Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Afrika iliwahi huko nyuma kupata wanasiasa mahiri na weledi na wazalendo kweli kweli kwa Bara lao na watu wake.
Wanasiasa wa aina ya Kwame Nkurumah na Mwalimu Nyerere ambao mabishano yao ya jinsi gani ya kuiunganisha Afrika yameacha athari kubwa sana mpaka sasa. Kulikuwa na wanamapinduzi kama kina Samora Macel na Mzee Jomo Kenyata ambao nusu ya maisha yao waliyatumia msituni kupigania haki na uhuru wa nchi zao na watu wake. Wanasiasa wa aina hii hawakuishi sana hadi kuonekana kubadilika tabia zao walipokuwa madarakani ukiondoa Nyerere.
Lakini katika Afrika jambo moja linaloshangaza ni pale baadhi ya wanamapinduzi au wanasiasa hao hao ambao wakiwa nje ya madaraka wanakuwa ni wanamapinduzi wa kweli kweli, wakiingia madarakani wanageuka ving'ang'anizi na wakandamizaji wakubwa wa wananchi wao ambao kabla ya kuingia madarakani walidai wanapigana kwa ajili yao.
Yoweri Museveni kimemtokea nini mpaka anaamini kwamba bila ya yeye kuwa Rais hakuna Uganda. Kwa nini Raila Odinga anaamini yeye pekee ndiye anayefaa kuwa mgombea Urais wa kupitia chama cha ODM. Nini kimembadilisha Mugabe mpigania uhuru aliyeheshimika sana kwenye miaka ya themanini kuwa vile alivyo leo? CCM hii ya leo lengo lake la kuundwa kwake lilikuwa ni kuwatetea wakulima na wafanya kazi. Lakini leo hii ndani ya chama hicho kumetamalaki ufisadi wa kutisha hadi ile hali ya kuamini kama kinaweza kujisafisa ni sawa sawa na Sifuri.
Hali hii inanifanya nijiulize, ni kitu gani huwa kinawatokea wanasiasa wengi wa Afrika wanaposhika madaraka?
Wewe unajua kinachotokea?