Siku nzuri inavyokwenda, we mwenyewe utaipenda.Kwako kunapoungua kwa mwenzako kunateketea

Rabonn

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
5,733
10,928
Habari gani wadau.

Poleni na majukumu, ndio maisha yalivyo kikubwa uhai.

Moja kwa moja kwenye mada.

Kwanza nimshukuru sana Mwenyezi Mungu, sifa na utukufu vimrudie yeye maana kui controll hii dunia na mipangilio yake ni kazi mnoo..imagine wewe unavyolia mwingine huko anacheka... na kuna mwingine huko analia kukuzidi.

Jana tar 06 march ni siku ambayo nilikua na siku mbaya sana japo kwa utu uzima wangu wala sio mgeni wa "bad days" sema ndio vile nyakati ngumu huwa hazizoeleki. Mwanangu wa 3 kuzalia jinsia Me umri wa miaka mi 4 alipandwa na homa kali sana sana ghafla mchana kiasi cha kuanza kupata mawenge na kuongea vitu visivyoeleweka kama malaria ilopanda kichwani.

Basi mke wangu kwakua ni mtu wa kusali sana ikampasa kuchukua hatua za kiimani pale kama first aid, na kwel hali ile ikapoteza dogo akarejewa na ufahamu, akamuandaa kisha akanipigia simu kunipa scenario .Nikashtuka sana na kwakua muda umekwenda sana nikamwambia asichelewe kwa kuningoja niwafuate (kwakua tuna usafiri mmoja tu na jana niliondoka na gari kwenda ofisini) bali achukue boda tukutane hospital.

Na kwakua ni muda umekwenda na tatizo limekua ghafla sana tufike hospitali ya wilaya tu hapo (naishi wilaya moja wapo katika mkoa wa pwani along Kilwa road).

Basi akafa ya hivyo baada ya mud na mimi nikafika hospitalini nikamkuta ameshasogeza zoezi na yuko foleni kuingia kwenye ufanyaji vipimo hivyo nikawa join.

Sasa hapa kwenye banda la kungoja kwenda kwenye vipimo tulipokua tunangoja ndio hasa ninachotaka ku share maana nilijikuta nasahau kama mimi pia ni matatizo ndio yamenipeleka pale..Nikajiona kama tatizo langu ni dogo sana na nikiwa kama mzazi mwenye watoto wa 4 na huyu wa nne ndio kwanza ana miezi mi 3 nilijikuta naumia sana na kumuonea huruma mtanzania mwenzangu mmoja niliyemkuta pale.

Ilikua hivi,

Tukiwa kwenye foleni, tuliwakuta waliosheheni pale ni wanawake zaidii..Wamevaa hijabu wamejitanda haswaaa na wengine wamekula nikabu.
Katika wote, kulikua na mabinti watatu waliokamata attention yangu na mke wangu.

Wawili Wa kwanza:
Hawa walikua mtu na dada yake ( niligundua kwa mujib wa maelezo niliyoyasikia baadae yakiendelea)

Dada mtu alikua ni mja mzito amekuja pale kwa matibabu.
Na huyu mdogo mtu alikua amempa kampani dada yake kufika pale.

Muhusika wa mwisho;
Huyu alikua ni bint mdogo sanaa nadhani hafika hata 20 years kwa umri na alikua amebeba katoto kachanga.Ni katoto kake.

Huyu binti mwenye mtoto mchanga alikua peke yake na alokia ashafanya vipimo hivyo baada ya sisi kufika akawa ndio anaitwa na daktari kwenda kuchukua majibu ili arudi kwa daktari.

Sasa wakat anainuka akamwomba yule dada mjamzito amshikie mtoto wake yeye afuate majibu.Na kwel ikawa hivyo.Ila cha ajabu sasa baada kama ya dakika 2 toka ampokee yule mtoto, huyu dada mjamzito ni aka change halaf akaongea kwa sauti huku kama anatetemeka akasema "NAMTUPA HUYU MTOTO"..akarudia hayo maneno mara 2 ghafla yule mdogo ake aliyemsindikiza kuja pale akamuwahi dada yake na kumpokonywa yule mtoto..

Sasa sisi (wengine tusiojua mambo mengi 😁 ya dunia) tukastaajabu kidogo nini kimempata huyu?
Ndio yule mdogo mtu aliyempokonya mtoto akasema "huyu dada yangu ana wadudu..(yaani ana mashetani)."
Akaendelea kusema kuwa "Huyu mtoto (mchanga yani) atakua sio wa kawaida.Anakitu ndani kibaya "

Nikawa makin kuusoma mchezo ila nipo kama sipo.

Ingawa wengine pale ishu ya yule dada kuwa na majini waliigundua haraka hata kabla ya maelezo ya yule mdogo mtu..Ujue pwani mambo ya uswahili ni kawaida sana sana..tiba za jadi huku wala sio kitu cha ajabu wala kificho.watu wanavifanya na kuvijadil waz waz .na nishakutana pia na scenario za hiz mimi binafsi.

Nikabaki najiuliza..mtoto huyu ana shida gani isiyo ya kawaida..Ni katoto ka changa sana na kwakua mimi mwanangu wa 4 ana miezi mi 3 basi yule mtoto mwingine anayezungumziwa nikahisi atakua hajazidi miezi miwili.Maana kwa kuwalinganisha na huyu wa kwangu yeye ni mkubwa kidogo na amechangamka zaid.

Basi yule binti akawa anasema dada yake huwa ana uwezo wa kuona vitu vibaya na huwa anapandisha majini kwahiyo yule mtoto mchanga atakua ana shida ngoja mama yake arudi aseme kama anajua.na akamaliza kwa kusema "hata mimi hapa nimembeba ila mwili wangu unasisimka hatari, huyu mtoto ana kitu"

Na kwel baada ya dakika kadhaa mama yule kichanga akarudi asijue kilichojiri .Akamchukua ..Ndipo dada mmoja akamuuliza yule mama wa kichanga kuwa "mwanao anasumbuliwa na nini?"

Akajibu "vipimo vinaonyesha hana tatizo, lakini ni mwaka mmoja sasa nahangaika naye"

E bwanaa eeehh!!!? Eti nini??
MWAKA MMOJA!!!.
Yaan yule mtoto niliyedhan ni mchanga hafika zaidi ya mwezi kumbe ana mwaka mmoja???

NILIUMIA VIBAYA SANA nikajaribu ku imagine like tatizo lile ndio mimi nahangaia na mwanangu..Moyo wangu uliuma sana na zaid kwakua kale kabint kenyewe ni kadogo sana nahis kalizaa shuleni!.na maisha yanaonekana sio poa...
Nikajiuliza mambo mengi kwa haraka bila majibu..

Mwisho wa siku yule dada majini akamwambia "SHOGA ANGU HILI SIO TATIZO LA HAPA ULIPOKUJA.HUYU MTOTO UTAMPOTEZA HUKU UNAMWONA.HANGAIKA MDOGO ANGU UZAZI SIO RAHISI..TAFUTA WATAALAMU WAMTIBIE MWANAO"

Waka exchange namba kisha yule binti akaondoka. Na kale kabinti ni kama kakawa excited kupata mawasiliano na yule dada mwenye majini aliye ahidi atamsaidia kupata watu wa kumfanyia tiba.

Ni tukio lililomiumiza sana na kunisahaulisha maswahib ya mwanangu kwa muda.

Mwisho
 
Pole kwa kuuguliwa na mtoto,mambo ya wakazi wa pwani na pwani yao yasikuvuruge sana wenyewe wameyazoea
Shukrani..na hakika kwa miaka 8 niliokaa pwani nimejifunza vitu vingi.Pwan ushirikina nje nje
 
Najiandaa kumchoma moto mchawi mmoja,mwenyewe anadhani kashinda na sijui,yule mbuzi ntavika tairi nimmwagie petrol,atafurahi
Chunga kuchukua sheria mkononi
 
Yeah he/she deserves it
Screenshot_20230307-222105~2.png
 
Back
Top Bottom