Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,265
SIKU NILIYOIONA SIMU KWA MARA YA KWANZA ODEON CINEMA 1955 AU 56 AU NYUMA YA HAPO KIDOGO SIJAVUKA UMRI WA MIAKA MINNE
Nakumbuka kama jana vile.
Nilikuwa mgonjwa na baba yangu mdogo Mzee Issa akanichukua kunipeleka hospitali.
Ilikuwa usiku lakini si usiku mkubwa kiasi cha saa moja hivi.
Nina hakika na hili kwa kuwa Mzee Issa kanibeba tunatoka nyumbani Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes Street) kwa miguu na nawaona watu mtaani njia nzima hadi tunafika New Street tunavuka Mnazi Mmoja tunapita kushoto tunaelekea Sultan Street (Libya Street).
Hapa Mnazi Mmoja palikuja kujengwa Mnara wa Uhuru. Siku zile Mnazi MMoja ile ilikuwa uwanja mtupu hauina chochote ni mchanga mtupu.
Tunaingia Ring Street (Sasa Jamhuri Street) tunapita pembeni ya Odeon Cinema tunaingia mitaa ya Uhindini jirani na Msikiti wa Sunni kulikuwa na hospitali maarufu sana ya daktari wa Kihindi nakumbuka ingawa sina hakika jina lake lilikuwa kama Dr. Koya.
Mama zetu wakimsifia sana kwa kutibu watoto.
Hii hospital imedumu hapo kwa miaka mingi hadi mimi nimekuwa mtu mzima nikipita pale nikiiona.
Baada ya kutibiwa baba yangu mdogo Mzee Issa miaka ile alikuwa kijana akawa ananirudisha nyumbani.
Ndipo tulipopita tena Odeon Cinema tukaingia ndani kwenye call box (kibanda cha simu) kilichokuwa pale ndani.
Baba yangu alikuwa kazini akifanyakazi Telephone Exchange.
Jumba hili hadi leo lipo.
Mzee Issa akatia pesa kisha akapiga simu kuzungumza na baba yangu kumfahamisha kuwa kanipeleka hospitali na nimetibiwa.
Mzee Issa akanipa simu nimwamkie baba yangu.
Sikuweza kuzungumza.
Miaka mingi ikapita.
Siku moja nikamhadithia Mzee Issa habari hii.
Alishtuka.
Akawa kashangaa kisha akaniuliza, ''Mohamed unakumbuka habari hii?''