Siasa za bongo na umangi meza wa viongozi wao

fiksiman

JF-Expert Member
May 17, 2008
402
104
Kwa wale wafuatiliaji wa siasa za tanzania hasa wanasiasa wa vyama vya mlengwa wa kushoto (si wapinzani hawa wanapinga nini)...utagundua kuwa hakuna chama kitachofanikiwa kuing'oa madarakani CCM hadi Yesu anarudi. Ndio nalazimika kusema hivi kutokana na tabia za viongozi wenyewe hasa wale wakuu kabisa.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema aliongoza mapinduzi ya kumtimua mpinzani wake mkuu katika nafasi ya uenyekiti wa Chama hicho Mhe. Benedicto Mutunguirehi uanachama kwa kile walichotuambia ni kukaidi agizo la Mwenyekiti huyo (si la kikao) la kuomba radhi kwa madai ya kukihujumu chama hicho alipofungua kesi mahamakani. inasemekana mutungirehi aligoma kufanya zoezi hilo na kumtolea maneno makali mdau huyo mkuu mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu. Sawa jamaa alitenda kosa. swali linakuja kwenye adhabu aliyopewa je inaendana na kosa lenyewe??? Hapa kiukweli Mrema kachemka maana tumegundua mzee wa guta mambo yalimfika shingoni, ikabidi atumie zengwe kufagia njia. FULL STOP.

Binafsi siamini kama Mutungurehi anaweza kuwa mpungufu wa shukrani hata baada ya kuwa mbunge kwa kupitia chama hicho na kukiwezesha TLP kuongeza mapato yake kupitia ruzuku na kuamua kukiangusha chama kwa makusudi. Ukiniuliza zaidi nitakwambia hii ndio staili inayoendelea katika vyma vyetu vya siasa na hata wakati mwingine kwenye taasisi zingine ikiwemo serikalini kwenyewe. Mkubwa hakosolewi na wala hapewi mpinzani si ndo maana jirani zangu wa CCM hawataki kumtambua mgombea yeyote atakayejitokeza kupimana ubavu na Mwenyekiti wao wa Taifa. NI UMANGI MEZA TUU HAKUNA JINGINE! Hebu niambie kwa kumbukumbu zako tukiweka kando CCM ni chama gani kingine cha upinzani kimepata viongozi wapya wa ngazi za juu kupitia demokrasia ya uchaguzi?? Jibu hakuna tena ukitaka kufukuzwa chama basi we jitokeze kama alivyofanya mtu fulani pale CUF sijajua hatma yake ila vijembe vinaendelea kutolewa.

Mrema, Lipumba, Mjomba Seif na wengine wengi ambao natarajia kuziona tena sura zao lwenye karatasi ya kupigia kura kama wagombea urais wamekaa madarakani kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote ya maana...tena mi naona ndo wanadumaza mfumo mzima wa demokrasia ya vyama vingi...yaani ni bure kabisa hawa watu. Waacheni vijana na watu makini kama Mutungirehi waje kutoa changamoto jamani tumechoka kuburuzwa. CCM tunajua ni chama cha wenye pesa wengine ni vibaraka tu pale ila pesa yako ndio itakupa ubunge, udiwani na hata Urais...wanyonge hatuna chetu, sasa na huku nako mnataka kuleta ufalme, uimla na umangi meza, kwanini??? Mnatukera sana tena hasa mimi mnaniudhi kupita kiasi.
 
Back
Top Bottom