Siasa Za Kujitegemea

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,063
2,471
Hivi kulikuwa na sera zozote za kulifanya taifa kuwa ni la kujitegemea? Au zilikuwa ni porojo tu? Mpaka sasa sio dalili zote kuwa Tanzania itaachana na misaada kutoka nje.
 
Zakumi,
Umepotea wapi? Ndiyo, tulikuwa tuna sera za kulifanya taifa lijitegemee. Lakini tulikosea pale tuliporuhusu misaada itumike kujenga sera hizo. Ukishaanza kukubali misaada kwa kila kitu inakuwa vigumu kusema sasa misaada hapana. Lakini pia ujue wakati huo baada ya uhuru tulikuwa na engineers wawili tu na madaktari 12. Sasa ili upate engineers na madaktari ilikuwa rahisi kukubali "msaada" wa kusomeshewa engineers na madaktari wako. Lakini kwa hivi sasa, ukizingatia utitiri wa madini tuliyogundua, ingefaa tubadilishe sera, tutumie madini yetu kuzibia pengo linalojazwa na misaada. Lakini je, viongozi tulio nao na wakubwa wao nje ya nchi watakubali?
 
Hey Jasusi:

Narudi kwa muda tu. Toka uchaguzi upite niliwaachia ukumbi mmalize hasira zenu. Anyway, nimemaliza kumpitia Mao Tse Tung. Na inaonyesha hakuwa mjamaa au mkomunisti kama vile sisi tunavyofikri. Ukomunisti wake ulikuwa wa extract high technology kutoka Russia, Kuua mila za kizamani za kiChina, na kuifanya China kuwa Superpower.

Kuhusiana na sisi kuwa ma mainjinia wawili wakati wa uhuru, ni kisingizio. Tunashindwa ni kuwa models za maendeleo. Na tunapokuwa na models, hakuna sustainability.
 
Back
Top Bottom