MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Kwa mwananchi yoyote ambaye yuko nje ya uwanja wa siasa za Zanzibar anaweza akajidanganya kama anazifahamu na kuzielewa siasa za Zanzibar. Siasa za Zanzibar ni zaidi ya wengi wazijuavyo!.
Kuzifahamu siasa za Zanzibar ni lazima uijongee historia yake kwa mapana na marefu. Ndani ya mapana na marefu ya historia ya Zanzibar utapata mshangao kama siyo simanzi.
Kuna baadhi ya kikundi cha watu au vyama vya siasa wamezivamia siasa za Zanzibar wakitumia msingi wa adui wa adui yako ni rafiki yako bila kuelewa kuwa hata yeye anaweza akawa pia ni adui yako.
Kwa watu wanaotumia fikra pana wanaweza wakaelewa msingi wa hoja yangu hasa wakioanisha na tukio la Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman lililotokea kwenye Bunge Maalum la Katiba ambapo ilibidi apate ulinzi ambao ni haki yake kikatiba kwa faida ya maisha yake na taifa kwa ujumla.
Itakumbukwa kuwa, kabla ya tukio hili kutokea, kulikuwa kuna ujumbe uliosambazwa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, ili kuwagombanisha na kuwafitinisha wajumbe wa kundi la 201 kutoka Zanzibar.
Ujumbe huo uliwataka wajumbe wa kundi la 201 kutoka Zanzibar, kuondoka bungeni ili theluthi mbili ya Katiba inayopendekezwa isipatikane. Kwa habari zaidi unaweza kusoma hapa,
Huwezi kuifuta historia ya Zanzibar kwa kutumia Katiba ya zamani au katiba mpya bila kujali kama ni Katiba ya Tanzania au Zanzibar.
Ndani ya siasa za Zanzibar, ninawafananisha CHADEMA na msemo usemao, Kwenye kila msafara wa mamba na kenge wamo.
Siasa za Zanzibar hazibebi political opportunist kama CHADEMA.

Ukijiuliza kwa nini haya yote yanatokea kwa upande wa Zanzibar, jibu utalipata kwa kuangalia historia ambayo ilizaa siasa ambayo ilizaa vyama vya siasa Zanzibar. Siasa za Zanzibar ni matokeo ya historia yake.