Siku hizi teknolojia inasoma akili za watu kuandaa matangazo ya mitandaoni

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Siku ya leo Teknolojia imenishangaza kidogo, nimewaza akilini kuhusu vikombe vile vidogo kwa kufunika na kutembea navyo, nikamuuliza jirani yangu pembeni yangu kuhusu lini anaenda kariakoo nimuagize, hata swali lenyewe halikuwa specific, nimesema tu "Lini unaenda kariakoo nikuagize vile vikombe vyetu". Siku google wala kusearch hiyo bidhaa popote mtandaoni

Punde si punde naingia instagram nakutana na Tangazo la namna hiyo lenye vikombe navyovitaka.

Sasa swali langu: How did they reread my mind?

Screenshot_20240222-125510_1.jpg
 
Labda ulichanja ikasomea huko maana kuna jamaa ameenda majuu anasema hakuulizwa passport in other words ameenda kama wale wasabato wetu wa mwaka 2007
 
Sikuhizi google wanakusanya taarifa za wateja hadi sio poa sijui kama tupo salama hata ukigugo neno moja huko gugo tayari taarifa yako wanayo
 
This mean "Instagram has access to your microphone" so, it hear whatever u speak.
 
Ni kwamba hilo tangazo limekuja right on time Na Sio kwamba teknolojia imekusoma.

Kitu ambacho teknolojia inaweza kukusoma ni ile kuangalia labla video za aina moja kwa muda mrefu hvy muda mwingi itakuwa inakuonyesha aina hizo za video.

Naona wachangiaji wengine wamechangia ndivyo sivyo.
 
kama uliisearch google basi lazima ikuletee matangazo huko Insta au facebook.

Mfano ukisearch mbwa tegemea kukutana na habari za mbwa
 
Ni kwamba hilo tangazo limekuja right on time Na Sio kwamba teknolojia imekusoma.
Kitu ambacho teknolojia inaweza kukusoma ni ile kuangalia labla video za aina moja kwa muda mrefu hvy muda mwingi itakuwa inakuonyesha aina hizo za video.

Naona wachangiaji wengine wamechangia ndivyo sivyo.
Hapo nikweli kabisa yaani Kila siku lazima niletewe Tengetengee Tengetengee tengere
 
Back
Top Bottom