Elections 2010 Siasa za Tanzania na ukweli wa mambo! Mtazamo wangu mimi

tikotiko

Member
Jul 9, 2010
26
0
Mwaka 2010 Tanzania inaingia kwenye mchakato wa kuchagua viongozi wake, kwa miaka mingine mi-5!! Wakati mwingine najiuliza sana nini umuhimu wa kujihusisha na uchaguzi wakati nchi hii haina demokrasia ya kweli na tayari tunawafahamu watakaotutatwala?

Kwa mfano pamoja na kwamba Kikwete HAJAFANYA LOLOTE LILE LA MAANA bado atarejeshwa madarakani kwa wingi wa kura zaidi ya asilimia 90%, na itakuwa hivyo kwa mgombea mwenza wake na kule Zanzibar japo upinzani una nguvu kidogo bado CCM hawatakosa kupata zaidi ya asilimia 60%!! Wanawezaje? Ni rahisi sana WIZI WA KURA….tumia Polisi, Jeshi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na wengineo weeengi ambao kwa kutumia nafasi zao watahakikisha zoezi la kunyang’any akura za wapinzani linafanikiwa!

Sasa kwa mantiki hii najiuliza KUNA HAJA GANI YA KUINGIA KWENYE UCHAGUZI? Yaani ukiach ahili la “kutekeleza demokrasia” ni bora wangetangaza tu kwamba tarehe fulani Kikwete, Shein na wengineo wataapishwa…ili zile fedha (mabilioni ya uchaguzi) ziende kwenye shughuli za kimaendeleo!!

Najua wengi watanipinga, wengi watanizodoa lakini ukitazama mabilioni ya shilingi ambazo CCM na serikali yake inapoteza kwa ajili ya uchaguzi inasikitisha, hasa pale unapolinganisha kiwango huduma muhimu za kijamii kwenye mahospitali, mashule na miundombinu!! Haya matatu yanaifanya nijiulize Kikwete amefanya nini??

Utamsikia Ooh kwenye kipindi changu nimejenga Chuo Kikuu Dodoma (si yeye, siyo CCM ni NSSF na kwa mantiki hiyo ni sisi wananchi tumejenga kile)!! Miaka mitano tangu aingie madarakani hakuna kinachoendelea! Fika UDSM utaona hali inavyokuwa mbaya, panageuka sasa kama shule ya sekondari! Hakuna ile “quality” tuliyoiacha pale 1980s na early 1990s…nadhani ndiyo maana tofauti na marais wenziwe waliokuwa wanapeleka wageni mashuhuri pale mlimani na kukutana na wanafunzi na wasomi yeye utamaduni huo ameukwepa….hawezi atiii!! Anajua ni aibu! Amepita pale, anapafahamu palivyo ameshindwa nini kujaribu hata kukiboresha chuo?? Halafu anatudanganya anataka kujenga kingine kule Mara? Kwa kilimo kipi anachotaka kukiendeleza? Huyu jamaa mnamuelewa kweli??

Jamani, miaka ya 80 kulikuwa na vyuo vya kilimo…Ilonga Morogoro, kule Ifakara, Mlingano Tanga na vinginevyo….wataalamu wengi sana wamepita huko na enzi zile tulifaidika sana na kazi zao!! Maafisa kilimo kila kona na nchi na walikuwa wamesoma haswa!! Kama kweli ana nia hiyo kwa nini asianze na hivi vyuo vidogo? Avirejesghee hadhi yake na kutafuta vijana waliohitimu kidato cha nne na sita waende huko kupata diploma nk….tungekuwa tumetengeneza wataalamu wengi sana wangeisaidia sekta ya kilimo….hajaliona hili, nadhani wala hajui kama hivyo vyuo bado vipo!!

Ohh, “nchi haina wataalamu wa ardhi…”, u***zi mtupu!! Kweli katika karne hii ambayo wenyewe wanasema “land has acquired value” tunashindwa kuandaa wapima ardhi wa kutosha kila wilaya? Hata wenye diploma tu au certificates zinazowawezesha kuwa na ujuzi wa kupima ardhi…ili tuwe sasa na maeneo yaliyopimwa na iwe rahisi kwa kila mtanzania kumiliki ardhi kwa uhalali? Kwa huyu jamaa, this was not an issue at all…hakuwahi kuwaza hilo!!

Amekuja na kitu anaita KILIMO KWANZA….!! Mnamuamini huyu? Mbona baba wa Taifa alikuwa nakwenda mapumziko kwao kijijini Butiama na kulima? Tena kwa mkono? Ule ulikuwa ni mfano wa kuigwa…Vipi huyu wa sasa anayedai amekulia kwenye chama na ni mjamaa? Sijawahi kumsikia ameenda kupalilia minanansi yake....

Itaendelea na kuendelea tena……ngoja ninywe maji
 
Back
Top Bottom