Sijui nimwambie

BIREGU

Member
Feb 10, 2013
31
8
Kaka yangu yupo masomoni ng'ambo Tangu mwaka jana,mwaka huu mwezi wa 10 atarudi likizo.Lakini mimi natamani arudi mapema nimwambie mambo ya mke wake.alipo kwenda huko aliniachia familia yake niwe namuangalia shemeji kwa maana ya kujua maendeleo yake pamoja na mtoto ( mwanae).Lakini siku moja shemeji yangu alinipigia simu akinitaka niende kwake usiku wa saa 5 na nusu kuna kitu anataka aniambie.nikatafuta usafiri nikafika kwake ,nilipofikatu na kugonga mlago alinifungulia na tukakaa sebureni lakini nikamuona kachangamuka sana,kama kalewa hivi!kisha akakaa kochi la mbele yangu yaani tukiwa tunatazamana.akaanza kwa kuniita shemeji kisha jina langu nimekuita nikwambie siri yangu,na sinabudi nikwambie tu vinginevyo nitazidi kuteseka,Unajua nakupenda sana alisema na natamani muda huu ambao kaka yako ayupo tujivinjari na itakuwa siri yetu,usidhani natania nimedhamilia na sikuwahi kuwa na nafasi ya kukueeleza haya.Nikapigwa butwaa na sikuamini maneno yake.Nikamsii sana anipe muda nilifikilie hilo.Ni mwezi sasa nahakikisha nikienda kwake nakuwa na marafiki zangu wawili au watatu,lakini ananisumbua sana kwenye simu akitaka nimpe jibu.Sasa wana janvi nifanyeje? kunawakati natamani nimwambie kaka akiwa huko huko,lakini najua anampenda sana mke wake nitamchanganya,na akirudi nitawezaje kumwambia wakati naogopa kuwa chanzo cha mwisho wa ndoa yao.najua aiwezekani kuanza mahusiano na mke wa kakaangu,ila kwangu nivigumu kumwambia kwani sijui atachukua hatua gani.Ushauri wenu jamani.
 
unajua mwanaume na mwanamke tofauti zao zipo hata kwenye shingo!
hebu hakikisha hilo!
ni hivi huna haja ya kumwambia kakako since umeshajua la kufanya kumuepuka shemeji yako!
huna sababu ya kumwambia kakako!
wil u please kuondoa jina la mtoto ,incase of anything!india ni mbali lakin jf inafika huko!lol
 
Duuu..kuvunja ndoa sio vizuri hivyo sishauri umwambie kakako.. Inawezekana shemeji yako kazidiwa tu na tamaa za mwili na ipo siku she will come back to her senses.Mwite mahali umtishie kuwa akiendelea na tabia hiyo basi hutasita kumwambia mumewe..Endelea kuepuka faragha nae maana anaweza kukutega
 
Kama kweli hutaki
mahusiano naye mweleze ukweli, unavyochelewa anaweza kudhani unataka
lakini unashindwa kusema...hiyo ni hatari kaa chonjo kaka

hyo ishu ni tata sana, unaweza kumkataa na akageuzia kbao na kudai ww ndo ulimtaka, pia unaweza mwambie bro nae hujui atareact namna gan anaweza muacha ama akamuuliza mkewe na mkewe akampa mbunye ya ukwe e nakuambia ww ndo ulimtongoza na bro akakugeuka....mwambie hata ww unampenda xana ila hamtafanya ivo na mwahidi utamfichia siri daima juu ya hlo alokuambia.
 
mwanangu anaitwa Jossef nipo masomoni. na nnna lidogo langu limemaliza chuo mwaka huu .I will be back!!!
 
Kaka yangu yupo masomoni Tangu mwaka jana,mwaka huu atarudi likizo.Lakini mimi natamani arudi mapema nimwambie mambo ya mke wake.alipo kwenda huko aliniachia familia yake niwe namuangalia shemeji kwa maana ya kujua maendeleo yake pamoja na mtoto yaani mwanae.Lakini siku moja shemeji yangu alinipigia simu akinitaka niende kwake usiku wa saa 5 na nusu kuna kitu anataka aniambie.nikatafuta usafiri nikafika kwake ,nilipofikatu na kugonga mlago alinifungulia na tukakaa sebureni lakini nikamuona kachangamuka sana,kama kalewa hivi!kisha akakaa kochi la mbele yangu yaani tukiwa tunatazamana.akaanza kwa kuniita shemeji kisha jina langu nimekuita nikwambie siri yangu,na sinabudi nikwambie tu vinginevyo nitazidi kuteseka,Unajua nakupenda sana alisema na natamani muda huu ambao kaka yako ayupo tujivinjari na itakuwa siri yetu,usidhani natania nimedhamilia na sikuwahi kuwa na nafasi ya kukueeleza haya.Nikapigwa butwaa na sikuamini maneno yake.Nikamsii sana anipe muda nilifikilie hilo.Ni mwezi sasa nahakikisha nikienda kwake nakuwa na marafiki zangu wawili au watatu,lakini ananisumbua sana kwenye simu akitaka nimpe jibu.Sasa wana janvi nifanyeje? kunawakati natamani nimwambie kaka akiwa huko huko,lakini najua anampenda sana mke wake nitamchanganya,na akirudi nitawezaje kumwambia wakati naogopa kuwa chanzo cha mwisho wa ndoa yao.najua awezekani kuanza mahusiano na mke wa kakaangu,ila kwangu nivigumu kumwambia kwani sijui atachukua hatua gani.Ushauri wenu jamani.
Inaonekana bado una akili ya kitoto sana, sijui ni kwa vipi hata shemeji yako amekupenda mtoto mdogo kama wewe. Kuandika hapa taarifa zote ikiwemo jina la mtoto na mahali alipo kakako na mwezi anaorudi likizo inatosha kabisa kusema umeshamwambia kakako kuhusu kinachoendelea nyumbani na kwa namna moja au nyingine umeshiriki kuvunja ndoa ya kakako iwapo kakako atajua kwamba mkewe alikuwa anakutaka wewe kimapenzi.
Binafsi nimeshakuwa na mke wa kaka wa aina hiyo, sikuwahi kumwambia kaka, na tuliendelea kuwa marafiki hadi mwisho. Namna nzuri ni kumtia moyo, na kukubali kwamba ana wakati mgumu kutokana na kutokuwepo kwa kakako, na baada ya hapo mwambie kwamba wewe na yeye kufanya hilo haiwezekani. Na mhakikishie kwamba hiyo ni siri yenu hutakaa umwambie kakako. Vinginevyo ukikataa tu, bila kuonyesha kumjali, atamwambia kakako kwamba wewe ulikuwa unamtaka, ndivyo walivyo. So kuwa rafiki wa kweli, mtie moyo, na mhakikishie usalama. Ila ningekushauri uedit hii post na kuondoa vielelezo ambavyo vinaonyesha wazi unayemwongelea. Mimi nimeanza kwa kuviondoa kwenye quotation yangu.
 
Pole lakini kazi sio ndogo, haya mwambie shemeji natamani lakini kujaribu siwezi.....
 
Inaonekana bado una akili ya
kitoto sana, sijui ni kwa vipi hata shemeji yako amekupenda mtoto mdogo
kama wewe. Kuandika hapa taarifa zote ikiwemo jina la mtoto na mahali
alipo kakako na mwezi anaorudi likizo inatosha kabisa kusema
umeshamwambia kakako kuhusu kinachoendelea nyumbani na kwa namna moja au
nyingine umeshiriki kuvunja ndoa ya kakako iwapo kakako atajua kwamba
mkewe alikuwa anakutaka wewe kimapenzi.
Binafsi nimeshakuwa na mke wa kaka wa aina hiyo, sikuwahi kumwambia
kaka, na tuliendelea kuwa marafiki hadi mwisho. Namna nzuri ni kumtia
moyo, na kukubali kwamba ana wakati mgumu kutokana na kutokuwepo kwa
kakako, na baada ya hapo mwambie kwamba wewe na yeye kufanya hilo
haiwezekani. Na mhakikishie kwamba hiyo ni siri yenu hutakaa umwambie
kakako. Vinginevyo ukikataa tu, bila kuonyesha kumjali, atamwambia
kakako kwamba wewe ulikuwa unamtaka, ndivyo walivyo. So kuwa rafiki wa
kweli, mtie moyo, na mhakikishie usalama. Ila ningekushauri uedit hii
post na kuondoa vielelezo ambavyo vinaonyesha wazi unayemwongelea. Mimi
nimeanza kwa kuviondoa kwenye quotation yangu.

yap simple tu, et anashndwa kucheza na saikolojia ya mwanamke
 
Kaka,
::
Sio kila ukweli unatakiwa kusemwa.
=

no ugen wa jukwaa tu akizoe atakuwa mjanja, wengi huanza humu kwa kusema ukwel bt as the day goes anagundua hapa c mahala pakuanika kila k2 live.
 
Mwambie hutaki, na hata kaka ako acfaham coz utakuwa chanzo cha mgogoro.
 
wewe kama hutaki kumgegeda nipigie mie pande nimpe raha ...hahahaha
anyways ukweli ni kwamba usimgegede huyo mke wa bro bana...sasa wewe usimgegede na wala usimwambie kaka yako kuhusu mke wake kukutaka wewe kimapenzi. ni siri yenu wote wawili. kazi kwake kaka yako na ndoa yake.

this is y nasema hamna wanawake wakuoa siku hizi
 
Ukimwambia kaka yako sio tuu unaweza vunja ndoa yake, bali unaweza kuvunja undugu na kaka yako pale ambapo mke wake atakapo kataa na uonekane wewe ni muongo. Muepuke kabisa shemeji yako kwa kuhakikisha humpi nafasi ya kutimiza azima yake hiyo. Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
 
Duuu..kuvunja ndoa sio vizuri hivyo sishauri umwambie kakako.. Inawezekana shemeji yako kazidiwa tu na tamaa za mwili na ipo siku she will come back to her senses.Mwite mahali umtishie kuwa akiendelea na tabia hiyo basi hutasita kumwambia mumewe..Endelea kuepuka faragha nae maana anaweza kukutega
Huo ni mtego mbaya sana, kuna wengine wasipokubaliwa huwa wanawahi kushitaki wao. Usishangae kukuta mdada anamwambia mumewe kuwa mdogo wako ananotaka...
 
mwanangu anaitwa Jossef nipo masomoni. na nnna lidogo langu limemaliza chuo mwaka huu .I will be back!!!

AH TARATIBU! banaaaa!unaona sasa dogo unavoharibu mambo!oh!nilisema mimi india sio mbali kihivyo jamani!
mzee mzima mkonowapaka temea mate chini bana!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom