Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti

Asante sana aaah! kumbe umempa Baba Julie, nimekuwekea mzigo wako hapo pemben

Ndiyo nampa pole kwa kushindwa kujua wajibu wake kama kichwa cha familia, na matokeo ndiyo hayo nani alaumiwe mke au mtoto laa....
 
Ndiyo nampa pole kwa kushindwa kujua wajibu wake kama kichwa cha familia, na matokeo ndiyo hayo nani alaumiwe mke au mtoto laa....
Ina maana mwanamke akili zake ni za kushikiwa? yeye mwanamke ametimiza wajibu wake wa kuwa mke? ninavyojua mke ni mshauri wa mume akishindwa mume na mke ameshindwa hapo hakuna mshindi hapo haki iko kwa julie tu
 
NI SHIIDA!-21


ILIPOISHIA
Alichokifanya Bitungu ni kutoka moja kwa moja hadi bafuni na kuoga kwa mara nyingine kisha akavaa nguo na kulipia mule gesti na kuondoka.
“Kama anajijua ni mke wa mtu basi na mimi ni mume wa mtu, naenda kuusema ukweli wote kwa huyo mumewe anayetaka kula sahani moja na mimi.”
SONGA NAYO SASA...


Hakujali giza lililokuwa limefunika. Muda wa saa nne za usiku wala haukumtisha ndiyo kwanza alielekea moja kwa moja hadi kituo cha daladala ambapo napo alikuta patupu. Daladala nyingi zilikuwa zimeshakwenda kupaki lakini hilo halikumuuza kichwa Bitungu.


“Haiwezekani nikaingia matatizoni eti kisa mwanamke!”
Alijiongelea mwenyewe Bitungu huku akisubiri usafiri wa daladala. Hadi nusu saa inakatika bado hakukuwa na dalili zozote za kutokea kwa daladala zaidi ya Bitungu kuendelea kujiegesha kwenye eneo maalum la kukaa abiria.


“Lakini? Hivi kwa nini nisirudi kulala halafu asubuhi nikadamkia huko? Hapana ila nisubiri kwanza tu.”
Bado akili ya Bitungu haikuwa imekaa sawa. Baada ya kukaa kwa muda moyo wake ukaingiwa na furaha. Furaha baada ya kuiona daladala ikiingia kituoni hapo ikitokea katikati ya jiji la Dar.
“Haipakizi tena hii, inaenda kulala.”


Aliongea kondakta wa ile daladala baada ya Bitungu kupitisha mguu wake akitaka kuingia ndani.
“Kama haipakizi sawa nitaenda kulala hukohuko inapolala.”


“Mwana mbona husikii! Hii inalala hapo pembeni mpaka asubuhi saa kumi na mbili ndiyo inahamsha tena.”
“Lakini nyie makonda mnajifanyaga wajanja sana, mnasema haipakizi halafu baada ya muda inapakiza tuwaeleweje?”


Aliongea Bitungu kwa jazba. Lengo lake akilini lilikuwa ni kutoka tu maeneo yale ya Bagamoyo hata kama atafika mjini usiku mnene ingekuwa sawa tu ili mradi atoe dukuduku lake kwa baba Juliana.


Ile daladala ilipomaliza kushusha ilijisogeza hadi pembeni na kupaki. Bitungu alinyong’onyea ikambidi akubaliane na ukweli kuwa muda ule alikuwa amechelewa. Alichokifanya ni kurudi mpaka kwenye ile gesti kwa mara ya pili na kuchukua chumba kingine kwa lengo la kudamkia asubuhi na mapema kwa mama Juliana akauseme ukweli kwa mumewe.
***
Hadi asubuhi kunakucha, si mama Juliana wala baba Juliana ama Juliana aliyekuwa ameamka. Wote walikuwa wamepitiwa na usingizi. Haikuwa kawaida ya baba Juliana kupitiwa na usingizi kiasi kile ila ilimtokea kwa kuwa alikuwa bado hajisikii vizuri kiafya.


Juliana alikuwa mtu wa kwanza kushtuka chumbani kwake. Alitoka hadi sebuleni ambapo saa yao ya ukutani ilimuonyesha kuwa tayari ilikuwa imetimia saa mbili za asubuhi. Kumbukumbu za kichapo cha jana yake usiku bado zilimtawala akilini. Kikubwa kilichomuuma zaidi ni kuendelea kuchanganywa kimapenzi na Bitungu. Aliiwasha simu yake na kumpigia Bitungu.


“Bitungu mpenzi!”
“Niambie sweet, vipi mzima jamani!”
“Bitu miye naumwa na nataka uje unione nyumbani?”
“Unaumwa? Nini tatizo?”


“Bitu naumwa kwa kukuwaza wewe, unaniweka kwenye wakati mgumu wakati unajua fika kuwa nakupenda!”“Sijakuelewa? Nakuweka katika wakati mgumu kivipi wakati wajua fika bado nipo huku Bagamoyo na wafanyakazi wenzangu na huku semina iliyonileta itaisha baada ya wiki.”
“Nikuulize kitu bebi?”


“Nakusikiliza uliza tu?”
“Unanipenda kabisa kutoka moyoni au unanitamani embu niambie ukweli bebi wangu, samahani lakini!”
“Hapana sweet kama ningekuwa nakutamani mbona ningeshaachana na wewe siku nyingi tangu nilipomaliza shida zangu kwa mara ya mwisho.”


“Nafurahi kusikia hivyo lakini kuna jambo moja linanitatiza kweli.”
“Lipi hilo na mbona leo umeamka na maswali hivyo mpenzi wangu?”
“Yote hiyo kwa sababu nakupenda, nakuwaza kila muda na sipendi kukupoteza hata siku moja.”
“Hata miye sipendi nikuache, haya niambie kinachokutatiza kipi hasa?”


“Bebi niambie ukweli wako kabisa maana siku nikigundua nitaumia sana! Niambie ukweli umeoa ama hujaoa?”“Ningeoa mke si ungemuona? Uko peke yako mpenzi wangu na ndiyo maana hata tunavyokutana huwa sina wasiwasi wowote.”
“Kweli bebi wangu?”


Juliana alimtega Bitungu kwa makusudi, lengo lake ni kummbana atambue kuwa anashiriki mapenzi na familia moja yaani yeye na mama yake. Kila alipokuwa akitaka kumwambia ukweli alikuwa akisita na kumfanya aongee mengine. Mateso aliyoyapata jana yake usiku yalikuwa yamesababishwa na Bitungu huyohuyo kwa kiasi kikubwa.


Moyo wake Juliana ulishamwambia kuwa aachie ngazi. Amwachie mama yake aendeleze mapenzi yao. Juliana alijikaza kwa muda akakaa kimya kisha akaikata ile simu aliyokuwa akiongea na Bitungu. Baada ya kuikata akaamua kutuma meseji ya hasira na ya mwisho kwa Bitungu.


“Naomba unielewe kwa makini! Kuanzia sasa sitakuita tena mpenzi, bebi wala honey. Mapenzi ya mimi na wewe Bitungu naomba yaishie hapa leo hii. Nilikupenda Bitungu lakini ukweli nilioujua ndiyo umenifanya kuchukua maamuzi haya magumu, ukweli wa wewe kuto....”
TUKUTANE JUMAMOSI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom