George Jinasa
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 399
- 52
Kuhusu kumpigia kura mtu fulani kwa misingi ya dini ni 'speculations' tu. Hakuna kwenye data. Kwamba baadhi ya viongozi wa dini waliwahubiria waumini wao wapige kura kiaina inaweza kuwa kweli ingawa baadhi ya viongozi wa dini walisingiziwa pia. Mimi ninataka tukiongea vitu tuongee vile ambavyo tunaweza kuvithibitisha na kama hatuwezi na bado tunaviongelea tunakuwa tunajidhalilisha. Namna hii ya kufikiri mimi naiita 'intellectual masturbation'.
Ndio maana hata mimi sisemi kwamba viongozi wote wa dini walihubiri hivyo. Nimesema inaweza kuwa wachache sana kati yao. Nakubali pia wapo waliosingiziwa. Na hilo la kuwepo watu au vyombo vya habari kuwasingizia viongozi wa dini kuhubiri udini ni tatizo la hisia za udini ambayo halipaswi kuachwa bila dawa.
Naheshimu mtizamo wako juu ya kuongea tunavyoweza kuthibitisha japo natofautiana nawe kimtizamo. Kama unasema mtu fulani specifically amefanya kosa fulani huna haki ya kuongea bila ushahidi. Ila kama kuna tuhuma za ujumla kuwepo kwa tatizo fulani una haki ya kulijadili kulingana na vyanzo vya tuhuma hiyo hata kama huna uhakika wa ukweli wa tuhuma hizo. Ni katika kujadili tuhuma hizo ndipo pia mnaweza kubaini ukweli au uongo wa tuhuma hizo. Kukaa kimya inaweza kuwa tatizo kama tuhuma hizo zikiwa za kweli. Mimi kwa msimamo wangu kila kinachosemwa kina chanzo. Ima aliekisema alikisikia na kukielewa vibaya au amekipotosha kwa makusudi. Tutaelewaje ukweli juu ya hili kama tutakaa kimya na kuogopa kusema kwa kuwa hatuna takwimu? Mara nyingine hata kujadiliana juu ya mambo haya ni aina moja wapo ya utafiti . Ndio maana toka mwanzo sijawa tayari kumnyoshea mkono mtu yoyote.