu yako, baba anataka kuongea na wewe!"
"Haloo!""Nisikilize kwa makini mama Juliana! Nina jambo zuri nataka kukwambia mke wangu!"
"Nakusikia mume wangu!""Nitachelewa kurudi leo lakini ikifika saa moja nitakuhitaji uje sehemu sawa?"
"Haya niambie ni wapi?"

"Kuna sehemu nitakuelekeza baadaye tukishaambiwa rasmi hapa ofisini kwani bosi wetu ametushtukiza kuwa leo mke wake amewasili mchana na jioni tutajumuika naye katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.""Haya utaniambia mume wangu ngoja niandae nguo ya kuvaa kabisa!"

Baba Juliana akawa ameshacheza na akili ya mkewe. Akaikata simu kwa makogo huku akiamini mtego wake utanasa kwa asilimia zote. Akamtumia na meseji ya msisitizo.
"Usisahau kunibebea na koti langu la suti nililisahau!"
"Haya, umesema saa moja!"
"Ndiyo?"

"Sasa simu yangu unayo nitakujaje mume wangu?"
"Tumia simu hiihii ya Juliana!"
"Haya baadaye basi!"
"Sawa usisahau mke wangu uwepo wako ni muhimu sana kwa siku ya leo.
***
Ilipofika saa kumi na mbili baba Juliana alikuwa bado kazini. Malengo yake ni kuwakutanisha Bitungu pamoja na mama Juliana ili aujue ukweli. Hakuwa ameiwasha ile simu ya mama Juliana tangu mara ya mwisho wamalize kutumiana meseji.

Kitendo cha kuwasha tu simu ya mama Juliana aliyokuwa nayo, meseji mfululizo zikaanza kuingia, zote zikiwa ni lawama kutoka kwa Bitungu."Sweet, kwa nini unanifanyia hivi? Mbona unanizimia simu lakini muda wote nakutafuta?"

Baba Juliana akamjibu meseji karibia zote.
"Sorry bebi wangu jamani, huku kwetu umeme ulikatika na hapa nilipo ndiyo kwanza simu nachati na wewe huku ikiwa kwenye chaji.

"Haya muda si umeshafika jamani fanya basi tukutane mwenzio nina hamu na wewe kweli!"
"Tena una bahati nimeshatoka Bagamoyo tangu saa saba za mchana, nipo maeneo ya Tegeta."
"Huko unafuata nini bwana njoo tukutane baa ya Sweet Mama hapa karibia na Sinza Mori kuna gesti moja nzuri sana."

"Basi nipe nusu saa sweet wangu."
Bitungu alikuwa na pupa. Hakutaka kuambiwa chochote, meseji kutoka kwa baba Juliana kwa kutumia simu ya mama Juliana zilimchanganya. Asilimia zote alijua anachati na mama Juliana.
Shangwe zilimtawala baba Juliana na kujiona zoezi lake linaenda kukamilika ndani ya muda mchache. Tayari alikuwa ameshamteka akili Bitungu na kumsubiria ajilete tu.

"Nimeshafika sweet wangu uko wapi?"
"Nitachelewa bebi ila chukua chumba kabisa kisha niambie namba ngapi nitakuja moja kwa moja."
Muda wote baba Juliana alikuwa eneo la nje ya Baa ya Sweet Mama akimsubiri Bitungu. Bitungu alifika na kuchukua chumba namba 32 kisha akatuma meseji.
"Nimeshafika! Nipo chumba namba 32."

"Haya bebi wangu nipo maeneo hayahaya nikute mlango wazi huko!"
Mama Juliana naye alikuwa amewasili. Alikuwa ameongozana na Juliana lakini alipofika alishikwa na mshangao baada ya kumkuta mumewe akiwa amekaa mwenyewe huku kukiwa hakuna dalili yoyote ya sherehe.

"Juliana amefuata nini hapa?"
"Mume wangu si umeniambia sherehe nikaona bora tuwe wote!"
"Ok, sasa tunaelekea kwenye chumba namba 32 kwenye sherehe yenyewe."

Hofu kubwa ilianza kumjaa mama Juliana. Mapokezi hakukuwa na mhudumu hivyo wakaongoza moja kwa moja wote watatu huku akisitasita lakini baba Juliana alikuwa nyuma yake akimsukuma.
"Sherehe ipo humu ndani ingia!"
Baba Juliana akamsukuma mkewe, akafungua kitasa na kuingia huku akibaki nje ya mlango na Juliana.
"Sweet wangu!"

Haraka Bitungu akamuwahi mama Juliana.
"Nani?"Kabla Bitungu hajamalizia, baba Juliana akiwa na Juliana wakaingia chumbani. Bitungu akashangaa zaidi."Bitungu?"

Juliana uzalendo ukamshinda akasimulia yote kuhusu Bitungu alivyowachanganya na mama yake huku mama Juliana akibaki hajielewielewi.

"Nimejua yote kuanzia mwanzo kisha wewe mama kuanzia leo mimi na wewe ndiyo basi baki na huyo mpumbavu wako. Meseji zote hizi hapa kama ushahidi kwa ndugu zako."
************************MWISHOOOOOO*******************
MICHEPUKO HAIFAI TUSITAFUTE SABABU ZA KUTUFANYA TUCHEPUKE KWANI HAKUNA ALIYEKAMILIKA KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE TUVUMILIANE NA KUCHUKULIANA KAMA TULIVYOKUBALIANA KATIKA MAHUSIANO YETU JIULIZE UTACHEPUKA NA WANGAPI? KAMA UNAONA KNA MAPUNGUFU KWA MWENZIO NI VEMA MKATAFUTA SULUHISHO LA PAMOJA.

KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHER ULIKUWA NAMI MLETA STORI DAUDI1 THE KING
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom