shule zipi nzuri za private boarding?

Lasthope

Senior Member
Jun 5, 2008
149
6
Wajameni naombeni msaada kwenye tuta, najua humu wapo watu wa aina zote which means kila swali au tatizo laweza kutatuliwa. Mimi naomba mnisaidie kujua shule za secondary za private boarding, girls only would be better au hata mchanganyiko as last choice. ningependa kujua ada ni ngapi according to different experiences. Kindly help yani natafuta shule lakini sijui nianzie wapi zaidi ya kuuliza watu maana kama mjuavyo shule za bongo hazina websites.
Thanks in advance
 
I think you should try to be a lil specific. Unataka shule ya o-level au A-level. Alaf kuna swala zima la dini. Shule nyingi za girls naona ni za dini ya Kristu. alaf sema kabisa if money aint a problem. kuna ada nyingine ukitajiwa utashangaa kama wewe ni Mtanzania wa kawaida kama mimi.

Shule nzuri ni ipi?????? Ask yourself
-Mazingira ya Kusoma
-Spoon feeding education
-Chakula
-Uhusiano kati ya Mwalimu na mwanafunzi
-Do u want knowledge au good results za National Exams
-Any extra curricula activities like sports and games
 
Asante six six, kwa ujumla nataka shule ambayo mtoto atakuwa na uwezo wa kupata knowledge na siyo spoon feeding, and offcourse at the end of the day afaulu mtihani maana akifeli the whole meaning inakuwa hakuna. Pia ni 0level ndo natafuta. Swala la ada pia ni muhimu ndo maana nikasema nitashukuru kama nitajua na ada ya specific shule inayoutajwa ili nijue kama nita afford au sitaweza. Swala la chakula si muhimu sana maana mi mwenyewe nilisoma nakula kande na ugali maharage kila siku, knowing hiyo ndo stardard food for most of the schools then it shouldnt be a problem. Kuhusu dini ni yoyote as long as hiyo shule haina ubaguzi.
Thaks for the questions umenisaidia nieleweeke zaidi.
 
kuna St.Joseph Millennium iko Goba,mbezi juu....ni ya Roman, ni nzuri kwa maono yangu. Ila ni mchanganyiko(lakini nafikiri wajua shule za seminary jinsi zilivyo, kuna ndugu zangu wanasoma pale kwa kweli naona imewasaidia sana na wamebadilika kitaaluma, tabia n.k. ada ni m.1.7 kwa mwaka,ni boarding school.... mwaka jana ilikuwa ni ya kumi kwa mtihani wa kidato cha pili na ndiyo walikuwa wanafunzi wa kwanza kwa shule yao..... hawana ubaguzi
 
Hapo nilipopa-bold ujumbe nimeupata..
 
ha ha ha ,Panatisha eeh, nafikiri kama mtu unauwezo si mbaya sana, muhimu mtoto apate elimu bora na si bora elimu[

Kwa kweli hata kama nina vijisenti, uamuzi wa kumpeleka mtoto ktk shule ya 1.7 m kwangu ni muhali. Labda awe na prospect ya kuwa new Albert Einstein ndo ntafikiria mara 2..

Naomba usinihukumu kwa hili..
 
St MARIAN BAGAMOYO ama almaarufu kwa BAYO. ni shule ya wasichana tupu.Ada zaidi ya laki nane,ipo ndani ya tano bora miaka 10 mfululizo.mtoto akipata wastani chini ya 80 wana m drop.Inauhusiano mzuri sana kati ya walimu na wanafunzi ni shule ya kikatoliki .

nyingine ni shule ya UJAMAA ni mchanganyiko ipo kati ya IGUNGA na NZEGA ada laki nne,statistics yao unaweza ingia ktk web ya wizara ukaangalia matokeo yao.
 
huyo mkuu wa mwanzo wa shule wa St. Marian kwa sasa yuko St.Joseph Millennium... ni sister anayeijua kazi yake na kuithamini..
 
st francis girls secondary school mbeya, ni ya kwanza kitaifa kwa miaka kadhaa, ada siyo kubwa , ila kuipata ni lazima mtoto awe na bongo ya kufaulu mitihani. wakishafanya mitihani ya kuingia pale, sisiter huyooo na mapepa yake na mwalimu mmoja hadi ujerumnai anarudi january na matokeo.

hakuna ubaguzi au upendeleo,kikwete, sumaye etc na wengine wamefanya majaribio ya kupeleka watoto pale bila kufaulu.

watoto wanajipikia wenyewe wanafundisjwa real life
 
Jee vipi kwa wavulana nauliza kama zipo skuli private boarding na ada yake pia nauliza kama malipo ya ziada kwani nasikia baadhi zina aplication fees pia nitapenda kuzijuwa
Ahsante
 
wanabodi kwanza tuelewe kuwa misingi bora ya elimu huanzia pale nyumbani,kuna ile general IQ build up kwa mtoto, tuwe acive kuwajengea watoto tabia ya kujiamini na kujiona wanaweza.Na haswa wanapokuwa primary school tuwaangilie kwa ukaribu mno maendeleo yao. Baada ya haya ndipo tugeukie shule sasa. Binafsi napenda sana shule zinazonjenga mtoto ajitegemee na sio kuwa spoon fed. Ajengwe kumuogopa Mungu na kuheshimu wenzake wote regardless of their faith,color,race,sex,etc. Na hapo ndipo kura yangu inadondokea kweye shule za misheni. Tuwe wakweli na nafsi zetu, wakatoliki na elimu hawana mchezo, maadili na mazingira ya nidhamu kwao ni namba moja. Hata hao viongozi kuanzia kikwete wanakimbiza watoto wao huko na wakifika huko adabu mbele.

Someone asked about boys school
hapa Dar ipo Feza boys ni nzuri kwa nidhamu na elimu.Inaendeshwa na waturuki. Ada ya sekondari boarding ni Tsh Millioni 3
 
ni kweli kwa wavulana feza ni nzuri sana, kitabia vijana wanakuwa gentlemen, bila kujali alilelewa vipi kabla, ila spoon feeding imewaharibu wajinga, na hakuna kufanya kazi yoyote zaidi ya kusoma. Wanakula vizuri sana na wanafaulu pia sana.
Shule za misheni za kikatoliki na kilutheri wanazingatia sana nidhamu ya muda, muda wa kazi, kusoma, kusali, na kucheza kidogo. Hazingatii comfort sana.
mfano Zile za lushoto na St. Josef Goba watoto wanalalamika chakula etc.
Kuchagua sekondari ya mtoto kunataka mzazi namtoto waongee wajue wanategemea nini, kama ni michezo hakuna pa kwenda ila Mgulani au Filbert Bayi.
Choice ya wavulana ni ndogo sana kuliko ya wasichana.
kuna shule zina programs za lugha, sanaa, music nk. Mtoto wako anaweza kukuongoza, mpe homework mwenyewe pia.

mimi mwenyewe huwa natafuta shule kwa kufuata imani, extracurricula activities, nidhamu ya waalimu na wafanyakazi na jinsi wanavyowasiliana na wanafunzi. Elimu hii ya vitabuni hii ipo tu, mtoto atayajua tu kama tukimkalia kooni. (kufaulu mitihani ni muhimu pia)
 
Asanteni sana wadau kwa msaada mlioutoa, ni kweli mmenipanua mawazo sana. nilikuwa sijui pa kuanzia kabisaaa, ila kwa hizi ada inabidi wazazi tujifikirie mara mbili kabla ya kuongeza watoto, haya mambo0 sayo mambo otherwise watoto watishia kuwa kina kayumba tu lol.
 
Hapo nilipopa-bold ujumbe nimeupata..

Hizo ni shule za mafisadi wa kati kama kuna mtu ana uwezo wa kumsomesha mtoto katika shule aghali namna hiyo kuliko hata masters basi kuna ushahidi wa kutosha kuwa mtandao wa mafisadi ni mkubwa!

Good school sio tu nzuri kwa elimu bali affordable. Isiwe kusomesha ndio na wazazi/walezi washindwe kabisa na vita dhidi ya umaskini.

Huwa anyway napenda kuongelea majority vote na sii tabaka la watu kiduchu ambao wengi ni mafisadi, au ni products za mafisadi nk.
Cheers
 
Back
Top Bottom