Lutala
JF-Expert Member
- Jun 17, 2010
- 848
- 103
Rais Kikwete awaweka njia panda maaskofu, masheikh Send to a friend
Monday, 21 June 2010 08:53
Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa
Phinias Bashaya, Bukoba
RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba, wanasiasa waoga wanaoweza kutafuta madaraka kwa udini ni hatari na kuomba taasisi za dini nchini, kuwafundisha waumini wao kuwakataa wanasiasa hao kwenye uchaguzi wa Oktoba kwani wanawaeza kuingiza nchi katika maangamizi makubwa.
Kauli ya Rais imekuja kipindi ambacho baadhi ya wanasiasa wameanza kutumia udini, kutafuta madaraka katika uchaguzi mkuu huo wa Oktoba mwaka huu, ambao mkuu huyo wa nchi anatarajiwa kugombea tena ngwe ya pili na leo anachukua fomu Dodoma.
Onyo hilo alilitoa mjini Bukoba, alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Jubilee ya Injili katika Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ambayo pia yalihudhuriwa na wawakilishi wa majimbo rafiki kutoka nchi mbalimbali duniani.
Rais alionya, "mchezo wao ni mauti yetu sote, tusiwaendekeze ,siku ambayo tutaruhusu ubaguzi huo ndiyo mauti yetu, tujihadhari na viongozi hawa waoga na wasiojiamini ambao wanapenda madaraka kwa gharama yoyote.
Alifafanua kwamba, wapo wanasiasa waoga na wasiojiamini ambao wako tayari kutafuta madaraka kwa gharama yoyote kwa kutaka kueneza ubaguzi dhidi ya wapinzani wao, ili kujiimarisha kisiasa na kuwaomba viongozi hao, wasiwape nafasi kwani wanaweza kuipeleka nchi katika machafuko makubwa.
Mkuu huyo wa nchi, aliwataka viongozi wa madhehebu ya dini kuwaelekeza waumini wao kuwachagua viongozi waadilifu na kuwasaidia kuwatambua viongozi safi na ubora wa sera za vyama mbalimbali vya kisiasa.
Katika kuonyesha msisitizo, pia Rais alibainisha kwamba serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa kuabudu huku akionya kuwa siasa zina tabia ya kuchochea ubaguzi na kuwaomba viongozi hao kulisaidia taifa ili lisielekee kwenye misingi itakayowafanya watanzania kubaguana.
Aliongeza kwamba, madhehebu ya dini yana wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuwaandaa viongozi watakao kuwa na maadili mema ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya rushwa na maasi yanayokwenda kinyume na utamaduni wa Watanzania.
Awali, kabla ya Rais Kikwete kuelekea katika eneo la maadhimisho hayo, kundi kubwa la wananchi lilijikusanya nje ya Ikulu ndogo mjini hapa likidai linataka kumuona rais ili ashinikize kufanyika kwa zoezi la kuwatafuta ndugu zao wanaodaiwa kufa maji katika ajali ya mtumbwi iliyotokea juzi.
Kundi hilo ambalo baadhi yao walidai wamewapoteza ndugu zao huku wakiwa hawaoni jitihada zinazofanywa na serikali kuwatafuta baadaye lilifuatwa na maafisa wa usalama na kuwataka waondoke eneo hilo kwani wasingeweza kumuona rais na badala yake kushauriwa kumfuata mkuu wa wilaya ya Bukoba Samwel Kamote.
Wananchi hawakufanikiwa kumuona kiongozi huyo baada ya kudhibitiwa na wanausalama huku Alistides Gerase (43) akisimulia jinsi alivyookoka na kuwashuhudia abiria wenzake wakizama katika maji.
Mwananchi mwingine Bayona Honorath (32)alidai ndugu yake aliyekuwa abiria katika mtumbwi huo uliozama siku mbili zilizopita mwili wake ulikuwa haujapatikana.
Katika salamu zake Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Elisa Buberwa, alisema kanisa hilo litatumia fursa lilizonazo kuwaeliisha waumini wake jinsi ya kuwapata viongozi wenye uwezo na waadilifu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Askofu Buberwa aliweka bayana kwamba, kanisa hilo litawafundisha waumini kuzingatia sheria za uchaguzi kama zinavyoainishwa, ambapo pia sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Alex Malasusa pamoja na wawakilishi wa madhehebu mengine.