Tuangalie nyuma: Hayati Joseph Magufuli na madafu ya Odeon Cinema

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,267
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI NA MADAFU YA ODEON CINEMA​

Ndugu zangu hii clip ya Rais Magufuli akinywa madafu Odeon Cinema imenikumbusha mbali sana.

Kwanza imenikumbusha jengo la senema yenyewe ambayo sisi tumezaliwa tumeikuta na umaarufu wake kwa kuonyesha michezo ya Kihindi ya akina Ranjan na Babrao katika miaka ya 1950 na katika 1960s uwanja ukawa wa Amitabhachan na wenzake.

Pili hayo madafu aliyonunua rais mwenyewe amenikumbusha mshabiki mkubwa wa Sunderland na Simba - Bin Sudi ambae alikuwa muuza madafu mashuhuri hapo Odeon Cinema.

Lakini zaidi mimi nimekulia mitaa hiyo nyuma tu ya Odeon - Libya Street kwa hiyo kwa muda nilikuwa nimerudi nyumbani.

Rais Mwinyi aliondoa katika urais na Ikulu yenyewe ile "mysticism," iliyokuwapo ya kwanza urais wenyewe kutisha na jumba la Ikulu kutia hofu kama jumba la Count Dracula.

Rais Kikwete yeye alipochukua kiti cha urais ndiyo kabisa katika kazi ya urais ikawa imeingia, "flamboyance," haijapatapo kuonekana khasa jinsi mkewe Bi. Salma alivyoibadili Ikulu kwa haiba yake na kila kitu chake.

Ilipendeza sana kuwaona pamoja.

Rais Magufuli kaja na staili nyingine kabisa haijapatapo kuonekana ila kwa ufahamu wangu mahali pamoja Afrika - Misri.

Hii staili ya madafu imeshabihiana sana na staili ya Anwar Sadat akitokea mahali kama Taharir Square, Cairo (mfano wa Mnazi Mmoja) msafara ukasimama rais akasalimiana na wananchi kisha rais akakaribishwa chai na sandwitch na muuza mgahawa wa hapo na rais akakipokea kikombe na sandwitch akakaa kitako na kunywa.

Kama ilivyo Cairo punde sehemu yote ile itakuwa watu wameshajazana kumshuhudia rais anakunywa chai ya mtaani katika genge.

Nilipokuwa naangalia hii clip nikamkumbuka Anwar Sadat.

Hakika Rais Magufuli anatusuuza kwa haya kwani rais anakuwa mtu kama binadamu anavyokuwa.

Rais anakuwa mtu anaezungumza akacheka na kachekeshwa na akaonyesha furaha na kisha kuwafurahisha kwa kupiga duru ya madafu.

Sijui marais wajao watakuwaje.

1644426529394.png

Rais Magufuli na muuza madafu Odeon Cinema 2019
 
Mzee wangu hayo ni maigizo ya wakubwa,inakuwa imepangwa zamani hapo wanafuata script tu,rais hawezi kula ovyo mtaani kama mimi na wewe tunavyokula ovyo,kila anachokula rais wadaidizi wake huwa wamejiridhisha usalama wake,si ajabu huyo muuza madafu ni mtumishi wa ofisi yake.
Magufuli alijua kucheza na akili za watanzania kwa vitu kama hivi na tulivyo wajinga tukadhani anamaanisha
Kuna jamaa alimuuzia mhindi wa kuchoma dumila huku bastola ipo kiunoni.
Maigizo mengine ni kukosa cha kufanya au kutuona wajinga
 
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI NA MADAFU YA ODEON CINEMA

Sijui marais wajao watakuwaje...

View attachment 2114090
Rais Magufuli na muuza madafu Odeon Cinema 2019
Mkuu, umenikumbusha mbali sana. Kwanza, hilo jengo la senema la Odeon, japo mimi sikuishi maeneo hayo. Nilikuwa nikiishi Kurasini. Pili, mitaa ya Taharir Square jijini Cairo. Huko mimi niliishi Aguza; baadaye Zamalek; halafu Talaba na mwisho Mohandeseen ndipo nilipoondokea.
 
Mzee wangu hayo ni maigizo ya wakubwa,inakuwa imepangwa zamani hapo wanafuata script tu,rais hawezi kula ovyo mtaani kama mimi na wewe tunavyokula ovyo,kila anachokula rais wadaidizi wake huwa wamejiridhisha usalama wake,si ajabu huyo muuza madafu ni mtumishi wa ofisi yake.
Magufuli alijua kucheza na akili za watanzania kwa vitu kama hivi na tulivyo wajinga tukadhani anamaanisha
Kuna jamaa alimuuzia mhindi wa kuchoma dumila huku bastola ipo kiunoni.
Maigizo mengine ni kukosa cha kufanya au kutuona wajinga
Hilo la kuigiza, na kwamba vitu vinakuwa vimepangwa, sidhani kama ndivyo inavyokuwa mara zote. Mfano niliojionea kwamba si kila kitu anachofanya Rais lazima kiwe kimepangwa, ni mwaka 1970 nilipokuwa nasoma Pugu. Wakati huo, Mwalimu ndiye alikuwa Rais. Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Chou En Lai, alikuwa amekuja ziara Tanzania. Siku hiyo Mwalimu alimpeleka mgeni huyo kuona ujenzi wa reli ya Tazara nyuma kidogo ya shule ya Pugu, ukipita Mwakanga. Wakati wanarudi, pikipiki za msafara zilipita na baadaye gari inayotangulia msafara nayo ikapita kwa kasi na ving'ora juu. Tuliposikia hivyo ving'ora, tuliokuwa kwenye uwanja wa mpira, jirani na barabara, tukajisogeza barabarani. Baadaye gari la Rais na mgeni wake likatokea. Mwalimu alimsimamisha dereva, akateremka na mgeni wake kutusalimu. Gari ya nyuma ya msafara yenyewe ilisimama pia, wakati watangulizi wa msafara labda walikuwa wamepita hata Gongo la Mboto. Mwalimu aliongea nasi si chini ya dakika 15 hapo hapo barabarani, tukiwa wanafunzi tu. Hapakuwa na hata mwalimu mmoja kwa kuwa ilikuwa haikupangwa kwamba Rais atasimama hapo. Mwalimu alimuambia mgeni wake kwamba hiyo ndiyo shule aliyomalizia kufundisha kabla ya kuingia siasa. Dakika 7 au 8 baadaye ndipo tukaona watangulizi wa msafara wanarudi kwa kasi sana baada ya kutoliona gari la Rais kwa muda kwa kuwa kuna kona kali na miti mirefu mara tu baada ya kiwanja cha mpira. Walipomuona Rais amesimama akiongea nasi ndipo nyoyo zikatulia, wakageuza gari na pikipiki kuzielekeza mjini na kupaki wakisubiri Rais amalize mazungumzo yake. Walipomuona anaaga na kurudi garini ndipo nao wakaanza safari. Ni dhahiri kabisa kwamba kusimama kwa Rais hapo hakukuwa kumepangwa.
 
Huenda ni kweli mwalimu hakuwa mtu wa maigizo,ila kuna mheshimiwa mmoja kwa maigizo alikuwa hajambo,sema kuna watu aliwapata
 
Sahihisho dogo tu, Chou en Lai hakuwa waziri wa mambo ya nchi za nje. Alikuwa waziri mkuu.
 
Jamaa uliyeandika kwamba muuza wa Dumila alikuwa na Bastola kiunoni wakati anamuuzia Mahindi JPM acha UONGO,yule jamaa ni muuza mahindi tu pale na ninafahamiana nae sana,juzi tu amenisaidia kununua Shamba Dumila,acha habari za vijiweni
 
Jamaa muongo wewe
 
Back
Top Bottom