Mosalah_
JF-Expert Member
- Jul 10, 2018
- 314
- 720
Sitasahau kuna rafiki yangu nilipanda nae daladala akamuona mdada ana mtoto mchanga amesimama, wakati huo yeye alikua na siti amekaa, akamuomba kumsaidia mtoto yule dada yule dada akakubali.
Ila mimi nilimwambia Swahib kama umepanga kwa dhati kumsaidia huyu mdada we mpishe akae na mtoto wake, akasema oooh hamna sijui nini nini!
Haya wee mwisho wa siku aliachiwa mtoto kwenye daladala na yule dada akakimbia zake hatukujua alishukia wapi!
Jamaa alishapeleka barua kwa mdada mmoja aliekuwa shem wetu uchumba ukafa kisa huyo mtoto! Maana jamaa hakujua chakufanya zaidi ya kubaki na kale katoto mpaka leo kamekua sana na kanatuchangamsha sana kila nikiendaga kwa jamaa.
Inasikitisha na inachekesha maana jamaa alikuwa anataka kumtupa yule mtoto, na akasema kama mama yake amemuacha mimi ni nani!
Nikamuambia bro ukimtupa huyo mtoto wakwanza kukureport nitakuwa mimi ndugu yako wa damu kabisa! Kwenda polisi reception tukakutana na mdada ana nyodo balaa, nikamshauri tu ndugu yangu tumlee kijana akikua huenda akaja kututilia ubani siku tukifa tukapata angalau kukumbukwa.
Ila kiukweli nilikua namsaidia kuishauri huku namcheka sana, sisemi uongo. Ila dogo amekua sana siku hizi kanaongea kama kasuku, afya Ma-Sha-Allah na tumekapeleka nursery japo hakaelewi chochote kanaenda kufanya tu fujo na sisi baba zake kulipishwa vitu tu mitaani.
Basi bhana ndio hivyo anaitwa baba one, naitwa baba two. Shule hizo za chekechea mtoto kashajua one na two.
Ila we dada ulietukimbia na katoto hatukupi laana hata umetuletea baraka na kutufundisha majukumu, tumekua watu wazima now days Mungu akubariki sana. Na siku ukijitokeza uso wako eti kuja kumtaka huyu mtoto nadhani ndio hiyo siku utakuwa headgirl wa mortuary.
Note: Hii story siyo ya kwangu kuna sehemu nimeipata nikaipenda.