fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,065
Naomba wataaluma wa maswala ya ubinadamu, sheria za nchi, katiba, na saikolojia ya binadamu mnisaidie, tena mnisaidie sana. Nawakaribisha hata raia kama mimi wasio wataaluma wa maeneo hayo kutoa tafakuri zao.
Katika jamii yetu kuna mdudu, mdudu mbaya sana anaitwa community interferences, hivi karibuni katika jamii yetu hii ya kitanzania, ukifanya kazi kidogo ukajenga banglow, kununua gari, maisha bing bing kila mwanafamilia anakuhusudu, kila mwanajamii anakuhusudu, tena unatolewa mfano kwenu vikao mbali mbali kama sherehe au vilio kama mtu wa kuigwa.
Katika jamii yetu hii hii, kuna watu wanaitwa wananchi wenye hasira kali, hawa ni wale ambao kimsingi wamewahi kukutana na shubiri ya vibaka, walijeruhiwa. wakisikia kibaka yuko sehemu fulani wanakodi taksi kwenda na dumu la petroli ambayo wamenunua kwa pesa zao, huwaua hawa vibaka ambao huwa wameiba simu, nguo, ndoo, pochi yenye laki, jiko la mkaa etc. Ni mbaya mtu kuwa mwizi, lakini ni mbaya zaidi kufa bila msaada, ninarudi kwenye huruka ya binadamu, lazima ajisaidie kabla ya kusaidiwa, kosa lao hawa wanajisaidia kwa watu wanyonge ambao pia wanahitaji msaada wa watu wengine, vibaka hawaendi masaki, oysterbay etc ni kwetu buguruni kwa malapa, mtoni kwa azizi ali, keko, mwenge malalakuwa etc Hii ni hasira ya wananchi,wanahasira ya kuibiwa mali zao, ni haki yako kimsingi kukasirika, wanyonge tunanyongana, wababe wanabebana.
Je wananchi wenye hasira kali mbona hawaonekani kwenye ufisadi??? mbona mali inaibiwa tena ya taifa zima lakini sijasikia wananchi wenye hasira kali; kwani hasira ya pochi/kuku/simu inalingana na milioni 52 kwa siku???? RICHMOND, EPA etc??? Kama ukifanya kazi mwaka mmoja unagari nyumba na makorokolo kibao unasifiwa na familia/jamii kwa ujumla wakati huo ni wizi mweupe peeee, mbona fisadi anafukuzwa kazi baadhi yetu tunaandaa mapokezi ya kifalme???? kibaka anagundu gani??? jamii mbona haiko fair???? VIBAKA Nanyinyi Mkome japo adhabu yenu ni kubwa kuliko ya Mafisadi.
JE TUANZE KUONA WANANCHI WENYE HASIRA KALI KWA MAFISADI, petroli iko wapi kwa mafisadi??? Wezi wa mali ya UMMA, wezi wa Madaraka? Jee mkakati wa kuondoa vibaka kitaifa ni upi???
Nawasilisha.